Nalivua pendo...

Nalivua pendo...

Mwanajamii ushauri wangu ni huu.
Jaribu kuchunguza yafuatayo ndo kiini cha gogolo hilo.
1.FINANCIAL FACTOR
2.BED ROOM FACTOR
3.RELATIVES FACTOR.
Ndoa nyingi matatizo yanaanzia hapo juu.

Bwana Fidel
Factors kubwa hapa financial and bedroom factor. Ukikuta mwanaume au mwanamke wanagombana hadi kuachana kwa sababu ya hizi factor mbili husishangae. Ila ukikuta wapenzi wanagombana hadi kuachana kwa factor ya relatives then wao wenyewe wana weakness kubwa kwenye mifumo yao ya maisha na utatuzi wa migogoro. Sociologically in conflict theory perspective mara nyingi ugomvi wa kimapenzi ni hulka ya mpenzi mmoja kutoridhika na kitu au jambo kutoka kwa mwenzake. Suala la mtu wa tatu kwenye theory hii linachukuliwa kama minor case kutokana na nguvu ya mapenzi ambayo hata Functional theory inazungumzia mapenzi kama sehemu muhimu sana ya kufanya muunganiko wa watu wawili au familia mbili au makabila mawili au mataifa mawili ambayo kamwe hayakuwahi kuwa na fununu za kuungana.

Kwa suala la mwenzetu hapa inabidi aangalie hizo factors mbili kama hiyo ya tatu ya relatives imeshaanza kuwa kikwazo basi hapo kuna tatizo kubwa sana zaidi ya mapenzi yenyewe, ogopa sana kuchukiwa na ndugu wa upande mmoja.
 
Inaumiza sana! kwanza leo the whole day utakuwa unalia tu, yeye hujui hata yuko wapi na anafanya nini.. You need sometimes yourself, ili uweze kujipanga upya. Ushirikiano kwa wawili ni muhimu sana especially panapokuwa na matatizo, angalia yeye hana habari na wewe unajitahidi kutafuta mwafaka end then haonyeshi ushirikiano. Ona majibu yake yalivyo mabaya eti hana "future na wewe, uchukue utakacho".

Wewe anza ukiendelea kusubiri aamue yeye hata amua na utaendelea kuumia.

UNAPOJIKWAA INUKA, JIPANGUSE, ENDELEA NA SAFARI. DUNIA INAZUNGUKA NA MAISHA YANAENDELEA, KWAHIYO JIKAZE FIKIRIA CHA KUFANYA NA WALA USIKIMBILIE KUTAFUTA MBADALA WAKE KWANI NAE ANAWEZA AKAKUTENDA. Again pole sana dada, hauko peke yako.
 
kwanini unahic kwamba mwenzako hakuhitaji tena? na yeye labda anahic hivyo hivyo ndio mana mnategeana nani wa kumwanza mwenzie, mmeshawahi kuongelea tofauti zenu? unajua unaelezea ki juu juu mami chanzo cha haya yote mpaka kufikia huku ni nini?

Nyamayao maisha haya yataka moyo (nimekuPM) dada huenda ukaelewa vema.
 
Bwana Fidel
Factors kubwa hapa financial and bedroom factor. Ukikuta mwanaume au mwanamke wanagombana hadi kuachana kwa sababu ya hizi factor mbili husishangae. Ila ukikuta wapenzi wanagombana hadi kuachana kwa factor ya relatives then wao wenyewe wana weakness kubwa kwenye mifumo yao ya maisha na utatuzi wa migogoro. Sociologically in conflict theory perspective mara nyingi ugomvi wa kimapenzi ni hulka ya mpenzi mmoja kutoridhika na kitu au jambo kutoka kwa mwenzake. Suala la mtu wa tatu kwenye theory hii linachukuliwa kama minor case kutokana na nguvu ya mapenzi ambayo hata Functional theory inazungumzia mapenzi kama sehemu muhimu sana ya kufanya muunganiko wa watu wawili au familia mbili au makabila mawili au mataifa mawili ambayo kamwe hayakuwahi kuwa na fununu za kuungana.

Kwa suala la mwenzetu hapa inabidi aangalie hizo factors mbili kama hiyo ya tatu ya relatives imeshaanza kuwa kikwazo basi hapo kuna tatizo kubwa sana zaidi ya mapenzi yenyewe, ogopa sana kuchukiwa na ndugu wa upande mmoja.

Sipo
Namshukuru MUNGU nimebahatika kwa hilo. Ndugu zake yeye ni ndugu zangu sina shaka na hilo wanao upendo wa ajabu ambao kwa kweli nadiriki kusema hata kwetu hatuko hivyo! Am very lucky katika hili.

Na ninahofia athari itakayotokea wakijua what is going on between us. Sidhani kama watatuelewa ingawaje wanamfahamu vilivyo ndugu yao!
 
MwanajamiiOne!..

Pole kwa yaliyokukuta. Mahusiano ya kimapenzi yana changamoto zake na yanahitaji uvumilivu. Kama bado una hasira, usifanye uamuzi wowote sasahivi ila tulia na utafakari. Maamuzi yaje wakati umetulia na una amani..
 
mtu ukishafikia maamuzi hayo ni kwamba ni kweli umechoshwa na hutakiwi kugeuka nyuma milele....kama kitu kimekushinda/kuchosha kwanini ung'ang'ane tu?

Dada nyamayao husiseme hivyo bana (milele kabisa) unaondoa hata ule uwezekano wa EX-BF na EX-GL kujikumbushia jamani. Nway sometimes inahitaji msimamo kama huu lakini its very hard kama aliyepita alikuwa anakwea hadi juu ya mlima lakini the present anahishia upenuni mwa mlima.
 
Mpwa bado nipo nipo kwanza ila hii through books and research.

Unajua mpwa nini,kabla sijaoa nilikuwa nafikiri naijua ndoa sana baada ya kuoa mpwa na ile miezi ya honey moon kupita,mpwa nikagundua sijui kitu na nikahisi ninahitaji kurudi darasani.To be honest,ndoa ni ngumu mpwa na usione watu wanazeeka katika ndoa,wanayo mengi yakukusimulia.Jaribu kuangalia signature ya mtoa mada,there is something for you
 
Dada nyamayao husiseme hivyo bana (milele kabisa) unaondoa hata ule uwezekano wa EX-BF na EX-GL kujikumbushia jamani. Nway sometimes inahitaji msimamo kama huu lakini its very hard kama aliyepita alikuwa anakwea hadi juu ya mlima lakini the present anahishia upenuni mwa mlima.

sasa huyo x kama alikuona wa maana sana kwanini hakukununua jumla? mambo ya kwenda mbele na kurudi nyuma c mazuri, huwaga nawashauri ma rnds zangu kama umeamua kufanya kitu ufanye bila kujutia baadae, ndio kama hapo MJO aamua kuchukua maamuzi mengine afanye bila kugeuka nyuma na awe ameridhika kutoka rohoni sio afanye huku rohoni anaumia hiyo itam cost, sipo haya mambo ya kusema "kujikumbushia" hayatakiwi kupewa nafac.
 
Pole MJ1, hayo ndo mapenzi,
ila kukaa mwenyewe itakugharimu sana, pumzika kidogo, kisha chukua muda kusoma mwanaume unayemtaka awe ana kupa kampani, la sivyo kila siku utakua mtu wa mawazo, that is life " Some lessons are learned through pain.Vision clears only after eyes are washed with tears.At times we have to be hurt to be stronger for life and for love"..pole ila usisononeka sana maana kusononeka ni sababu mojawapo ya kukikaribisha kifo chako
 
Pole sana Mwanajamiione,hizo ni changamoto katika masiha na ni lazima uzikubali,maana pia pasipo kukutana na hizi changamoto tunajisahau,kingine nachoweza kushauri kwanza kubaliana na hiyo hali na pili kaa jaribu kutulia na kutafakari usikurupuke kusema unatafuta replacement tafakari kwakina,kwenye ulimwengu wa mapenzi kuna mambo mengi sana ya kuumizana,kukatishana tamaa so what i can say tulia na jitahidi pia kuwa bize i hope hiyo itakusaidia kwa kiasi fulani kuondoa mawazo yanayokusumbua.
 
Habari
Leo naungana na dada yangu Mwasity katika kile alichokiimba.....

Leo nalivua pendo, nililopenda zamani
Nabadili wangu mwendo, nami niwe furahani
Nimechoshwa na vitendo, visa na purukushani
Kweli mapenzi uvundo, apendwapo hathamini (By Mwasiti)

Hivi unapofikia hatua kama hii
1. Nini cha kufanya ili uendelee kuwa strong?
2. What to do ili isikusumbue (the quilty concious)
3. Ufanyeje ikusahaulishe mapema

Nauliza tu ndugu zangu maana...................mh

Ndugu yangu bado unalia utavimba bure!!niPM
 
Pole MJ1, hayo ndo mapenzi,
ila kukaa mwenyewe itakugharimu sana, pumzika kidogo, kisha chukua muda kusoma mwanaume unayemtaka awe ana kupa kampani, la sivyo kila siku utakua mtu wa mawazo, that is life " Some lessons are learned through pain.Vision clears only after eyes are washed with tears.At times we have to be hurt to be stronger for life and for love"..pole ila usisononeka sana maana kusononeka ni sababu mojawapo ya kukikaribisha kifo chako

Kifaru
Aksante ndugu yangu.
Kuanza mwanzo naamini nitaweza ingawa itaniumiza sana tatizo ni moyo unauma kumwachia huyu ingawa nimefika kikomo! Najiuliza kweli nitawezamsahau kiasi cha kujikuta siku moja namkumbuka kwa maovu yake (ambayo ni mengi)?. Kusema kweli am using a lot of energy to love him, to be with him utafikiri naishi na yai bichi jinsi unavyolitunza lisidondoke au glass ya champaign siku ya arusi...... maana hutaaford kuiangusha uivunje-utapata wapi nyingine?!
 
Wala usihofu MJ1, kumsahau hutoweza kumsahau, ila amini itafikia mahala ule uzito wake moyoni kwako utakua haupo, atakua mtu wa kawaida tu kwako, mimi mwenyewe ilishanitokea, nilichojifunza ni kwamba inatakiwa ukiwa kwenye mahusiano uwe na maisha yako tofauti na ya uchumba wenu, chukulia mwanaume/mwanamke ni kama mgeni ktk maisha yako hivyo aishi tokana na msingi wa maisha yako, asipoweza achukue hamsini zake, kama angekua ni mfumo wa usagaji chakula tumboni ukiondoka unakufa basi ndo umnganganie, lakini kumbe watu mmekutana, na huko nyuma ulikua unaishi bila yeye sasa uhofie nini akiondoka, ni maumivu makubwa lakini inatakiwa mtu uwe jasiri ili uweze kuwa na maisha mazuri, haamna kitu kibaya kwenye mapenzi kama kuji sacrifice kwa ajili ya mtu, ila pole utamsahau tu,
 
Hatujatengana kwa sababu mwenzangu hajatamka hilo ila actions zake tu zainadhihirisha kuwa hanihitaji tena.

...mj1, "you've got to get the mind cleared out before you put the truth in it" aliyatamka hayo Louis Farrakhan.

hayo matendo unayoyaona na kuyahisi ni dhana tu! dhana humpeleka mtu motoni akaja jijutia baadae,... tafadhali clear off hiyo suspicious mind kwanza...

Tuko pamoja kama vile tunategeana nani aanze ili lawama ziwe juu yake.

...unaona sasa? yeye amekutamkia au mmetamkiana "anza wewe!" ? No, ni dhana yako tu hiyo inayokupelekea huko, acha!

Cha moto nakiona .... ndo maana nafikiria bora tu niamue mimi potelea mbali lawama ili nisiendelee kuteseka

...hakuna cha moto wala nini, unajitia kiwewe tu kwa kuogopa kivuli! usijitishe na 'mawazo machafu' katika kipindi hiki cha gharika na mawimbi makali,.... sote tumepitia humo humo...

Ushawahi kusikia wimbo nahodha kajitosa baharini? well, hilo unalofikiria la potelea mbali 'bora ujitose baharini' liachie huko huko mawazoni, usilitende tafadhali. Madhara yake ni mazito kuliko unavyofikiri.

Unaacha usalama wa chombo unajitosa baharini kwenye papa na nyangumi? malenga wetu walisema "pupwe lina msisimo kwenye kondoo wenye manyoya haba!"... jivishe gamba la kobe! kama hakutaki mwache yeye ndiye akutamkie!

Halafu hayo mateso, au kuendelea kuteseka ni mambo ya kujitakia!
Epukana na mazoea,... "a bird in hand" ndugu yangu, kuwa mwangalifu.

Mnapitia kwenye dhoruba tu za mapenzi, usiachie nanga!
 
...mj1, "you've got to get the mind cleared out before you put the truth in it" aliyatamka hayo Louis Farrakhan.

hayo matendo unayoyaona na kuyahisi ni dhana tu! dhana humpeleka mtu motoni akaja jijutia baadae,... tafadhali clear off hiyo suspicious mind kwanza...

...unaona sasa? yeye amekutamkia au mmetamkiana "anza wewe!" ? No, ni dhana yako tu hiyo inayokupelekea huko, acha!

...hakuna cha moto wala nini, unajitia kiwewe tu kwa kuogopa kivuli! usijitishe na 'mawazo machafu' katika kipindi hiki cha gharika na mawimbi makali,.... sote tumepitia humo humo...

Ushawahi kusikia wimbo nahodha kajitosa baharini? well, hilo unalofikiria la potelea mbali 'bora ujitose baharini' liachie huko huko mawazoni, usilitende tafadhali. Madhara yake ni mazito kuliko unavyofikiri.

Unaacha usalama wa chombo unajitosa baharini kwenye papa na nyangumi? malenga wetu walisema "pupwe lina msisimo kwenye kondoo wenye manyoya haba!"... jivishe gamba la kobe! kama hakutaki mwache yeye ndiye akutamkie!

Halafu hayo mateso, au kuendelea kuteseka ni mambo ya kujitakia!
Epukana na mazoea,... "a bird in hand" ndugu yangu, kuwa mwangalifu.

Mnapitia kwenye dhoruba tu za mapenzi, usiachie nanga!
Aksante Mbu maneno yako mazito ila duh ngoja nijaribu maana sina tena nguvu wala uvumilivu.

Nitawezaje kuondoa dhana hiyo wakati unaona kabisa dharau na chuki usoni kwa mwenza? au na haya ni dhana? Mwenzangu huyu haoni vibaya kukwambia 'you know everything that is happening is because of YOU' au unajua wewe ni mfitini ? to me kwa kweli sidhani kama nawezamshutumu mpenzi wangu so direct naona hii- Blaming everything kwake?? tena macho makavu hata kama ninauhakika there is no truth about it?

Ntajaribu Mbu. Nitafuata ushauri wako!
 
...Kuanza mwanzo naamini nitaweza ingawa itaniumiza sana tatizo ni moyo unauma kumwachia huyu ingawa nimefika kikomo! Najiuliza kweli nitawezamsahau kiasi cha kujikuta siku moja namkumbuka kwa maovu yake (ambayo ni mengi)?. Kusema kweli am using a lot of energy to love him, to be with him utafikiri naishi na yai bichi jinsi unavyolitunza lisidondoke au glass ya champaign siku ya arusi...... maana hutaaford kuiangusha uivunje-utapata wapi nyingine?!

...😀 hapo kwenye wekundu Mj'1, wewe si wa kwanza kulitamka hilo wala si wa mwisho. Nishawasikia wanawake wengi wakiyatamka hayo kipindi cha misukosuko, na wengine wachache hata baada ya kuachana na wenzi wao...

Tatizo kila mwanaume (wa kisasa) utayekutana naye ana sifa hizo hizo za 'yai bichi'. Maovu ya mtu ni mwonekano wa tabia za nje, ambapo wewe ukiwa ni dereva wa mawazo yako una hiari ukwepe au uparamie.

Fikiria wewe ni dereva na mbele kuna shimo, ...Ukilikwepa hutaliumiza gari lako, ukiliparamia unajiumiza mwenyewe ilhali shimo linabakia pale pale. Mwache na 'kilema chake', huwezi kumtibu.

Chukulia mazuri yake (uliyompendea) yafunike hicho kilema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom