Nakerwa na wananchi wa Kanda ya Ziwa

Nakerwa na wananchi wa Kanda ya Ziwa

Oikos

Senior Member
Joined
May 5, 2011
Posts
198
Reaction score
111
Pamoja na ukweli kwamba kwa miaka yote tangu uhuru mpaka sasa watu ya kanda ya ziwa wamekuwa wakikandamizwa na kunyimwa elimu, bado kundi hili kubwa limeendelea kukumbatia chama ambacho kimekuwa sababu ya umasikini mkubwa kwa wengi katika eneo hilo.
- Kwa miaka yote Serikali ilihakikisha kuwa shule za Sekondari zinabakia chache ili vijana wasipate elimu
- Serikali ikaweka mkakati wa makusudi ili eneo hilo lisipewe Chuo Kikuu cha Serikali.....
Palikuwa na sababu gani kuvipanga Vyuo Vikuu.. Dar... Morogoro... Dodoma? Kwa nini kimoja kisingekwenda kanda Ya ziwa?
- Kwa makusudi Serikali ikaweka mikakati kuhakikisha mazao ya biashara kanda ya ziwa yanapata bei za kusuasua ili wananchi wawe hoi kiuchumi....

Imefika wakati wa kila mtu kutumia alicho nacho. Kanda ya ziwa amkeni sasa na mtumie wingi wenu kwa maslahi yenu.
Anayekuja huko kutaka uraisi, kwanza ajibu swali ataifanyia nini kanda hiyo inayoibiwa mali kila kukicha na wajanja janja wanaocheka cheka tu....?
Zungusha macho na uone ni mali kiasi gani zinatoka Kanda ya ziwa na manufaa yake ni nini?

KWA KWELI NINYI WA KANDA YA ZIWA MNANIKERA....

Hivi mtachezewa chezewa mpaka lini? Mtakanyagwa kanyagwa mpaka lini? Mtaibiwa ibiwa mpaka lini? Mtadanganywa danganywa mpaka lini?
NASEMA TENA: MNANIKERA.......................EBOOOOOOO....
 
Acheni ukabila, hautawafikisha popote.
 
Kwa Afrika ... It's not the vote that count ... It's who count the votes ... Hata Kama watachagua CDM 2015 , kkama Hakuna Tume Huru ya Uchaguzi ... Tegemea Maumivu na kukereka zaidi ... Mark my word!!!
 
Wacha ukweli usemwe. Hajasema kabila lolote hapa. viongozi na wabunge toka enzi za TANU na baadae CCM hawajawahi kutetea kanda ya ziwa ambapo idadi ya watanzania ni kubwa kuwarahisishia maendeleo yao kikanda. Tupo mbali na viwanda vya cement na vifaa vyakujengea lakini hata siku moja watu waccm hawajaona kama kuna haja ya serikali kuwapunguzia mzigo wakuvisafirisha ili vikapungua bei vifikapo huko.

Usafiri wa Gari moshi ulio kuwa nafuu matajiri waccm wameuangamiza ili watufikishie bidhaa kwa usafiri wa magari kwa faida kubwa, Muone hata Magufuli anakazana na kutengeneza barabara tu, je huwa akai katika baraza la mawaziri na akatetea train? ili tukapata mizigo kanda ya ziwa ikiwa ina bei nafuu?(kila kitu bei ipo juu tofauti na Dar, Moro, Tanga, Dodoma, Arusha, Mbeya, zanzibar, Nk kutokana na kusafirishwa mbali na viliko viwanda) wanaposhindwa kututolea ruzuku ya kuvisafirisha kwa nini hawaweki mkakati wa kuvijenga hukohuko kanda ya ziwa? (Mwanza, Musoma,Kagera) au jirani na hapo (tabora, Kigoma Singida, nk)


Kama sio kanisa la Katoriki kutusaidia tukapata Hospitali ya Bugando na Chuo kikuu cha sauti, pamoja na ukubwa wa kiuchumi ulioko huko kanda hii ingekuwaje sijui sisi ni watoto wa nani. Kwa kuwa sasa ccm imeshindikana kututoa katika karne ya 47, ngoja tuijaribu cdm huenda ikatuingiza katika ulimwengu wa digitali tukiwa salama. Mwanza, Musoma wameishaliona hilo na shinyanga. Kagera wameanza hasa Bukoba mjini na Karagwe.

Kigoma wao wana ngwe ya kwao ni safi kabisa. Jirani zetu Tabora wamelala, sijui kwa nini hawalioni hili! Bado ninaamini ukombozi wa chi hii utaanzia kanda ya ZIWA>
 
Kanda ya ziwa ndio yenye ushawishi , lazima ukombozi uanzie lakezone kwa kishindo
 
Mtuwache tupumue, hatunaa akili za kushikiwa kama akina fulani.

Kuchochewa tu muandamane wee afu mnakufaa nyie wakati wenzenu wanakunywa kideri na lushoro.

Kama chuo st agustine ipo.
 
Mleta uzi!nia na madhumuni yako si mazuri,huo umimi na ukanda unaojaribu kuusimamisha uishie hapo hapo,tengenezi huu uzi uje kwa mtazamo wa kujadilika.

BATTER AN UGLY FACE THAN UGLY MIND!!
 
Hakuna watu wanaoweza kuonewa milele hivyo siku za mabadiliko haziko mbali lakini siyo kanda ya ziwa ila nchi nzima
 
hapo heading inatoa picha ya ukabila na ukanda.mbona wapo wasomi wengi tu kutoka kanda ya ziwa kwani chuo kiki dsm ni kwa ajili ya wazaramo au hospital ya bugando ni kwa ajili ya wasukuma .wanao kwenda kusoma nje wanatakiwa waishi/kukulia air port
 
Unaamini katika 'end justify means?'
Bila kujali process nzima?

inabidi kuangalia process nzima lakini mchizi kaongea fact.

Lakini kwanini vitu viwe vinalundikana ukanda mmoja, wakati kuna kanda zingine.

Sasa watu wakiongea fact mnakimbilia huo ni ukabila, acheni watu waongee fact.

Sera za majimbo naona zinafaa zaidi.
 
Ukifika Musoma utashangaa kwa kweli utadhani hawakuwahi kutoa mwenye heshima Duniani na Mbinguni .I think is about time.Bugando mjumbe mmoja kasema ni hosp ya Kanisa katoliki na si serikali .
 
inabidi kuangalia process nzima lakini mchizi kaongea fact.

Lakini kwanini vitu viwe vinalundikana ukanda mmoja, wakati kuna kanda zingine.

Sasa watu wakiongea fact mnakimbilia huo ni ukabila, acheni watu waongee fact.

Sera za majimbo naona zinafaa zaidi.


Tuko mikoa zaidi ya sita yenye watu wengi,madini,samaki,mazao ya biashara hivi kwanini tusijitoe Tanzania tuanzishe nchi yetu? Tuna uwanja wa ndege mwanza tunaweza wasitufanye wapuuzi kwamba wao ndio wajanja saa hivi wanajenga bandari kwao kwa pesa za wananchi lakini Ziwa hamna kitu huu ni upuuzi
 
Huo ni mtaji wa CCM wakiwa maskini na hawana elimu ni rahisi kumpa chumvi, kanga, kofia au tishet na wanaonekana wamepewa zawadi kuuuubwa, inawezatokea mtu mwaka mzm hajapata hela ya kununulia nguo mpya so akipewa kanga moja bure atakulamba hata nyayo. Huwezi kumhonga chumvi mtu anayejiwezza na kujitambua thats why CCM hawataki tulemimike.
 
Ukifika Musoma utashangaa kwa kweli utadhani hawakuwahi kutoa mwenye heshima Duniani na Mbinguni .I think is about time.Bugando mjumbe mmoja kasema ni hosp ya Kanisa katoliki na si serikali .


Siyo kasema ni ya Kanisa ile Hospitali ni ya Rc serikali wanachangia kidogo mno kiuendeshaji sasa hebu tujiulize pesa za madini,samaki,mazao ya biashara zinatumika wapi? Mbona naona hazwasaidii watu wa Ziwa?
Kuna mradi gani wa serikali ulioko kanda ya ziwa? Wana mpango watu wa kanda ya ziwa wasisome? Mikoa sita hamna chuo kikuu cha Serikali? Hawa wanalengo lao si bure
 
Back
Top Bottom