MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,586
- Thread starter
- #61
...😀 hapo kwenye wekundu Mj'1, wewe si wa kwanza kulitamka hilo wala si wa mwisho. Nishawasikia wanawake wengi wakiyatamka hayo kipindi cha misukosuko, na wengine wachache hata baada ya kuachana na wenzi wao...
Tatizo kila mwanaume (wa kisasa) utayekutana naye ana sifa hizo hizo za 'yai bichi'. Maovu ya mtu ni mwonekano wa tabia za nje, ambapo wewe ukiwa ni dereva wa mawazo yako una hiari ukwepe au uparamie.
Fikiria wewe ni dereva na mbele kuna shimo, ...Ukilikwepa hutaliumiza gari lako, ukiliparamia unajiumiza mwenyewe ilhali shimo linabakia pale pale. Mwache na 'kilema chake', huwezi kumtibu.
Chukulia mazuri yake (uliyompendea) yafunike hicho kilema.
Siyo nia yangu kumfanya aonekane mbaya (of which sitaki kuamini ni mbaya) but hata yale niliyompendea hapo mwanzo yamefunikwa. Nilikuwa nampenda alivyoweza kunichekesha kunifurahisha kwa matani yake ila sasa siyapati kwani hata kukusemesha ni tabu.
- Nilimpenda kwa kile nilichodhania ni caring yake- kumbe alikuwa ananibembeleza tu niingie kumi nanane- alishaacha kitambo na badala yake yote nikawa nafanya mimi- kubembeleza mimi, vijizawadi mimi n.k.
Sijui ngoja nivumilie pengine atabadilika !!