Najutia tukio hili: Sikuweza kumsaidia rafiki yangu akajinyonga

Ninajua sikumuua lakini najilaumu kutomzuia ,najisemesha laiti ningefanya hivi au vile.
Alikueleza kwa nini anataka kujiua na nini ulimshauri hadi uhisi hukutimiza wajibu wako. Isije kuwa nae alikuwa hashauriki halafu unaumia tu bila sababu.
Pole mkuu.

Je, na wewe unapata wazo la kujiua?

Kama ndio, hilo wazo linakuijia wakati gani? kwamba, katika starehe zako, unatumia kiburudisho/kilevi gani?

Kwakuwa tunaogopa tusikupoteze, jitahidi kuachana na vitu vinavyo kuchanganya akili; maeneo mliyokuwa mkikutana na huyo mwendazake. Pia pata ushauri wa wataalamu e.g. wazee au psychologist.

KUMBUKA KUTULETEA MREJESHO KAMA HUJAFA
 
Thanks mkuu,nimeshafanya hivyo bado sina raha.Kuna kitu sijakiandika ndio kinachoniuma zaidi!
Sasa huu si unafiki, yaani hujui nini kinachokuumiza, lakini kuna kitu hujajiandika ndio kinachokuumiza zaidi. Akili za kijinga hizi. Za kipumbavu kabisa.
 
Majuto ya kinafiki tu asilimia kubwa wa Tanzania wagumu sana kutoa msaada kwa wanaohitaji msaada hila ukisikia amekufa ndio mnajifanya mnahuzuni na unatoa hela ya kusafirisha msiba wakati marehemu alishakuomba msaada Mara kibao ukakataa wakati uwezo ulikuwa nao na inawezakuwa ungemsaidia ungekua umeokoa maisha yake.
Eti na jambo linalomuumiza zaidi Ila hajaliandika, halafu anasema anajuta kwa asichokifahamu. Kinyeo kabisa yaani.
 
Pole sana! Inanikumbusha mimi miaka ya 90 mwanzoni. Nilikuwa nisafiri kwenda Dar bahati mbaya siku hiyo ndege ikaahirisha hai kesho yake. Basi ikanibidi nirudi zangu nyumbani. Ilipofika mida ya saa kumi na mja hivi, nikaamua kwenda sehemu kupata kiburudisha koo. Wakati naenda huko nilikutana na rafiki yangu, alikuwa akifanya kazi TRA, akataka niambatane naye, lakini akaghairi baadae kwani alidai ngoja aende kutazama sinema. Nilienda huko nilikokuwa nikienda na majira ya saa mbili usiku nilirudi zangu home. Nikiwa nimelala majira ya saa tano usiku niligongewa mlango, nikambiwa rafiki yako kachomwa kisu yuko hoi hospitali. Alichomwa kisu akiwa kabisa kakaribia nyumbani kwake mida ya saa nne akitoka kutazama sinema. Niliamka nikaongozana na majirani tukaelekea hospitali. Nakumbuka tulimkuta chumba cha daktari juu ya kitanda akiwa anakata roho. Na mimi nikamfunga macho!!!

Hadi leo huwa najilauma na kujiambia endapo ningeongozana naye labda mauti yasingemkuta. Rest in eternal peace my friend T.
Hongera kwa kupanda ndege!!
 
siku ya Idd nilimpigia simu rafiki yangu nikitaka kujua kwanini hakunialika/kunikaribisha kwenye IDD wala hakunitumia ujumbe hata zile za kufowadiana tu ( Yeye alikua mwislam) na tulikua na mazoea haya ya kukaribishana au hata kujuliana hali tu kila mara, basi nikapiga, haikupokelewa, nikazidi kupatwa mashaka maana haikua kawaida yake, nikajua akiona missed call yangu atanipigia, ila hadi asubuhi ya siku iliyofuata hakupiga, nikazidi kukosa amani. Nakumbuka ilikua mida ya saa tatu asubuhi nilikua nimetoka home nikapiga tena simu ila nikaanza kukosa tu amani bila sababu ya msingi, mara simu ikapokelewa na sauti ya kike, sikustuka maana ni kawaida simu yake siku nyingine kupokelwa na mke wake. Nilivyosikia sauti ya kike nikaanza kumtania "Shemeji imekuaje mmekula iddi peke yenu bila kunikaribisha?:" nikaona kama vile yule mtu hanifahamu, ikabidi nitulie nimuulize, wewe si ni mama fulani? Akajibu akasema "Mimi ni Shemeji yake, jana nilikua kwako Baba fulani ni mgonjwa, hivyo wakati naondoka nikasahau nikabeba simu yao nikaacha yangu, wapigie kwenye namba ya airtel"

Nikaipiga namba ya mshkaji akapokea mke wake akaniambia jamaa yako ni mgonjwa, nikamwambia mpe simu niongee nae, akasema hawezi hata kuongea, aagh kidogo sikuamini maana tangu nimefahamiana na jamaa zaidi ya 15 years ago sijawahi kusikia anaumwa kiasi hiki, shida nini akaniambia. nikawashauri wampeleke hospital........ila hawakuweza.

Jioni ya siku ile nikapiga simu tena, nikaambiwa jmaaa bado hali yake sio nzuri, nikaongea na ndugu zake na bado nikasisitiza wampeleke hospital, Kaka yake akanijibu kuwa ni vyema niende kwanza nikamuone then mambo ya hospital yatafuata, Siku ya Mechi ya Kazier Chiefs na Simba SA bikajisemea moyoni wacha hii mechi ikiisha niende kwake hata kama ni usiku nikamchukue nimpeleke hospital.

Mechi iliish akwa Simba kufungwa, nikasema wacha tu nikalale muda huu nitaenda asubuhi nikamchukue nimpeleke hospital maana ndugu zake walikua wanasema amerogwa hivyo sikutaka sana kuingilia mambo ya ndugu japo mkewe alinielewa.

Asubuhi saa kumi na moja moja kuna namba ngeni ilinipigia mara mbili ila sikusikia simu, saa 12 asubuhi nikaamka nisikilize DW nikaona missed calls, nikawa najiiliza huyu anayepiga simu mida hii nani? Kupiga ile namba nikapokelewa na KILIO cha Mwanamke, dah nilikufa ganzi aiseeee....

Pengine ningeacha kwenda mpirani jana yake ningeweza kumuokoa Jamaa......Hii scenerio bado mbichi kabisa, nimeshiriki kila kitu kwenye msiba wake but naona nina hatia kubwa sana. Pumzika kwa amani Kaka.
Hapa ina cha kujibu mbele ya Haki. Jiandae.
 
Pole mkuu.

Je, na wewe unapata wazo la kujiua?

Kama ndio, hilo wazo linakuijia wakati gani? kwamba, katika starehe zako, unatumia kiburudisho/kilevi gani?

Kwakuwa tunaogopa tusikupoteze, jitahidi kuachana na vitu vinavyo kuchanganya akili; maeneo mliyokuwa mkikutana na huyo mwendazake. Pia pata ushauri wa wataalamu e.g. wazee au psychologist.

KUMBUKA KUTULETEA MREJESHO KAMA HUJAFA
Hapana sina wazo la kujiua najisikia vibaya tu.
 
Kuna mmoja alikuja hapa jf kuomba ushauri..watu wakamponda Sana..wengine wakasema awaelekeze alipo wampelekee kamba..I see jamaa akajinyonga kweli..
Lakini wote waliondika huo ujinga waliomba msamaha yakaisha..
 
Kuna mmoja alikuja hapa jf kuomba ushauri..watu wakamponda Sana..wengine wakasema awaelekeze alipo wampelekee kamba..I see jamaa akajinyonga kweli..
Lakini wote waliondika huo ujinga waliomba msamaha yakaisha..
Walimuomba nani msamaha?
 
Wakuu Salaam,

Kama kichwa cha habari kinavyosema.

Niliwahi kuwa na rafiki yangu wa karibu sana,alikuwa sio mgonjwa au sikujua anaumwa. Tulikuwa tukikutana ana tabasamu zaidi ya mimi na muda wote alikuwa anafuraha mpaka mimi alikuwa ananishauri akiniona sina furaha.

Siku moja aliniambia anafikiria kujiua sikushtuka nikamshauri kidogo kama vile ushauri wa vijana, wiki mbili baadaye akajinyonga. Nimekaa na hili jambo muda mrefu sana lakini limegomakutoka kwenye nafsi yangu, sina furaha, najilaumu, ninahisi sikutimiza wajibu wangu sehemu fulani ambayo ukiniuliza ni sehemu ipi siijui lakini ninahisi kama rafiki yake nilifeli kumsaidia.

Huu ni mwaka wa 12 sasa naishi kwa maumivu makali sana na sijui nitajitoaje. Je, kuna mtu alishawahi kuwa katika mazingira kama yangu na alisahau vipi akawa na furaha na amani kama zamani?,Mimi nimeshindwa kutojilaumu! popote ulipo Suleiman Nisamehe!

Kama uliwahi kujutia kitu ambacho unahisi ungekifanya na hukukifanya hebu tirirka hapa tuone msaada unaoweza kupatikana.
Pole mkuu na kumbukumbu zikutiazo gerezani. Nakuona wewe pia ukipata depression ambayo usipochukua hatua ya kuona watabibu hasa washauri nasihi hali ya kujiua inaweza kukunyemelea. Acha kuwaza mwenyewe..nenda katibiwe kwa matabibu wa afya ya akili.
 
" Guilty Consciousness "
hali hio watakuwa nayo wanamatusi wa humu na kwengineko dhidi ya ushujaa wa kamanda JPM.

Ina nguvu sana hio kitu itawaandama daima kwa matusi walio na wanayo toa kwa Baba yetu JPM ,its hard to escape from it

watajiona wanahusika moja kwa moja na kifo chake kama ilivyo kwako hapo sasa ( Mtakuja kujionea wenyewe )
Kivipi?
 
Kuna watu mna nyoyo za kipekee aisee. Yaani uje kwangu tunazungumza halafu unambie unataka kujiua, mimi na akili yangu nikae chini nipoteze muda kujua kinachosababisha ujiue! Kwangu mimi ni big No

Unataka kujiua, wewe jiue tu na useme utakapojiulia tusihangaike kukutafuta.
 
Pole mkuu na kumbukumbu zikutiazo gerezani. Nakuona wewe pia ukipata depression ambayo usipochukua hatua ya kuona watabibu hasa washauri nasihi hali ya kujiua inaweza kukunyemelea. Acha kuwaza mwenyewe..nenda katibiwe kwa matabibu wa afya ya akili.
Asante mkuu kwa kunifariji.
 
Asante mkuu kwa maneno yako ya faraja na ya kunizidisha nisonge.Nimejifunza mengi kutokana na kuondoka kwake,nimejifunza nichukue hatua kwa mtu mwingine akinishirikisha jambo kama hili tena.Kusahau ndio imeshindikana mkuu.Namuona hadi leo,nahisi kuna wajib sikuuitimiza katika kumshauri kwangu.
Siku ya tukio nilienda kwenye harusi ya mfanyakazi mwenzangu alikuwa anaoa.Rafiki yangu huyo aliwapigia simu baadhi ya rafiki zake wengine kuwaaga,simu yangu niliisahau nyumbani siku hiyo sikwenda nayo kwenye harusini.Niliporudi alfajiri nilikuta missed calls nyingi sana,lakini kwa vile ni alfajiri ilikuwa nikasema nilale nitapiga kesho yake asubui.12 asubui nikagongewa mlango ya taarifa ya msiba.
Nililia sana,kwenye msiba wake nilmkumbatia mama yake nikalia sana na kumuomba nsamaha.Majibu ya mama yake aliniambia sina cha kuombea msanaha nilikuwa mtu mzuri sana kwa rafiki yangu.Laiti ningepokea ile simu nikaongea naye,laiti angeongea na mimi,labda yasingetokea hayo yote!
mkuu we amin nlokujuza hapoa awali, ka hutaka amini hayo nlokujuza hutaka uwe na amani daima mpaka nawe utaiacha hii dunia.
kuna wenye majibu yao
kuna wasio jua la kufanya
kuna wenye kutaka mtu wa kumsarport alichokiwaza
 
Back
Top Bottom