kedekede
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 5,298
- 7,646
Wakuu Salaam,
Kama kichwa cha habari kinavyosema.
Niliwahi kuwa na rafiki yangu wa karibu sana,alikuwa sio mgonjwa au sikujua anaumwa. Tulikuwa tukikutana ana tabasamu zaidi ya mimi na muda wote alikuwa anafuraha mpaka mimi alikuwa ananishauri akiniona sina furaha.
Siku moja aliniambia anafikiria kujiua sikushtuka nikamshauri kidogo kama vile ushauri wa vijana, wiki mbili baadaye akajinyonga. Nimekaa na hili jambo muda mrefu sana lakini limegomakutoka kwenye nafsi yangu, sina furaha, najilaumu, ninahisi sikutimiza wajibu wangu sehemu fulani ambayo ukiniuliza ni sehemu ipi siijui lakini ninahisi kama rafiki yake nilifeli kumsaidia.
Huu ni mwaka wa 12 sasa naishi kwa maumivu makali sana na sijui nitajitoaje. Je, kuna mtu alishawahi kuwa katika mazingira kama yangu na alisahau vipi akawa na furaha na amani kama zamani?,Mimi nimeshindwa kutojilaumu! popote ulipo Suleiman Nisamehe!
Kama uliwahi kujutia kitu ambacho unahisi ungekifanya na hukukifanya hebu tirirka hapa tuone msaada unaoweza kupatikana.