kedekede
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 5,298
- 7,646
- Thread starter
- #101
Namba moja!Pole kedekede kwa yaliyokukuta.
Taarifa ziko za aina tatu:
1. Kwa ajili ya kuzingatia (for noting):
Hii ni kwamba mtu anakuarifu kitu, ili ujue tu, kipo hicho kitu. Huna nafasi ya kufanya chochote kile kuhusu hicho kitu kukizuia au kukifanya kiendelee.
2. Kwa ajili ya Kupendekeza (for endorsement):
Hii ni pale mtu anapokuarifu kitu, ili ukichekeche na kuwa na nafasi ya kukipendekeza kiende kwa yeye ambaye anao uwezo wa kukizuia au kukifanya kiendelee. Kwenye hili unakuwa kwanza umezingatia (you have noted), halafu ukikubali kupendekeza jambo linaendelea mbele ya safari. Usipopendekeza, unaweza kumrudishia mwenyewe kwamba sipendekezi mpaka ufanye yafuatayo utakayotaka wewe ili upendekeze. Au unaweza kuendeleza mchakato kwa kutoa maoni yako kwamba hupendekezi, lakini taarifa isonge mbele. Mtoa maamuzi atajua kwamba hukupendekeza, lakini umeruhusu mchakato uendelee. Yeye ataweza kutoa uamuzi kurudisha suala kwako lirekebishwe mpaka ukubali kupendekeza, au ataendelea na mchakato huku akizingatia kwamba hukupendekeza.
3. Kwa ajili ya Kuridhia (For Approval):
Hii ni pale unapoletewa taarifa kwamba kitu fulani hakiwezi kufanyika, mpaka wewe utoe uamuzi kwamba kifanyike au kisifanyike.
Kwa hiyo, ile taarifa uliyopewa inaangukia fungu lipi?