Nakubaliana na hoja ya bandari ya Bagamoyo lakini siyo kwa masharti na ujanja ujanja ya Wachina, ambao si marafiki wa kweli kama mnavyodhani

Sasa nyie mlitaka China awekeze mradi mkubwa kama huo halafu asirudishe hela yake?- Nyie vipi?
Yaani mnapenda vya bure bure tu?
Haya basi msimpe mchina, tafuteni hela zenu wenyewe mjenge, nakuhakikishia in 80 years hamtakuwa na hela ya kujenga hiyo bandari wala hela ya kujenga Economic Zone iliyokuwa imekusudiwa!.
Na Gharama za ujenzi za Dola bilion 10 za Leo za huo mradi miaka 30 ijayo zitakuwa dola bilioni 30!

China sera yake ni WIN-WIN, Siyo akupe mihela yote halafu asiwe na uhakika wa kurudisha hela yake.

Halafu hiyo bandari haiwezi kuua bandari ya Dar, Mkataba hauui bandari ya Dar

Tumezubaa kuchukua hili dili, kesho Mkenya anakwenda kuweka kitu cha maana hapo Lamu, na SGR tayari anayo japo kwa mbinde. Tumeshapigwa gepu la maana na Kenya kwa sababu ya kujivutavuta na umasikini Jeuri

Well said, be blessed - yaani uzubaifu wetu defies logic. Ni kweli kabisa Kenya lilkuwa na wasi wasi kuhusu ujenzi wa Babdari ya B'Moyo hivi sasa watakuwa wamefurahishwa na kusua sua kwetu hilo litawapa mwanya wa kujenga Bandari yao ya Lamu faster faster kwa kuingia ubia na Wachina wawajengee Bandari na viwanda.
 
Akumulikaye mchana usiku akuchoma Yaani SGR kenya ile kuanza Ku operate tu wachina wakaanza kuiba direct from day one ya kukusanya mapato ya SGR kenya
Kwani tatizo liko wapi, si Wachina wamejenga reli kwa hela zao wenyewe unataka wasirudishe mkopo wao wa ujenzi wa reli?

Nilisha sema humu kwamba hawawezi kurudia makosa waliyo fanya wakati wa ujenzi na uendeshaji wa reli ya TAZARA - karibu miaka hamsini imekwisha pita hawajalipwa hata senti tano za mkopo wao wa Matrillion tangu wakabidhi reli - hawawezi kurudia ujinga huo, hivi sasa watajenga reli/Bandari kwa mkopo lakini wanahakikisha wanakusanya mapato na kurudisha deni lao lote halafu baadae ndio wanawa kabidhi Mali zenu - nani anaweza kuwalahumu Wachina - once bitten twice shy.
 
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi.

Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
duuuh
 
Mkuu angalia kwanza source za taarifa hizi potofu - ni vizuri kuwa makini sana na propaganda zinazo enezwa na MSM for Geopolitics reasons Mara nyingi hazina ukweli wowote.

Mtu ungesema nchi husika zilikwenda Umoja wa Mataifa na kuishtaki Uchina kwamba imewaingiza kwenye mikataba tata hapo ningekuelewa, lakini haya mambo yakubuni tu yenye lengo lakuichafua Uchina siyo fresh hata kidogo - we angalia sources za taarifa hizi utakuta ni: New York times, Washington Post,Reuters, BBC, CNN, Al Jazeera no - Hii inakupa picha gani? Kuwa makini mkuu.
Mimi ningekushauri uyasome hayo makubaliano. Maana naona kama nabishana na Ndugai hapa
 
Mkuu mbona kama unarudia dirty campaign za nchi za magharibi specifically USA kuhusu ubaya wa ujio wa Wachina Barani Africa.

Mambo mengi unayo yasema kuhusu ubaya wa Wachina Barani Africa hayana tofauti na rhetoric za John Bolton mshauri wa Trump kuhusu masuala ya usalama - mwanzo nilifikiri labda ume-quote handouts zinazo tolewa na John Bolton na Pompeo katika vita yao ya kukabiliana na Chinese influence in Continental Africa na kwingineko (a joke).

Sisemi Wachina ni Malaika, lakini tuzianze ku- emulate campaign za magharibi zenye lengo la kuwachafua Wachina, wanao wasema sema Wachina wao wanaingia ubia na hao katikanaduala ya uwekezaji mfano London Dock, British Telecoms, Masuala ya wasiliano Ujerumani, Bandari Uguriki, Ujenzi wa reli za mwendo kasi kwenye baadhi ya miji huko USA na Ujerumani, Leo hii watu hao hao wanadai eti "Wachina ni wezi na matapeli!!!"

Kwani sisi tunaona ugumu gani kuzungumza na Wachina tukafikia muhafaka bila ya kuanza kujenga hoja za kukashifu Wachina ambao ni taifa pekee lenye uwezo na nia nzuri ya kutujengea viwanda vingi chini na kuongeza ajira kwa vijana.
Nadhani kuna ushahidi wa kutosha kwa nchi ambazo zilifanya kile ambazho Tanzania ilitaka kufanya, na hili nimeliweka wazi katika baadhi ya post hapo juu
 
Okay, kama unaona
Well said Mkuu, best kaandika maneno mengi lakini hayana substance zaidi tu ya kupiga porojo za ooooh Wachina si watu wazuri, Wachina si watu wazuri...maneno ya mtaani!

Toa sababu za msingi kwa nini Wachina ni watu wazuri, la sivyo unakuwa mtupu zaidi yangu. Na sijui kwa nini, nimeorodhesha baadhi ya nchi zilizoingia katika hili tatizo na Wachina, na kwa sasa ncho kama Djibouti zinahaha kujikwamua toka makucha ya wachina. Kwa nini mnakuwa na mapenzi upofu na wachina kiasi hiki lakini? Kwa sababu shemeji zenu wanamililiki Yutong?
 
Wachina wakijenga bandar wataitumia mbaka kuha kutukabidh itakuwa aifai tena kwa matumiz inabid tuikarabat upya
 
Embu mtusaidie mashaart ya kwenye huo mkataba yakoje mpaka sasa nasikia tu Zitto, Spika mara serikali mara mkokoteni

Mkuu acha unafiki ukiweka hapa unaweza kudadavua hata peg moja Au unajua ni kama stori za juma na Rosa
 
Back
Top Bottom