wacha ukweli usemwe. Hajasema kabila lolote hapa. Viongozi na wabunge toka enzi za tanu na baadae ccm hawajawahi kutetea kanda ya ziwa ambapo idadi ya watanzania ni kubwa kuwarahisishia maendeleo yao kikanda. Tupo mbali na viwanda vya cement na vifaa vyakujengea lakini hata siku moja watu waccm hawajaona kama kuna haja ya serikali kuwapunguzia mzigo wakuvisafirisha ili vikapungua bei vifikapo huko. Usafiri wa gari moshi ulio kuwa nafuu matajiri waccm wameuangamiza ili watufikishie bidhaa kwa usafiri wa magari kwa faida kubwa, muone hata magufuli anakazana na kutengeneza barabara tu, je huwa akai katika baraza la mawaziri na akatetea train? Ili tukapata mizigo kanda ya ziwa ikiwa ina bei nafuu?(kila kitu bei ipo juu tofauti na dar, moro, tanga, dodoma, arusha, mbeya, zanzibar, nk kutokana na kusafirishwa mbali na viliko viwanda) wanaposhindwa kututolea ruzuku ya kuvisafirisha kwa nini hawaweki mkakati wa kuvijenga hukohuko kanda ya ziwa? (mwanza, musoma,kagera) au jirani na hapo (tabora, kigoma singida, nk)
kama sio kanisa la katoriki kutusaidia tukapata hospitali ya bugando na chuo kikuu cha sauti, pamoja na ukubwa wa kiuchumi ulioko huko kanda hii ingekuwaje sijui sisi ni watoto wa nani. Kwa kuwa sasa ccm imeshindikana kututoa katika karne ya 47, ngoja tuijaribu cdm huenda ikatuingiza katika ulimwengu wa digitali tukiwa salama. Mwanza, musoma wameishaliona hilo na shinyanga. Kagera wameanza hasa bukoba mjini na karagwe. Kigoma wao wana ngwe ya kwao ni safi kabisa. Jirani zetu tabora wamelala, sijui kwa nini hawalioni hili! Bado ninaamini ukombozi wa chi hii utaanzia kanda ya ziwa>
big like