Naliona anguko la Kibanda

Naliona anguko la Kibanda

Nadhani kosa alilolifanya ndg mtoa mada ni kusema gazeti mama. Lakini kwa mjibu wa taratibu za kibiashara, in business language, Tanzania Daima is related to CHADEMA (Is a related party) as the party (CHADEMA) and the Newspaper (Tanzania Daima) are under the control and ownership of same person, Mr Mbowe. Mpigeni tu madogo ndugu mtoa mada lakini basic understanding ya mahusiano kati ya CHADEMA na Tanzania Daima iko very clear.

Sorry for using Kisw-english.

Sasa ndo naelewa kuwa CCM wana magazeti zaidi ya uhuru na mzalendo. Kwa kuwa RA ni kigogo huko CCM basi na magazeti yake ya mtanzania na Rai pia ni ya CCM. Ndugu unajua kufanya uchambuzi. Teh teh teh!!!
 
kuna kinacho kusumbua ila kwa 7bu unaona haya kukisema unaamua kujificha nyuma ya magazeti,sema wazi kwambA naichukia chadema japo ni chama makini utaeleweka tu kuliko watu kuanza kutilia shaka uwezo wako wa kufikiri
 
Majibu yangu kwa Kaka Kibanda

Huku nikitambua uwezo na weledi wa kaka yangu Absolom kibanda imenibidi niandike makala kuongelea baadhi ya hoja alizotoa katika makala yake ya wiki iliyopita kuhusu uamuzi wa uvccm wa kuunda kamati ya kufanya mabadiliko ndani ya jumuiya.

Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi ulifanya kikao cha Baraza kuu la vijana takribani wiki moja iliopita. Kama ilivyo kawaida Baraza hilo linapokutana linavuta hisia na mawazo ya wasomi wazee vijana na wanajamii wote wa Tanzania.

Maamuzi makubwa na mazito yalifanywa na Umoja wa Vijana, kubwa zaidi ni uamuzi makini na wa kisayansi wa kuyapitia mafanikio na matatizo ya umoja huo kama chombo cha chama kinachopaswa kuongoza vita dhidi ya kukipatia chama ushindi ,na kuyatafutia suluhisho na majibu ya kudumu.

Nauita uamuzi huu mzito kwa msingi mkubwa kuwa unalenga kuleta mabadiliko makubwa ambayo yatafanyika kisayansi na ni wazi kuwa taasisi hio italeta changamoto mpya katika tasnia ya siasa hapa nchini kwa kiwango ambacho umetoa mshituko mkubwa kwa wapinzani wa chama cha Mapinduzi kwa ujumla.

Moja ya eneo kubwa ambalo limeonyesha kuwagusa sana wapinzani wa UVCCM in uamuzi wa kujenga umoja ndani ya UVCCM na jumihia yenye nidhamu. Chama chenye viongozi wanaofuata misingi ya uwajibikaji na uongozi wa pamoja, uongozi wa viongozi wanaotoa madukuduku yao ndani ya chama na katika vikao rasmi na sio kulopoka hovyo kwenye vyombo vya habari na majukwaani.

Vyombo vingi vya habari, hasa vile vyenye nia ya kupotosha mambo mengi mazuri yanayofanywa na serkali yameonekana ama kupotosha au kuficha ukweli wa yale yalioamuliwa na UVCC kwa faida ya Chama na UVCCM kwa ujumla.

Moja ya maneno ambayo nilidhani ningeyaongelea kidogo ni makala maarufu ambayo mimi pia ni msomaji wake, makala ya Rafiki yangu Kibanda ya Tuendako. Makala hiyo ilijaribu kuonyesha kuwa tatizo linalotukabili kama Umoja wa Vijana na Chama ni tatizo la kiuongozi, na anatazama umoja wa vijana kama taasisi iliopotoka na hailengi kutatua matatizo ya kweli ya vijana.

Makala hiyo inashindwa kueleza na kupambanua muanguko wa kiuchumi duniani na athari zake kwa Tanzania, na unaponyooshea kidole serikali bila kuonyesha kuwa si Tanzania peke yake imekumbwa na matatizo makubwa ya kiuchumi kwa kiwango cha maisha kuwa magumu kwa wananchi wake ni kutotendea haki wasomaji wa makala husika.

Ni wajibu wa kila mwandishi mwenye weredi kukangalia pia juhudi za serikali ya chama cha mapinduzi kutatua matatizo muhimu ya watanzania. Moja ya sehemu za msingi kabisa za kuangalia ni pamoja na juhudi za kujenga majengo ya shule za kata na sasa serikali inaangalia kwa umakini walimu wa kwenda kufundisha shule hizo.

Chuo kikuu cha Dodoma ni alama ya mafanikio ya ujenzi wa elimu ya juu hapa nchini, tiba na afya imeshuhudiwa katika mapambano dhidi ya HIV na malaria, uwekaji wa vifaa vya maabara katika hospital za wilaya na mikoa pamoja na uanzishaji wa kitengo maalumu cha magonjwa ya moyo katika hospital kuu ya Muhimbili ni moja ya sehemu chache sana ambazo zimegusa moja kwa moja maendeleo ya watanzania.

Ni kweli kuwa serikali haijafanikiwa sana katika huduma za umeme na maji. Lakini bado maji yametiliwa mkazo mkubwa hasa kwa juhudi zilizofanyika katika programu ya maji mijini. Mikoa ya Shinyanga na tabora na baadhi ya maeneo imeanza kupata maji toka ziwa Victoria katika mradi mkubwa na ulioleta ubishani wa kimataifa.

Bado mafanikio ya nchi ni wajibu wa kila mwananchi kuyatekeleza na kutoa mchango wake mahali alipo. Si busara hata kidogo kwa waandishi mahili kufanya wananchi wajisahau na kudhania kuwa ugumu wa maisha yao unatokana na chama kilichoko madarakani na siyo juhudi za kila mtu kwa kufanya kazi zaidi na pia kufanya kazi za ziada, kwa mfano mwandishi mahili wa habari kwanini asianzishe kijalida chake binafsi kitoke mara moja kwa mwezi badala ya kungojea mshahara tu.

Watanzania wengi wamekua mabingwa wa kulalamika na kulaumu bila ya kujiuliza ni wangapi wanaofanya kazi wanatumia muda wa muajiri ama wa kazi katika facebook na jamiiforums,wangapi wanaingia kazini saa moja asubuhi na kutoka saa 11 jioni,ama wangapi wanaingia saa 2 na kutoka saa 8 kwa kutoa udhuru wakati huo wametumia masaa 3 katka mitandao ya kijamii ama wakilumbana ama wakitafuta marafiki na mwisho wa mwezi wakipokea ujira wao.

Ugumu wa maisha ambao tumekua tukiulilia ni kwa kiasi gani kama watanzania tunauchangia uchumi kushuka kwa kiasi gani kama watanzania tunauchangia kushuka uzalishaji wetu unaendena na mahitaji yetu Binafsi?

Ni wazi juhudi kubwa ya makala mbalimbali zimekuwa ni kuonyesha kuwa jibu la matatizo yote ya nchi yetu ni Chadema kuingia madarakani na siyo wananchi wenyewe kujituma na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kwa uzalendo.

Kupigia debe matatizo ya watu kuwa majibu na suluhisho lake ni Chama cha Chadema kuingia madarakani ni hoja nyepesi za maswali magumu. Kuna mambo kadhaa ambayo bado tunapaswa kujiuliza juu ya tamaduni za nchi yetu na mustakabali mzima wa tunakoelekea. Utamaduni wetu utazame hasa nini watanzania wanatarajia toka vyama chama cha siasa.

Je, ni kweli kuwa watanzania wako tayari kuhamasishwa na kuagizwa na wanasiasa uchwara kuvamia vyombo vya dola ili kudai madaraka waliokosa upinzani kwenye kura halali na za kidemokrasia au kikidhi hamu ya kupata madaraka hata kwa njia haramu kama ambavyo tulishuhudia kule Arusha.

Je, ni kweli watanzania wako tayari waandamane kila mkoa toka January mpaka desemba na kuongea siasa asubuhi mpaka jioni bila ya kufanya kazi, na bado wapate maendeleo kwa kusikiliza sauti za ukakamavu za upinzani waliovaa nguo nzito za khaki zenye kuashiria mapambano na vita dhidi ya upande usiohitaji vita wala ghasia za namna hio ?

Je ni kweli maandamano toka January mpaka Desemba bila ya kujulikana unaandamana kudai nini na ukiyapima ubora wa mafanikio yake kwa kuangalia vifo vya watanzania na damu inayomwagiga kuwa ndio ubora wa Chama mbadala cha Chama cha Mapinduzi?.

Je ni kweli kuwa matatizo yote ya Tanzania yanaletwa na CCM na kuwa ili Tanzania igeuke peponi kwenye raha basi Chadema ipewe madaraka ili Waziri wa mambo ya ndani awe Mheshimiwa Tindu Lissu, Waziri wa mambo ya Nje awe Mh Lucy Owenya ambaye ni binti wa kwanza wa Mh Ndesambulo .Mh. Mbowe ndio awe Waziri Mkuu wetu na Muheshimiwa Ndesamburo kama Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa na wengine wengi kama Mh. Mbilinyi (a.k.a Mr. Two) kama Waziri wa ujenzi na mawasiliano nap engine Mh. Godbless Lema awe wazir wetu wa Viwanda na Biashara

Wanaweza kujenga serikali bora lakini tabia na mienendo yao haina utulivu wa kutosha wa kiakili na kifikra wa kongoza nchi yetu tuipendayo yenye amani, umoja na upendo. Wanapaswa kujitazama upya na kutambua nchi haibomolewi kisha inajegwa bali ujenzi wa nchi ni mwendelezo wa kudumu na hata kama utakuwa wa kupokezana vijiti kwa vyama mbalimbali haitomaanisha kuwa kila chama kikiwa cha upinzani kitakuwa kinavunja misingi ya utaifa na kungojea kujenga upya kikiingia madarakani.


Ndio maana tamko la Umoja wa vijana lenye lengo la kujivua gamba, kujenga umoja na kutengeneza ajenda ya nidhamu katika jumuia na chama imekuwa pigo kubwa kwa wapinzani wa CCM, ambao walikuwa wanafaidika na malumbano na makundi ya ndani ya chama kama ajenda zao za kuwapa ushindi ndani ya chaguzi


Wanajua sasa jumuia mpya inazaliwa, jumuia ambayo Beno Malisa na Hussein Bashe watashirikiana kupambana na vijana wa Chadema wanaopenda kuona damu inamwagika nchini mwetu, kwa hakika ili ni anguko la upinzani na mawakala wao hasa wale ambao waliandika kwa kichwa kikubwa kuwa “Uvccm yawatangazia vita Sumaye na Sita” Huku wakijua ni uongo na si kweli hata kidogo UVCCM walitoa tamko hilo.Nia yao ni kuendelea kugombanisha watu ndani ya CCM na jumuhia zake.

Umoja wa vijana utakaozaliwa utapita nyumba kwa nyumba, na mtu kwa mtu kuwakumbusha kuwa sio utamaduni wetu kutukanana na kupigana na wala kutoka madaraka kwa kumwaga damu za ndugu zetu, pia utawakumbusha kuwa maendeleo ya vijana wa chi hii yatatokana na kufanya kazi kwa bidii na kwa maarifa.


Nchi haiwezi kuendelea kwa kutoyaeleza na kuyatafakari kwa mapana matatizo yanayoikabili Tanzania yetu. Na mtu yeyote anaedai kuwa Tanzania haijaendelea mpaka sasa kwa sababu ya uongozi wa CCM ni uvivu wa kufikiri na wepesi wa kutafuta majibu rahisi bila utafiti wala upembuzi.

Tunahitaji wananchi wenye uzalendo, na uzalendo huu hauwezi kujengwa kwa visingizio na majibu mepesi ya kudai nchi ina ombwe la uongozi. Ombwe la uongozi ambao leo Chadema na mawakala wao wanaongelea ni tabia ya Rais ambayo amekuwa akiionyesha katika uongozi wake.

Aiba hii ya uongozi ambayo Chadema na mawakala wao wanaita ni ombwe la uongozi ni pamoja na Rais kuwapatia wapinzani nafasi ya kuandamana, kuhutubia, na mwishowe wanaitumia vibaya kwa kudanganya watanzania kuwa watawapatia Cement kwa shilingi elfu tano, uhuru wa vyombo vya habari kuandika ambayo navyo vimetumia vibaya bila kujali athali zake kwa kauli za uchochezi dhidi ya amani yetu.

Ni wazi uchochezi na mitazamo kama hii ina nia mbili kubwa nazo ni kumfanya Raisi akatae tama kujenga nchi kwa kuamini kuwa pamoja na kazi nzuri anayoifanya kujituma kwa hali na mali kusaidia nchi yake, bado waandishi wachache na wachovu wa kufikiri wanamkejeli na kumsimanga. Kwao hakuna jema analofanya Rais wanaliona labda atangaze kuivunja CCM ndio kwao litakuwa ni bora.

Nia ya pili ni kumlazimisha aendeshe nchi kwa mkono wa chuma, kukandamiza demokrasia na kuondoa uhuru wa kujadiliana na kifikiri, uhuru ambao umethibitishwa wazi wazi kuwa unatumika vibaya. Uhuru ambao Mh.Rais amautoa kwa nia njema na sasa unatumika vibaya kwa nia ya kuvunja amani na umoja wetu.

Waandishi wanandike na kujadili Richmond na dowansi kwa miaka nenda miaka rudi kana kwamba wanagubu la kimaisha na kiuchumi, na hivyo basi utafiti wao umeonyesha kuwa limesababishwa na Richmond.Ni kweli hatuwezi kuendelea mpaka kadhia hii ifutwe kwenye usawa wa dunia Ndio maana sikupata mshuko pale mkulima mmoja alipolalamika wilaya ya mbinga kuwa mvua haijanyesha kwa sababu ya Richmond.

Tunayo mengi ya kujadili ili kuijenga nchi yetu. Tunatakiwa kubadilika na kuangalia tunafanya nini kesho ili nchi isonge mbele, je, tukae vijiweni kuanzia asubuhi mpaka usiku ni suluhisho la maendeleo yetu, vyombo vya habari vimekemea tabia hii ya uvivu uliojaa miongoni mwetu au tunapewa tu majibu mepesi kwa kutojituma na kufanya kazi kwa bidii ni tatizo la CCM.Tusiwadanganye kirahisi watanzania hasa kwa kuwaaminisha kuwa matatizo ya kiuchumi ya dunia ambayo yameithiri Tanzania na nchi zote za Africa yameletwa na CCM.

Vijana wanamaliza chuo kikuu shahada za ualimu, hawataki tena kurudi mashuleni na hasa shule za vijijini na kwenda kusaidia watoto wa wakulima wa nchi hii eti kwa madai hakuna vitendea kazi. Wakati wao wenyewe walitoka huko huko vijijini na kuna walimu walijitolea na hizo zana duni na wakawafundisha mpaka wakafikia hapo na sasa wamehitimu masomo yao.

Serikali inagharamia kwa fedha nyingi kusomesha madaktari ambao hatima yake wote wanataka kukaa dar es Salaam, sababu ni hizo hizo kuwa mawilayani hakuna hospitali zenye vifaaa vya kutosha. Huku tukisahau sisi wote tumezaliwa hukohuko vijijini, tumekulia na kutibiwa mpaka tumekuwa watu wazima, visingizio hivi ni sababu ya kukosa kuwajibika na wajibu wa kizalendo kwa taifa letu.

Tunafanya nini sisi kama watanzania kujenga mapenzi kwa nchi yetu. Kuwatuma vijana wakafanye kazi popote kusaidia ndugu zao wanaongojea huduma zao.Sehemu kadhaa za Tanzania ambazo leo tunaambiwa kuwa vijana wetu waliomaliza elimu za juu hawataki kwenda tunagundua kuwa wapo wageni mbalimbali wanaotoka nchi za ng’ambo wanakwenda kufanya kazi kwa njia ya kujitolea tena wanatoka nchi zenye maisha ya hali ya juu kama marekani na ulaya.

Tunawajibu wa kuhimizana kufanya kazi kwa bidii, weredi na maarifa, kujenga uzalendo wa kweli na kuipenda nchi yetu. Hakuna chama ambacho kitaleta migogolo ya kijamii na kuitawala Tanzania alafu kuamini amani hii wanaoichezea watairudisha tena. Anayejenga nchi na kuibomoa nchi ni mwananchi mwenyewe.Ni wajibu wa vijana na hasa vijana wa CCM kuongoza ulinzi wa nchi yetu.

Umefika wakati Waandishi kama kaka yangu KIBANDA kabla ya kutuhumu serekali atueleze huko TUENDAKO tunahitaji watanzania wanaoweza kufanya kazi masaa 18 na kupumzika masaa 6,tunahitaji taifa ambalo vijana wake hawaanzi weekend jumatano,kwani sasa tunavijana ambao Jtano wanaanza wkend kwa kwenda kwa Lady Jaydee,alhamis Ngwasuma,Ijumaa Bilcanas Ladies free,Jmosi Cocobeach,Jpili Nyama Choma katika baa za jirani na makazi yetu,kwa aina hii ya vijana tutalia maisha magumu na tutapenda kusikia majibu rahisi yanayotolewa na wanasiasa wasiotoa majibu yenye mashiko.

Nilitarajia kaka yangu kibanda angewekeza nguvu kubwa kuwaambia vijana walio katika sekta iliyo rasmi hasa walio ajiriwa maofisini wasitumie muda wa muajiri ktk Facebook kutafuta ma girlfreand na Maboy freand,katika jamii forums bali muda wakazi watumie kufanya kazi ili kuleta tija ktk taifa letu.

Nilitarajia waandishi kama kaka yangu kibanda wakatumia muda mwingi kuwaambia watanzania wenye macho lakini ambao wameamua kutokuona ,wenye masikio lakini wameamua kutosikia wenye nguvu lakini wameamua kutotumia nguvu zao kufanya kazi kuwa maendeleo tulionayo yameletwa kwa jitihada za serekali pamoja na nguvu za wananchi,nina amini leo kijiji cha kina kibanda ambacho wakati yeye anasoma idadi ya shule zilizopo si zile alizoaacha mara ya mwisho wakati anasoma,Barabara alotumia kuja DAR si ile alotumia miaka 30 iliyopita.

Kibanda alitakiwa kutumia kalamu yake kuwafundisha umuhimu wa watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuzalisha na si kulalamika na kusikiliza ngoijera na hadithi za kusadikika za wanasiasa ambao wanavaa magwanda ya mgambo na chama ambacho kina ukumbi unaongoza kuharibu amaadili ya vijana wetu,nilitarajia kibanda amwambie MBOWE asifungue bilicanas jtano bali starehe zianze jmamosi angalaua vijana wafanye kazi siku tano kwa wiki,nilitarajia kibanda amwambie mbowe jinsi anavoharibu maadili ya vijana wan chi hii kupitia ukumbi wake unaanza starehe kuanzi jtano mpaka jpili,watanzania hasa vijana wanafanya kazi jatatu,jnne baada ya hapo ni starehe tunatarajia maendeleo.

Hitoimisho kaka kbanda taifa hili linahitaji uwajibikaji tumia kalamu yako kuwakumbusha watanzania wajibu wao wa kufanya kazi ili wawe na MORAL authority kuinyoshea serekali kidole
 
maneno meeeeeeeeeeengiiiiiiiiiii lakini pumba tupu. Umejibi kisichijibika kwani kila chama kina taratibu zake katika kutatua matatizo yake ya ndani.

Huwezi kuwa mwalimu wa darasa usilolifundisha.

nakupa pole
 
Kwa kuwa Kibanda ni mhariri wa gazeti la propaganda la Chadema, basi haya yatakuwa majibu ya UVCCM kwa Chadema.

Makala ndefu hivi ungeweka kama attachment wanaotaka wa-download.
 
Kwa kuwa Kibanda ni mhariri wa gazeti la propaganda la Chadema, basi haya yatakuwa majibu ya UVCCM kwa Chadema.

Makala ndefu hivi ungeweka kama attachment wanaotaka wa-download.

Laiti mngejua kwamba pamoja na uhariri wake kwenye gazeti hilo la chadema yeye ni msemaji wa kakikundi fulani cha wana CCM wanaowania hatamu za nchi hii msingejadili uchadema wake. ndiye mhariri mtendaji wa jarida la UMOJA ambalo hivi karibuni litakuwa gazeti la kila siku la kuwasafisha jamaa fulani.
 
Kamwambie aliyekutuma kwamab sasa vijan na watanzania kwa ujumla hatudanganyiki
huna hata aibu mbu wewe


majibu yangu kwa kaka kibanda

huku nikitambua uwezo na weledi wa kaka yangu absolom kibanda imenibidi niandike makala kuongelea baadhi ya hoja alizotoa katika makala yake ya wiki iliyopita kuhusu uamuzi wa uvccm wa kuunda kamati ya kufanya mabadiliko ndani ya jumuiya.

Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ulifanya kikao cha baraza kuu la vijana takribani wiki moja iliopita. Kama ilivyo kawaida baraza hilo linapokutana linavuta hisia na mawazo ya wasomi wazee vijana na wanajamii wote wa tanzania.

Maamuzi makubwa na mazito yalifanywa na umoja wa vijana, kubwa zaidi ni uamuzi makini na wa kisayansi wa kuyapitia mafanikio na matatizo ya umoja huo kama chombo cha chama kinachopaswa kuongoza vita dhidi ya kukipatia chama ushindi ,na kuyatafutia suluhisho na majibu ya kudumu.

Nauita uamuzi huu mzito kwa msingi mkubwa kuwa unalenga kuleta mabadiliko makubwa ambayo yatafanyika kisayansi na ni wazi kuwa taasisi hio italeta changamoto mpya katika tasnia ya siasa hapa nchini kwa kiwango ambacho umetoa mshituko mkubwa kwa wapinzani wa chama cha mapinduzi kwa ujumla.

Moja ya eneo kubwa ambalo limeonyesha kuwagusa sana wapinzani wa uvccm in uamuzi wa kujenga umoja ndani ya uvccm na jumihia yenye nidhamu. Chama chenye viongozi wanaofuata misingi ya uwajibikaji na uongozi wa pamoja, uongozi wa viongozi wanaotoa madukuduku yao ndani ya chama na katika vikao rasmi na sio kulopoka hovyo kwenye vyombo vya habari na majukwaani.

Vyombo vingi vya habari, hasa vile vyenye nia ya kupotosha mambo mengi mazuri yanayofanywa na serkali yameonekana ama kupotosha au kuficha ukweli wa yale yalioamuliwa na uvcc kwa faida ya chama na uvccm kwa ujumla.

Moja ya maneno ambayo nilidhani ningeyaongelea kidogo ni makala maarufu ambayo mimi pia ni msomaji wake, makala ya rafiki yangu kibanda ya tuendako. Makala hiyo ilijaribu kuonyesha kuwa tatizo linalotukabili kama umoja wa vijana na chama ni tatizo la kiuongozi, na anatazama umoja wa vijana kama taasisi iliopotoka na hailengi kutatua matatizo ya kweli ya vijana.

Makala hiyo inashindwa kueleza na kupambanua muanguko wa kiuchumi duniani na athari zake kwa tanzania, na unaponyooshea kidole serikali bila kuonyesha kuwa si tanzania peke yake imekumbwa na matatizo makubwa ya kiuchumi kwa kiwango cha maisha kuwa magumu kwa wananchi wake ni kutotendea haki wasomaji wa makala husika.

Ni wajibu wa kila mwandishi mwenye weredi kukangalia pia juhudi za serikali ya chama cha mapinduzi kutatua matatizo muhimu ya watanzania. Moja ya sehemu za msingi kabisa za kuangalia ni pamoja na juhudi za kujenga majengo ya shule za kata na sasa serikali inaangalia kwa umakini walimu wa kwenda kufundisha shule hizo.

Chuo kikuu cha dodoma ni alama ya mafanikio ya ujenzi wa elimu ya juu hapa nchini, tiba na afya imeshuhudiwa katika mapambano dhidi ya hiv na malaria, uwekaji wa vifaa vya maabara katika hospital za wilaya na mikoa pamoja na uanzishaji wa kitengo maalumu cha magonjwa ya moyo katika hospital kuu ya muhimbili ni moja ya sehemu chache sana ambazo zimegusa moja kwa moja maendeleo ya watanzania.

Ni kweli kuwa serikali haijafanikiwa sana katika huduma za umeme na maji. Lakini bado maji yametiliwa mkazo mkubwa hasa kwa juhudi zilizofanyika katika programu ya maji mijini. Mikoa ya shinyanga na tabora na baadhi ya maeneo imeanza kupata maji toka ziwa victoria katika mradi mkubwa na ulioleta ubishani wa kimataifa.

Bado mafanikio ya nchi ni wajibu wa kila mwananchi kuyatekeleza na kutoa mchango wake mahali alipo. Si busara hata kidogo kwa waandishi mahili kufanya wananchi wajisahau na kudhania kuwa ugumu wa maisha yao unatokana na chama kilichoko madarakani na siyo juhudi za kila mtu kwa kufanya kazi zaidi na pia kufanya kazi za ziada, kwa mfano mwandishi mahili wa habari kwanini asianzishe kijalida chake binafsi kitoke mara moja kwa mwezi badala ya kungojea mshahara tu.

Watanzania wengi wamekua mabingwa wa kulalamika na kulaumu bila ya kujiuliza ni wangapi wanaofanya kazi wanatumia muda wa muajiri ama wa kazi katika facebook na jamiiforums,wangapi wanaingia kazini saa moja asubuhi na kutoka saa 11 jioni,ama wangapi wanaingia saa 2 na kutoka saa 8 kwa kutoa udhuru wakati huo wametumia masaa 3 katka mitandao ya kijamii ama wakilumbana ama wakitafuta marafiki na mwisho wa mwezi wakipokea ujira wao.

Ugumu wa maisha ambao tumekua tukiulilia ni kwa kiasi gani kama watanzania tunauchangia uchumi kushuka kwa kiasi gani kama watanzania tunauchangia kushuka uzalishaji wetu unaendena na mahitaji yetu binafsi?

Ni wazi juhudi kubwa ya makala mbalimbali zimekuwa ni kuonyesha kuwa jibu la matatizo yote ya nchi yetu ni chadema kuingia madarakani na siyo wananchi wenyewe kujituma na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kwa uzalendo.

Kupigia debe matatizo ya watu kuwa majibu na suluhisho lake ni chama cha chadema kuingia madarakani ni hoja nyepesi za maswali magumu. Kuna mambo kadhaa ambayo bado tunapaswa kujiuliza juu ya tamaduni za nchi yetu na mustakabali mzima wa tunakoelekea. Utamaduni wetu utazame hasa nini watanzania wanatarajia toka vyama chama cha siasa.

Je, ni kweli kuwa watanzania wako tayari kuhamasishwa na kuagizwa na wanasiasa uchwara kuvamia vyombo vya dola ili kudai madaraka waliokosa upinzani kwenye kura halali na za kidemokrasia au kikidhi hamu ya kupata madaraka hata kwa njia haramu kama ambavyo tulishuhudia kule arusha.

Je, ni kweli watanzania wako tayari waandamane kila mkoa toka january mpaka desemba na kuongea siasa asubuhi mpaka jioni bila ya kufanya kazi, na bado wapate maendeleo kwa kusikiliza sauti za ukakamavu za upinzani waliovaa nguo nzito za khaki zenye kuashiria mapambano na vita dhidi ya upande usiohitaji vita wala ghasia za namna hio ?

Je ni kweli maandamano toka january mpaka desemba bila ya kujulikana unaandamana kudai nini na ukiyapima ubora wa mafanikio yake kwa kuangalia vifo vya watanzania na damu inayomwagiga kuwa ndio ubora wa chama mbadala cha chama cha mapinduzi?.

Je ni kweli kuwa matatizo yote ya tanzania yanaletwa na ccm na kuwa ili tanzania igeuke peponi kwenye raha basi chadema ipewe madaraka ili waziri wa mambo ya ndani awe mheshimiwa tindu lissu, waziri wa mambo ya nje awe mh lucy owenya ambaye ni binti wa kwanza wa mh ndesambulo .mh. Mbowe ndio awe waziri mkuu wetu na muheshimiwa ndesamburo kama waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa na wengine wengi kama mh. Mbilinyi (a.k.a mr. Two) kama waziri wa ujenzi na mawasiliano nap engine mh. Godbless lema awe wazir wetu wa viwanda na biashara

wanaweza kujenga serikali bora lakini tabia na mienendo yao haina utulivu wa kutosha wa kiakili na kifikra wa kongoza nchi yetu tuipendayo yenye amani, umoja na upendo. Wanapaswa kujitazama upya na kutambua nchi haibomolewi kisha inajegwa bali ujenzi wa nchi ni mwendelezo wa kudumu na hata kama utakuwa wa kupokezana vijiti kwa vyama mbalimbali haitomaanisha kuwa kila chama kikiwa cha upinzani kitakuwa kinavunja misingi ya utaifa na kungojea kujenga upya kikiingia madarakani.


Ndio maana tamko la umoja wa vijana lenye lengo la kujivua gamba, kujenga umoja na kutengeneza ajenda ya nidhamu katika jumuia na chama imekuwa pigo kubwa kwa wapinzani wa ccm, ambao walikuwa wanafaidika na malumbano na makundi ya ndani ya chama kama ajenda zao za kuwapa ushindi ndani ya chaguzi


wanajua sasa jumuia mpya inazaliwa, jumuia ambayo beno malisa na hussein bashe watashirikiana kupambana na vijana wa chadema wanaopenda kuona damu inamwagika nchini mwetu, kwa hakika ili ni anguko la upinzani na mawakala wao hasa wale ambao waliandika kwa kichwa kikubwa kuwa "uvccm yawatangazia vita sumaye na sita" huku wakijua ni uongo na si kweli hata kidogo uvccm walitoa tamko hilo.nia yao ni kuendelea kugombanisha watu ndani ya ccm na jumuhia zake.

Umoja wa vijana utakaozaliwa utapita nyumba kwa nyumba, na mtu kwa mtu kuwakumbusha kuwa sio utamaduni wetu kutukanana na kupigana na wala kutoka madaraka kwa kumwaga damu za ndugu zetu, pia utawakumbusha kuwa maendeleo ya vijana wa chi hii yatatokana na kufanya kazi kwa bidii na kwa maarifa.


Nchi haiwezi kuendelea kwa kutoyaeleza na kuyatafakari kwa mapana matatizo yanayoikabili tanzania yetu. Na mtu yeyote anaedai kuwa tanzania haijaendelea mpaka sasa kwa sababu ya uongozi wa ccm ni uvivu wa kufikiri na wepesi wa kutafuta majibu rahisi bila utafiti wala upembuzi.

Tunahitaji wananchi wenye uzalendo, na uzalendo huu hauwezi kujengwa kwa visingizio na majibu mepesi ya kudai nchi ina ombwe la uongozi. Ombwe la uongozi ambao leo chadema na mawakala wao wanaongelea ni tabia ya rais ambayo amekuwa akiionyesha katika uongozi wake.

Aiba hii ya uongozi ambayo chadema na mawakala wao wanaita ni ombwe la uongozi ni pamoja na rais kuwapatia wapinzani nafasi ya kuandamana, kuhutubia, na mwishowe wanaitumia vibaya kwa kudanganya watanzania kuwa watawapatia cement kwa shilingi elfu tano, uhuru wa vyombo vya habari kuandika ambayo navyo vimetumia vibaya bila kujali athali zake kwa kauli za uchochezi dhidi ya amani yetu.

Ni wazi uchochezi na mitazamo kama hii ina nia mbili kubwa nazo ni kumfanya raisi akatae tama kujenga nchi kwa kuamini kuwa pamoja na kazi nzuri anayoifanya kujituma kwa hali na mali kusaidia nchi yake, bado waandishi wachache na wachovu wa kufikiri wanamkejeli na kumsimanga. Kwao hakuna jema analofanya rais wanaliona labda atangaze kuivunja ccm ndio kwao litakuwa ni bora.

Nia ya pili ni kumlazimisha aendeshe nchi kwa mkono wa chuma, kukandamiza demokrasia na kuondoa uhuru wa kujadiliana na kifikiri, uhuru ambao umethibitishwa wazi wazi kuwa unatumika vibaya. Uhuru ambao mh.rais amautoa kwa nia njema na sasa unatumika vibaya kwa nia ya kuvunja amani na umoja wetu.

Waandishi wanandike na kujadili richmond na dowansi kwa miaka nenda miaka rudi kana kwamba wanagubu la kimaisha na kiuchumi, na hivyo basi utafiti wao umeonyesha kuwa limesababishwa na richmond.ni kweli hatuwezi kuendelea mpaka kadhia hii ifutwe kwenye usawa wa dunia ndio maana sikupata mshuko pale mkulima mmoja alipolalamika wilaya ya mbinga kuwa mvua haijanyesha kwa sababu ya richmond.

Tunayo mengi ya kujadili ili kuijenga nchi yetu. Tunatakiwa kubadilika na kuangalia tunafanya nini kesho ili nchi isonge mbele, je, tukae vijiweni kuanzia asubuhi mpaka usiku ni suluhisho la maendeleo yetu, vyombo vya habari vimekemea tabia hii ya uvivu uliojaa miongoni mwetu au tunapewa tu majibu mepesi kwa kutojituma na kufanya kazi kwa bidii ni tatizo la ccm.tusiwadanganye kirahisi watanzania hasa kwa kuwaaminisha kuwa matatizo ya kiuchumi ya dunia ambayo yameithiri tanzania na nchi zote za africa yameletwa na ccm.

Vijana wanamaliza chuo kikuu shahada za ualimu, hawataki tena kurudi mashuleni na hasa shule za vijijini na kwenda kusaidia watoto wa wakulima wa nchi hii eti kwa madai hakuna vitendea kazi. Wakati wao wenyewe walitoka huko huko vijijini na kuna walimu walijitolea na hizo zana duni na wakawafundisha mpaka wakafikia hapo na sasa wamehitimu masomo yao.

Serikali inagharamia kwa fedha nyingi kusomesha madaktari ambao hatima yake wote wanataka kukaa dar es salaam, sababu ni hizo hizo kuwa mawilayani hakuna hospitali zenye vifaaa vya kutosha. Huku tukisahau sisi wote tumezaliwa hukohuko vijijini, tumekulia na kutibiwa mpaka tumekuwa watu wazima, visingizio hivi ni sababu ya kukosa kuwajibika na wajibu wa kizalendo kwa taifa letu.

Tunafanya nini sisi kama watanzania kujenga mapenzi kwa nchi yetu. Kuwatuma vijana wakafanye kazi popote kusaidia ndugu zao wanaongojea huduma zao.sehemu kadhaa za tanzania ambazo leo tunaambiwa kuwa vijana wetu waliomaliza elimu za juu hawataki kwenda tunagundua kuwa wapo wageni mbalimbali wanaotoka nchi za ng'ambo wanakwenda kufanya kazi kwa njia ya kujitolea tena wanatoka nchi zenye maisha ya hali ya juu kama marekani na ulaya.

Tunawajibu wa kuhimizana kufanya kazi kwa bidii, weredi na maarifa, kujenga uzalendo wa kweli na kuipenda nchi yetu. Hakuna chama ambacho kitaleta migogolo ya kijamii na kuitawala tanzania alafu kuamini amani hii wanaoichezea watairudisha tena. Anayejenga nchi na kuibomoa nchi ni mwananchi mwenyewe.ni wajibu wa vijana na hasa vijana wa ccm kuongoza ulinzi wa nchi yetu.

Umefika wakati waandishi kama kaka yangu kibanda kabla ya kutuhumu serekali atueleze huko tuendako tunahitaji watanzania wanaoweza kufanya kazi masaa 18 na kupumzika masaa 6,tunahitaji taifa ambalo vijana wake hawaanzi weekend jumatano,kwani sasa tunavijana ambao jtano wanaanza wkend kwa kwenda kwa lady jaydee,alhamis ngwasuma,ijumaa bilcanas ladies free,jmosi cocobeach,jpili nyama choma katika baa za jirani na makazi yetu,kwa aina hii ya vijana tutalia maisha magumu na tutapenda kusikia majibu rahisi yanayotolewa na wanasiasa wasiotoa majibu yenye mashiko.

Nilitarajia kaka yangu kibanda angewekeza nguvu kubwa kuwaambia vijana walio katika sekta iliyo rasmi hasa walio ajiriwa maofisini wasitumie muda wa muajiri ktk facebook kutafuta ma girlfreand na maboy freand,katika jamii forums bali muda wakazi watumie kufanya kazi ili kuleta tija ktk taifa letu.

Nilitarajia waandishi kama kaka yangu kibanda wakatumia muda mwingi kuwaambia watanzania wenye macho lakini ambao wameamua kutokuona ,wenye masikio lakini wameamua kutosikia wenye nguvu lakini wameamua kutotumia nguvu zao kufanya kazi kuwa maendeleo tulionayo yameletwa kwa jitihada za serekali pamoja na nguvu za wananchi,nina amini leo kijiji cha kina kibanda ambacho wakati yeye anasoma idadi ya shule zilizopo si zile alizoaacha mara ya mwisho wakati anasoma,barabara alotumia kuja dar si ile alotumia miaka 30 iliyopita.

Kibanda alitakiwa kutumia kalamu yake kuwafundisha umuhimu wa watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuzalisha na si kulalamika na kusikiliza ngoijera na hadithi za kusadikika za wanasiasa ambao wanavaa magwanda ya mgambo na chama ambacho kina ukumbi unaongoza kuharibu amaadili ya vijana wetu,nilitarajia kibanda amwambie mbowe asifungue bilicanas jtano bali starehe zianze jmamosi angalaua vijana wafanye kazi siku tano kwa wiki,nilitarajia kibanda amwambie mbowe jinsi anavoharibu maadili ya vijana wan chi hii kupitia ukumbi wake unaanza starehe kuanzi jtano mpaka jpili,watanzania hasa vijana wanafanya kazi jatatu,jnne baada ya hapo ni starehe tunatarajia maendeleo.

Hitoimisho kaka kbanda taifa hili linahitaji uwajibikaji tumia kalamu yako kuwakumbusha watanzania wajibu wao wa kufanya kazi ili wawe na moral authority kuinyoshea serekali kidole
 
Una chuki binafsi na Kibanda!Kibanda aliongea kama mTZ na akatoa ushauri kwa Uvccm,lakini ww lawama zako zote kwa m2 mmoja,ushauri wako mtumie kwenye email yake,Jf lete mambo ya mustakabali wa nch,sio ya m2 mmoja!
 
M-bongo,

Asante kwa makala ila ni ndefu sana sana......

Jitahidi ziwe fupi na zinaeleweka. Anyway, ndiyo kipaji ambacho wengine wanacho na wengine hatuna.

UVCCM kuna tatizo na inabidi mkae mlijadili. Mambo ya Kamoga kukurupuka na kusema Waziri Sitta siyo Mlezi na siku inayofuata wanakuja vijana wengine na kusema "Kamoga kachemsha?" Mhhhh...............
 
Aisee nimejaribu kupitia makala yako ndefu lakini naona sipati pointi yoyote, nakupatia tu feedback kwamba hauelewiki na jaribu kuwa brief but to the point, hizi blah blah sidhani kama zitasomwa na wengi. Ingekuwa makala ya Mwanakijiji, Absaloum, na wengine wa aina hiyo ingesomwa lakini kwa yako hii na wasiwasi!
 
Kwani hiyo makala ya kibanda haiwezi kupatikana ibandikwe humu!!
 
Code:
Aiba hii ya uongozi ambayo Chadema na mawakala wao wanaita ni ombwe la uongozi ni pamoja na Rais kuwapatia wapinzani nafasi ya kuandamana, kuhutubia, na mwishowe wanaitumia vibaya kwa kudanganya watanzania kuwa watawapatia Cement kwa shilingi elfu tano, uhuru wa vyombo vya habari kuandika ambayo navyo vimetumia vibaya bila kujali athali zake kwa kauli za uchochezi dhidi ya amani yetu.
Unachekesha yaani unataka kutuambia Jakaya Kikwete yuko juu ya sheria yaani anawapa ruhusa ya maandamano,wewe unashangaza,Katiba hii hii mbovu uhuru wa wananchi kukusanyika na kuchanganyika na hata kuandamana
 
Silly, kwa kuwa nyumba ya jirani inawaka moto na yako lazima iwake moto. Eti uchumi wa dunia, wana resources tulizo nazo? Ok uchumi wa dunia ni mbovu, je ni kwa sababu ya corruption tena grand corruption kama tunayoiona hapa tena ikifanywa na watu 10 tu!!
Je huko kuna vijana wajinga kama nyie wa uvccm wanaotaka kuingia Ikulu ili na wale,maana yake ni uvccm wanaotaka kuendeleza ufisadi, ili nao wale.
Tunawaomba mkamjibu kijana mwenzenu Nyamsenda, ebu endelezeni mjadala aliouanzisha na nyinyi, msirukie wazee.
Je ukwasi mlionao mmeutoa wapi, mnanunuliwa tu.Vijana wa nchi hii waliofanywa maskini hawawezi kusiliza WALANg MULIWA.Mmelanguliwa kama kama kama vile hamna macho.Mnapigwa bei ,maana thamani yenu ni matumbo. Mbonahamuwatetei vijana wenzenu.AU MMESHIBA DEEP GREEN loot.
 
mmbongo kweli ulichoandika hakieleweki. vp umekurupushwa tu na watu uwatetee nawe ukatoka bila kujiandaaa? nafikiri tuangalie zaidi mambo ya kitaifa bla bla kama hizi tusizipe nafasi.
 
Utetezi wa serikali na ccm usio na mashiko. Msukosuko wa uchumi duniani siyo kigezo kwa watu kuwa corupt tz, na si hoja ya uvccm kutetea mafisadi. Jifunze kuandika makala kama yako kwa aya 2 au 3 huku ukitoa ujumbe kamili uliokusudia.
 
mimi nina swali moja tu kwa viongozi wote akiwemo kikwete na hao vilaza wengine wanaotaka tuamini matatizo haya yanatokana na uchumi wa dunia kutikiswa, ok tusema mimi nimewaamini na tufanye sisi uchumi wetu unaendana na hao wengine
kwa kila kinachotokea huko na huku kwetu kinatokea, sasa swali langu
je sasa uchumi wa dunia umerudi sana mbona hali sisi inazidi kuwa ngumu harafu mbona sisi hali ngumu ilianza kabla ya mtikisiko au sisi tulianza kutikiswa zamani na bado tunatikiswa kiuchumu mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom