Najihisi nina mkosi kwenye mapenzi

Post #1 Hadi #228, ukisoma vizuri kwa umakini majibu anayotoa mlengwa naona Tone haishabiiani.
Topic hii naona kama ni Indirect method ya kutafuta kitu.

Big Brains watanielewa
 
Kuna huyu mmoja nilimwambia babe sipendi tabia ya kuniomba hela kwani nami nimeajiriwa kama wewe,akakasirika akanambia nimemdharau,tena tuliongea tukiwa wenyewe sehemu tulivu kwa ipole na ustaarabu,sasa kosa langu li wapi?
Duuh!..hata mimi ningesepa mdogo mdogo..noti rait.
 
Hawa niwaongeleao ni wafanyakazi kabisa,sio wachovu wa kwa mama ntilie.wamesoma wanakazi na mishahara mizuri tu
Huko kwenye friends ndio kabisaa walinigeuza gari la mshahara,nikaacha hata kutoka out
Anyway Asante kwa ushauri,nadhni dawa ni kuishi Kama Niko kisiwani kuepuka hii roho.
unaitaji kumuona Dr wa psychologist [therapist]unaitaji tibaa...sio kwa kuji down kiasi hicho.hela yako inakutesa
 
Nipe namba zako za simu ili tushauriane
Mimi ni mwanamke wa miaka 27,sijaolewa,Sina mtoto,Sina mpenzi,nimepanga naishi na mdogo wangu mmoja yuko kidato cha nne sasa.

Tatizo langu ni moja tangu nianze kujihusisha na mapenzi napata wanaume ama wapenzi wanaoniomba hela na kutaka mie ndiyo niwahudumie.Nina kazi ndio ya kawaida tu ila sijui kumwomba mwanaume hela.

Ni mtoto wa pekee,niliyelelewa na wajomba baada ya wazazi kuondoka duniani.Nilipitia kipindi kigumu sana wakati nakua na kwenye elimu yangu,hiyo ikanijengea kujiamini na kujitafutia vyangu.

Sijui kujigamba,sichezei pesa kwa mambo yasiyo ya msingi ila nina roho ya huruma sana. Naweza kuwa na milioni hata 5 kwenye akaunti na bado nikapanda daladala ama kula kwa mama ntilie mtaani au kazini.

Mpenzi wa Kwanza alikuwa ananipiga mizinga sana baada ya kuja kwangu na kuona navyoishi,hatukudumu tukaachana sababu hiyo,kwani hakuwahi nipa hata senti yake ila yeye amenilia hela zangu nyingi.

Wa pili ilikuwa hivyo hivyo kila leo alikuwa anapanga mbinu za kunitoa hela,nikaona isiwe shida nikaachana naye. Wa tatu alikuwa ananisema niache kuwapa watu hela ila akishika simu yangu anajifowafia hela toka line yangu ya mpesa,halafu ananikashifu kuwa najidai kuwa na hela wakati sijawahi mweleza hayo,ila alikuwa anachunguza akaunti zangu za m-pesa na benki akanifosi nikampa hadi pasiwedi akawa akihitaji hela anatoa bila kunitaarifu. Nikaona isiwe tabu nikaachana naye.

Sasa hivi yapata mwaka niko single na nimeamua kutokudate tena manake napata magarasa tu.

Naombeni ushauri nakosea wapi? Kiukweli siwezi kuomba hela na nikiomba kama nina uhitaji nisipopewa basi najikalia kimya tu.

Kwanini wanaume waniombe hela?kasoro yangu ni Nini?na katika wote hao hakuna niliyemtongoza walinotongoza wenyewe.

Mie sipendi kuomba wala kuombwa hela. Naumia sana kama mwanamke. Naona wananitongoza kwa lengo la kunichuna,lakini mbona mie navaa kawaida,nala kawaida,siyo mtu wa starehe. Tatizo ni nini?
 
Pole sana dear
 
Jamani nadhani hamjanielewa,wananifosi mie ndiyo nifanye hayo,sijawah jitolea fanya hivyo.Mfano Kuna siku tulikwenda kula sehemu baada ya kumaliza akanambia lete hela tulipe nikamjobu sina,akanambia hebu simu yako,akatazama salio mpesa akaona laki na ishirini,akamwambia mhudumu lete namba ya mpesa tukulipe,mhudumu akaleta namba,nikamwambia hii hela ina kazi,akasema we lipa bill ntakurudishia,na hakuwahi rudisha hata nilipomkumbusha.Roho iliniuma sana,nikakaa kimya tulipomaliza tukaondoka,nilipofika nyumbani nikafuta namba yake na ukawa mwisho wa hayo mahusiano.
Kwahiyo point sijipi majukumu,wananifosi niwape hela,nilipe bill nakadhalika.

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
Kuna mama mmoja alishawahi kuwa dean of student pale ardhi university mtafute atakusaidia ushauri, huyu maza alishanisaidia sana kipindi nasumbuliwa na mambo flani,
NB: anatoa ushauri wa maneno sio pesa
 
pole sana....kizazi dume kinaangamia kabisa...ila jiamini usiingie kichwa kichwa.....jithaminishe wewe kama wewe....mchomekee dinner sehemu nzuri ya kawaida....mcheki yuko responsible.....usikibali kirahisi...kubali ktk uhalisia...kwamba "HE CAN HANDLE LITTLE THING"....then msogeze hatua B, C........utamjua vema.....mmeumbwa kwa ajili yetu.....tun mbinu lukuki....
 
Awamu hii yautawala wanaume wanaopenda kitonga niwanaume wenye familia kabisa, wanachokifanya wanakuja kwako ili uwasaidie kutunza familia zao. Wachunguze hao maex wako kama hawana wake nawatoto/mtoto
 
Back
Top Bottom