MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 33,574
- 53,613
Tatizo la Upweke kwa Vijana wa Umri wako linatokea wapi?
Huna marafiki, watoto, Mume, Mke mshinde mnaangalia pamoja Ottoman?
Bado kuna social network Instagram,Tiktok, Facebook, JF
Kwa Dunia ya sasa tatizo la Upweke linawasumbua zaidi Watu wenye Umri Mkubwa hasa Wazee, ingawa kwa upande wa Nchi yetu Tatizo sio kubwa kutokana na kuwa Wazee wengi huwa wanakufa kabla ya Umri Mkubwa.
Unaweza ukawa na vyote hivyo ila bado ujikute mpweke, ni hsli ya kawaida kwa binadamu kujihisi hivyo mara moja moja, tumeshuhidia watu maarufu wakijitoa uhai kisa upweke, mtu aliyeishi kwa kuzingirwa na mashabiki na marafiki lakini kumbe kiaina alikua mwenyewe.
Ushauri wangu kwa mleta mada ipuuze hiyo hali itakuondoka yenyewe, imewahi kunitokea mimi nikajishangaa maana nimezungukwa na familia kama baba, nina majirani, nina watu wengi tunacheka kila siku lakini nikawa ghafla nateseka upweke.
Nilipambana ikanitoka yenyewe.