Nalivua pendo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nalivua pendo...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Jul 15, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Habari
  Leo naungana na dada yangu Mwasity katika kile alichokiimba.....

  Leo nalivua pendo, nililopenda zamani
  Nabadili wangu mwendo, nami niwe furahani
  Nimechoshwa na vitendo, visa na purukushani
  Kweli mapenzi uvundo, apendwapo hathamini (By Mwasiti)

  Hivi unapofikia hatua kama hii
  1. Nini cha kufanya ili uendelee kuwa strong?
  2. What to do ili isikusumbue (the quilty concious)
  3. Ufanyeje ikusahaulishe mapema

  Nauliza tu ndugu zangu maana...................mh
   
 2. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,800
  Likes Received: 2,480
  Trophy Points: 280
  yamekukuta ndugu yangu.sema wakuu wakusaidie vinginevyo..........................mhhhhhhhhhhhhhh
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapo Mwana tafuta kipoozeo cha pembeni anakuwa spare tyre ukiona uvundo unajirestisha kwa spare wewe huoni hata mafiga yapo matatu.
   
 4. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mie nafikiri cha kwanza ni kuwa makini na maamuzi yako.Je ni kweli its the time to quit.Pia ni vizuri ukazungumza na hisia zako,je ni kweli hakuna utakachokuwa ukikimiss baada ya kulivua pendo na kama kipo je hauwezi kucompromise na maudhi unayoyapata.Yaani ukavumilia maudhi huku unapata unachokihitaji,kwani ndivyo maisha yalivyo.Mwisho usijekujaribu kupingana na hali halisi,if its over,it is.Ingawa katika uzoefu wangu nimegundua kutengeneza penzi imara is a process,Iam sure you know it my sister.
   
 5. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nalo hili neno mpwa.Anajua ila alitaka litoke kwako,maana wawili nyie kama simba na yanga
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mtu ukishafikia maamuzi hayo ni kwamba ni kweli umechoshwa na hutakiwi kugeuka nyuma milele....kama kitu kimekushinda/kuchosha kwanini ung'ang'ane tu?
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  . Ndugu yangu we walitwambia wahenga kua uyaone... na leo ninayaona ah!

  Sina cha kusema mie yaani hapa kila kitu kizito! Akili haifanyi kazi, moyo unaniuma yet nimeshindwa mie ......
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  ............ Seriously Fidel Is that a solution kwa kweli?

  Kwa niliyonayo sidhani kama natamani tena ulimwengu huu wa mapenzi!! Huyo kipoozeo ntamtesa tu bure!
   
 9. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,800
  Likes Received: 2,480
  Trophy Points: 280

  Pole sana ndugu yangu umefumania au umeletewa nyumba ndogo nyumbani kwako au mumeo/shemeji harudi kabisa? aiseeeeeeee pole ndo hapo unapoaambiwa mahusiano ni strategic decision siyo lele mama.

  Pole sanaaaaaaa
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nakwambia hii ndo solution lakini hakikisha kipoozeo mnaenda kupima ili nawe uwe na uhakika na unachokitafuna.
  Unaelewa nini maana ya mapenzi?
  Si unataka usuuze nafsi na moyo wako uburudike basi hiyo ndo solution mbona yeye anasuuzika huko ambako hukujui?
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndo maisha yetu wanadamu yalivyo. Nilichojifunza ni kuwa ni lazima nijue kusameheana pia kupo especially kama kuna bond ya watoto maana vinginevyo rough zinazochezwa zitaathiri kila upande.
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  .. Kwa kweli mpaka hapa nilipofikia onadhani it is the time.... kwa sababu kama mwenzio amefikia hatua ya kuanza kutoona uwezekano wa ninyi kuwa pamoja (and say it) mwa muda ujao, achilia mbali maudhi madogo madogo na kashfa je bado si muda muafaka?

  Sawa kabisa usemacho lakini unapozungumza na hisia zako bado unampenda na katu makosa yake huyaoni kama ni kitu kwani unampenda kwa dhati, unafanyaje? wakati yeye ndo anaonekana kabisa kuregrete kuwa na wewe na pia ameshaamua hataki tena kuendelea (ingawa anafungwa na sheria na hajui atatokaje-either kwa kuogopa lawama toka kwa watu)

  .... Nakuelewa ndugu yangu. Na penzi imara linaweza kutengenezeka kama pana ushirikiano kati ya wawili nyie, siyo we unahangaika kulitengeneza wakati mwenzio lengo lake ni kuliteketeza
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hehehe analijua hilo haamini kama hii ndo solution.
  Hakuna haja ya kuunza kuwaza na kuumia moyoni wkt kitu kinatatulika tu simple. Watu wanaumia bure jaribu kuignore mambo yatakwenda bambam.
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Dada yamenikuta sina hata nguvu ya kusema........ huweziamini hapa niko natiririkwa na machozi ka bomba la mvua! Sijui nifanye nini wala nianzie wapi!
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hehehehe utajuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuta kumfahamu.
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndio ukubwa.Lakini kama maisha yetu yalivyo kwamba tunakuja na kwenda, basi hata matatizo nayo yanakuja na kwenda. Jipe moyo utashinda.
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Bora yangekuwa hayo dada!

  Hivi ulishawahi kuwa na mwenzio ukahisi kuwa anaregret kuwa na wewe (hisia zako tu) halafu siku ikatokea akakwambia tu out of no where- we do not have future? Halafu baada ya sentence hiyo akwambie chagua chochote utakacho uchukue halafu baada ya hapo husikii tena sauti yake?

  Mbaya zaidi wewe uwe bado unampenda!
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Fidel .......... shukuru MUNGU hayajakukuta ndugu yangu !
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ndahani nashukuru kwa kunipa moyo ila mh maana kama kuvumilia ni mwngi nimevumilia lakini mwishoni naona nashindwa. kwa nini mimi tu, mimi tu niwe nabembeleza kila siku hata kama makosa kafanya yeye?
  mimi tu niwe naumia kwa sabau yake?... kwa nini mimi tu ndo niwe nahangaika to make it work? ... mimi tu why mimi tu? jamani ah
   
 20. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,800
  Likes Received: 2,480
  Trophy Points: 280

  Ndugu yangu pole kweli hapo ni pakubwa na sijui kama utapata ufumbuzi wa haraka kikubwa tafuta vacation kakae mbali na eneo alipo ili ujitulize kabisa.

  Ila ndugu yangu mlikuwa kwenye ndoa au mahusiano ya kimapenzi tu.kama ni ndoa basi mwaweza mshirikisha hata aliyewafungisha ndoa kama muwa wakristo au shekh kama muwaislam.

  Kingine mlibahatika kuwa na watoto?kama bado hilo halitakufaa angalia chanzo cha yote hayo kwa kuwa kama imetokea mara moja na ghafla jaribu kukaa chini fikiria kitu kilichopelekea hayo yote.

  ni hayo tu ndugu yangu.once again pole sana.
   
Loading...