MREJESHO:
Kama wengi mlivyoshauri, jana nilifika Ngome-Upanga majira ya saa 9 alasiri. Nikapokelewa na na maafande pale getini nikaulizwa shida yangu, nikajieleza kwa ufupi, kabla ya kukaribishwa ndani nikapewa kiti kwanza nikae palepale getini na kupewa pole!
Afande mmoja muungwana sana ambaye alionekana ndio kiongozi wa walinzi wa siku ya jana pale getini, akaniomba nionyeshe nyaraka zozote (kama ninazo) kuthibitisha namdai. Nikatoa mkataba na commitment aliyoifanya Kwa maandishi nilipokutana nae mara ya mwisho Desemba mwaka Jana na kuahidi kunilipa ifikapo tar 29/01/2024.
Kwanza maafande wakanishangaa kwanini nimemruhusu akae muda wote huo bila kumbananisha alipe au nimfukuze.
Wakaniuliza kama nina picha yake nikawaonyesha picha yake aliyoweka Whatsapp. Baadhi ya maafande wakamtambua.
Wakaniomba sana kwamba nisipeleke hili swala ndani, watakachofanya ni kwamba watawasiliana nae ili j3 aje alipe au kama hana pesa achukue mkopo anilipe j3 hiyohiyo.
Kwahiyo wakaniomba nifike Ngome j3 kabla ya saa sita mchana. Nitamkuta mdeni wangu. Nikachukua namba ya yule afande in charge nikasepa zangu.
Wakuu, leo asubuhi wakati naamka nimekuta msg za mdeni wangu akinibembeleza kwamba j3 tukutane pale Ngome nje anilipe pesa yangu yote


. Nadhani wale maafande wenzake wameshampigia.
Ndugu zangu, nawashukuru sana kwa ushauri. JF forever! Nimepanga akishanilipa tu j3 namlamba na notice ya mwezi mmoja ahame.
ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI.