Nakubaliana na hoja ya bandari ya Bagamoyo lakini siyo kwa masharti na ujanja ujanja ya Wachina, ambao si marafiki wa kweli kama mnavyodhani

Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Watu acheni kuongea mambo kwa hisia. Magufuli anafanya mambo mengi kwa mihemuko ya kihisia - na hata anaweza kukutumbua na kukurudisha katika cheo chako ndani ya dakika tano. Lakini kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hapaswi kulaumiwa.

Na kabla hamjaanza kumlaumu mnapaswa kuelewa alichositisha ni nini hasa - ni ujenzi wa bandari au ni ujenzi wa bandari kwa makubaliano yaliyopo kati yetu na China? Nimesikitishwa sana na udhaifu na umbumbumbu wa Ndugai na Bunge katika hili. Na ningekuwa raisi wa nchi hii, huenda ningemuweka ndani Kikwete kwa kosa la uhaini kwa kukubali masharti kama yaliyopo kati yetu na Wachina kwa ajili ya hii bandari na SGR.

Kumbukeni SGR kwa mfano, makubaliano yalikuwa kati ya Tanzania na China. Magufuli aliingia akaupiga chini na kuanza kuingia makubaliano na Uturuki kwa awamu ya kwanza. Mmejiuliza kwa nini?

Nataka niwatahadharishe Watanzania wenzangu. Wachina huwa sio marafiki kama watu wengi wanavyofikiria. Ni wajanja mno. Afrika kwa sasa inapaswa kutambua kwamba hatari ya uhuru wa nchi zake wa kiuchumi na hata kisiasa kwa sasa hailetwi na mataifa ya magharibi, bali inaletwa na China. Hata siku moja usiingie kichwa kichwa ukiwa kiongozi wa nchi katika mkataba na China kwa sababu wanakuja kama marafiki zetu wasioingilia mambo yetu ya ndani. Utajikuta siku moja sehemu ya nchi yako imechukuliwa na waChina, au kufanywa mtumwa wa kiuchumi na kisiasa wa China kwa mamia ya miaka.

Hata wachina kutujengea Makao Makuu ya AU (African Union) pale Addis Ababa, nimewauliza watu, hivi mna uhakika gani kwamba kila neno mnalosema pale ndani ya hizo ofisi, au document mnayoandika, Mchina hawasikilizi na kujua mmeamua nini kata katika vikao vyenu vya siri? Yaani mnachoona ni msaada tu toka China na kupofushwa kiasi hicho?

Magufuli kuna mengi sana sikuungi mkono, lakini kwa hili la kusitisha huu mpango wa kujengewa bandari na SGR na waChina nakupongeza sana. Kuna nchi za Afrika ambazo ziliingia mikataba ya miradi mikubwa na muda mrefu na Wachina na sasa zinajuta na kulia. Acha turudi mezani na kuona ni jinsi gani tunaweza kujenga bandari Bagamoyo bila kuuza nchi na uhuru wetu kwa Wachina.

Kumbuka, Magufuli hajasitisha ujenzi wa bandari Bagamoyo kwa kuwa hataki kujenga bandari Bagamoyo. Amekataa kujenga bandari hiyo kwa masharti yaliyowekwa na Wachina. Aungwe mkono badala ya kulaumiwa, na alaumiwe kwa yanayostahili yeye kulaumiwa, lakini sio hili la bandari.
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Embu mtusaidie mashaart ya kwenye huo mkataba yakoje mpaka sasa nasikia tu Zitto, Spika mara serikali mara mkokoteni
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi.

Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
 
Praetorian

Praetorian

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
7
Points
45
Praetorian

Praetorian

Member
Joined Apr 19, 2019
7 45
Kutaka kuaminisha uma kwamba mkataba ni mbovu bila kuweka masharti mabovu ya huo mkataba nadhani ni porojo na ushabiki usio na kichwa wala miguu. Wasomi hupinga kwa hoja zenye ushahidi na siyo ambacho wewe unakifanya hapa. Huitendei haki taaluma yako pamoja na pesa ya karo ya waliokusomesha.
 
ELI-91

ELI-91

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Messages
2,824
Points
2,000
ELI-91

ELI-91

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2014
2,824 2,000
pamoja na kuwaita wazungu mabeberu JPM yuko makini sana na wachina, na ukiangalia kwa makini anawaamini zaidi wazungu/waarabu kuliko wachina na yuko sahihi 100%, china ya leo inataka kufanya kilichofanywa na ufalme wa uingereza miaka 100 iliyopita, kwakifupi wanataka kuigeuza afrika kua koloni lake
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Kutaka kuaminisha uma kwamba mkataba ni mbovu bila kuweka masharti mabovu ya huo mkataba nadhani ni porojo na ushabiki usio na kichwa wala miguu. Wasomi hupinga kwa hoja zenye ushahidi na siyo ambacho wewe unakifanya hapa. Huitendei haki taaluma yako pamoja na pesa ya karo ya waliokusomesha.
Sasa jambo ambalo wewe hujui au kwa kuwa tu hujaona huo ushahidi halifanyi liwe porojo. Huo ni uwezo mdogo wa kufikiri. Mikataba mingapi unafahamu masharti yake? Hata Wabunge walikataliwa kuiona.

Na unafikiri kwamba Watanzania ni wajinga kiasi hicho wakatae tu kitu chenye faida kwao kwa sababu za kilevi tu au uendawazimu fulani? Au unafikiri Magufuli amekataa bandari kujengwa Bagamoyo kwa kuwa anataka ikajengwe Chato kama ile International Airport?

Umeona kilichozitokea nchi zilizokubali masharti ya China kwa miradi hii mikubwa? Waulize hata jirani hapa Kenya

Pia soma hapa

  • Last year, with more than $1 billion in debt to China, Sri Lanka handed over a port to companies owned by the Chinese government. Now Djibouti, home to the US military’s main base in Africa, looks about to cede control of another key port to a Beijing-linked company, and the US is not happy about it.
  • Last Tuesday in Beijing, the Malaysian prime minister, Mahathir Mohamad, announced that his country was canceling two multibillion-dollar Chinese projects because Malaysia can’t repay its debts. “We do not want a situation where there is a new version of colonialism,” Malaysia’s leader told his grim-faced host, Premier Li Keqiang.
  • Sri Lanka was so indebted to China after approving a string of ambitious projects that it was forced last year to lease a port in Hambantota to a Chinese company for 99 years.
  • Pakistan, too, is reportedly to be the site of a Chinese-only community, this one for 500,000, near the port of Gwadar, which China is building as part of its “string of pearls” project to construct ports, possibly for the use of its navy, across the Indian Ocean to Africa.
  • Myanmar is trying to renegotiate a $10 billion port project; Nepal wants to halt construction on two Chinese-built hydroelectric dams. Other nations are so in hock to China that they say little, but things there have already approached a point where analysts believe that debt crises are almost inevitable.
 
M

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
5,763
Points
2,000
M

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
5,763 2,000
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi. Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
Kwanza nikupongeze wewe na mleta UZI kwa ufafanuzi wa hi kitu; hata mimi naungana na nyie kumpongeza mhe rais kuhusiana na hili la bandari ya Bagamoyo; nchi ilikua inauzwa jumla. Kuna kitu kimoja tu Watanzania nadhani tujitafakari, tumekua wasahaulifu mno, hili jambo lilijadiriwa hata humu wakati ule wa Mkwere/JK na hope ndio sababu hata JK mwenyewe alikua anasita sita kusaini mkataba. Big up sana mhe No kwa hili, kuna mengne mengi siyaungi mkono but kwa hili, big YES.
 
Praetorian

Praetorian

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
7
Points
45
Praetorian

Praetorian

Member
Joined Apr 19, 2019
7 45
Na unafikiri kwamba Watanzania ni wajinga kiasi hicho wakatae tu kitu chenye faida kwao kwa sababu za kilevi tu au uendawazimu fulani? Au unafikiri Magufuli amekataa bandari kujengwa Bagamoyo kwa kuwa anataka ikajengwe Chato kama ile International Airport?
Hao Watanzania unaotaka kuwatetea hapa kwamba wako makini wana historia ndefu ya kukataa mambo mengi sana yenye faida kubwa kiuchumi kwao kwa kujificha chini ya kivuli cha uzalendo. Hili la Bagamoyo SEZ halitakuwa la kwanza wala la mwisho. Ningekuona muungwana kama ungesema tuombe Serikali itoe sababu za msingi kwanini imekataa kuendelea na mradi mkubwa namna hii. Spika wa Bunge ameongea kiuungwana sana kwa kusema anaomba Serikali itoe maelezo zaidi kwasababu yenyewe ndiyo inafahamu zaidi kuliko Bunge. Sasa wewe unaposema mkataba ni mbovu na Jakaya anatakiwa kufungwa kwa uhaini, unataka watu wazima tukueleweje ?
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Hao Watanzania unaotaka kuwatetea hapa kwamba wako makini wana historia ndefu ya kukataa mambo mengi sana yenye faida kubwa kiuchumi kwao kwa kujificha chini ya kivuli cha uzalendo. Hili la Bagamoyo SEZ halitakuwa la kwanza wala la mwisho. Ningekuona muungwana kama ungesema tuombe Serikali itoe sababu za msingi kwanini imekataa kuendelea na mradi mkubwa namna hii. Spika wa Bunge ameongea kiuungwana sana kwa kusema anaomba Serikali itoe maelezo zaidi kwasababu yenyewe ndiyo inafahamu zaidi kuliko Bunge. Sasa wewe unaposema mkataba ni mbovu na Jakaya anatakiwa kufungwa kwa uhaini, unataka watu wazima tukueleweje ?
Mkuu, soma post zangu utaona mie nampinga na kumkosoa sana Magufuli kwa mambo mengi hadi nimeonywa ninatafutwa na Wasiojulikana, lakini sio hili. Kuna mikataba mingi sana ilisainiwa wakati wa Kikwete ambayo ukiangalia dondoo za makubaliano unaweza ukaililia Tanzania, kutia ndani na ule wa SGR na Wachina ambao uliopolewa ukiwa karibu kuanza kupikwa. Sasa huu wa Bandari ni mbaya hata zaidi, unakufanya ujiulize, hivi hawa kina Chenge walikuwa wanatumia akili kweli? Ni uhaini mtupu.
 
Praetorian

Praetorian

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
7
Points
45
Praetorian

Praetorian

Member
Joined Apr 19, 2019
7 45

Last year, with more than $1 billion in debt to China, Sri Lanka handed over a port to companies owned by the Chinese government. Now Djibouti, home to the US military’s main base in Africa, looks about to cede control of another key port to a Beijing-linked company, and the US is not happy about it.

Last Tuesday in Beijing, the Malaysian prime minister, Mahathir Mohamad, announced that his country was canceling two multibillion-dollar Chinese projects because Malaysia can’t repay its debts. “We do not want a situation where there is a new version of colonialism,” Malaysia’s leader told his grim-faced host, Premier Li Keqiang.

Sri Lanka was so indebted to China after approving a string of ambitious projects that it was forced last year to lease a port in Hambantota to a Chinese company for 99 years.
Tafadhali fanya utafiti kabla hujakimbilia kuandika vitu vikubwa kama hivi. Financing ya mradi wa Bagamoyo ni tofauti kabisa na hizo nchi ulizozijata hapo juu kwasababu umefanywa chini ya B.O.T (Build, Operate and Transfer) ambapo serikali za Uchina na Oman zingejenga hiyo bandari kwa pesa zao na kuiendesha kwa miaka 30 kisha kuiachia Tanzania umiliki wa hiyo bandari. Sri-Lanka ilichukua mkopo ya moja kwa moja ili kujenga bandari na wakashindwa kulipa, Tanzania haijachukua mkopo bali imetoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo Debt-Trap inatokea wapi ?
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Tafadhali fanya utafiti kabla hujakimbilia kuandika vitu vikubwa kama hivi. Financing ya mradi wa Bagamoyo ni tofauti kabisa na hizo nchi ulizozijata hapo juu kwasababu umefanywa chini ya B.O.T (Build, Operate and Transfer) ambapo serikali za Uchina na Oman zingejenga hiyo bandari kwa pesa zao na kuiendesha kwa miaka 30 kisha kuiachia Tanzania umiliki wa hiyo bandari. Sri-Lanka ilichukua mkopo ya moja kwa moja ili kujenga bandari na wakashindwa kulipa, Tanzania haijachukua mkopo bali imetoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo Debt-Trap inatokea wapi ?
Hahaha! Mkuu, yaani B.O.T ni worse than kuwa na loan. Kumbuka kwenye B.O.T una transfer baada ya ku-realize targeted interest, ambayo Wachina huwa wanakuambia Transfer itafanyika baada ya miaka 33 tu. But nakuambia, hakuna kitu kama hicho kitatokea kwa nchi zote zenye B.O.T na China.

Na waliochukua loans wakadhani labda ni nafuu kuliko B.O.T waligundua wameingia mkenge mkubwa, kwa kuwa masharti ya ku-default payment ya loan yanaeletea condition ya "Operate" kwa 99 years (Sri Lanka was so indebted to China after approving a string of ambitious projects that it was forced last year to lease a port in Hambantota to a Chinese company for 99 years)

Najua ninachoongea, trust me.
 
MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Messages
1,303
Points
2,000
MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2017
1,303 2,000
UKOLONI MAMBOLEO UMETAMALAKI,
KAMA MLIMANI CITY ILIVYOKODISHWA 50yrs,
hapa nilipo nina 37+50=85 ndio chuo kikuu watapewa yale majengo yashaoza nyang'anyang'a
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
15,492
Points
2,000
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
15,492 2,000
..mradi unahusisha BANDARI na VIWANDA.

..na wawekezaji wanatoka CHINA na OMAN.

..Sasa kwanini tunazungumzia bandari na Wachina peke yake?

..Pia TANZANIA / SEREKALI inawekeza FEDHA kiasi gani ktk miradi hiyo?

..kuna wakati tulisikia SEREKALI itapewa kiasi fulani cha HISA ikiwa itakubali kuwafidia wananchi waliotoa ardhi yao kwa mradi.

..baadae zikatoka habari kwamba, kutokana na UKATA wa fedha, SEREKALI ime-surrender hisa zake kwa kuwaachia wawekezaji jukumu la kulipa wananchi waliotoa ardhi kwa mradi.

..maoni yangu ni kwamba kiwango cha mchango wa serekali ktk mradi huu kina-determine kiwango cha hisa na aina ya masharti yanayotolewa na wawekezaji.
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
UKOLONI MAMBOLEO UMETAMALAKI,
KAMA MLIMANI CITY ILIVYOKODISHWA 50yrs,
hapa nilipo nina 37+50=85 ndio chuo kikuu watapewa yale majengo yashaoza nyang'anyang'a
MKuu, afadhali hata iwe 50. Wachina huwa wanataka miaka 99!
 
A

Alex Mbwilo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Messages
305
Points
250
A

Alex Mbwilo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2013
305 250
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi. Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
Nipo pamoja na Serkali kama masharti yenyewe ndio hayo!.viongozi wetu wa sasa lazima wawe makini sana, watu weupe hawanaga nia nzuri na sisi weusi toka kuumbwa kwa Dunia
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Kwanza nikupongeze wewe na mleta UZI kwa ufafanuzi wa hi kitu; hata mimi naungana na nyie kumpongeza mhe rais kuhusiana na hili la bandari ya Bagamoyo; nchi ilikua inauzwa jumla. Kuna kitu kimoja tu Watanzania nadhani tujitafakari, tumekua wasahaulifu mno, hili jambo lilijadiriwa hata humu wakati ule wa Mkwere/JK na hope ndio sababu hata JK mwenyewe alikua anasita sita kusaini mkataba. Big up sana mhe No kwa hili, kuna mengne mengi siyaungi mkono but kwa hili, big YES.
Mkuu mleta uzi na mtoa ufafanuzi ni mtu mmoja, mie 😃

Tatizo ni kwamba, kwa kuwa kuna madudu mengi ambayo Magufuli anafanya, watu wamefikia kudhani kila analofanya ni dudu. Nilishasema humu ndani, kuna madudu mengi anafanya, lakini ukiniuliza kati ya Magufuli na Mkwere nani awe raisi, basi nitakuambia Magufuli.

Vivyo hivyo sintaacha kumwambia Magufuli na CCM yake kuwa sio kila kidu wanachofanya Wapinzani ni madudu. Kuna mambo CCM wanafanya ni madudu makubwa ya kutisha afadhali mara mia wapinzani.
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
15,492
Points
2,000
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
15,492 2,000
Tatizo ni kwamba, kwa kuwa kuna madudu mengi ambayo Magufuli anafanya, watu wamefikia kudhani kila analofanya ni dudu. Nilishasema humu ndani, kuna madudu mengi anafanya, lakini ukiniuliza kati ya Magufuli na Mkwere nani awe raisi, basi nitakuambia Magufuli.

Vivyo hivyo sintaacha kumwambia Magufuli na CCM yake kuwa sio kila kidu wanachofanya Wapinzani ni madudu. Kuna mambo CCM wanafanya ni madudu makubwa ya kutisha afadhali mara mia wapinzani.
..huenda masharti ni mabaya kwasababu serekali haiwekezi chochote ktk mradi huo.

..So far tumesikia masharti mabaya ya Wachina kuhusu bandari.

..Je, masharti ya Waomani kuhusu viwanda yakoje?

..inawezekana hatuhitaji bandari, Je viwanda navyo hatuvihitaji?
 
DOHOO

DOHOO

Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
31
Points
125
DOHOO

DOHOO

Member
Joined Oct 17, 2012
31 125
Hahaha! Mkuu, yaani B.O.T ni worse than kuwa na loan. Kumbuka kwenye B.O.T una transfer baada ya ku-realize targeted interest, ambayo Wachina huwa wanakuambia Transfer itafanyika baada ya miaka 33 tu. But nakuambia, hakuna kitu kama hicho kitatokea kwa nchi zote zenye B.O.T na China.

Na waliochukua loans wakadhani labda ni nafuu kuliko B.O.T waligundua wameingia mkenge mkubwa, kwa kuwa masharti ya ku-default payment ya loan yanaeletea condition ya "Operate" kwa 99 years (Sri Lanka was so indebted to China after approving a string of ambitious projects that it was forced last year to lease a port in Hambantota to a Chinese company for 99 years)

Najua ninachoongea, trust me.
Mbona sasa na wewe hueleweki ......kwa majibu yako ni dhahiri B.O.T is bether than loan........
 
Forum statistics

Threads 1,295,454
Members 498,335
Posts 31,212,531
Top