Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Usimroge mkuu [emoji28], twende kwa mwajiri ukiwa na backup ya malalamiko yako.

Pole sana!
 
Duu hapa duniani Kuna akili za Kila aina.
 
Umeandika nini hiki umelewa au huyo mbwa anaweza kufanya nini? Unajua hao majina yao yameandikwa kwa pencil?
 
Mungu katuumba tofauti sana aisee.
Sehemu uliyovuja jasho lako kuipata anatokeaje 'mpumbavu' mmoja kukupasua kichwa napo kwa mgongo wa aina ya kazi yake?

Kuna wakati kwa baadhi ya watu ukiwaonyesha ustaarab wanakuona wewe Boya.
Na huyu ndio wa kumumgeuza mfano kwa wapangaji wenzake wengine.

Sasa iko hivi;
Kwa vyovyote vile ipo siku atarudi nyumbani kwake
Iwapo wewe unavyo vielelezo kuwa kweli ni Mpangaji wako
(Mikataba na hiyo ahadi kuwa angekulipa januari kama ipo kimaandishi nayo nenda nayo)
Peleka vyote Ofisi ya Serikali za Mitaa.

Huko unawapanga kabisa kuwa pamoja na kutaka walishughulikie tatizo lako vilevile ungependa kujua yupo kambi gani? Hivyo wasisahau kumuuliza, akiropoka Kambi yake baaasss kaisha.
Utasikiliza anawaambia nini Serikali ya Mtaa.
Lakini kama bado anazingua,
Kiburi kitaisha sababu Ma-boss wake ukiwaambia kuwa ni msumbufu watamnyoosha tena ikibidi unamzushia kuwa alikuwa anakurusharusha kichurwa ukimdai Pesa zako na kuwa huwa anatamba kuwa yeye ndio Mkuu wa 'Batalioni' nzima hapo Kambini, KITAKACHOMTOKEA UTAFURAHI.

Nawasilisha.
 
Hili Jambo Dogo Sana Unalipwa Chap Chap
Unatakiwa Kujua Anafanya Kambi Gani Unalipwa Halafu Unamtoa Home
Mpangaji Msumbufu Umepataje Nafasi Ya Kumpa Gap Mpaka Deni Linafika Million


Toa Mrejesho Chap Hapa Kama Umelipwa Ama Vp
 
Usijaribu kupangisha mwanajeshi au polisi kwenye nyumba yako

Hao watu wanajionaga km vile wako kambini, kodi hawalipi, wanamakelele hawana ustaarab hata kdg

Ni bora umpangishe baamedi au malayerrr...ataenda kuuza lkn mwisho wa mwezi kodi yako anakupa.
 
Hao Ni Wapangaji Kama Wengine Na Wanalipa Vema Tu
 
Mkuu umewasilisha vema kabisa.

Ngoja nifanyie kazi ushauri wako ambao unawiana na ushauri uliotolewa na wengi humu ndani.

Huyu ni wa kuruka nae jumla jumla.
 
Hili Jambo Dogo Sana Unalipwa Chap Chap
Unatakiwa Kujua Anafanya Kambi Gani Unalipwa Halafu Unamtoa Home
Mpangaji Msumbufu Umepataje Nafasi Ya Kumpa Gap Mpaka Deni Linafika Million


Toa Mrejesho Chap Hapa Kama Umelipwa Ama Vp
Ni kweli nimekosea kum-tolerate kwa kipindi chote hicho.

Anyaway, wazungu wanasema 'better late than never'. Ngoja nishughulike nae. Nitaleta mrejesho humu.
 
Sitarudia kosa tena mkuu. Ujinga wakati wa kwenda tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…