Nakubaliana na hoja ya bandari ya Bagamoyo lakini siyo kwa masharti na ujanja ujanja ya Wachina, ambao si marafiki wa kweli kama mnavyodhani

S ndio wanaibeba ccm. Kila kukicha gambas mnafunga safari China mpaka mabomu ya arusha waliyatoa huko china, tena mpaka jiwe kawasifia hadharani na kuwaponda wazungu waziwazi, halafu hiyo yote tisa, watuonyeshe hiyo mikataba isije ikawa wanasema hivi kumbe ni vile.
MKuu, afadhali hata iwe 50. Wachina huwa wanataka miaka 99!
 
Watu acheni kuongea mambo kwa hisia. Magufuli anafanya mambo mengi kwa mihemuko ya kihisia - na hata anaweza kukutumbua na kukurudisha katika cheo chako ndani ya dakika tano. Lakini kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hapaswi kulaumiwa.

Na kabla hamjaanza kumlaumu mnapaswa kuelewa alichositisha ni nini hasa - ni ujenzi wa bandari au ni ujenzi wa bandari kwa makubaliano yaliyopo kati yetu na China? Nimesikitishwa sana na udhaifu na umbumbumbu wa Ndugai na Bunge katika hili. Na ningekuwa raisi wa nchi hii, huenda ningemuweka ndani Kikwete kwa kosa la uhaini kwa kukubali masharti kama yaliyopo kati yetu na Wachina kwa ajili ya hii bandari na SGR.

Kumbukeni SGR kwa mfano, makubaliano yalikuwa kati ya Tanzania na China. Magufuli aliingia akaupiga chini na kuanza kuingia makubaliano na Uturuki kwa awamu ya kwanza. Mmejiuliza kwa nini?

Nataka niwatahadharishe Watanzania wenzangu. Wachina huwa sio marafiki kama watu wengi wanavyofikiria. Ni wajanja mno. Afrika kwa sasa inapaswa kutambua kwamba hatari ya uhuru wa nchi zake wa kiuchumi na hata kisiasa kwa sasa hailetwi na mataifa ya magharibi, bali inaletwa na China. Hata siku moja usiingie kichwa kichwa ukiwa kiongozi wa nchi katika mkataba na China kwa sababu wanakuja kama marafiki zetu wasioingilia mambo yetu ya ndani. Utajikuta siku moja sehemu ya nchi yako imechukuliwa na waChina, au kufanywa mtumwa wa kiuchumi na kisiasa wa China kwa mamia ya miaka.

Hata wachina kutujengea Makao Makuu ya AU (African Union) pale Addis Ababa, nimewauliza watu, hivi mna uhakika gani kwamba kila neno mnalosema pale ndani ya hizo ofisi, au document mnayoandika, Mchina hawasikilizi na kujua mmeamua nini kata katika vikao vyenu vya siri? Yaani mnachoona ni msaada tu toka China na kupofushwa kiasi hicho?

Magufuli kuna mengi sana sikuungi mkono, lakini kwa hili la kusitisha huu mpango wa kujengewa bandari na SGR na waChina nakupongeza sana. Kuna nchi za Afrika ambazo ziliingia mikataba ya miradi mikubwa na muda mrefu na Wachina na sasa zinajuta na kulia. Acha turudi mezani na kuona ni jinsi gani tunaweza kujenga bandari Bagamoyo bila kuuza nchi na uhuru wetu kwa Wachina.

Kumbuka, Magufuli hajasitisha ujenzi wa bandari Bagamoyo kwa kuwa hataki kujenga bandari Bagamoyo. Amekataa kujenga bandari hiyo kwa masharti yaliyowekwa na Wachina. Aungwe mkono badala ya kulaumiwa, na alaumiwe kwa yanayostahili yeye kulaumiwa, lakini sio hili la bandari.
asante sana mkuu
 
Mkuu mleta uzi na mtoa ufafanuzi ni mtu mmoja, mie 😃

Tatizo ni kwamba, kwa kuwa kuna madudu mengi ambayo Magufuli anafanya, watu wamefikia kudhani kila analofanya ni dudu. Nilishasema humu ndani, kuna madudu mengi anafanya, lakini ukiniuliza kati ya Magufuli na Mkwere nani awe raisi, basi nitakuambia Magufuli.

Vivyo hivyo sintaacha kumwambia Magufuli na CCM yake kuwa sio kila kidu wanachofanya Wapinzani ni madudu. Kuna mambo CCM wanafanya ni madudu makubwa ya kutisha afadhali mara mia wapinzani.
Na hili ndio tatizo kubwa tulilonalo Watanzania, tukisifia magufuli wote tunaonekana ni wana ccm na tukisia upinzani tunaitwa Chadema, wengine hata KADI za chama tu hatujui zinauzwaga Tsh ngapi. Well, nakubaliana na wewe kabisa kwa hili la Bagamoyo
 
Uko sahihi kiongozi.
Ukiwa na utawala wa kujishukushuku unakuwa unaona unaibiwa tu.
Leo ni miaka 50 ya Uhuru, Kama siyo JK kutujengea angalau terminal III yenye hadhi hapo JKN airport leo tungeenfelea kuwa na terminal yenye jengo la hadhi ya Mini Super Market!!!

Leo tunaona miaka 50 ya mchina kuendesha bandari ni miingi wakati ndani ya muaka hiyi 50 tumeshindwa kujenga shule za kutosha watoto wetu.

Isitoshe hata kama mchina anakusanya yeye hela lazima itakuwepo mechanism ya wao kutugea chetu ikiwemo kodi mbalimbali kama vile VAT etc. Najua Mchina anataka akusanye yeye kwa sababu anajua Bongo rushwa imetamalaki, watu watapitisha mzigo kimagumashi bila kulipa tozo stahiki, kwa hiyo anaona bora akusanye yeye kisha kilicho chetu atupe!. Na pia hii ni Kinga dhidi ya serikali ya bongo kuwacheleweshea malipo yao ya kila mwezi/mwaka.

Miaka 50 kwa taifa siyo mingi!
Tumepoteza Dili la maana sana!!

Umesahau pia kuwa Mchina na rushwa ni kama uji na mgonjwa.....
 
Na hili ndio tatizo kubwa tulilonalo Watanzania, tukisifia magufuli wote tunaonekana ni wana ccm na tukisia upinzani tunaitwa Chadema, wengine hata KADI za chama tu hatujui zinauzwaga Tsh ngapi. Well, nakubaliana na wewe kabisa kwa hili la Bagamoyo
Umenena vema sana Mkuu, na huo ndio uzalendo halisi. Mie sina kadi ya chama chochote wala mpango wa kuwa nayo.
 
Sasa nyie mlitaka China awekeze mradi mkubwa kama huo halafu asirudishe hela yake?- Nyie vipi?
Yaani mnapenda vya bure bure tu?
Hapana, tunataka tu kuwa na mktataba ulio fair. Kama Mchina anasema atashika bandari kwa miaka 99 ili arudishe faida ndio aikabidhi kwetu, basi na sisi tunamwambia tutamrudishia hiyo fedha yake kwa miaka hiyo hiyo 99 bila kukosa kila mwaka.

Kwa nini tukisema tutamrudishia sisi ila tuiendeshe bandari wenyewe atake mkataba wa miaka 33 lakini akisema yeye ndio ataiendesha atake mkataba wa miaka 99? Hivi anafikiri sie ndondocha?
 
Baadhi ya vitu hua nampongeza Magufuli ni kutoku-fall kwa upumbavu kama huu. Vitu kama hivi vinamfanya anaonekana mtu smart kabisa, ila hujakaa sawa mara watekaji, mara bashite, mara udikteta uchwara, fungafunga then mazuri yote anayofanya yanaonekana shit.
 
Uko sahihi kiongozi.
Ukiwa na utawala wa kujishukushuku unakuwa unaona unaibiwa tu.
Leo ni miaka 50 ya Uhuru, Kama siyo JK kutujengea angalau terminal III yenye hadhi hapo JKN airport leo tungeenfelea kuwa na terminal yenye jengo la hadhi ya Mini Super Market!!!

Leo tunaona miaka 50 ya mchina kuendesha bandari ni miingi wakati ndani ya muaka hiyi 50 tumeshindwa kujenga shule za kutosha watoto wetu.

Isitoshe hata kama mchina anakusanya yeye hela lazima itakuwepo mechanism ya wao kutugea chetu ikiwemo kodi mbalimbali kama vile VAT etc. Najua Mchina anataka akusanye yeye kwa sababu anajua Bongo rushwa imetamalaki, watu watapitisha mzigo kimagumashi bila kulipa tozo stahiki, kwa hiyo anaona bora akusanye yeye kisha kilicho chetu atupe!. Na pia hii ni Kinga dhidi ya serikali ya bongo kuwacheleweshea malipo yao ya kila mwezi/mwaka.

Miaka 50 kwa taifa siyo mingi!
Tumepoteza Dili la maana sana!!

Mkuu, amini nakuambia, Mchina akikuambia miaka 50 kwenye mkataba kuna kipengele kitasema usiporudisha katika miaka 50 ataichukua kwa miaka 99. Na ukisema hcho kipengele hakifai anakataa kubadili. Hapo bado hajasema anataka usiendeleze Mtwara na Tanga, na usitumie tena ya Dar es Salaam kwa meli za mzizigo toka nje wakati hii bandari ikifanya kazi!

Ebo, mwache arudi China akale majongoo!
 
Bandari siyo mkopo, ni investment tu China anainvest , anarudisha hela yake na faida basi kisha anatuachia bandari. Modality yake haina tofauti na mmiliki wa chombo cha usafiri anampa dereva akiendeshe anaweka watu wake wa kumletea hesabu, pesa yake ikisharudi na faida yake basi chombo anampa dereva kiwe chake. Sasa hapo ni jukumu la dereva kuhakikisha anafanya kazi vizuri na konda wa tajiri hesabu ipatikane ndani ya wakati ili baadae chombo kiwe chake. HAKUNA MKOPO HAPO
 
Kuna tofauti Mkuu. Kumbuka ardhi ni yetu, maji ni yetu na bandari iko ndani ya nchi yetu. Sasa huwezi kulinganisha na kumpa gari dereva ambae gari si lake.

Tunaanzisha miradi ili isaidie maendeleo ya uchumi wetu, sio tu itoe huduma. Kama hi hivyo tungealika wewekezaji waje wajenge reli, waendeshe mashirika ya ndege nk, bila sie kujali kufaidika kiuchumi ili mradi tutapanda hizo ndege.
 
Kweli kabisa, lakini twende World Bank, au African Development Bank. Ila tatizo, Magufuli alishagombana na World Bank, mambo ya ushoga na haki za binadamu!
Magufuli wakati mwingine ana munkhali,anatunisha misuli pasipo sababu kwani akinyamaza kimya anapata hasara gani?
 
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi.

Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
Weka terms za mkataba wala si porojo au tafasri zako
 
Sasa jambo ambalo wewe hujui au kwa kuwa tu hujaona huo ushahidi halifanyi liwe porojo. Huo ni uwezo mdogo wa kufikiri. Mikataba mingapi unafahamu masharti yake? Hata Wabunge walikataliwa kuiona.

Na unafikiri kwamba Watanzania ni wajinga kiasi hicho wakatae tu kitu chenye faida kwao kwa sababu za kilevi tu au uendawazimu fulani? Au unafikiri Magufuli amekataa bandari kujengwa Bagamoyo kwa kuwa anataka ikajengwe Chato kama ile International Airport?

Umeona kilichozitokea nchi zilizokubali masharti ya China kwa miradi hii mikubwa? Waulize hata jirani hapa Kenya

Pia soma hapa

  • Last year, with more than $1 billion in debt to China, Sri Lanka handed over a port to companies owned by the Chinese government. Now Djibouti, home to the US military’s main base in Africa, looks about to cede control of another key port to a Beijing-linked company, and the US is not happy about it.
  • Last Tuesday in Beijing, the Malaysian prime minister, Mahathir Mohamad, announced that his country was canceling two multibillion-dollar Chinese projects because Malaysia can’t repay its debts. “We do not want a situation where there is a new version of colonialism,” Malaysia’s leader told his grim-faced host, Premier Li Keqiang.
  • Sri Lanka was so indebted to China after approving a string of ambitious projects that it was forced last year to lease a port in Hambantota to a Chinese company for 99 years.
  • Pakistan, too, is reportedly to be the site of a Chinese-only community, this one for 500,000, near the port of Gwadar, which China is building as part of its “string of pearls” project to construct ports, possibly for the use of its navy, across the Indian Ocean to Africa.
  • Myanmar is trying to renegotiate a $10 billion port project; Nepal wants to halt construction on two Chinese-built hydroelectric dams. Other nations are so in hock to China that they say little, but things there have already approached a point where analysts believe that debt crises are almost inevitable.
Sijaona inayozungumzia mradi wa SEZ bagamoyo. Hii ni kutaka kutumia mazingira tofauti kutetea hoja nyingine. Je terms za mkataba wa bagamoyo ziko sawa na ulichodokeza hapo?
 
Watu acheni kuongea mambo kwa hisia. Magufuli anafanya mambo mengi kwa mihemuko ya kihisia - na hata anaweza kukutumbua na kukurudisha katika cheo chako ndani ya dakika tano. Lakini kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hapaswi kulaumiwa.

Na kabla hamjaanza kumlaumu mnapaswa kuelewa alichositisha ni nini hasa - ni ujenzi wa bandari au ni ujenzi wa bandari kwa makubaliano yaliyopo kati yetu na China? Nimesikitishwa sana na udhaifu na umbumbumbu wa Ndugai na Bunge katika hili. Na ningekuwa raisi wa nchi hii, huenda ningemuweka ndani Kikwete kwa kosa la uhaini kwa kukubali masharti kama yaliyopo kati yetu na Wachina kwa ajili ya hii bandari na SGR.

Kumbukeni SGR kwa mfano, makubaliano yalikuwa kati ya Tanzania na China. Magufuli aliingia akaupiga chini na kuanza kuingia makubaliano na Uturuki kwa awamu ya kwanza. Mmejiuliza kwa nini?

Nataka niwatahadharishe Watanzania wenzangu. Wachina huwa sio marafiki kama watu wengi wanavyofikiria. Ni wajanja mno. Afrika kwa sasa inapaswa kutambua kwamba hatari ya uhuru wa nchi zake wa kiuchumi na hata kisiasa kwa sasa hailetwi na mataifa ya magharibi, bali inaletwa na China. Hata siku moja usiingie kichwa kichwa ukiwa kiongozi wa nchi katika mkataba na China kwa sababu wanakuja kama marafiki zetu wasioingilia mambo yetu ya ndani. Utajikuta siku moja sehemu ya nchi yako imechukuliwa na waChina, au kufanywa mtumwa wa kiuchumi na kisiasa wa China kwa mamia ya miaka.

Hata wachina kutujengea Makao Makuu ya AU (African Union) pale Addis Ababa, nimewauliza watu, hivi mna uhakika gani kwamba kila neno mnalosema pale ndani ya hizo ofisi, au document mnayoandika, Mchina hawasikilizi na kujua mmeamua nini kata katika vikao vyenu vya siri? Yaani mnachoona ni msaada tu toka China na kupofushwa kiasi hicho?

Magufuli kuna mengi sana sikuungi mkono, lakini kwa hili la kusitisha huu mpango wa kujengewa bandari na SGR na waChina nakupongeza sana. Kuna nchi za Afrika ambazo ziliingia mikataba ya miradi mikubwa na muda mrefu na Wachina na sasa zinajuta na kulia. Acha turudi mezani na kuona ni jinsi gani tunaweza kujenga bandari Bagamoyo bila kuuza nchi na uhuru wetu kwa Wachina.

Kumbuka, Magufuli hajasitisha ujenzi wa bandari Bagamoyo kwa kuwa hataki kujenga bandari Bagamoyo. Amekataa kujenga bandari hiyo kwa masharti yaliyowekwa na Wachina. Aungwe mkono badala ya kulaumiwa, na alaumiwe kwa yanayostahili yeye kulaumiwa, lakini sio hili la bandari.

Mkuu mbona kama unarudia dirty campaign za nchi za magharibi specifically USA kuhusu ubaya wa ujio wa Wachina Barani Africa.

Mambo mengi unayo yasema kuhusu ubaya wa Wachina Barani Africa hayana tofauti na rhetoric za John Bolton mshauri wa Trump kuhusu masuala ya usalama - mwanzo nilifikiri labda ume-quote handouts zinazo tolewa na John Bolton na Pompeo katika vita yao ya kukabiliana na Chinese influence in Continental Africa na kwingineko (a joke).

Sisemi Wachina ni Malaika, lakini tuzianze ku- emulate campaign za magharibi zenye lengo la kuwachafua Wachina, wanao wasema sema Wachina wao wanaingia ubia na hao katikanaduala ya uwekezaji mfano London Dock, British Telecoms, Masuala ya wasiliano Ujerumani, Bandari Uguriki, Ujenzi wa reli za mwendo kasi kwenye baadhi ya miji huko USA na Ujerumani, Leo hii watu hao hao wanadai eti "Wachina ni wezi na matapeli!!!"

Kwani sisi tunaona ugumu gani kuzungumza na Wachina tukafikia muhafaka bila ya kuanza kujenga hoja za kukashifu Wachina ambao ni taifa pekee lenye uwezo na nia nzuri ya kutujengea viwanda vingi chini na kuongeza ajira kwa vijana.
 
Umeongea maneno mengi lakini hujatupa habari mpya, my point is...ukitaka kuzungumzia kitu ambacho kimeshazungumziwa na watu kadhaa usirudie maneno yale yale, give us new information!
 
..huenda masharti ni mabaya kwasababu serekali haiwekezi chochote ktk mradi huo.

..So far tumesikia masharti mabaya ya Wachina kuhusu bandari.

..Je, masharti ya Waomani kuhusu viwanda yakoje?

..inawezekana hatuhitaji bandari, Je viwanda navyo hatuvihitaji?

Well said JokaKuu, tatizo letu kuu ni ukosefu wa kuchangamkia fursa zilizo wazi wazi tu tofauti na wenzetu wa Kenya - kazi kutumbukiza masuala ya politics hata ambapo sio mahala pake.

Sisi hatuwekezi chochote zaidi ya aridhi halafu tunataka kuwakalia kooni watu ambao wabataja kutumia fedha zao kujenga Bandari pamoja na Viwanda vya maana Nchini, ni Taifa gani linaweza kujitolea kugharimia ujenzi wa Bandari na viwanda at a go? Kwani wakiendesha Bandari kwa miaka33 kwa kuyulipa kodi yetu tutapata hasara gani, na tumewekeza nini hasa zaidi ya aridhi. Kinacho shangaza zaidi kuna Watanzania wenye mawazo ya ajabu sana, yaani wako radhi B'moyo ibaki pori kuliko kuruhusu Wachina wajenge Bandari na viwanda. Naona visingizio vya kutojengwa hydro electric power station katika mto wa Rufiji kwenye miaka ya 1970s yanataka kujirudia tena kwenye Badari ya Bagamoyo,tutakuja kushtuka tena baada ya miaka hamsini kupita.
 
Mkuu mbona kama unarudia dirty campaign za nchi za magharibi specifically USA kuhusu ubaya wa ujio wa Wachina Barani Africa.

Mambo mengi unayo yasema kuhusu ubaya wa Wachina Barani Africa hayana tofauti na rhetoric za John Bolton mshauri wa Trump kuhusu masuala ya usalama - mwanzo nilifikiri labda ume-quote handouts zinazo tolewa na John Bolton na Pompeo katika vita yao ya kukabiliana na Chinese influence in Continental Africa na kwingineko (a joke).

Sisemi Wachina ni Malaika, lakini tuzianze ku- emulate campaign za magharibi zenye lengo la kuwachafua Wachina, wanao wasema sema Wachina wao wanaingia ubia na hao katikanaduala ya uwekezaji mfano London Dock, British Telecoms, Masuala ya wasiliano Ujerumani, Bandari Uguriki, Ujenzi wa reli za mwendo kasi kwenye baadhi ya miji huko USA na Ujerumani, Leo hii watu hao hao wanadai eti "Wachina ni wezi na matapeli!!!"

Kwani sisi tunaona ugumu gani kuzungumza na Wachina tukafikia muhafaka bila ya kuanza kujenga hoja za kukashifu Wachina ambao ni taifa pekee lenye uwezo na nia nzuri ya kutujengea viwanda vingi chini na kuongeza ajira kwa vijana.
Well said Mkuu, best kaandika maneno mengi lakini hayana substance zaidi tu ya kupiga porojo za ooooh Wachina si watu wazuri, Wachina si watu wazuri...maneno ya mtaani!
 
Mkuu, amini nakuambia, Mchina akikuambia miaka 50 kwenye mkataba kuna kipengele kitasema usiporudisha katika miaka 50 ataichukua kwa miaka 99. Na ukisema hcho kipengele hakifai anakataa kubadili. Hapo bado hajasema anataka usiendeleze Mtwara na Tanga, na usitumie tena ya Dar es Salaam kwa meli za mzizigo toka nje wakati hii bandari ikifanya kazi!

Ebo, mwache arudi China akale majongoo!
Hivi hayo unayoyasema umeyaona wapi wewe, si ni hisia tu unaongelea? Umeona terms za huo mkataba au unapiga tu porojo shehe?
 
Sasa jambo ambalo wewe hujui au kwa kuwa tu hujaona huo ushahidi halifanyi liwe porojo. Huo ni uwezo mdogo wa kufikiri. Mikataba mingapi unafahamu masharti yake? Hata Wabunge walikataliwa kuiona.

Na unafikiri kwamba Watanzania ni wajinga kiasi hicho wakatae tu kitu chenye faida kwao kwa sababu za kilevi tu au uendawazimu fulani? Au unafikiri Magufuli amekataa bandari kujengwa Bagamoyo kwa kuwa anataka ikajengwe Chato kama ile International Airport?

Umeona kilichozitokea nchi zilizokubali masharti ya China kwa miradi hii mikubwa? Waulize hata jirani hapa Kenya

Pia soma hapa

  • Last year, with more than $1 billion in debt to China, Sri Lanka handed over a port to companies owned by the Chinese government. Now Djibouti, home to the US military’s main base in Africa, looks about to cede control of another key port to a Beijing-linked company, and the US is not happy about it.
  • Last Tuesday in Beijing, the Malaysian prime minister, Mahathir Mohamad, announced that his country was canceling two multibillion-dollar Chinese projects because Malaysia can’t repay its debts. “We do not want a situation where there is a new version of colonialism,” Malaysia’s leader told his grim-faced host, Premier Li Keqiang.
  • Sri Lanka was so indebted to China after approving a string of ambitious projects that it was forced last year to lease a port in Hambantota to a Chinese company for 99 years.
  • Pakistan, too, is reportedly to be the site of a Chinese-only community, this one for 500,000, near the port of Gwadar, which China is building as part of its “string of pearls” project to construct ports, possibly for the use of its navy, across the Indian Ocean to Africa.
  • Myanmar is trying to renegotiate a $10 billion port project; Nepal wants to halt construction on two Chinese-built hydroelectric dams. Other nations are so in hock to China that they say little, but things there have already approached a point where analysts believe that debt crises are almost inevitable.

Mkuu angalia kwanza source za taarifa hizi potofu - ni vizuri kuwa makini sana na propaganda zinazo enezwa na MSM for Geopolitics reasons Mara nyingi hazina ukweli wowote.

Mtu ungesema nchi husika zilikwenda Umoja wa Mataifa na kuishtaki Uchina kwamba imewaingiza kwenye mikataba tata hapo ningekuelewa, lakini haya mambo yakubuni tu yenye lengo lakuichafua Uchina siyo fresh hata kidogo - we angalia sources za taarifa hizi utakuta ni: New York times, Washington Post,Reuters, BBC, CNN, Al Jazeera no - Hii inakupa picha gani? Kuwa makini mkuu.
 
Back
Top Bottom