Nakerwa na wananchi wa Kanda ya Ziwa

Nakerwa na wananchi wa Kanda ya Ziwa

Mumewaachia michwa wa CCM wawafanye watakavyo na mali zenu kwa sababu ya kuwa na madiwano wa kasorobo matokeo yake halmashauri hazipati pesa inayosthili kufanya maendeleo lakini kwa umuhimu wa mchango wa kiuchumi basi vipaumbele kama angalau chuo kikuu kimoja uwanja wa ndege wenye hadhi na bandari yenye hadhi ,yaani nyie hata vivuko tuu ni taabu sasa wapi mutajiokoa changamkeni CCM ni wakusukuma tu ,walishindwa kujenga malambo yakunyweshea mifugo wasukuma waache kutangatanga nchi nzima wakitafuta malisho huku kila siku wakipambana na wakulima
 
you are not serious,,,,,,wahaya,wakerewe,wajita ni kati ya makabila yanayotoa wasomi wa kutegemewa nchini,,wasukuma wanashikila judiciary na wahaya,,,wakurya hawako nyuma,,,nadhani kama tunakukera itabidi tujitenge tuwa nchini na tubaki na robo tatu ya pato la taifa tunalochangia,migodi yetu,serengeti inayoongoza kwa watalii,,ziwa victoria,ardhi yenye rutuba na mashujaa waliojaa jeshini pia wasomi wote wa wahaya,wakerewe,wajita na wasukuma,,,,
Nani aliyekwambia kanda ya ziwa inachangia robo tatu ya pato la taifa?
 
wasomi wa kand ya ziwa wanapenda kukaa kwenye mataa yajij la dsm.hawajui kuwa kwao kunaoza.wakifa ndo utuletea maiti.
 
Kanda ya ziwa imekuwa na watu wasio na njozi zozote.Imebaki ni kutahiri mabinti, UCHAWI, KUTETEMEKEA VIONGOZI WANAFIKI, na kula mabaki ya samaki achilia mbali wazungu kuua wana mara wanapokatiza mbugani.ITS SHAME KWA KWELI-UMEFIKA WAKATI WA KUAMKA SASA,AMKENI WANA KANDA YA ZIWA.
HATA WABUNGE WETU NI WALE WANAOSINZIA SINZIA BUNGENI. LOO,MUNGU ATUREHEMU WANA KANDA YA ZIWA victoria.
 
Mleta hoja umenena. Napenda kuunga mkono hoja kwa aslimia 100+!

Ni dhahiri kuwa kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza,Mara,Shinyanga,Tabora,Kagera,Kigoma na mkoa mpya wa Simiyu imeonewa,iimepuuzwa,imenyonywa na imenyanyaswa kiasi cha kutosha tangu enzi za Mwalimu Nyerere.Ujinga,Unyonge na Upole wa watu hawa ndiyo umewafanya waonewe,wanyonywe na wanyanyaswa kiasi cha kutosha.Ukweli na Uwazi!

Kijiografia Mikoa hii ina utajiri wa raslimali za asili ambazo Mwenye enzi Mungu aliziweka kwa maksudi maalumu. Lakini kutokana na wajanja wachache,waroho na wenye tamaa ya madaraka katika nchi hii Mikoa ya Kanda ya Ziwa ndiyo imeendelea kushikilia mkia katika nyaza za Kielimu,Kiuchumi na Kiutawala!!!

Mpaka leo huwa najiuliza kwanini Mwalimu J.K.Nyerere(RIP) akiwa mwasisi wa Taifa hili alishindwa kuchukua hatua za maksudi za kuiendeleza Kanda hii kuanzia Kielimu,Kiuchumi na Kiutawala.Badala yake aliamua kuwaweka pembeni ndugu zake wa Kanda ya Ziwa na kuelekeza nguvu zake kwa kanda zingine kama Pwani,Kaskazini,Kusini na Nyanda za Juu.

Niliwahi kuambiwa na wazee wa kisukuma kuwa Washashi(Jamii ya Wazanaki,Wailkizu,Wakurya n.k.)wana kawaida ya choyo. Hivyo Nyerere akiwa Mzanaki alichukua asili ya uchoyo na kuamua kuwanyanyasa Wasukuma ambalo ndilo kabila kubwa kuliko yote Kanda ya Ziwa na Tanzania yote kwa ujumla. Niliambiwa kwamba Nyerere alikuwa anajua nguvu ya kabila ya Wasukuma kama kabila kuwa wakielemika na kuwa na nguvu ya Kiuchumi basi utawala wake ungelikuwa mashakani! Kwa hiyo Nyerere akaamua kutumia njia chafu za KIKOLONI za DEVIDE&RULE na DO NOT EDUCATE THEM yaani wagawanye uwatawale na uwanyima elimu!!

Hakika Nyerere alifanikiwa katika hilo maana Mzanaki huyu alihakikisha shule za sekondari zinajengwa chache sana na hakukuwa na Chuo Kikuu hata kimoja mpaka Nyerere alipoiaga dunia. Shule za sekondari Kanda ya Ziwa zilikuwa za kuhesabu moja moja ukilinganisha na kanda zingine kama Kaskazini. Nakumbuka kulikuwa na sekondari chache kama Kahororo, Bwiru Boys& Girls,Shybush/com,Tabora Boys,Mara Sek,Musoma Alliance na Tarime Girls, basi!!Ilhali ukilinganisha na Kanda kama Kasakazini mkoa wa Kilimanjaro peke yake ulikuwa na zaidi ya sekondari 50!Kwa kweli hapa Nyerere hakuwatendea haki watu wa Kanda ya Ziwa na alijua kile alichokuwa amekipanga.

Kuna viongozi muhimu waliokuwa wanainukia toka Kanda ya Ziwa lakini Nyerere alihakikisha hao jamaa hawafurukuti na mara nyingi alitumia mbinu za kuwaweka ndani au kuwapeleka nje ya nchi kuwa mabalozi wa kudumu. Kuna mifano hai kama kina Bomanis Family:Marehemu Paulo Bomani,Emanuel Bomani,Judge Mark Bomani. Paulo Bomani akiwa kiongozi wa chama cha Wakulima chenye nguvu-Nyanza Federation alijikuta akipewa Ubalozi wa kudumu huko Marekani mpaka watu wakamsahau. Jaji Mark Bomani alianza kama Mwanasheria Mkuu wa Tanzania miaka ya 1960s lakini Nyerere alipoona anaanza ku-gain popularity akampemperusha kwenye Ubalozi cjui nchi gani mpaka anarudi Tanzania watu walishamsahau.

Mbali na kina Bomani kulikuwa na kina Kasela Bantu,kina Abdulla Fundikira na waliokuwa watemi(wafalme) enzi za mkoloni,Nyerere alihakikisha wananyamazishwa kwa hila au kwa kupewa ubalozi au kazi ambazo hazina exposure kwa Watanzania hasa Wana Kanda wenzao wa Ziwa.

Mpaka leo hii more than 50yrs of independence watu wa Kanda ya Ziwa hawana mbele wala nyuma. Pamoja na kugunduliwa kwa madini ya thamani kama Almasi za Mwadui,Dhahabu za Kahama,Geita, Ulyanhulu, Tulawaka na maeneo mengine bado mikoa ya Kanda ya Ziwa inaoneka iko nyuma vibaya sana kimaendeleo. Almasi na Dhahabu kutoka mikoa hii zinavunwa na majamazi wanaojiita wawekezaji baada ya sera ya ugenishaji wa migodi yote! Bado mikoa hii na wilaya zake hazina BARABARA ZA LAMI kwa sehemu kubwa! Bado wakulima wa Pamba,Kahawa,Mahindi,Karanga n.k. wameendelea kuwa fukara.Ukija kwa wavuvi hali ni hiyo hiyo. Masoko yote ya mazao ya Kilimo yamevamiwa na matapeli wanaoshrikiana na serikali kununua mazao ya wakulima kwa bei za kutupa huku wao wakijipatia faida nono.

Bado elimu katika mikoa hii ni duni sana. Hakuna Chuo Kikuu cha serikali hata kimoja. Pongezi zieende kwa taasisi za kidini kwa kuanzisha chuo Kikuu cha St. Augustine pale Mwanza vinginevyo watu wa Kanda hii wangelishia kusikia tu kuwa kuna vyuo vikuu vya UDSM,Sokoine,UDOM,Mzumbe n.k.

Inasikitisha kuona kwamba upuuzi huu bado umeendelezwa na awamu zote chini ya CCM kuidhulumu mikoa ya Kanda ya ziwa. Wito wangu kwa Watanzania wa Kanda ya Ziwa ni kwamba sasa TUSEME BASI INATOSHA! Kwamba tumeonewa kiasi cha kutosha,tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Ujinga wetu,Unyonge wetu na Upole wetu ndiyo umesababisha haya yote.

Adui mkuu wa watu wa Kanda ya ziwa ni chama Twawala CCM kwa hiyo basi dawa ni kuking'oa chama cha CCM kutoka kwenye uongozi hapo mwaka 2015. Naamini hili litawezekana kwa vile sasa tupo kwenye mchakato wa Katiba mpya ambayo itapatikana mapema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015. Lazima Watanzania wa Kanda ya Ziwa washikane kwa hali na mali ili kukitupilia mbali chama dhalimu cha CCM ili kuweza kujikomboa.

Nina amini kuna maeneo ambayo yameonyesha nia ya kutaka mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2010. Mkoa wa Mwanza na hasa Jiji la Mwanza walionyesha kuwa hawataki tena kuburuzwa na chama cha Mafisadi wa CCM. Lakini pia UK(Ukerewe) hawakubaki nyuma. Shinyanga hali kadhalika walionyesha cheche zao pamoja na hila na mbinu chafu za kuchakachua matokeo kama Shinyanga Mjini bado CHADEMA ilichukua majimbo ya Meatu na Maswa Magharibi. Kigoma, Musoma?Mara na Kagera CDM walipata Ubunge.

Tunaomba mwaka 2015 kasi ya kuiondoa CCM kwa kutumia Katiba Mpya ifikie aslimia 99.999 kama siyo 100.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Kanda ya Ziwa na watu wake.

Ng'wabeja sana.
 
Inaonekana viongozi wanapenda kura za watu wa Kanda ya ziwa lakini hawawapendi wananchi wa kanda hiyo.
Inasikitisha sana....
 
Sawa, lakini kumbuka aliyelala akiamka utakitema ulichowahi kukila. na sasa tayari aliyelala keshaamka! hebu vuta kumbukumbu uchaguzi wa mkuu 2010 mwanza na shinyanga mjini. ambapo ilikuwa ni mikoa pekee tanzania iliyotazamwa kama mfano wa kuigwa, hasa kwa chaguzi zinazofuta. hebu angalia matukio ya kule karagwe, bukoba na geita juzijuzi. ni kwamba, watu kule hawataki tena hili nyinyi-emu na li-siri-kali lake .
 
Huu sio ukabila...kwa sababu kanda ya ziwa ina makabila mengi kuliko kanda zote...hivyo sio ishu ya ukabila...
Sera ya Serikali kutokea kitambo ni kufanya even development atleast kwa kila kanda....as in Kenya every province has public university!
Kanda ya ziwa na umuhimu wake katika mapato ya Taifa hili ni moja ya maeneo yenye miundo mbinu duni hata hilo jiji lao (Mwanza) wakati Dar wanasema imeendelea kwa sababu ya its income...sasa kanda ya ziwa haijaendelezwa kwa sababu ya its low income?
Sio kwamba kanda ya ziwa hawaoni...ila hawafurahii mfumo huu wa rasilimali kwa sasa ndo maana CHADEMA imepata majimbo mengi nadhani kuliko mikoa yote Tanzani kutoka Shinyanga....Pia CCM kupoteza wilaya zote za jiji la Mwanza....na hata Musoma mjini ni CHADEMA....
Wasijiulize kwa nini wanakosa majimbo...majibu ni thread hii!
 
Wana Mwanaza wanyewe ndiyo wanaizamisha Mwanza labda mtoa mada tufahamishe Nyanza nani kaifirisi.
 
Wana Mwanaza wanyewe ndiyo wanaizamisha Mwanza labda mtoa mada tufahamishe Nyanza nani kaifirisi.

Kanda ya Ziwa sio Mwanza.....na Kanda ya Ziwa has nothing to do with Nyanza....au hujui Kagera walikuwa na yao...pia shinyanga walikuwa SHIRECU!
Tuambie mwana Mwanza gani alihujumu public university kujengwa Mwanza????
 
Juzi tuu hapa tundu lisu kaandaa mkutano tabata daresalama, akaambulia wachaga kadhaa tuu akaanza kutukana watu wa daresalama kwamba hawana mwamko wa kisiasa, na watu wa daresalama ndiyo watachelewesha "ukombozi" wake.

Leo hii kuna mwingine anatukana watu wa kanda ya ziwa. Kwani si mmeshampata rwakatare na ludovick? hao hawatoshi tuu? au hao siyo wa kanda ya ziwa?

Mmetuletea udini na sasa mnaongezea na ukabila....;
 
Ninakubaliana na hoja yako yaukandamizaji, lakini mguu uliosimamia ni wa bandia mkuu. Huwezi kutuhubiri kwa basi la ukabila na ukanda, hiyo ni sumu mbaya.
Nikukumbushe machache. Wasomi wengi wa nchi hii wametoka kanda ya ziwa, matajiri wengi ni wenyeji wa kanda ya ziwa. Viongozi wengi mashuhuri wanatokea huko, akiwemo magufuli, na mengine mengi mazuri. Labda nikufahamishe tu kwa swala la vyuo vikuu, vyuo vikuu vinachukua wanafunzi from Tanzania nzima, hivyo chuo hata kikajengwe Mbamba Bay kule Ruvuma bado watanzania wa Kigoma watasoma.
Mimi nafkiri siasa za ukanda tuachane nazo, badala yake tujenge taifa moja lisilo na nyufa na virakaraka. After all, muasisi wa taifa hili, baba wa taifa, ni mwennyeji wa huko. Sipati picha angekuwa na mawazo kama ya kwako ingekuwaje. Ni mawazo hayohayo ndio yanayomtesa baba Rizi1 ameondoa mpango wa muda mrefu wa kujenga bandari kubwa Tanga itakayosaidia kuzipunguzia mzigo barabara za Dar - Chalinze, ameipeleka Bagamoyo, Uwanja wa ndege wa kimataifana wenyewe unataka ujengwe Bagamoyo.
Hiyo ni sumu mbaya mdau, tuiache na tujenge taifa moja. Kama kanda ya ziwawakalalamika, Ruvuma nao wakalalamika, Mtwara, Kigoma, Rukwa ... Tuache hii sumu mbaya, tudai maendeleo kwa kuzingatia tija ya rasilimali, ikiwemo rasirimali watu, na si vinginevyo. Ni mtazamo wangu
 
Mbona bora ninyi Je Magharibi si ndio balaa!Bila shaka ndo maana wanawaita wabishi ili kuwakata makali!
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana.

Hawa hawa wanaolaumu uongozi wa TANU/CCM kutokufanya lolote kwenye kanda zao ni hawa hawa wanaompongeza Mwl Nyerere kila kukicha kwa uongozi bora ambao haukuweza kufanya chochote katika kijiji alichotoka achilia mbali mkoa au kanda.

Hii inaonyesha ni jinsi gani baadhi ya Watanzania hawana uhakika na kile wanachokitaka kwa wanasiasa au malalamiko yao yanakuwa yameshinikizwa na jicho moja la kisiasa.
 
Mkuu kwa historia ya nchi hii mikoa ya kanda ya ziwa ilipaswa kuwa juu sana angalau kwenye vitu mhimu kama barabara na elimu kumbuka kilimo cha pamba, madini, mbuga za wanyama, samaki...

Ni kweli mkuu lakini mapato ya raslimali hizo, ndo yamejenga kaskazini na kuwapa jeuri ya kutuita wajinga. Lakini ujinga una mwisho.
 
Ninakubaliana na hoja yako yaukandamizaji, lakini mguu uliosimamia ni wa bandia mkuu. Huwezi kutuhubiri kwa basi la ukabila na ukanda, hiyo ni sumu mbaya.
Nikukumbushe machache. Wasomi wengi wa nchi hii wametoka kanda ya ziwa, matajiri wengi ni wenyeji wa kanda ya ziwa. Viongozi wengi mashuhuri wanatokea huko, akiwemo magufuli, na mengine mengi mazuri. Labda nikufahamishe tu kwa swala la vyuo vikuu, vyuo vikuu vinachukua wanafunzi from Tanzania nzima, hivyo chuo hata kikajengwe Mbamba Bay kule Ruvuma bado watanzania wa Kigoma watasoma.
Mimi nafkiri siasa za ukanda tuachane nazo, badala yake tujenge taifa moja lisilo na nyufa na virakaraka. After all, muasisi wa taifa hili, baba wa taifa, ni mwennyeji wa huko. Sipati picha angekuwa na mawazo kama ya kwako ingekuwaje. Ni mawazo hayohayo ndio yanayomtesa baba Rizi1 ameondoa mpango wa muda mrefu wa kujenga bandari kubwa Tanga itakayosaidia kuzipunguzia mzigo barabara za Dar - Chalinze, ameipeleka Bagamoyo, Uwanja wa ndege wa kimataifana wenyewe unataka ujengwe Bagamoyo.
Hiyo ni sumu mbaya mdau, tuiache na tujenge taifa moja. Kama kanda ya ziwawakalalamika, Ruvuma nao wakalalamika, Mtwara, Kigoma, Rukwa ... Tuache hii sumu mbaya, tudai maendeleo kwa kuzingatia tija ya rasilimali, ikiwemo rasirimali watu, na si vinginevyo. Ni mtazamo wangu

Unajua tatizo la wazee wa Mapande aka Majimbo hawaamini katika umoja wa Kitaifa. Ni wabaguzi waliopitiliza ndo maana hawaoni aibu kueneza upuuzi wao.
 
Back
Top Bottom