Najutia tukio hili: Sikuweza kumsaidia rafiki yangu akajinyonga

" Guilty Consciousness "
hali hio watakuwa nayo wanamatusi wa humu na kwengineko dhidi ya ushujaa wa kamanda JPM.

Ina nguvu sana hio kitu itawaandama daima kwa matusi walio na wanayo toa kwa Baba yetu JPM ,its hard to escape from it

watajiona wanahusika moja kwa moja na kifo chake kama ilivyo kwako hapo sasa ( Mtakuja kujionea wenyewe )
😂😂😂😂 we jamaa bana
 
Kuna mzee mmoja alitokea kunikubar sana, na mimi nilimuheshimu na kumsikiliza.

Ikatokea siku moja mida ya saa 2 usiku akanioigia simu, kwa vile nilikua kwenye bus nikajisemea ngoja nisipokee nitampigia baada ya saa moja nimsikilize anataka kusemaje.

Hee bahati mbaya nikajisahau mazima, kesho yake jioni alifariki ghafra.

Kifo chake kilinitesa sana nilijiona kama vile mimi ndo nimemuua.

Inasikitisha sana haya mambo.
 
Pole mkuu,haya mambi nadhani yanahitaji devine intervention
 
Kuna tukio najitahidi kulisahau ila kila baada ya muda nalikumbuka na linaniumiza Sana..eeh mwenyezi Mungu tusaidie
 
" Guilty Consciousness "
hali hio watakuwa nayo wanamatusi wa humu na kwengineko dhidi ya ushujaa wa kamanda JPM.

Ina nguvu sana hio kitu itawaandama daima kwa matusi walio na wanayo toa kwa Baba yetu JPM ,its hard to escape from it

watajiona wanahusika moja kwa moja na kifo chake kama ilivyo kwako hapo sasa ( Mtakuja kujionea wenyewe )
Naona umeamua kuvaa nguo za kuogelea harusini..
 
Ona tu na wew usijinyoje maana unaonekana una roho ndogo sana mambo madogo hayo yanakuumizaje kichwa wanaume 5years!?
 
Nimejaribu sana imeshindikana!
Mmh... .... Kheri yako umeongea kwa public...

Lkn..upepo huo unao..

Toa sadaka na muombee dua .na ishi nae kwa kumfikiria alivyoumia mpaka kujinyonga.kwa mda..hali hiyo itaondoka..mtapumzika nyote!!

Haikuwa kosa lako ila jukumu la kumsaidia kwa kiasi flani lilikuwa lako..
 
Wakuu Salaam,

Kama kichwa cha habari kinavyosema.

Niliwahi kuwa na rafiki yangu wa karibu sana,alikuwa sio mgonjwa au sikujua anaumwa. Tulikuwa tukikutana ana tabasamu zaidi ya mimi na muda wote alikuwa anafuraha mpaka mimi alikuwa ananishauri akiniona sina furaha.

Siku moja aliniambia anafikiria kujiua sikushtuka nikamshauri kidogo kama vile ushauri wa vijana, wiki mbili baadaye akajinyonga. Nimekaa na hili jambo muda mrefu sana lakini limegomakutoka kwenye nafsi yangu, sina furaha, najilaumu, ninahisi sikutimiza wajibu wangu sehemu fulani ambayo ukiniuliza ni sehemu ipi siijui lakini ninahisi kama rafiki yake nilifeli kumsaidia.

Huu ni mwaka wa 12 sasa naishi kwa maumivu makali sana na sijui nitajitoaje. Je, kuna mtu alishawahi kuwa katika mazingira kama yangu na alisahau vipi akawa na furaha na amani kama zamani?,Mimi nimeshindwa kutojilaumu! popote ulipo Suleiman Nisamehe!

Kama uliwahi kujutia kitu ambacho unahisi ungekifanya na hukukifanya hebu tirirka hapa tuone msaada unaoweza kupatikana.
Bas bhana wakati nasoma sekondari ilitokea nikapata dada ambaye alinipenda sana kiufupi tuliivana vizuri na kila mtu akawa anajua sisi ni ndugu wakat huo yeye anasomea ualimu mimi niko form2. Boyfrend wake alikua akinichukulia mie shemeji yake kabisa kwa kipindi hicho mie mdogo wao dada p yupo ualimu na mpenzi wake yeye kwasabu kwao kulikua na uwezo alipelekwa form5&6.

Kumbuka hawa wapenzi walianza mapenzi yao tangu wakiwa shule ya msingi ila sekondar walitenganishwa japo hawakuacha mawasiliano ila ukubwan ndiyo kama hivo walikuja wakakutana tena na mapenz yakaanza upyaaaa.

Japo kulikua na tofaut wakat wanasomea masomo ya juu kwasabu msichana tayar alianza kuwa na mabuz ili ajiendeshe kimaisha kutokana na maisha ya kwao kuwa dun hivyo hata aliyekua akimsomesha kazi yake hiyo ni buz lake na alikua na mabuz wengine pia ambao sasa mie kama mdogo mtu nilikua nawajua kwasabu ndo nilikua natumika kimawasiliano hasa ukizingatia miaka hiyo simu hazikua sana.
Baadae tulikua! na wale wapenz japo walizaa lakin walitengana kutokana na mwanaume alijua tabia za dem wake akachoka.
Ila sasa wakati wanaachana wote walikua washapata kazi mwanaume anafanyia dar mwanamke anafanyia mkoani vijijni huko mie nami nikawa nimekua nikapata boyfrend ambaye ni rafiki yake na shemeji yangu kwahiyo mara nyingi nilikua nikionana na shemeji na dada pia kwa wakat tofaut .

Sasa gafla dada akaumwa mi sikujua kumbe chanzo cha kuachana kwao ni pamoja na huyu dada alipata ukimwi kwahiy kama mnavyojua tena ukiumwi unaua mie mda mrefu kidogo sijawasiliana na dada kutokana na majukumu nilienda kusoma nje ya nchi kurudi nikawa nimejishkiza kwenye ofis ya serikal ambayo boyfrend wangu alikua anaijua siku hiyo nikapokea simu kuwa dada yako p amefariki dah! Niliumia sana kwakua pia sikupata nafas ya kwenda kuzika siku zikapita.

Siku hiyo nikaamua nimpigie dadaake na p simu kumjulia hali uwii nilikutana na shutma nzito sana kuwa mimi nilianza kutembea na shemeji yangu na nilikua najifanya nampelekea zawadi dada p na kumueleza mambo ya shem kumbe mnafiki tu yaan nilipata shutuma nyingi mnooo na kwamba dada p kafa akinitaja kuwa mimi ni mnafiki saana na amenichukia hata akifa nisiende kuzika asee niliumia kwa kipindi kirefu mnoo kutokans na hizo shutma saana!

Nikawa nataman dada p afufuke au mimi nife nikutane naye huko kwa mungu nimwambie siyo kweli maneno aliyoambiwa!
Hadi siku moja nikaota dada p amekuja akanikuta uwanjan akawa ananiambia twwnde mdogo wangu twende kule niliko huku ulipo siyo pazuri et ananivuta mkono mi nikawa nakataa ila nikamwambia dada p huko uliko naimani ni pakujua ukwel sasa je umejua ukweli kuhusu mimi na shemeji? Akaniambia ndiyo mdogo wangu siyo kweli kumbe ni watu tu walituchonganisha ndiyo maana nakwambia nifuate huku ulipo siyo pazuri utataseka tu. Nikamwambia hapana we bora umejua ukweli mie huko siend wewe nenda tu!
Baada ya ile ndoto nadhan sasa ndiyo roho yangu ikapumua japo hadi leo sitakagi kumuona ndugu yake yoyote kwasabu wameshanihukumu tayar na siwez kuwabadilisha tena.
 
Mmh... .... Kheri yako umeongea kwa public...

Lkn..upepo huo unao..

Toa sadaka na muombee dua .na ishi nae kwa kumfikiria alivyoumia mpaka kujinyonga.kwa mda..hali hiyo itaondoka..mtapumzika nyote!!

Haikuwa kosa lako ila jukumu la kumsaidia kwa kiasi flani lilikuwa lako..
Asante mkuu nitafanya hivyo!
 
Wakuu Salaam,

Kama kichwa cha habari kinavyosema.

Niliwahi kuwa na rafiki yangu wa karibu sana,alikuwa sio mgonjwa au sikujua anaumwa. Tulikuwa tukikutana ana tabasamu zaidi ya mimi na muda wote alikuwa anafuraha mpaka mimi alikuwa ananishauri akiniona sina furaha.

Siku moja aliniambia anafikiria kujiua sikushtuka nikamshauri kidogo kama vile ushauri wa vijana, wiki mbili baadaye akajinyonga. Nimekaa na hili jambo muda mrefu sana lakini limegomakutoka kwenye nafsi yangu, sina furaha, najilaumu, ninahisi sikutimiza wajibu wangu sehemu fulani ambayo ukiniuliza ni sehemu ipi siijui lakini ninahisi kama rafiki yake nilifeli kumsaidia.

Huu ni mwaka wa 12 sasa naishi kwa maumivu makali sana na sijui nitajitoaje. Je, kuna mtu alishawahi kuwa katika mazingira kama yangu na alisahau vipi akawa na furaha na amani kama zamani?,Mimi nimeshindwa kutojilaumu! popote ulipo Suleiman Nisamehe!

Kama uliwahi kujutia kitu ambacho unahisi ungekifanya na hukukifanya hebu tirirka hapa tuone msaada unaoweza kupatikana.
Alikueleza kwa nini anataka kujiua na nini ulimshauri hadi uhisi hukutimiza wajibu wako. Isije kuwa nae alikuwa hashauriki halafu unaumia tu bila sababu.
 
Mbona tayari dalili zimeanza.

Ndio maana niliwaambia wapuuzi fulani, inawezakuwa jamaa huyu alikukwaza kwa namna moja au nyingine, kitendo cha yeye kufa na bado unamtukana unajitafutia ugonjwa mbaya sana wa majuto.

Kifo ni form nyingine ya maisha ya kiumbe, hatujui labda kinapewa uwezo zaidi ya huu tulio nao,au kinakuja kwa namna tofauti hapa hapa duniani tena.
Ni unafiki kumsifia mtu aliyekuumiza baada ya kufa. Ili uishi kwa furaha na amani ya moyo, ishi bila unafiki. Yaani blue anaita blue na nyeusi ubaiita nyeusi.
 
Back
Top Bottom