Nakubaliana na hoja ya bandari ya Bagamoyo lakini siyo kwa masharti na ujanja ujanja ya Wachina, ambao si marafiki wa kweli kama mnavyodhani

Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Watu acheni kuongea mambo kwa hisia. Magufuli anafanya mambo mengi kwa mihemuko ya kihisia - na hata anaweza kukutumbua na kukurudisha katika cheo chako ndani ya dakika tano. Lakini kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hapaswi kulaumiwa.

Na kabla hamjaanza kumlaumu mnapaswa kuelewa alichositisha ni nini hasa - ni ujenzi wa bandari au ni ujenzi wa bandari kwa makubaliano yaliyopo kati yetu na China? Nimesikitishwa sana na udhaifu na umbumbumbu wa Ndugai na Bunge katika hili. Na ningekuwa raisi wa nchi hii, huenda ningemuweka ndani Kikwete kwa kosa la uhaini kwa kukubali masharti kama yaliyopo kati yetu na Wachina kwa ajili ya hii bandari na SGR.

Kumbukeni SGR kwa mfano, makubaliano yalikuwa kati ya Tanzania na China. Magufuli aliingia akaupiga chini na kuanza kuingia makubaliano na Uturuki kwa awamu ya kwanza. Mmejiuliza kwa nini?

Nataka niwatahadharishe Watanzania wenzangu. Wachina huwa sio marafiki kama watu wengi wanavyofikiria. Ni wajanja mno. Afrika kwa sasa inapaswa kutambua kwamba hatari ya uhuru wa nchi zake wa kiuchumi na hata kisiasa kwa sasa hailetwi na mataifa ya magharibi, bali inaletwa na China. Hata siku moja usiingie kichwa kichwa ukiwa kiongozi wa nchi katika mkataba na China kwa sababu wanakuja kama marafiki zetu wasioingilia mambo yetu ya ndani. Utajikuta siku moja sehemu ya nchi yako imechukuliwa na waChina, au kufanywa mtumwa wa kiuchumi na kisiasa wa China kwa mamia ya miaka.

Hata wachina kutujengea Makao Makuu ya AU (African Union) pale Addis Ababa, nimewauliza watu, hivi mna uhakika gani kwamba kila neno mnalosema pale ndani ya hizo ofisi, au document mnayoandika, Mchina hawasikilizi na kujua mmeamua nini kata katika vikao vyenu vya siri? Yaani mnachoona ni msaada tu toka China na kupofushwa kiasi hicho?

Magufuli kuna mengi sana sikuungi mkono, lakini kwa hili la kusitisha huu mpango wa kujengewa bandari na SGR na waChina nakupongeza sana. Kuna nchi za Afrika ambazo ziliingia mikataba ya miradi mikubwa na muda mrefu na Wachina na sasa zinajuta na kulia. Acha turudi mezani na kuona ni jinsi gani tunaweza kujenga bandari Bagamoyo bila kuuza nchi na uhuru wetu kwa Wachina.

Kumbuka, Magufuli hajasitisha ujenzi wa bandari Bagamoyo kwa kuwa hataki kujenga bandari Bagamoyo. Amekataa kujenga bandari hiyo kwa masharti yaliyowekwa na Wachina. Aungwe mkono badala ya kulaumiwa, na alaumiwe kwa yanayostahili yeye kulaumiwa, lakini sio hili la bandari.
 
Praetorian

Praetorian

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
7
Points
45
Praetorian

Praetorian

Member
Joined Apr 19, 2019
7 45
Hahaha! Mkuu, yaani B.O.T ni worse than kuwa na loan. Kumbuka kwenye B.O.T una transfer baada ya ku-realize targeted interest, ambayo Wachina huwa wanakuambia Transfer itafanyika baada ya miaka 33 tu.
Unapotosha uma, Pakistan na Uchina wamefanya B.O.T kwenye bandari ya Gwadar kwa muda wa miaka 40 na siyo miaka 33 kama madai yako yanavyosema. Halafu naomba utupe mifano hai ni sehemu gani miradi ya B.O.T inayofadhiliwa na Uchina ikashindwa kufikia malengo na kusababisha matatizo. Ukishindwa kuleta ushahidi basi kama nilivyosema utakuwa ni mpiga porojo tu.
 
uniq

uniq

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
4,651
Points
2,000
uniq

uniq

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
4,651 2,000
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi. Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
Kweli kabisa mimi nasimama na Rais kwa hili. Nilisikia jamaa wanataka kuendesha ile bandari kwa miaka 99 ndio waikabidhi kwa Tz.

Mimi bado nauliza mkataba wa hii bandari si ile mikataba kama tisa hivi ilisainiwa kwa siku moja watu waka uliza kwanini??
Na kukawa na tetesi za mpeleka ngada alie iweka tz rehani??
 
sblandes

sblandes

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2010
Messages
3,571
Points
2,000
sblandes

sblandes

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2010
3,571 2,000
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi. Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
Hakuna haja tujenge wenyewe kama inabidi.
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Hakuna haja tujenge wenyewe kama inabidi.
Kweli kabisa, lakini twende World Bank, au African Development Bank. Ila tatizo, Magufuli alishagombana na World Bank, mambo ya ushoga na haki za binadamu!
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,854
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,854 2,000
Kweli kabisa mimi nasimama na Rais kwa hili. Nilisikia jamaa wanataka kuendesha ile bandari kwa miaka 99 ndio waikabidhi kwa Tz.

Mimi bado nauliza mkataba wa hii bandari si ile mikataba kama tisa hivi ilisainiwa kwa siku moja watu waka uliza kwanini??
Na kukawa na tetesi za mpeleka ngada alie iweka tz rehani??
Sidhani kama ile ilikuwa ni mikataba. Ilikuwa ni makubaliano ya kushirikiana katika mambo hayo tisa. Ila masharti ya Mkataba yalikuja baadae na yakiwa katika harakati za kusainiwa, pamoja na SGR, ndio Magufuli akaipiga chini.
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
2,732
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
2,732 2,000
Sasa nyie mlitaka China awekeze mradi mkubwa kama huo halafu asirudishe hela yake?- Nyie vipi?
Yaani mnapenda vya bure bure tu?
Haya basi msimpe mchina, tafuteni hela zenu wenyewe mjenge, nakuhakikishia in 80 years hamtakuwa na hela ya kujenga hiyo bandari wala hela ya kujenga Economic Zone iliyokuwa imekusudiwa!.
Na Gharama za ujenzi za Dola bilion 10 za Leo za huo mradi miaka 30 ijayo zitakuwa dola bilioni 30!

China sera yake ni WIN-WIN, Siyo akupe mihela yote halafu asiwe na uhakika wa kurudisha hela yake.

Halafu hiyo bandari haiwezi kuua bandari ya Dar, Mkataba hauui bandari ya Dar

Tumezubaa kuchukua hili dili, kesho Mkenya anakwenda kuweka kitu cha maana hapo Lamu, na SGR tayari anayo japo kwa mbinde. Tumeshapigwa gepu la maana na Kenya kwa sababu ya kujivutavuta na umasikini Jeuri
 
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
21,901
Points
2,000
idawa

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
21,901 2,000
Tatizo serikali ya ccm inafanya mambo kwa siri halafu wanalamisha tuunge mkono.

Ifike wakati baada ya mikataba iwekwe wazi wananchi tuijadili kwa kina tujue kwamba tuunge mkono ama la.
 
R

rupa

Member
Joined
Oct 11, 2016
Messages
49
Points
150
Age
28
R

rupa

Member
Joined Oct 11, 2016
49 150
pamoja na kuwaita wazungu mabeberu JPM yuko makini sana na wachina, na ukiangalia kwa makini anawaamini zaidi wazungu/waarabu kuliko wachina na yuko sahihi 100%, china ya leo inataka kufanya kilichofanywa na ufalme wa uingereza miaka 100 iliyopita, kwakifupi wanataka kuigeuza afrika kua koloni lake
Siyo yeye aliyewasifia wachina openly na kuponda wazungu?
 
SueIsmael

SueIsmael

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2013
Messages
430
Points
1,000
SueIsmael

SueIsmael

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2013
430 1,000
Sasa jambo ambalo wewe hujui au kwa kuwa tu hujaona huo ushahidi halifanyi liwe porojo. Huo ni uwezo mdogo wa kufikiri. Mikataba mingapi unafahamu masharti yake? Hata Wabunge walikataliwa kuiona.

Na unafikiri kwamba Watanzania ni wajinga kiasi hicho wakatae tu kitu chenye faida kwao kwa sababu za kilevi tu au uendawazimu fulani? Au unafikiri Magufuli amekataa bandari kujengwa Bagamoyo kwa kuwa anataka ikajengwe Chato kama ile International Airport?

Umeona kilichozitokea nchi zilizokubali masharti ya China kwa miradi hii mikubwa? Waulize hata jirani hapa Kenya

Pia soma hapa

  • Last year, with more than $1 billion in debt to China, Sri Lanka handed over a port to companies owned by the Chinese government. Now Djibouti, home to the US military’s main base in Africa, looks about to cede control of another key port to a Beijing-linked company, and the US is not happy about it.
  • Last Tuesday in Beijing, the Malaysian prime minister, Mahathir Mohamad, announced that his country was canceling two multibillion-dollar Chinese projects because Malaysia can’t repay its debts. “We do not want a situation where there is a new version of colonialism,” Malaysia’s leader told his grim-faced host, Premier Li Keqiang.
  • Sri Lanka was so indebted to China after approving a string of ambitious projects that it was forced last year to lease a port in Hambantota to a Chinese company for 99 years.
  • Pakistan, too, is reportedly to be the site of a Chinese-only community, this one for 500,000, near the port of Gwadar, which China is building as part of its “string of pearls” project to construct ports, possibly for the use of its navy, across the Indian Ocean to Africa.
  • Myanmar is trying to renegotiate a $10 billion port project; Nepal wants to halt construction on two Chinese-built hydroelectric dams. Other nations are so in hock to China that they say little, but things there have already approached a point where analysts believe that debt crises are almost inevitable.
Alipoulizwa Mkurugenzi Mkuu was China Merchant Holdings Group:

"Q: The media have talked a lot about the Hambantota port deal, a 99-year lease signed in July 2017 with the Sri Lankan authorities to address its debt to China after the port did not attract the business to repay the loan. Would this kind of deal be possible in Africa?

A: Our investment in Hambantota is entirely based on commercial considerations. It is a public-private partnership project jointly developed with the port authority of Sri Lanka and has nothing to do with debt relief. At the same time, our investment in Africa is also completely business driven."

Praetorian

Praetorian

Member
Joined
Apr 19, 2019
Messages
7
Points
45
Praetorian

Praetorian

Member
Joined Apr 19, 2019
7 45
Sasa nyie mlitaka China awekeze mradi mkubwa kama huo halafu asirudishe hela yake?- Nyie vipi?
Yaani mnapenda vya bure bure tu?
Haya basi msimpe mchina, tafuteni hela zenu wenyewe mjenge, nakuhakikishia in 80 years hamtakuwa na hela ya kujenga hiyo bandari wala hela ya kujenga Economic Zone iliyokuwa imekusudiwa!.
Na Gharama za ujenzi za Dola bilion 10 za Leo za huo mradi miaka 30 ijayo zitakuwa dola bilioni 30!

China sera yake ni WIN-WIN, Siyo akupe mihela yote halafu asiwe na uhakika wa kurudisha hela yake.

Halafu hiyo bandari haiwezi kuua bandari ya Dar, Mkataba hauui bandari ya Dar

Tumezubaa kuchukua hili dili, kesho Mkenya anakwenda kuweka kitu cha maana hapo Lamu, na SGR tayari anayo japo kwa mbinde. Tumeshapigwa gepu la maana na Kenya kwa sababu ya kujivutavuta na umasikini Jeuri
Waulize kwanini Pakistan ambaye ana mradi kama huu na serikali ya Uchina, tena wa miaka 40 kule Gwadar halalamiki kama wao wanavyolalamika. Tena ameenda mbali zaidi ambapo amemuingiza Saudi Arabia kwenye huo mradi ambapo anajenga Oil Refinery yenye thamani ya zaidi ya Trillioni 20 za kitanzania. Hakuna vya bure siku hizi kwenye hii dunia ya kibepari.
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
2,732
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
2,732 2,000
Waulize kwanini Pakistan ambaye ana mradi kama huu na serikali ya Uchina, tena wa miaka 40 kule Gwadar halalamiki kama wao wanavyolalamika. Tena ameenda mbali zaidi ambapo amemuingiza Saudi Arabia kwenye huo mradi ambapo anajenga Oil Refinery yenye thamani ya zaidi ya Trillioni 20 za kitanzania. Hakuna vya bure siku hizi kwenye hii dunia ya kibepari.
Uko sahihi kiongozi.
Ukiwa na utawala wa kujishukushuku unakuwa unaona unaibiwa tu.
Leo ni miaka 50 ya Uhuru, Kama siyo JK kutujengea angalau terminal III yenye hadhi hapo JKN airport leo tungeenfelea kuwa na terminal yenye jengo la hadhi ya Mini Super Market!!!

Leo tunaona miaka 50 ya mchina kuendesha bandari ni miingi wakati ndani ya muaka hiyi 50 tumeshindwa kujenga shule za kutosha watoto wetu.

Isitoshe hata kama mchina anakusanya yeye hela lazima itakuwepo mechanism ya wao kutugea chetu ikiwemo kodi mbalimbali kama vile VAT etc. Najua Mchina anataka akusanye yeye kwa sababu anajua Bongo rushwa imetamalaki, watu watapitisha mzigo kimagumashi bila kulipa tozo stahiki, kwa hiyo anaona bora akusanye yeye kisha kilicho chetu atupe!. Na pia hii ni Kinga dhidi ya serikali ya bongo kuwacheleweshea malipo yao ya kila mwezi/mwaka.

Miaka 50 kwa taifa siyo mingi!
Tumepoteza Dili la maana sana!!
 
Kamwene

Kamwene

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
1,130
Points
2,000
Age
21
Kamwene

Kamwene

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
1,130 2,000
Watu acheni kuongea mambo kwa hisia. Magufuli anafanya mambo mengi kwa mihemuko ya kihisia - na hata anaweza kukutumbua na kukurudisha katika cheo chako ndani ya dakika tano. Lakini kwa hili la kusitisha ujenzi wa bandari ya Bagamoyo hapaswi kulaumiwa.

Na kabla hamjaanza kumlaumu mnapaswa kuelewa alichositisha ni nini hasa - ni ujenzi wa bandari au ni ujenzi wa bandari kwa makubaliano yaliyopo kati yetu na China? Nimesikitishwa sana na udhaifu na umbumbumbu wa Ndugai na Bunge katika hili. Na ningekuwa raisi wa nchi hii, huenda ningemuweka ndani Kikwete kwa kosa la uhaini kwa kukubali masharti kama yaliyopo kati yetu na Wachina kwa ajili ya hii bandari na SGR.

Kumbukeni SGR kwa mfano, makubaliano yalikuwa kati ya Tanzania na China. Magufuli aliingia akaupiga chini na kuanza kuingia makubaliano na Uturuki kwa awamu ya kwanza. Mmejiuliza kwa nini?

Nataka niwatahadharishe Watanzania wenzangu. Wachina huwa sio marafiki kama watu wengi wanavyofikiria. Ni wajanja mno. Afrika kwa sasa inapaswa kutambua kwamba hatari ya uhuru wa nchi zake wa kiuchumi na hata kisiasa kwa sasa hailetwi na mataifa ya magharibi, bali inaletwa na China. Hata siku moja usiingie kichwa kichwa ukiwa kiongozi wa nchi katika mkataba na China kwa sababu wanakuja kama marafiki zetu wasioingilia mambo yetu ya ndani. Utajikuta siku moja sehemu ya nchi yako imechukuliwa na waChina, au kufanywa mtumwa wa kiuchumi na kisiasa wa China kwa mamia ya miaka.

Hata wachina kutujengea Makao Makuu ya AU (African Union) pale Addis Ababa, nimewauliza watu, hivi mna uhakika gani kwamba kila neno mnalosema pale ndani ya hizo ofisi, au document mnayoandika, Mchina hawasikilizi na kujua mmeamua nini kata katika vikao vyenu vya siri? Yaani mnachoona ni msaada tu toka China na kupofushwa kiasi hicho?

Magufuli kuna mengi sana sikuungi mkono, lakini kwa hili la kusitisha huu mpango wa kujengewa bandari na SGR na waChina nakupongeza sana. Kuna nchi za Afrika ambazo ziliingia mikataba ya miradi mikubwa na muda mrefu na Wachina na sasa zinajuta na kulia. Acha turudi mezani na kuona ni jinsi gani tunaweza kujenga bandari Bagamoyo bila kuuza nchi na uhuru wetu kwa Wachina.

Kumbuka, Magufuli hajasitisha ujenzi wa bandari Bagamoyo kwa kuwa hataki kujenga bandari Bagamoyo. Amekataa kujenga bandari hiyo kwa masharti yaliyowekwa na Wachina. Aungwe mkono badala ya kulaumiwa, na alaumiwe kwa yanayostahili yeye kulaumiwa, lakini sio hili la bandari.
Ningependa kujua tu kuwa hayo masharti ni yap? Maana nasoma tu masharti, masharti ni masharti yepi?
 
Kamwene

Kamwene

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
1,130
Points
2,000
Age
21
Kamwene

Kamwene

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
1,130 2,000
Kwa kifupi wanataka katika mazingira fulani waendeshe wao ile bandari, na kukusanya mapato yote wala TRA wasiguse pale. Pia wanataka ukanda mkubwa zaidi wa kuwekeza pale, wajenge majengo yao ya kuishi na biashara na maofisi. Pia wanataka wawekezaji wa lile eneo wawe wanawaruhusu wao pamoja na nani akubaliwe nani akataliwe kuwekeza lile eneo. Yote hayo wafanye hadi fedha yao irudi, bila kuingiliwa. Na pia wanataka ile iwe ndio bandari kuu pekee Tanzania, iwe marufuku kuziendeleza bandari za Tanga, Mtwara na hata Zanzibar ikiwezekana. Kwa kifupi, lile eneo liwe "Small China country".

Sasa niambie Raisi gani mwenye akili atakubali vitu kama hivyo? Halafu kina Ndugai na Bunge lake dhaifu wanasema afadhali tuache SGR waChina watujengee bandari - kwa masharti hayo?
Alaaa kumbe waambie watapata taabu sana dadeq
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
15,283
Points
2,000
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
15,283 2,000
Najua Mchina anataka akusanye yeye kwa sababu anajua Bongo rushwa imetamalaki, watu watapitisha mzigo kimagumashi bila kulipa tozo stahiki, kwa hiyo anaona bora akusanye yeye kisha kilicho chetu atupe!. Na pia hii ni Kinga dhidi ya serikali ya bongo kuwacheleweshea malipo yao ya kila mwezi/mwaka.
Mchina eti sio mwizi nenda Kenya wachina ndio hakusanya mapato ya SGR. Serikali ya Kenya haina hamu na mapato kukusanyea na mchina. Kenya wachina wamewaibia mamilioni ya dola ya mauzo ya tiketi za SGR za abiria na mizigo kupitia mfumo wao wa kukusanya mapato. Chezea mchina wewe.
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
2,732
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
2,732 2,000
Mchina eti sio mwizi nenda Kenya wachina ndio hakusanya mapato ya SGR. Serikali ya Kenya haina hamu na mapato kukusanyea na mchina. Kenya wachina wamewaibia mamilioni ya dola ya mauzo ya tiketi za SGR za abiria na mizigo kupitia mfumo wao wa kukusanya mapato. Chezea mchina wewe.
Sasa kama Wakenya wanajua wameibiwa na ushahidi wanao si waende mahakamani, maana wizi siyo sehemu ya mkataba kuibiana.

Sema kuna baadhi ya Wakenya watakuwa wanashirikiana na baadhi ya wachina kuiba, na hilo siyo kosa la Serikali ya China
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
15,283
Points
2,000
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
15,283 2,000
Sasa kama Wakenya wanajua wameibiwa na ushahidi wanao si waende mahakamani, maana wizi siyo sehemu ya mkataba kuibiana.

Sema kuna baadhi ya Wakenya watakuwa wanashirikiana na baadhi ya wachina kuiba, na hilo siyo kosa la Serikali ya China
Akumulikaye mchana usiku akuchoma Yaani SGR kenya ile kuanza Ku operate tu wachina wakaanza kuiba direct from day one ya kukusanya mapato ya SGR kenya
 
Forum statistics

Threads 1,295,450
Members 498,335
Posts 31,212,482
Top