The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 378
Habari wana jamii..
Nimekuja kulimwaga hapa ili nipate ahueni ya moyo. Kwa wale watakaojifunza lolote na iwe hivyo.
Ni miaka miwili sasa nimekuwa na huyu mpenzi wangu ambaye nilimpenda sana hata yeye akawa analisema wazi jinsi ninavyoonyesha upendo kwake. Aliniumiza mara kadhaa na kuniacha mara kadhaa ila mimi nilikuwa wa kwanza kuomba msamaha hata kwa kosa lake. Amenifanya nilie mara kwa mara. Amenifanya niumie moyo wangu mara kwa mara.
Kila aliponiambia ananiacha, nilikua napata mshituko na kukosa furaha muda wote. Nilipiga magoti kumwomba Mungu juu yake. Nikamuomba arudi kwani nitamvumilia.
Alirudi, hakunifanyia visa muda mrefu mpaka juzi. Hakuongea chochote kuhusu kuniacha ila wanajamii, kwa mara ya kwanza nimeweza kutamka kuwa aachane na mimi na usiku wake nikalala usingizi mzuri sana. Sijajutia kuachana naye.
Mpaka leo sijaongea nae kwa simu wala kuonana naye. Nina furaha kujiona kama niliyetua mzigo fulani uliokuwa kichwani mwangu. Sijutii hata chembe. Sisikitiki hata kidogo.
Nadhania kuchukua maamuzi ya kuwa na familia yenye mama na mtoto mmoja tu yaani single parent. Nashawishika kusema single mothers wana furaha sana. Nami nataka kuwa hivyo. Natafuta furaha. Nimelivua pendo nililopenda zamani.
Funzo: USIJARIBU KUMUUMIZA ALIYEKUPENDA KWA MOYO WAKE WOTE KWA KUDHANI HATA UMFANYEJE ATAENDELEA KUKUPENDA. MOYO UNAPOBEBA MABAYA MENGI, NAFASI YA UPENDO HUPUNGUA NA BAADAE HUPOTEA KABISA.