Namchukia mzee wangu!

Namchukia mzee wangu!

Jana Ulirudi Usiku

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
2,360
Reaction score
2,281
Nimezaliwa katika familia ya kawaida tu iliyokidhi mahitaji ya msing mwaka 1988. Baba yangu alikuwa mwalimu ila baadaye akaacha bila kutoa sababu za msingi. Sababu yake kubwa ninapomuuliza ni "walikuwa wakinionea wivu na walikuwa wananiroga hasa mkuu wangu wa kazi". Huwa nachukia nikisikia majibu haya na huondoka upesi kwani naweza hata kumpiga(japo naomba isije kutokea). Mama yangu ni wale mama wa nyumbani, alikutana na huyu mzee kwenye biashara, alikuwa akiuza viazi vitamu. Ni darasa la saba.

Tangu utoto tumeishi maisha naweza kusema hatukutakiwa kuishi maisha hayo, ukizingatia mzee alikuwa mfanyakazi na from nowhere akaacha kazi. Najiulizaga mno je, hakufikiria kuwa atakuwa na familia? Je alitoka mwanafunzi na hivyo akakimbia hasira za wanajamii?

Hatukuwahi kulala njaa, tulikuwa tunakula na niseme ukweli toka najitambua mzee alikuwa akitupenda mno kwa kidogo alichonacho, alijitahidi mno wanawe tusipate shida kwa kutupa kila tulichotaka ndani ya uwezo wake. Alikuwa akitutoa out n.k, katika hili naweza kusema familia yetu ni zile familia za kawaida ila tuliishi maisha ya kizungu huenda kuzidi hata baadhi ya watoto wa matajiri.

Tatizo likaja kwenye nyumba tuliyoishi, ilikuwa mbovu kulinganisha na maisha tuliyoishi. Mzee sijui alikuwa kachanganyikiwa au la, nyumba ndani haina sakafu ni vumbi tu, na wakati huo bado ilikuwa ya nyasi. Mama alikuwa akimshawishi wakarabati nyumba, alichokuwa anajibu "mtoto anayeona hapa hapamfai basi ahame" (hapo ni tayari ni mtu mzima kidogo najitambua), nilikuwa nachukia na namchukia mno kwa kaulo hizi.

Mbaya zaidi uwezo alikuwa nao kwa wakati huo kwani alikuwa mlinzi wa shirika la serikali fulani, tena wa kudumu wa kuajiriwa na serikali. Nilikuwa naona aibu mno nilipotembelewa na classmates wangu hasa wa kike (nilizidi kumchukia mzee).

Mama alikuwa akisema hutu baba yenu hanishirikishi chochote na hela zake sijui zinaishia wapi, na mzew akiulizwa kuhusu hilo alikuwa mkali mno(kwa hili chuki yangu iliendelea kukua).

Siku moja akaniambia, "mimi nimesgajitoa mhanga na maisha haya, naishi pabovu wakati wafanyakazi wenzangu wana nyumba, nataka nyie wanangu muwe mnaheshimika na mjenge ninyi hizo nyumba bora zenye sakafu kama mnavyodai". Nilimuelewa kwa kauli hii japo kidogo. Nilimuuliza kama haoni aibu akajibu " sioni aibu ni maisha niliyochagua, kama hamtaki muhame". Nilichukia mno kwa marudio ya kauli hizi.

Sasa ni mtu mzima na nimefanikiwa kidogo ila si kama ninavyotaka, naendelea kupambana. Mzee katika masuala ya ada alikuwa hasumbui kabisa, alikuwa analipa ada mpaka inabaki change na naidai shule, kwenye mambo ya elimu kwa kweli hakutaka masihara. Ila shida ni maendeleo home ikiwemo nyumba.

Nina kaka zangu wote alipoteza hela nyingi kuwapigania, acha dada zangu pia( japo walipuyanga na hela zilipotea). Katika hili nampongeza kwa 5%. Pia, mwenye kujali elimu ya dada zangu, kwani kuna mmoja alikuwa anatembea kwa miguu umbali mrefu kumpelekea baadhi ya mahitaji shule.

Pia kaka yangu mkubwa alimpa laki 3 kwa wakati huo ili aongezee kwenye biashara yake(hili hakumshirikisha bi mkubwa, na bi mkubwa alilalamika) japo bro huyu alikula mtaji. Kaka zangu wote walikataa shule kwa vinywa vyao. Waliharakia maisha, na sasa wanahaha!

Huyu mzee hela za kununua mashamba mbona anazo? Za kununua radios, TV's n.k, kwa nini ashindwe kutenga japo laki 1.5 kwa wakati ule aboreshe nyumba? Yaani simuelewagi kabisa huyu dingi, anatupambania kwenye elimu sasa kwanini asi-fight kukarabati nyumba? Kila siku ugomvi na bi mkubwa ilikuwa nk issues hizo hapo.

Pia dada zangu wote walikataa shile kwa vinywa vyao japo mzee wakati huo alitaka kuwaendeleza(nampongeza kwenye hilo). Simuelewi huyu mzee na namchukia niseme wazi, kwa sababu anasababisha aibu kwa familia, nakumbuka nyumba ndani vumbi yeye anataka kuweka king'amuzi, huu niliona upuuzi tu.

Mfano kuna wakati alishindwa kusave hela za maandalizi ya mimi kuingia chuo, muda umefika wenzangu wanakwenda chuo mimi naranda randa tu home kwenye kibanda kibovu chenye vumbi(shame), halafu tunaanza kuhangaika kuomba omba kwa mkuu wa wilaya na mbunge msaada mimi na yeye, tulikuwa tunatembea ofisi zote na kukumbana na dharau tu(shame).

Nikitakiwa kujiunga jkt mujibu, alininunulia vifaa vyote kama ilivyoelekezwa(nampongeza kwa 10% kwani alinunua vyenye bei na ubora mkubwa), ila kwa nini ashindwe kukarabati nyumba? Ambayo inabeba heshima za mtu?

Nimeaibika mno na inatosha, nilishindwa hata kulete demy ghetto kwa upuuzo huu huu, mazingira mabovu yapo hovyo hovyo. Pia, ni kwa nini japo hana hela ya kutosha ila anamsaliti bi mkubwa na wasichana mabinti kuliko bi mkubwa?( japo hufanya kwa kificho sana)Hiyo sio aibu?

Kwa nini amfiche bi mkubwa mshahara wake? Niishie hapa...

Sitaki kuongea mengi naona nitakufuru na mimi sitaki kukufuru, kikubwa ni hayo tu, jamani nishaurini kwani inafika wakati hata kuonana naye sitaki. NB:

Huyu mzee alimaliza form four mwaka 1974!
 
Wewe ndo mwenye matatizo na unahitaji maombi maana hayo ni mapepo mkuu!! Umesema haujawahi kulala na njaa,mzee amewatunza kwa kila kitu, wewe unafikiri hiyo hela alikuwa anaokota ???jitafakari upya na mpende mzee wako!!
Wakolosai 3:20
Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
 
90% ya vijana wa mjin tulio fanikiwa na wanaovimba mjin uko kijijin au manyumban kwao walkotoka ndio ua pako katika mazngira hayo hii maana yake nkwamba sio kwamba wazaz wetu hawaon nyumba kali no ila n mind set zao kwamba akiangalia yeye alipokua akiishi kwa baba ake apo kwake anaona amepga hatua sana sasa n wajibu wako ww kufkir nje ya boks either kwako pawe vile unavyotaman au umjengee nyumba ya ndoto zako pembem ya nyumba yake il aone tofaut na usije jichanganya ukamvunjia nyumba yake kisa unataka kumjengea ya kigae huta amin.. na ndio utasema hana shukran na utamchukia mara mbil kikubwa jbane jenga nyumba ya familia pemben ya hyo nyumba yake
nawasilisha
mbebalawama
spkin from exprienc.
 
Chukua simu mpigie mzee wako leo umshukuru kwa kulipa ada,kuwatoa out na kununua msosi na nguo,huyo mzee ni mfano wa kuigwa,kuna wazee hata ada hawalipi chakula ndani shida,jilaumu mwenyewe aliyekwambia usifaulu nani
Na amtumie pesa angalau 200K mzee akanywe bia.
Sio kazi rahisi kulea familia hasa ada na chakula.
Sema Asante kwa baba yako achana na mambo ya nyumba nzuri,ukikaza makalio utajenga nyumba yako na kuweka tiles nk.
 
Nimezaliwa katika familia ya kawaida tu iliyokidhi mahitaji ya msing mwaka 1988. Baba yangu alikuwa mwalimu ila baadaye akaacha bila kutoa sababu za msingi. Sababu yake kubwa ninapomuuliza ni "walikuwa wakinionea wivu na walikuwa wananiroga hasa mkuu wangu wa kazi".

Huwa nachukia nikisikia majibu haya na huondoka upesi kwani naweza hata kumpiga(japo naomba isije kutokea).
Mama yangu ni wale mama wa nyumbani, alikutana na huyu mzee kwenye biashara, alikuwa akiuza viazi vitamu. Ni darasa la saba.

Tangu utoto tumeishi maisha naweza kusema hatukutakiwa kuishi maisha hayo, ukizingatia mzee alikuwa mfanyakazi na from nowhere akaacha kazi.

Najiulizaga mno je, hakufikiria kuwa atakuwa na familia? Je alitoka mwanafunzi na hivyo akakimbia hasira za wanajamii?

Hatukuwahi kulala njaa, tulikuwa tunakula na niseme ukweli toka najitambua mzee alikuwa akitupenda mno kwa kidogo alichonacho, alijitahidi mno wanawe tusipate shida kwa kutupa kila tulichotaka ndani ya uwezo wake.

Alikuwa akitutoa out n.k, katika hili naweza kusema familia yetu ni zile familia za kawaida ila tuliishi maisha ya kizungu huenda kuzidi hata baadhi ya watoto wa matajiri.

Tatizo likaja kwenye nyumba tuliyoishi, ilikuwa mbovu kulinganisha na maisha tuliyoishi. Mzee sijui alikuwa kachanganyikiwa au la, nyumba ndani haina sakafu ni vumbi tu, na wakati huo bado ilikuwa ya nyasi.

Mama alikuwa akimshawishi wakarabati nyumba, alichokuwa anajibu "mtoto anayeona hapa hapamfai basi ahame" (hapo ni tayari ni mtu mzima kidogo najitambua), nilikuwa nachukia na namchukia mno kwa kaulo hizi.

Mbaya zaidi uwezo alikuwa nao kwa wakati huo kwani alikuwa mlinzi wa shirika la serikali fulani, tena wa kudumu wa kuajiriwa na serikali. Nilikuwa naona aibu mno nilipotembelewa na classmates wangu hasa wa kike(nilizidi kumchukia mzee).

Mama alikuwa akisema hutu baba yenu hanishirikishi chochote na hela zake sijui zinaishia wapi, na mzew akiulizwa kuhusu hilo alikuwa mkali mno(kwa hili chuki yangu iliendelea kukua).

Siku moja akaniambia, "mimi nimesgajitoa mhanga na maisha haya, naishi pabovu wakati wafanyakazi wenzangu wana nyumba, nataka nyie wanangu muwe mnaheshimika na mjenge ninyi hizo nyumba bora zenye sakafu kama mnavyodai".

Nilimuelewa kwa kauli hii japo kidogo. Nilimuuliza kama haoni aibu akajibu " sioni aibu ni maisha niliyochagua, kama hamtaki muhame". Nilichukia mno kwa marudio ya kauli hizi.

Sasa ni mtu mzima na nimefanikiwa kidogo ila si kama ninavyotaka, naendelea kupambana.

Mzee katika masuala ya ada alikuwa hasumbui kabisa, alikuwa analipa ada mpaka inabaki change na naidai shule, kwenye mambo ya elimu kwa kweli hakutaka masihara. Ila shida ni maendeleo home ikiwemo nyumba.

Nina kaka zangu wote alipoteza hela nyingi kuwapigania, acha dada zangu pia( japo walipuyanga na hela zilipotea). Katika hili nampongeza kwa 5%.

Simuelewi huyu mzee na namchukia niseme wazi, kwa sababu anasababisha aibu kwa familia, nakumbuka nyumba ndani vumbi yeye anataka kuweka king'amuzi, huu niliona upuuzi tu.

Mfano kuna wakati alishindwa kusave hela za maandalizi ya mimi kuingia chuo, muda umefika wenzangu wanakwenda chuo mimi naranda randa tu home kwenye kibanda kibovu chenye vumbi(shame), halafu tunaanza kuhangaika kuomba omba kwa mkuu wa wilaya na mbunge msaada mimi na yeye, tulikuwa tunatembea ofisi zote na kukumbana na dharau tu(shame).

Nikitakiwa kujiunga jkt mujibu, alininunulia vifaa vyote kama ilivyoelekezwa(nampongeza kwa 10% kwani alinunua vyenye bei na ubora mkubwa), ila kwa nini ashindwe kukarabati nyumba? Ambayo inabeba heshima za mtu?

Nimeaibika mno na inatosha, nilishindwa hata kulete demy ghetto kwa upuuzo huu huu, mazingira mabovu yapo hovyo hovyo... Niishie hapa.

Sitaki kuongea mengi naona nitakufuru na mimi sitaki kukufuru, kikubwa ni hayo tu, jamani nishaurini kwani inafika wakati hata kuonana naye sitaki.

Mkuu naomba nikuambie tu kuna watu wako hivyo, yaani yeye material things haziko sana akilini mwake... sasa bahati mbaya akapata mke aliye hivyo inakuwa balaa. Lakini mshukuru na umpende tu mzee wako. Jitahidi weka wewe mazingira mazuri ukiweza.
 
Back
Top Bottom