Nakerwa na wananchi wa Kanda ya Ziwa

Nakerwa na wananchi wa Kanda ya Ziwa

Kanda ya ziwa ndio yenye ushawishi , lazima ukombozi uanzie lakezone kwa kishindo
No! Ukombozi hauwezi kuanzia huko, wamelala mno. Migodi yote mikubwa iko kwao, mifugo mingi iko kwao, mbuga maarufu iko kwao, samaki wa export wapo kwao, lakini bado tu hawajaamka! Wana kila rasilimali inayotakiwa kwa ukombozi, kasoro kitu moja tu.
 
Pamoja na ukweli kwamba kwa miaka yote tangu uhuru mpaka sasa watu ya kanda ya ziwa wamekuwa wakikandamizwa na kunyimwa elimu, bado kundi hili kubwa limeendelea kukumbatia chama ambacho kimekuwa sababu ya umasikini mkubwa kwa wengi katika eneo hilo.
- Kwa miaka yote Serikali ilihakikisha kuwa shule za Sekondari zinabakia chache ili vijana wasipate elimu
- Serikali ikaweka mkakati wa makusudi ili eneo hilo lisipewe Chuo Kikuu cha Serikali.....
Palikuwa na sababu gani kuvipanga Vyuo Vikuu.. Dar... Morogoro... Dodoma? Kwa nini kimoja kisingekwenda kanda Ya ziwa?
- Kwa makusudi Serikali ikaweka mikakati kuhakikisha mazao ya biashara kanda ya ziwa yanapata bei za kusuasua ili wananchi wawe hoi kiuchumi....

Imefika wakati wa kila mtu kutumia alicho nacho. Kanda ya ziwa amkeni sasa na mtumie wingi wenu kwa maslahi yenu.
Anayekuja huko kutaka uraisi, kwanza ajibu swali ataifanyia nini kanda hiyo inayoibiwa mali kila kukicha na wajanja janja wanaocheka cheka tu....?
Zungusha macho na uone ni mali kiasi gani zinatoka Kanda ya ziwa na manufaa yake ni nini?

KWA KWELI NINYI WA KANDA YA ZIWA MNANIKERA....

Hivi mtachezewa chezewa mpaka lini? Mtakanyagwa kanyagwa mpaka lini? Mtaibiwa ibiwa mpaka lini? Mtadanganywa danganywa mpaka lini?
NASEMA TENA: MNANIKERA.......................EBOOOOOOO....
We "omerah" acha hizo bhana!
 
Kwa Afrika ... It's not the vote that count ... It's who count the votes ... Hata Kama watachagua CDM 2015 , kkama Hakuna Tume Huru ya Uchaguzi ... Tegemea Maumivu na kukereka zaidi ... Mark my word!!!

Nachofahamu mimi ni silaha ya mnyonge umoja,2kiamua nani awe kiongozi atakuwa tuu.
 
hapo heading inatoa picha ya ukabila na ukanda.mbona wapo wasomi wengi tu kutoka kanda ya ziwa kwani chuo kiki dsm ni kwa ajili ya wazaramo au hospital ya bugando ni kwa ajili ya wasukuma .wanao kwenda kusoma nje wanatakiwa waishi/kukulia air port
Wewe mkwapua simu, kwani bungando ni ya serikali? wasukuma wameonewa sana ifike wakati waseme basi yatosha...maji ya kunywa shida, usafiri shida, shule shida, wakilima vipamba vyao mnawapangia bei bila kujari gharama walizotumia, dawa za mifugo tabu tupu, aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaagh!!!!! wasukuma wenzangu amkeni acheni upimbi
 
Hamjamaliza la udini mnatuletea la ukabila, ptuuu
Hahahah! Bado unatamani kufika Mwanza kupitia Nairobi ati! Iringa wameshaondoa lami ya zamani na kuweka mpya, ilhali Mtwara-Dar hapajapata kuwa na lami kwa kilometa zote. Wote Iringa na Mtwara wanalipa kodi. Bila kuishtua hii serikali mambo hayaendi.
 
No! Ukombozi hauwezi kuanzia huko, wamelala mno. Migodi yote mikubwa iko kwao, mifugo mingi iko kwao, mbuga maarufu iko kwao, samaki wa export wapo kwao, lakini bado tu hawajaamka! Wana kila rasilimali inayotakiwa kwa ukombozi, kasoro kitu moja tu.
Walinyiwa elimu mkuu, kuna kipindi mkoa wa shy na ukubwa wake wote ulikuwa na sekondari kama kumi tu hivi na nimiaka ya 90 sasa pata picha hapo watoto wanasoma au wanachunga ngombe tu na wakike wakifikisha miaka 15 ni kuolewa tu...
 
Majibu ya swali lako utayapata 2015,tumechoka kuongea
 
fikiri vizuri kama wewe si mwenyeji wa huko huna uchungu wowote wanaoupata vijana na wakazi wa kanda ya ziwa,hivyo unapochangia utumie akili badala ya kuropoka.
Pointi muhimu sana! Kwa nini kanda ya ziwa wapangiwe bei ya kuuziwa pamba kwenye soko huria? Waache soko lipange bei.
 
Hahahah! Bado unatamani kufika Mwanza kupitia Nairobi ati! Iringa wameshaondoa lami ya zamani na kuweka mpya, ilhali Mtwara-Dar hapajapata kuwa na lami kwa kilometa zote. Wote Iringa na Mtwara wanalipa kodi. Bila kuishtua hii serikali mambo hayaendi.
Mkuu kwa historia ya nchi hii mikoa ya kanda ya ziwa ilipaswa kuwa juu sana angalau kwenye vitu mhimu kama barabara na elimu kumbuka kilimo cha pamba, madini, mbuga za wanyama, samaki...
 
Mtuwache tupumue, hatunaa akili za kushikiwa kama akina fulani.

Kuchochewa tu muandamane wee afu mnakufaa nyie wakati wenzenu wanakunywa kideri na lushoro.

Kama chuo st agustine ipo.
Hujui unacho kiongea unalopoka tu bora ukae kimya kama hujui watu wa kanda ya ziwa wanavyo pigika...
 
Ukabila na Udini nyie mtauacha lini?!!!
Yaani wewe watu wakihoji mambo mhimu ya maisha yao wewe unasema ukabila na udini..kama ukabila ndiyo ulivyo acha tuwe wakabiala na si tunataka lami mpaka vichochoroni kama kilimanjaro eboooo...
 
Hakuna ukabila hapo,kama unadhani kuna ukabila, yataje ni makabila mangapi anayazungumzia
 
Kaka Johson Alex OTIENO... chaguzi ni very trick... umoja ndio... lakini wa TZ tumegawanywa na njaa na uwoga... ni rahisi sana kwa Tume ya Uchaguzi kuchakachua kura na bado pasiwe na umoja wa kupambana nao....

Tukubali tu bila TUME HURU ... CHADEMA haina kitu 2015.

Nachofahamu mimi ni silaha ya mnyonge umoja,2kiamua nani awe kiongozi atakuwa tuu.
 
Pamoja na ukweli kwamba kwa miaka yote tangu uhuru mpaka sasa watu ya kanda ya ziwa wamekuwa wakikandamizwa na kunyimwa elimu, bado kundi hili kubwa limeendelea kukumbatia chama ambacho kimekuwa sababu ya umasikini mkubwa kwa wengi katika eneo hilo.
- Kwa miaka yote Serikali ilihakikisha kuwa shule za Sekondari zinabakia chache ili vijana wasipate elimu
- Serikali ikaweka mkakati wa makusudi ili eneo hilo lisipewe Chuo Kikuu cha Serikali.....
Palikuwa na sababu gani kuvipanga Vyuo Vikuu.. Dar... Morogoro... Dodoma? Kwa nini kimoja kisingekwenda kanda Ya ziwa?
- Kwa makusudi Serikali ikaweka mikakati kuhakikisha mazao ya biashara kanda ya ziwa yanapata bei za kusuasua ili wananchi wawe hoi kiuchumi....

Imefika wakati wa kila mtu kutumia alicho nacho. Kanda ya ziwa amkeni sasa na mtumie wingi wenu kwa maslahi yenu.
Anayekuja huko kutaka uraisi, kwanza ajibu swali ataifanyia nini kanda hiyo inayoibiwa mali kila kukicha na wajanja janja wanaocheka cheka tu....?
Zungusha macho na uone ni mali kiasi gani zinatoka Kanda ya ziwa na manufaa yake ni nini?

KWA KWELI NINYI WA KANDA YA ZIWA MNANIKERA....

Hivi mtachezewa chezewa mpaka lini? Mtakanyagwa kanyagwa mpaka lini? Mtaibiwa ibiwa mpaka lini? Mtadanganywa danganywa mpaka lini?
NASEMA TENA: MNANIKERA.......................EBOOOOOOO....

you are not serious,,,,,,wahaya,wakerewe,wajita ni kati ya makabila yanayotoa wasomi wa kutegemewa nchini,,wasukuma wanashikila judiciary na wahaya,,,wakurya hawako nyuma,,,nadhani kama tunakukera itabidi tujitenge tuwa nchini na tubaki na robo tatu ya pato la taifa tunalochangia,migodi yetu,serengeti inayoongoza kwa watalii,,ziwa victoria,ardhi yenye rutuba na mashujaa waliojaa jeshini pia wasomi wote wa wahaya,wakerewe,wajita na wasukuma,,,,
 
Ni kweli Kanda ya Ziwa wanaonewa na kudhulumiwa na serikali. hebu fikiria, kule kanda ya ziwa kuna karibu kila aina ya utajiri.

  • [*=1]1. Nguvukazi ( asilimali watu )
    [*=1]2.Madini ( Dhahabu, Almasi )
    [*=1]3. Ziwa ( Bandari na samaki)
    [*=1]4.Utalii ( Serengeti, Rubondo )

Na mengine mengi yenye kuweza kumnufaishi mkazi wa kanda ya ziwa. lakini sasa imekuwa kinyume serikali inabeba kila kitu na wananchi wanabaki na umaskini wa kutupwa. mfano badala ya samaki iwanufaishe wakazi wa Mwanza kiuchumi na kiafya , wamekuwa wakibakishiwa mifupa tu ya mapanki, huku samaki zikienda Russia na kuwanufaisha wahindi tu wanaomiliki fisheries hapo .

Ukija upande wa Madini huko Geita , dhahabu imeshindwa kabisa kumnufaisha mzawa wa Geita , zaidi ya kusikia wakifukuzwa kila mara hata kwenye machimbo madogo waliyoanzisha. na hii ni tamaa ya CCM ya kushindwa kutosheka na kutaka kumnyanganya mtanzania hata kidogo alichonacho. Ukienda Geita miundombinu. Huduma ya Afya iko Chini. kiujumla sioni ambacho kinafanya na serikali ya CCM katika kumwezesha mtanzania wa kawaida ili aweze kunufaika na rasilimali zinazomzunguka. Miundombinu mingi iliyopo kanda ya ziwa ni ile aliyoacha mkoloni, mfano ni MV Victoria pamoja na reli ya kati. shule asilimia nyingi ni zile walizoacha wakoloni ama zilizojengwa na wamisionari.

na serikali bila kujali hilo, wao ndio wanazidi kuuchuma utajiri wa Kanda ya ziwa na kuuhamishia dar es salaam huku wazawa wa Kanda ya ziwa wakiachwa weupe.
kwani ni lazima kila kitu kiwe Dar es salaam?. kama Kanda ya ziwa inafuata baada ya Dar es salaam kwa kuwa na idadi kubwa ya watu , ni kwanini wasipewe vipaumbele pia?. kama kanda ya ziwa inaongoza kwa kulipa kodi baada ya dar es salaam, ni kwanini wasipatiwe huduma zote maalumu?
Nasema kwamba Kanda ya ziwa imebakwa na kunyanyaswa kiuchumi. Kanda ya ziwa inatakiwa ikombolewe kutoka katika makucha ya CCM, iwe kesho , mwaka kesho ama kutwa , kwa mwenye mapenzi na Kanda hii asisubiri 2015 ili aanze jitihada za kuikomboa kanda ya ziwa, Ukombozi unaanza leo. Vijana wa Kanda ya Ziwa acheni kulala.
 
Wacha ukweli usemwe. Hajasema kabila lolote hapa. viongozi na wabunge toka enzi za TANU na baadae CCM hawajawahi kutetea kanda ya ziwa ambapo idadi ya watanzania ni kubwa kuwarahisishia maendeleo yao kikanda. Tupo mbali na viwanda vya cement na vifaa vyakujengea lakini hata siku moja watu waccm hawajaona kama kuna haja ya serikali kuwapunguzia mzigo wakuvisafirisha ili vikapungua bei vifikapo huko. usafiri wa Gari moshi ulio kuwa nafuu matajiri waccm wameuangamiza ili watufikishie bidhaa kwa usafiri wa magari kwa faida kubwa, Muone hata Magufuli anakazana na kutengeneza barabara tu, je huwa akai katika baraza la mawaziri na akatetea train? ili tukapata mizigo kanda ya ziwa ikiwa ina bei nafuu?(kila kitu bei ipo juu tofauti na Dar, Moro, Tanga, Dodoma, Arusha, Mbeya, zanzibar, Nk kutokana na kusafirishwa mbali na viliko viwanda) wanaposhindwa kututolea ruzuku ya kuvisafirisha kwa nini hawaweki mkakati wa kuvijenga hukohuko kanda ya ziwa? (Mwanza, Musoma,Kagera) au jirani na hapo (tabora, Kigoma Singida, nk)
Kama sio kanisa la Katoriki kutusaidia tukapata Hospitali ya Bugando na Chuo kikuu cha sauti, pamoja na ukubwa wa kiuchumi ulioko huko kanda hii ingekuwaje sijui sisi ni watoto wa nani. Kwa kuwa sasa ccm imeshindikana kututoa katika karne ya 47, ngoja tuijaribu cdm huenda ikatuingiza katika ulimwengu wa digitali tukiwa salama. Mwanza, Musoma wameishaliona hilo na shinyanga. Kagera wameanza hasa Bukoba mjini na Karagwe. Kigoma wao wana ngwe ya kwao ni safi kabisa. Jirani zetu Tabora wamelala, sijui kwa nini hawalioni hili! Bado ninaamini ukombozi wa chi hii utaanzia kanda ya ZIWA>

Jamani tuwe makini, mi nadhani upole wa hawa jamaa wa kanda ya ziwa umesaidia nchi yetu kuendelea kuwa na amani. Nasema hivyo kwa sababu mwaka juzi 2011 wakati wa bajeti nilifuatilia mjadala wa wizara ya Nishati na Madini nikasikiliza jinsi Mbunge Ma Malecela alivyomshambulia Ngeleja eti kisa alikuwa ametenga bajeti ya vijiji 9 jimboni kwake! hoja hapa ni je hao wananchi wa jimbo la waziri hawakuwa wanastahili umeme au vipi? Ingekuwa vipi kama wanalake zone nao wangekuwa wanahoji why wao barabara zao, reli yao ni mbofumbofu tu, pamba yao iliyotelekezwa na Serikali kwa miaka mingi sasa wakati tunafahamu kabsa nchi hii kuna maeneo wanaishi next level kwa sababu tu viongozi wao walifanya upendeleo wa mgao wa rasilimali fedha!
 
Hivi ule mpango wa chuo cha Mwl Nyerere uliishia wapi? Au Katavi University of Agriculture imenyakua meager resources meant for Nyerere University of Agriculture Butiama?
 
Jamani tuwe makini, mi nadhani upole wa hawa jamaa wa kanda ya ziwa umechangia kuwepo kwa amani ya nchi yetu. Ni kweli wamenyanyasika kiasi cha kutosha katika levels mbalimbali. Mfano mwaka juzi 2011 wakati wa mjadala bajeti ya Nishati na Madini nilimsikia Ma Malecela akimlalamikia Ngeleja eti kisa Ngeleja alikuwa ametenga bajeti ya umeme kwa vijiji 9 jimboni kwake. Sasa hoja hapa ni je kwani hao wananchi wa jimbo la waziri Ngeleja hawakustahili kupata hiyo huduma ya umeme vijijini kamac wanavyopata wengine. Nini vijiji 9 bana, mbona sote tuna fahamu jinsi baadhi ya mikoa nchini ilivyonufaika kutokana na upendeleo wa viongozi waliokuwa madarakani tangu tupate uhuru!

Kwa hiyo tusiwabeze watu wa lake zone, hao wakiamka na kuamua hakuna wa kuwazuia kukamata nchi hii!
 
Back
Top Bottom