Mleta hoja umenena. Napenda kuunga mkono hoja kwa aslimia 100+!Ni dhahiri kuwa kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza,Mara,Shinyanga,Tabora,Kagera,Kigoma na mkoa mpya wa Simiyu imeonewa,iimepuuzwa,imenyonywa na imenyanyaswa kiasi cha kutosha tangu enzi za Mwalimu Nyerere.Ujinga,Unyonge na Upole wa watu hawa ndiyo umewafanya waonewe,wanyonywe na wanyanyaswa kiasi cha kutosha.Ukweli na Uwazi! Kijiografia Mikoa hii ina utajiri wa raslimali za asili ambazo Mwenye enzi Mungu aliziweka kwa maksudi maalumu. Lakini kutokana na wajanja wachache,waroho na wenye tamaa ya madaraka katika nchi hii Mikoa ya Kanda ya Ziwa ndiyo imeendelea kushikilia mkia katika nyaza za Kielimu,Kiuchumi na Kiutawala!!! Mpaka leo huwa najiuliza kwanini Mwalimu J.K.Nyerere(RIP) akiwa mwasisi wa Taifa hili alishindwa kuchukua hatua za maksudi za kuiendeleza Kanda hii kuanzia Kielimu,Kiuchumi na Kiutawala.Badala yake aliamua kuwaweka pembeni ndugu zake wa Kanda ya Ziwa na kuelekeza nguvu zake kwa kanda zingine kama Pwani,Kaskazini,Kusini na Nyanda za Juu.Niliwahi kuambiwa na wazee wa kisukuma kuwa Washashi(Jamii ya Wazanaki,Wailkizu,Wakurya n.k.)wana kawaida ya choyo. Hivyo Nyerere akiwa Mzanaki alichukua asili ya uchoyo na kuamua kuwanyanyasa Wasukuma ambalo ndilo kabila kubwa kuliko yote Kanda ya Ziwa na Tanzania yote kwa ujumla. Niliambiwa kwamba Nyerere alikuwa anajua nguvu ya kabila ya Wasukuma kama kabila kuwa wakielemika na kuwa na nguvu ya Kiuchumi basi utawala wake ungelikuwa mashakani! Kwa hiyo Nyerere akaamua kutumia njia chafu za KIKOLONI za DEVIDE&RULE na DO NOT EDUCATE THEM yaani wagawanye uwatawale na uwanyima elimu!!Hakika Nyerere alifanikiwa katika hilo maana Mzanaki huyu alihakikisha shule za sekondari zinajengwa chache sana na hakukuwa na Chuo Kikuu hata kimoja mpaka Nyerere alipoiaga dunia. Shule za sekondari Kanda ya Ziwa zilikuwa za kuhesabu moja moja ukilinganisha na kanda zingine kama Kaskazini. Nakumbuka kulikuwa na sekondari chache kama Kahororo, Bwiru Boys& Girls,Shybush/com,Tabora Boys,Mara Sek,Musoma Alliance na Tarime Girls, basi!!Ilhali ukilinganisha na Kanda kama Kasakazini mkoa wa Kilimanjaro peke yake ulikuwa na zaidi ya sekondari 50!Kwa kweli hapa Nyerere hakuwatendea haki watu wa Kanda ya Ziwa na alijua kile alichokuwa amekipanga.Kuna viongozi muhimu waliokuwa wanainukia toka Kanda ya Ziwa lakini Nyerere alihakikisha hao jamaa hawafurukuti na mara nyingi alitumia mbinu za kuwaweka ndani au kuwapeleka nje ya nchi kuwa mabalozi wa kudumu. Kuna mifano hai kama kina Bomanis Family:Marehemu Paulo Bomani,Emanuel Bomani,Judge Mark Bomani. Paulo Bomani akiwa kiongozi wa chama cha Wakulima chenye nguvu-Nyanza Federation alijikuta akipewa Ubalozi wa kudumu huko Marekani mpaka watu wakamsahau. Jaji Mark Bomani alianza kama Mwanasheria Mkuu wa Tanzania miaka ya 1960s lakini Nyerere alipoona anaanza ku-gain popularity akampemperusha kwenye Ubalozi cjui nchi gani mpaka anarudi Tanzania watu walishamsahau.Mbali na kina Bomani kulikuwa na kina Kasela Bantu,kina Abdulla Fundikira na waliokuwa watemi(wafalme) enzi za mkoloni,Nyerere alihakikisha wananyamazishwa kwa hila au kwa kupewa ubalozi au kazi ambazo hazina exposure kwa Watanzania hasa Wana Kanda wenzao wa Ziwa. Mpaka leo hii more than 50yrs of independence watu wa Kanda ya Ziwa hawana mbele wala nyuma. Pamoja na kugunduliwa kwa madini ya thamani kama Almasi za Mwadui,Dhahabu za Kahama,Geita, Ulyanhulu, Tulawaka na maeneo mengine bado mikoa ya Kanda ya Ziwa inaoneka iko nyuma vibaya sana kimaendeleo. Almasi na Dhahabu kutoka mikoa hii zinavunwa na majamazi wanaojiita wawekezaji baada ya sera ya ugenishaji wa migodi yote! Bado mikoa hii na wilaya zake hazina BARABARA ZA LAMI kwa sehemu kubwa! Bado wakulima wa Pamba,Kahawa,Mahindi,Karanga n.k. wameendelea kuwa fukara.Ukija kwa wavuvi hali ni hiyo hiyo. Masoko yote ya mazao ya Kilimo yamevamiwa na matapeli wanaoshrikiana na serikali kununua mazao ya wakulima kwa bei za kutupa huku wao wakijipatia faida nono. Bado elimu katika mikoa hii ni duni sana. Hakuna Chuo Kikuu cha serikali hata kimoja. Pongezi zieende kwa taasisi za kidini kwa kuanzisha chuo Kikuu cha St. Augustine pale Mwanza vinginevyo watu wa Kanda hii wangelishia kusikia tu kuwa kuna vyuo vikuu vya UDSM,Sokoine,UDOM,Mzumbe n.k. Inasikitisha kuona kwamba upuuzi huu bado umeendelezwa na awamu zote chini ya CCM kuidhulumu mikoa ya Kanda ya ziwa. Wito wangu kwa Watanzania wa Kanda ya Ziwa ni kwamba sasa TUSEME BASI INATOSHA! Kwamba tumeonewa kiasi cha kutosha,tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Ujinga wetu,Unyonge wetu na Upole wetu ndiyo umesababisha haya yote. Adui mkuu wa watu wa Kanda ya ziwa ni chama Twawala CCM kwa hiyo basi dawa ni kuking'oa chama cha CCM kutoka kwenye uongozi hapo mwaka 2015. Naamini hili litawezekana kwa vile sasa tupo kwenye mchakato wa Katiba mpya ambayo itapatikana mapema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015. Lazima Watanzania wa Kanda ya Ziwa washikane kwa hali na mali ili kukitupilia mbali chama dhalimu cha CCM ili kuweza kujikomboa.Nina amini kuna maeneo ambayo yameonyesha nia ya kutaka mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2010. Mkoa wa Mwanza na hasa Jiji la Mwanza walionyesha kuwa hawataki tena kuburuzwa na chama cha Mafisadi wa CCM. Lakini pia UK(Ukerewe) hawakubaki nyuma. Shinyanga hali kadhalika walionyesha cheche zao pamoja na hila na mbinu chafu za kuchakachua matokeo kama Shinyanga Mjini bado CHADEMA ilichukua majimbo ya Meatu na Maswa Magharibi. Kigoma, Musoma?Mara na Kagera CDM walipata Ubunge.Tunaomba mwaka 2015 kasi ya kuiondoa CCM kwa kutumia Katiba Mpya ifikie aslimia 99.999 kama siyo 100.Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Kanda ya Ziwa na watu wake.Ng'wabeja sana.