Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Sitaki afikishe mwezi hapa kwangu. Next stop ni Upanga mkuu, nimeshauriwa na wadau nikaombe taarifa zake pale na kumshtaki pia; naweza kupata msaada.
Achana na mambo ya kufatana kazini...wewe mwambie ahame tu kwani amekataa ?

Utatengeneza bifu zito kama ukianza mambo hayo ya kuhalibiana kazi.
 
Pole sana ndgu! Ulicheka na nyani sasa unavuna mabuwa. Ktk biashara ondoa kitu kinachoitwa huruma, Kuna watu hawana mishipa ya aibu.
 
Khaa!kwa hiyo wapo juu ya sheria au ameyatimba kivipi?Acha kumtisha mwenzio
Sio wapo juu ya sheria hao jamaa wanajipata sana, inakuwaje mjeda ashindwe kulipa kodi huoni kuna tatizo hapo, haiwezekani kushindwa kulipa kodi wakati anapokea mshahara mara mbili kila mwezi, ninachohisi kuna mchezo anamchezea ameona jamaa muoga, mimi kumwambia hivyo sio kumtisha ni kumzindua tu aamke kutoka usingizini, mimi naishi mwenyewe kwenye nyumba yangu na vyumba vipo na umaskini wangu nilionao sijawahi kuwaza kupangisha mtu yeyote, kama ingelikuwa ni lazima kupangisha kwa kujiongezea kipato, hata siku moja haitotokea kukaa na magwanda wa aina yeyote kujadiliana nae mkataba wa kupangishana, hapo ndipo alipoyatimba, umenielewa?
 
Ni vile tu sina muda mkuu.

Ila ningeamua kuruka naye mbona hakuna rangi angeacha kuona.

Ni vile tu kila nikifikiria kumuharibia mtu kibarua chake roho inakuwa nzito.
Kwa nini umuharibie kibarua chake wakati ishu ni simple tu, cha msingi usiende kwa ubabe hao jamaa wanafagilia sana mambo hayo utakuja kushtuka uko mbinguni washakutoa roho, kwanza wana umoja kishenzi halafu kama nati zimelegea fujo ndio wanalolipenda, nenda nae kistaarabu na mpe muda ahame, akishindwa muondoe kwa sheria zinavyotaka, siku ukimuhamisha usiende peke yako nenda na serikali nzima itakuwa ngumu kukuattack,
 
H Hopeless kabisa wew....ukisoma ulichoandika utaweza jicheka.....yaan niuze nyumba kwa kuhofia mpangaji?
 
Ndiyo tatizo la hawa CPL, huwa wanapenda wahudumiwe kwa kutukuzwa flani, kwa kuwa alipita Depo. Ni uonevu huu, pole sana.

Mpe notice kwanza ili uwe umefuata taratibu za kumwondoa. Kisha ndiyo ziende harakati za kiutaratibu za kumtoa kwenye nyumba yako.

Kama akiendelea ksumbua kutoka na kulipa malimbikizo ya deni, na kwa kuwa hujui kambi yake, basi peleka shauri lake HQ (Upanga) ila jitahidi uwe na nyaraka zote.

Ova
 
Ndiyo tatizo la hawa CPL, huwa wanapenda wahudumiwe kwa kutukuzwa flani, kwa kuwa alipita Depo. Ni uonevu huu, pole sana.


Ova
Mimi hao ndio huwa nawakomesha, akishaleta swaga za ujeshi akidhani ananitisha ndipo ninapofurahi, kama nilikuwa namhudumia kwa unyenyekevu nabadili, tunaenda sawa.

Ila sio katika namna ya kuvunjiana heshima, nambana kwa kutumia utaratibu uliowekwa. Sijui kwanini, mwisho huwa wanakuwa wapole.

Atanifanya nini? Kichwani kuna mtu ananipaga kiburi nitakuja kupigwa mimi jamani!
 
Una uhakika nyumba ni yako na una uhakika wewe ni mwanaume?
 
Akili za loser hizi..umejaa uoga mwili mzima
 
Achana na mambo ya kufatana kazini...wewe mwambie ahame tu kwani amekataa ?

Utatengeneza bifu zito kama ukianza mambo hayo ya kuhalibiana kazi.
Mkuu, sio kwamba bifu siliwezi, nalimudu haswa, huyu ni bwana mdg sana kwangu.

Nataka ajifunze, asije akafanya kama alivyofanya kwangu akihamia kwengine.
 
Mkuu mbona unanilezea kama unanifahamu vile [emoji1]

Ni vile tu tunatumia ID fake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…