Baada ya kufunga maombi, rafiki yangu akapatwa na janga

De Opera

JF-Expert Member
May 23, 2013
471
922
Habari wana JF?

Natumaini mnaendelea vizuri!

NB: Nimeandika hii kwa niaba! Nimesimuliwa hadi chozi likatoka.

Wapwa, kuna suala linaniumiza sana kichwa nalo ni kuhusiana na kinachompata rafiki yangu kwa sasa.

Stori iko hivi:
Mimi na rafiki yangu tulikutana katika harakati za maisha, tukaamua tufanye harakati zetu kwa ushirikiano pia kama familia.

Tulifungua biashara na kwa vile rafiki yangu hakuwa na ueledi na ile biashara, niliisimamia mimi mwenyewe.

Kiumri rafiki yangu ni mkubwa, anafamilia na mimi sina familia(Single) yaani tunaishi nyumba moja(Kwake).

Sasa rafiki yangu katika harakati ghafla akawa amepata harakati zingine za kusafirisha mizigo kutoka dubai kuja Tanzania.

Maisha yakaendelea hivo, ilikuwa siku, miezi, sasa ni kama mwaka na nusu. Yeye akawa anasafiri mi nabaki na familia yake na anaweza akawa anamaliza wiki kadhaa ndio anakuja.

Rafiki yangu akawa akija ananisimulia, amenunua nyumba kubwa na magari matatu tayari, akawa haulizii hata ile biashara yetu inaendeleaje.

Katika ile biashara mi nikaona inakuwa ngumu, hata nikifanya matangazo kwenye radio, vipeperushi, wateja sipati. Hata nikipata wateja ni kidogo. Nikipata hela haikai, yote inaisha hata hakuna cha maana nilichofanya.

Mwili wangu ukabadilika. Nikawa nahisi muwasho baadhi ya sehemu za mwili. Mwili ukawa wa kivivu. Akili ikalala, kuamka naamka saa nne asubuhi. Nikisema nifanye jambo la maana, akili inaleta uvivu silikamilishi jambo. Mara nikaanza kuwa nahisi kuna vitu vinanitembelea mwilini.

Sasa, baada ya kuulizia kwa watu wanaofahamu hiyo hali, nikaambiwa nimerogwa, nina jini pia. Nimefungwa kwa nguvu za giza.

Baada ya kuambiwa hivo, nikaona dalili pia, ikabidi nifunge maombi.

Sasa ni miezi kama miwili hivi ninaomba na ninamuomba Mungu kuwa 'Aniondelee shetani huyu aliye katika mwili wangu. Na kama ametumwa na mtu kuja kuiba baraka zangu na kuharibu maisha yangu, eeh Mungu muwajibishe mtu huyu. Yale yote aliyonifanyia yamrudie yeye'.

Wapwa, baada ya kuendelea na maombi, rafiki yangu hadi sasa ndiye amekuwa matatizoni. Amekula hasara ya mamilioni ya pesa kwa muda tu huu mfupi. Anadaiwa mali za watu. Hadi sasa, yupo gerezani. Nyumba yake imechukuliwa na gari zake zote.

Wapwa, baada ya kukaa kutafakali, nimeona kama msukosuko wa rafiki yangu ni kama ndio mkanda uliofunga maisha yangu, kwani kuna baadhi ya maneno nakumbuka yanadhihirisha kuwa inawezekana ikawa.

Kuna siku tulikuwa tunaangalia movie, ilikuwa inazungumzia jinsi familia inavyopambana kuokoa maisha ya mtoto wao aliyekuwa anatatizo la figo. Wazazi hao, waliamua kuenda kuteka mtoto mwingine ili wamtoe figo.
Sasa nikamuuliza rafiki yangu kwamba 'Hivi unaweza ukatoa uhai wa mtu mwingine ili maisha yako yaendelee kuwa mazuri?'

Rafiki yangu akajifanya kama hajasikia. Nikarudia tena kumuuliza, ila aliinamisha kichwa na kuwa kama mtu mwenye wasiwasi na hakujibu chochote.

Kingine ni kuna msemo niliwahi kuusikia kutoka kwa watu akisema kamwe hawezi kuniachia niende. Sasa nikajiuliza, haiwezi niachia kivipi?.

Kiukweli wapwa, hayo ndiyo yaliyopo hadi sasa. Kesi inaendelea na mimi maombi yanaendelea. Nikizidi kuomba kesho inazidi kuwa kubwa. Mimi naihurumia familia yake!

Mimi sihukumu moja kwa moja kuwa anaweza kuwa yeye, ila tu ninahisi kutokana na yanayoendelea, kwani kwa mtu mwenye akili na uelewa, kama kuna vitu haviko sawa anatambua tu.
 
Adui huwa hayupo mbali wanakuwaga mbele ya uso wako ili usitilie maanani.... Maneno ndio mawazo ya mtu juu yako braza.
Kupona kwako kufa kwake .. Huruma yako Kifo chako.
Jichanganye Mchawi / mshirikina hasamehewi ... Mungu ataamua, wewe kaza kamba.
Amen 🙏
 
Pole sana mkuu, scenario uliyopitia ni Kama niliyowahi kupitia, yule kwangu hakutaka nihame kabisa, alienda kuvuruga uhamisho na kuufunga nisihame na baada ya maombi nilihama . Adui hatoki mbali mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom