MCHUMIA JUAN
Member
- Jun 15, 2015
- 94
- 22
Ahsante sana Ngwananzengo.
Hao wote unaowaona wanajidai kuponda ni fans zangu wa kisirisiri, wanachukia sana kunichukia na hawana raha wasiponiona na nimewaona toka Ramadhan imeanza wananichokoza makusudi kabisa, ili wanione nikichangia japo kiduchu.
Kusema kweli swaum siyo inayonizuwia kuingia JF huwa nnaingia kila nnapopata wasaa, kinachonizuwia ni kuwa nimejiwa na ugeni wa wanangu na wake zao wameamuwa summer holiday hii waje kuniona na kufunga swaum zao Tanzania, wengine hawajawahi kabisa kufunga hapa. Kwa hiyo wana ni keep busy sana, ingawa nashkuru ndugu jamaa na marafiki wanawaalika sana kwa hiyo hupata ahueni ya kuwaandalia wageni lakini huwa katika pirika za kufatana kila wanapoalikwa kwani wengine wanaogopa hawana uzoefu sana na culture yetu, wanahisi labda watakosea kitu kwa watu, na mimi nna act kama tour guide wao. na ukichukulia kuwa hawa hawataki kabisa kukaa mjini ambapo ndiyo karibu na ndugu na jamaa wengi wanaowaalika, wao wanataka baada ya kufuturu na kusali isha turudi Mkuranga, kwa hiyo nnakuwa extra occupied.
Nnashukuru kwa kunikumbuka na nnadhani wote tungekuwa productive sana tungekuwa kama wewe, hata pale tusipokubaliana tuwe tunapajadili bila chuki. Ahsante kwa hilo.
Nipo na huwa nnaingia na mtaniona tu ngoja hawa wageni wazowee na waanze ku take over mashughuli yao ya nyumbani mtaniona tu.
Nnawatakia wote mfungo mwema na wale makobe kama Daudi Mchambuzi nnawatakia Ramadhan njema. Hili li Daudi Mchambuzi halifungi Ramadhan wala Kwaresima, sijuwi ni jitu la aina gani hili, limakalia ushambenga tu. Tuliombee kwa Allah linaweza likarudi kwenye njia iliyonyooka.
Leo nipo.
Ramadhan Kareem.
kuna vjana wangu nliwaambia kwamba kuna dada anaitwa faizafoxy nataman nkutane na huyu mtu n mwelevu,anajenga hoja,anadefend hoja,anajbu hoja kwa mifano sahih na kila anachoulzwa utadhan tayar alishajua ataulzwa hcho ana majbu at her finger tips hongera sn i wish to see u one day.