Pakawa
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 8,202
- 14,122
Pole kwa yaliyokukuta. Usife moyo zidi kusonga mbele i know you can do it.
Mahusiano ni mtihani mkubwa katika maisha kuna wanaofaulu kuna wanaoshindwa.
kushindwa kwako mtihani huu katika maisha haina maana hukuwa na hekima au busara
ya kuweza kushinda mtihani. Nafahamu ni rahisi kwetu sisi kukushauri hiki na kile lakini
ni wakati mgumu sana kwako lakini usikubali hata kidogo hii hali ikaitawala akili yako kukufanya ujione kama dunia yote umeibeba wewe. Endelea na shughuli zako kama kawaida jaribu kujenga furaha katika moyo wako kila siku uamkapo asubuhi kikubwa na muhimu usifanye kosa la kusema utatafuta mwingine wa kucover hiyo nafasi utaweza kuumizwa zaidi. Furaha katika maisha si lazima uwe katika mahusiano/ndoa kila kitu kina wakati wake naamini ipo siku utapata yule ambaye hataiumiza roho yako kiasi hiki.