Nakubaliana na mawazo ya Thadei Ole Mushi. Polepole anakosea sana

blogger

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
10,449
12,602
HUMPHREY POLEPOLE SI KUBEZA

Na Thadei Ole Mushi.

Huenda Polepole yupo sahihi lakini Madhara ya anachokisema ni makubwa mno.

1. Yeye kama Kiongozi ana Platform kubwa zaidi kuliko Mimi na wewe ya kushauri Kwa kumfuata Mkuu wa Mkoa DSM wakajadiliana kuhusu wamachinga.

2. Kauli hizi zinaweza kusababisha Maandamano ya Vijana Kwa kuwa yametolewa na Kiongozi.

3. Sio mara ya kwanza Polepole anawaona wenzake kuwa kichwani hakuna kitu. Aliwahi kuanzisha kipindi Cha Papo Kwa Papo akawa anagombeza viongozi wenzake kwenye simu kuanzia Diwani Hadi Waziri. Polepole huwa anaamini yeye pekee ndiye mwenye akili ndio maana anawafundisha uongozi.

4. Kauli ya Kwamba anamtetea Rais sio kweli huwezi kumtetea halafu wakati huo huo uchochee wamachinga kiasi Hicho. Polepole kama Mbunge ana channel ya kumfikia Rais Kirahisi kuliko Mimi na wewe kusema hadharani kuwa Wamachinga wanaonewa halafu unajidai kumpenda anayeongoza Serikali ni unafiki.

5. Niliwahi kutoa Option kuwa Polepole ili atulie anahitaji mambo mawili aidha apewe Uwaziri, Unaibu Waziri au apelekwe kuwa Balozi nje ya nchi. Kwa huu Ubunge wake atawasumbua sana wenzake Serikalini na ndio anaoutumia kukagua wenzake 😂😂😂😂

6. Unaweza Kumdharau ila kauli zake Kwa watu wenye matatizo yao binafsi yanaweza kuwa na impact kubwa sana anachofanya hapa sio kutatua tatizo Bali ni kutengeneza tatizo. Yeye kama sehemu ya Uongozi anatakiwa atoe solutions sio kuchochea Tabaka la chini.

7. CCM na Serikali inagimbanishwa na Wamachinga, inagimbanishwa na vijana, inagimbanishwa na waliojiajiri Kwa kukosa ajira. Si kauli ya kusikiliza na kuiacha.

Narudia huenda Humphrey Polepole ana mawazo mazuri Sana ila njia anayotumia kufikisha mawazo yake sijaipenda.

Ole Mushi
0712702602.

MY TAKE..

CCM bado haiko pamoja na Mama. Hii movement ya Polepole haina afya kwa taifa hAta kidogo.
 
Pole Pole anaomboleza kwa mtindo tofauti na ule wa waombolezaji wengine. Anamkumbuka Hayati JPM na anashindwa tena kumpatia uhai mwingine ili maisha aliyoyazoea yaendelee kuwepo.

Inafika wakati inambidi mtu akubaliane na maisha halisi kwamba aliyempenda hayupo tena duniani, inabidi mwenye kumpenda hayati alazimike kuwa mtu mpya kichwani mwake na katika matendo yake ya kila siku.
 
Acheni uchonganishi nini kibaya kasema.Tatizo la upinzani wa nchi hii umebaki kusubiri majanga tu
 
Polepole anatumika uonekane Tz kuna uhuru wa maoni na uhuru wa kukosoa.

Ionekane hata wakiifuta Chadema no impact mbona wakosoaji wapo CCM pia.

In short ni maigizo kama maigizo mengine wameamua kumbrand Polepole kwa manufaa mapana ya CCM.
 
Ni mawazo na utashi wake, kama wewe unavoona mambo Yale hayana afya vilevile na yeye anaona wenye mtazamo tofauti na yeye kuhusu hilo wanazingua,

Kuhusu wamachinga serikali inapaswa kulihandle very careful,
 
Jinsi alivyosaliti katiba ya wananchi kwa kuua mawazo ya kimageuzi aliyokua nayo sababu ya kuunga mkono uvunjanii sheria kwa vipande vya fedha akae akifahamu jinamizi litamuandama kila aendako..

Yote kwa yote ni kuwa haamini ni kuwa waliyemuona kama mungu hayupo tena
 
Back
Top Bottom