Namchukia mzee wangu!

Kuna watoto ambao Baba zao wapo na hawafanyi kitu alichofanya Baba yako , kuna watoto wametelekezwa na Baba zao, wewe umejua kusoma na kuandika na kuongea kingereza Kwa Ada iliotokana na nguvu ya Baba yako umekula chakula umeshiba Kwa Nguvu ya Baba yako af confidently bila aibu unakuja na akili zako za ajabu kumchafua Baba yako ina maana hio ndo shukran unayomlipa Kwa kukutunza
 
Unakujaje kumtangaza Baba yako ana vimada huku JF hivi nguvu yote aliyowekeza kwako af aje kushuhudia toto alilosomesha ndo linamlipa Kwa namna hii si unatafuta laana Mzee, bro Kwa kwel umeniudhi maana Kama mzazi katimiza aliyotakiwa kutimiza basi mshukuru Mungu maana wengine hatukupata bahati uliyopata bro
 
Aheri usingezaliwa kabisa
Mzee kapata hasara kubwa Sana kwako

Pigana Acha wenge dogo

Mie nikiwa 17yrs nimemaliza la Saba nilijenga geto langu mwenyewe, kama nini si usakafie Tu na kuweka bati shame on you

Unamlalamimia mshua unamlundiki mabalaa, unampa sifa biyako mkubwa, huyu bi yako mkubwa kafanya nini akili kamasi kabisa

Kaombe msamaha laana inakufuata hutakuwa na kikao duniani
Moja ya madhara ya mtoto wa kiume kukaa jikoni na mama Yao ndo haya kazi itakua ni kuchagua mabaya ya Baba Tu , ina maana jamaa alikua haoni mama yake ni golikipa Tu anakaaa nyumbani haleti kitu na mpambanaji ni Mzee Tu lkn Kwa sasa anaona Mzee wake ni mjinga
 
Nimezaliwa katika familia ya kawaida tu iliyokidhi mahitaji ya msing mwaka 1988. Baba yangu alikuwa mwalimu ila baadaye akaacha bila kutoa sababu za msingi. Sababu yake kubwa ninapomuuliza ni "walikuwa wakinionea wivu na walikuwa wananiroga hasa mkuu wangu wa kazi".

Huwa nachukia nikisikia majibu haya na huondoka upesi kwani naweza hata kumpiga(japo naomba isije kutokea).
Mama yangu ni wale mama wa nyumbani, alikutana na huyu mzee kwenye biashara, alikuwa akiuza viazi vitamu. Ni darasa la saba.

Tangu utoto tumeishi maisha naweza kusema hatukutakiwa kuishi maisha hayo, ukizingatia mzee alikuwa mfanyakazi na from nowhere akaacha kazi.

Najiulizaga mno je, hakufikiria kuwa atakuwa na familia? Je alitoka mwanafunzi na hivyo akakimbia hasira za wanajamii?

Hatukuwahi kulala njaa, tulikuwa tunakula na niseme ukweli toka najitambua mzee alikuwa akitupenda mno kwa kidogo alichonacho, alijitahidi mno wanawe tusipate shida kwa kutupa kila tulichotaka ndani ya uwezo wake.

Alikuwa akitutoa out n.k, katika hili naweza kusema familia yetu ni zile familia za kawaida ila tuliishi maisha ya kizungu huenda kuzidi hata baadhi ya watoto wa matajiri.

Tatizo likaja kwenye nyumba tuliyoishi, ilikuwa mbovu kulinganisha na maisha tuliyoishi. Mzee sijui alikuwa kachanganyikiwa au la, nyumba ndani haina sakafu ni vumbi tu, na wakati huo bado ilikuwa ya nyasi.

Mama alikuwa akimshawishi wakarabati nyumba, alichokuwa anajibu "mtoto anayeona hapa hapamfai basi ahame" (hapo ni tayari ni mtu mzima kidogo najitambua), nilikuwa nachukia na namchukia mno kwa kaulo hizi.

Mbaya zaidi uwezo alikuwa nao kwa wakati huo kwani alikuwa mlinzi wa shirika la serikali fulani, tena wa kudumu wa kuajiriwa na serikali. Nilikuwa naona aibu mno nilipotembelewa na classmates wangu hasa wa kike(nilizidi kumchukia mzee).

Mama alikuwa akisema hutu baba yenu hanishirikishi chochote na hela zake sijui zinaishia wapi, na mzew akiulizwa kuhusu hilo alikuwa mkali mno(kwa hili chuki yangu iliendelea kukua).

Siku moja akaniambia, "mimi nimesgajitoa mhanga na maisha haya, naishi pabovu wakati wafanyakazi wenzangu wana nyumba, nataka nyie wanangu muwe mnaheshimika na mjenge ninyi hizo nyumba bora zenye sakafu kama mnavyodai".

Nilimuelewa kwa kauli hii japo kidogo. Nilimuuliza kama haoni aibu akajibu " sioni aibu ni maisha niliyochagua, kama hamtaki muhame". Nilichukia mno kwa marudio ya kauli hizi.

Sasa ni mtu mzima na nimefanikiwa kidogo ila si kama ninavyotaka, naendelea kupambana.

Mzee katika masuala ya ada alikuwa hasumbui kabisa, alikuwa analipa ada mpaka inabaki change na naidai shule, kwenye mambo ya elimu kwa kweli hakutaka masihara. Ila shida ni maendeleo home ikiwemo nyumba.

Nina kaka zangu wote alipoteza hela nyingi kuwapigania, acha dada zangu pia( japo walipuyanga na hela zilipotea). Katika hili nampongeza kwa 5%.

Pia mwenye kujali elimu ya dada zangu, kwani kuna mmoja alikuwa anatembea kwa miguu umbali mrefu kumpelekea baadhi ya mahitaji shule.

Pia kaka yangu mkubwa alimpa laki 3 kwa wakati huo ili aongezee kwenye biashara yake(hili hakumshirikisha bi mkubwa, na bi mkubwa alilalamika) japo bro huyu alikula mtaji.

Kaka zangu wote walikataa shule kwa vinywa vyao. Waliharakia maisha, na sasa wanahaha!

Huyu mzee hela za kununua mashamba mbona anazo? Za kununua radios, TV's n.k, kwa nini ashindwe kutenga japo laki 1.5 kwa wakati ule aboreshe nyumba??

Yaani simuelewagi kabisa huyu dingi, anatupambania kwenye elimu sasa kwanini asi-fight kukarabati nyumba? Kila siku ugomvi na bi mkubwa ilikuwa nk issues hizo hapo.

Pia dada zangu wote walikataa shile kwa vinywa vyao japo mzee wakati huo alitaka kuwaendeleza(nampongeza kwenye hilo).

Simuelewi huyu mzee na namchukia niseme wazi, kwa sababu anasababisha aibu kwa familia, nakumbuka nyumba ndani vumbi yeye anataka kuweka king'amuzi, huu niliona upuuzi tu.

Mfano kuna wakati alishindwa kusave hela za maandalizi ya mimi kuingia chuo, muda umefika wenzangu wanakwenda chuo mimi naranda randa tu home kwenye kibanda kibovu chenye vumbi(shame), halafu tunaanza kuhangaika kuomba omba kwa mkuu wa wilaya na mbunge msaada mimi na yeye, tulikuwa tunatembea ofisi zote na kukumbana na dharau tu(shame).

Nikitakiwa kujiunga jkt mujibu, alininunulia vifaa vyote kama ilivyoelekezwa(nampongeza kwa 10% kwani alinunua vyenye bei na ubora mkubwa), ila kwa nini ashindwe kukarabati nyumba? Ambayo inabeba heshima za mtu?

Nimeaibika mno na inatosha, nilishindwa hata kulete demy ghetto kwa upuuzo huu huu, mazingira mabovu yapo hovyo hovyo..

Pia ni kwa nini japo hana hela ya kutosha ila anamsaliti bi mkubwa na wasichana mabinti kuliko bi mkubwa?( japo hufanya kwa kificho sana)Hiyo sio aibu?

Kwa nini amfiche bi mkubwa mshahara wake? Niishie hapa...

Sitaki kuongea mengi naona nitakufuru na mimi sitaki kukufuru, kikubwa ni hayo tu, jamani nishaurini kwani inafika wakati hata kuonana naye sitaki. NB:

Huyu mzee alimaliza form four mwaka 1974!
Shida ni wewe kutoleta mademu home kwenu au??
Shukuru kwa kidogo alichokupatia na muombee dua njema
 
Aheri usingezaliwa kabisa
Mzee kapata hasara kubwa Sana kwako

Pigana Acha wenge dogo

Mie nikiwa 17yrs nimemaliza la Saba nilijenga geto langu mwenyewe, kama nini si usakafie Tu na kuweka bati shame on you

Unamlalamimia mshua unamlundiki mabalaa, unampa sifa biyako mkubwa, huyu bi yako mkubwa kafanya nini akili kamasi kabisa

Kaombe msamaha laana inakufuata hutakuwa na kikao duniani
Shukrani kaka!
 
Ukute Mzee wako ni afisa mzalendo wa serikali anayelinda taifa. Siku akifariki usishangae akafunikwa na bendera.

Mheshimu mzee wako Mkuu, mambo ya yeye na mama yako waachie wenyewe hujui nani kazingua nini.
Hapo unaniogopesha mno, kwa life lile sidhani kama kuna kitu kama hicho!
 
Hata kama bado namchukia tu! Nyumba mbovu halafu ... Sitaki niendelee, nisije tukana.
Subiri ujenge ya kwako,hiyo nyumba mnayoishi ni yake wewe unalilia nini,karidhika mwenyewe na mke wake,hata kama mkewe haridhiki mbona haondoki hapo nyumbani,na ukitaka kujua mkewe karidhika mnaedelea kuzaliwa humo humo,acha hizo bana......
 
kuwa na amani kama aliwaweka nyinyi priority, that's what is important mkuu, kuna wakati nilimchukia mzazi wangu,,,ila ulikua ni utoto,i came to realize he is the best dad ever, mkuu appreciate efforts tena umuonyeshe una appreciate before its too late, kila mtu ana journey yake hapa duniani,ndio maana nikakwambia fight for your kids wasiwe na insecurities ulizokua nazo ila usim blame mzazi wako,he did the best he could...
We ongea tu mwenzio alishindwa kulia tunda kimasihara kwenye nyumba ya baba yake ....hivyo akisoma wenzie walivyo kula tunda kimasihara home kwao roho inataka imtoke
 
Itoshe kusema mtoa mada ni wale ambao Baba anauza ngombe ili kupeleka ngombe ingine shule, akili za kiduanzi Sana hizi . Shubaamiti wahedi
 
Subiri ujenge ya kwako,hiyo nyumba mnayoishi ni yake wewe unalilia nini,karidhika mwenyewe na mke wake,hata kama mkewe haridhiki mbona haondoki hapo nyumbani,na ukitaka kujua mkewe karidhika mnaedelea kuzaliwa humo humo,acha hizo bana......
Nyie mboga saba kaeni pembeni
 
Itoshe kusema mtoa mada ni wale ambao Baba anauza ngombe ili kupeleka ngombe ingine shule, akili za kiduanzi Sana hizi . Shubaamiti wahedi
Sasa matusi yanakujaje hapa wewe wa kishua! Nyie mboga 7 hamtoelewa, kaeni kimya.
 
Tuheshimiane, acha ujinga.
Yaaani comments zote hizi 99% zipo against na wewe hujistukii tu bro.....?


Kama hizo hazitoshi naongeza na hiii...!

"Sogeza sikio nikunong'oneze ....bao lako wewe Bora mzee angemwaga pembeni" maana umekuwa kirusi kwake.
 
Tuheshimiane, acha ujinga.
Yaani. Pamoja na comments zote hizi 99% zipo against na wewe lkn bado hujistukii tu.....?

Kama hiyo haitoshi chukua na hii sogeza sikio nikunong'oneze "Bro hili bao lililo sababisha wewe utokee Bora mzee wako angewamwagia hao michepuko wake mgongoni akiwa anawala style" ingemsaidia Sana kwa maisha ya mbeleni kuepukana na virus Kama wewe.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom