Fahamu kama namba yako ya NIDA ilitumika kusajili laini za simu usizozifahamu kwa mawakala wajanja wa kusajili laini

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,681
3,065
Wasalaam.

Ili kujua unabonyeza *106# kisha usajili wa NIDA (Utaingiza NIDA ID yako), baada ya hapo zitakuja namba zote zilizosajiliwa kwa ID yako ya NIDA. Kama namba haijui siyo yako maana yake wakala (agent) alifanya ujanja kutumia ID yako kusajili line nyingine.

Ukishaona kwenye list namba haijui basi unaenda kwenye shop iliyokaribu nawe una claim, then customer care anakuambia uweke finger print kisha hiyo namba inafutwa.

Kutokana na watu wengi kutokuwa na NIDA, mawakala wengi walitumia ujanjaujanja wa kusajili line kwa kutumia ID ya mtu mwingine na kuuza hizo line kati ya elfu 5 hadi elfu 20, inategemea watakavyokuona na uhitaji wako.

Mawakala wanafanyaje ujanja? Ukienda kusajili line yako atakwambia weka dole gumba lako baada ya dakika atakwambia network inasumbua hebu ingiza tena, ukifanya hivyo basi hapo jua umeumia, ile ya kwanza amesajili line ya mtu mwingine na ya pili anasajili line yako, kama haujui hiyo mbinu hauwezi kumstukia maana wapo very smart.

Kwahiyo, wote mlionunua line kwa mawakala zilizosajiliwa kwa NIDA maarufu kama Take Away, mjiandae kisaikolojia.

Utabonyeza mbili halafu utaweka namba yako ya NIDA, mwisho utatumiwa SMS ya namba zako zote ulizozisajili kama kuna namba haujaisajili utaenda kwenye shop yoyote ya kampuni ya simu ambayo wewe ni mteja wao halafu utapewa fomu ya ku-remove namba ambazo huzitambui.

20200211_072411.jpg

Jumanne NJEMA.
 
It is useless maana unakupa tuu laini uliyoko kwenye simu unatumia kuhakiki usajili. Uhakiki ungekuwa na maana kama ungekulotea namba za mitandao yote
Umeenda mbali kidogo kidogo...n kwamba wakala
It is useless maana unakupa tuu laini uliyoko kwenye simu unatumia kuhakiki usajili. Uhakiki ungekuwa na maana kama ungekulotea namba za mitandao yote
Sio useless...n kwamba kama umeenda kwa wakala wa voda atasajili line za wakala wa voda tu na sio mtandao mwingine ...hivyo sio rahis anapokuambia uweke tena dole gumba ukaweka kwenye mashine ya kusajili mtandao ambao n tofauti.
 
Umeenda mbali kidogo kidogo...n kwamba wakala

Sio useless...n kwamba kama umeenda kwa wakala wa voda atasajili line za wakala wa voda tu na sio mtandao mwingine ...hivyo sio rahis anapokuambia uweke tena dole gumba ukaweka kwenye mashine ya kusajili mtandao ambao n tofauti.
Huu uhakiki ungefaa uwe "ENABLED" kwenye mtandao wa TCRA ili aone namba alizosajili kampuni zote za simu hapa Tanzania. Mfano mimi nilimsajilia laini mama yangu mzazi kashindwa kuitumia na laini umeshafungwa ila mimi sina uwezo wa ku "UNREGISTER" itoke kabisa kwa jina langu
 
Back
Top Bottom