Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Nakaribia kudhulumiwa, naombeni ushauri

Taratibu za kumtoa mpangaji ni zilezile wala hazina tofauti shirikisha uongozi wa mtaa mpe notisi ahame ndani ya miezi mitatu ikiisha miez mitatu toa vitu vyake nje.

Kama una nia ya kuendelea kudai hela yako kamfungulie kesi ya madai mahakamani, mahakama itatoa summons ataenda na utapata haki yako.
 
Unajua umeandika kama sisi humu ndio majirani zake huyo afande, sikiliza mdogo wangu, wakati wowote unapopatwa na tatizo lolote jaribu kuwa mtulivu na kama unahitaji ushauri toa maelezo ya kutosha yanayohusiana na msaada unaohitaji, pia usikurupuke kutoa hukumu au kuchukuwa maamuzi kwa kutumia hasira au utashi wako binafsi, unaweza kuwa umeonewa, umedhulumiwa, au vyovyote itakavyokuwa, lakini dunia hii haki pekee haikufanyi uwe na sauti mbele ya mamlaka au sheria, hususan upande huo wa magwanda, kwao wao hakuna sheria za duniani wala za mbinguni zinazofanya kazi, kwahiyo kuwa makini huyo anaweza hata kukunyanganya hiyo nyumba akasema ni yake na mamlaka ikakuweka wewe ndani na kusema ulitaka kumdhulumu, kwa kifupi umeyatimba, nakushauri mvumilie na mpe siku au mwezi kama hajalipa mwambie mimi nyumba nauza, utamuwachia msala huyo atakaekuja kununua, kwa kifupi umeyatimba.
Hakuna lolote, hajayatimba, hao jamaa umiwashitaki kikosini wanakatwa pesa kwa nguvu.
 
Umeanza vizuri halafu ukapuyanga mwishoni .

Mkuu, sisi wengine huwa hatupendi kutumia vyeo vyetu, kwasababu kama nikiamua kutumia mamlaka niliyonayo naweza kuathiri hata kibarua cha huyu bwana mdogo.

Na ndio maana hata nikienda kambini kwake siwezi kujitambulisha mimi na nani, nitaenda kama mwenye nyumba wa kawaida tu tena mkulima wa nyanya kule Lushoto .

Mimi nimelelewa vizuri na namwamini Mungu. Ndio maana niko tayari hata kumsamehe kwasababu pesa inatafutwa, kama niliweza kujenga kwa jasho langu; hiyo milioni moja pointi kdg haiwezi kuniathiri kwa chochote.
 
Ni typing error tu, lengo ni jina /madai.
Kwa mwajiri wake ni rahisi zaidi kupata msaada. Wanasikiliza malalamiko ya raia dhidi ya askari wao.

Polisi ni kisheria zaidi, lakini itawalazimu kuomba ushirikianao wa mwajiri wake.
Its your choice mkuu.
Ooh nimeelewa mkuu. Pole kwa kuteleza.

Nitafanya kama ulivyoshauri.

Kwasababu sina uhakika na kambi yake basi nitaanzia Lugalo nione kama wanaweza kunisaidia.
 
Nenda Makao Makuu ya Jeshi pale Ngome Upanga kawaeleze masaibu yako pale lazima upate msaada,nenda pale na majina yake kamili kuhusu kambi hiyo sio muhimu wao wenyewe watampata ndani ya robo saa tuu.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Dah mkuu ASANTE sana. Umenifungua pakubwa.

Kesho mapema tu ntakuwa pale na ntaleta mrejesho humu.
 
Taratibu za kumtoa mpangaji ni zilezile wala hazina tofauti shirikisha uongozi wa mtaa mpe notisi ahame ndani ya miezi mitatu ikiisha miez mitatu toa vitu vyake nje.

Kama una nia ya kuendelea kudai hela yako kamfungulie kesi ya madai mahakamani, mahakama itatoa summons ataenda na utapata haki yako.
Nashukuru sana mkuu.
 
Ple sana mkuu.

Unaweza kuchukua hatua zifuatazo ili kutatua suala lako.......

Ripoti suala hilo polisi, wape taarifa zote unazozijua kuhusu mwanajeshi huyo, jina lake na maelezo mengine yanayohusiana na suala hilo na mkataba wa upangaji. (mzunguko utakuwa mrefu maana lazima waombe kibari)

Au

Peleka malalamiko yako jeshini(mwajiri wake) Waulize kuhusu mchakato wa kuripoti vitendo vya jinai/ madai vilivyofanywa na mwanajeshi na waulize jinsi wanavyoshughulikia maswala kama hayo. (Kama jina ni sahihi, anapatikana haraka na utalipwa mapema)
Migogoro ya ardhi likiwemo hilo la kodi hayapokelewi polisi kwa sababu hiyo sio jinai bali ni shauri la madai hivyo apeleke shauri lake baraza la ardhi na nyumba la wilaya.
 
Unajua umeandika kama sisi humu ndio majirani zake huyo afande, sikiliza mdogo wangu, wakati wowote unapopatwa na tatizo lolote jaribu kuwa mtulivu na kama unahitaji ushauri toa maelezo ya kutosha yanayohusiana na msaada unaohitaji, pia usikurupuke kutoa hukumu au kuchukuwa maamuzi kwa kutumia hasira au utashi wako binafsi, unaweza kuwa umeonewa, umedhulumiwa, au vyovyote itakavyokuwa, lakini dunia hii haki pekee haikufanyi uwe na sauti mbele ya mamlaka au sheria, hususan upande huo wa magwanda, kwao wao hakuna sheria za duniani wala za mbinguni zinazofanya kazi, kwahiyo kuwa makini huyo anaweza hata kukunyanganya hiyo nyumba akasema ni yake na mamlaka ikakuweka wewe ndani na kusema ulitaka kumdhulumu, kwa kifupi umeyatimba, nakushauri mvumilie na mpe siku au mwezi kama hajalipa mwambie mimi nyumba nauza, utamuwachia msala huyo atakaekuja kununua, kwa kifupi umeyatimba.
Yes.
Kweli Maisha magumu, kama umempangisha nyumba mzima anaweza kutengeneza documents akampiga hiyo nyumba
 
Hawa watu wanaitwa askari si watu wa kufanya nao ukaribu hata kidogo, kama ni urafiki uwe wa kupeana tu salamu barabarani ila kuwaingiza kwenye maisha yako binafsi hasa ya kifedha utaishia kulia
 
Nenda hapo Upanga kama ulivyoshauriwa ukiwa na kopi ya nyaraka zote muhimu zitakazokusaidia ktk mdai yako, muhimu majina yake matatu,hao wanaokushauri umsubiri arudi vp kama anajiandaa kwenda zake nje ya nchi kwamwaka mzima.
Pia naomba kuuliza je haishi nafamilia ambayo ingekusaidia kujua kambi yake
 
Unajua umeandika kama sisi humu ndio majirani zake huyo afande, sikiliza mdogo wangu, wakati wowote unapopatwa na tatizo lolote jaribu kuwa mtulivu na kama unahitaji ushauri toa maelezo ya kutosha yanayohusiana na msaada unaohitaji, pia usikurupuke kutoa hukumu au kuchukuwa maamuzi kwa kutumia hasira au utashi wako binafsi, unaweza kuwa umeonewa, umedhulumiwa, au vyovyote itakavyokuwa, lakini dunia hii haki pekee haikufanyi uwe na sauti mbele ya mamlaka au sheria, hususan upande huo wa magwanda, kwao wao hakuna sheria za duniani wala za mbinguni zinazofanya kazi, kwahiyo kuwa makini huyo anaweza hata kukunyanganya hiyo nyumba akasema ni yake na mamlaka ikakuweka wewe ndani na kusema ulitaka kumdhulumu, kwa kifupi umeyatimba, nakushauri mvumilie na mpe siku au mwezi kama hajalipa mwambie mimi nyumba nauza, utamuwachia msala huyo atakaekuja kununua, kwa kifupi umeyatimba.
Acha kutisha watu wewe kayatimba yap sheria zipo Na haki itapatikana muhimu yeye kujua cha kufanya akiwa na ushahidi,

Watu kama wewe ndio manaochangia usumbufu kama huu kisa vyeo vyenu
 
Kama hutaki mambo mengi sijui mahakamani ,sijui polisi n.k ...

fanya hivi...

Nenda kwa mjumbe mwambie humtaki huyo mpangaji kwako na sababu ni hii.

hapo atapewa mwezi mmoja au siku kadhaa kama week 2 hivi za kuhama na atahama na

Ikibidi kabisa mtishie huyo mpangaji kwamba utaenda kazini kwake kushitaki kama atagoma kuhama. yaani asipohama huyo labda sijui..
 
Mkuu watu kama hao uwa wanajiandaa kusumbuana usikute ni mhaya au mnyaki wewe ukienda kwa mjumbe yeye anaenda baraza la ardhi na nyumba na mauongo kibao na hakuna sehemu yenye urasimu kama huko jambo dogo tu ambalo lingeweza kuisha kwa wiki au wiki mbili linachukua miaka mitano na hata ukija kushinda aambiwe akulipe fidia hana chochote cha kukulipa labda ungesema dawa ya wajinga kama hao ni kuwaroga tu kama kweli huo uchawi upo.
 
Back
Top Bottom