Najihisi nina mkosi kwenye mapenzi

Najihisi nina mkosi kwenye mapenzi

Kwanini aniombe?mbona mie sijawah waomba?huoni tatizo hapo?haimaanoshi huwa sikwami,ila nikikwama natafuta naopga nao dili wananikopesha halafu nalipa
Hao unaowapata ni wakubwa kwako au wadogo? Kama ni wakubwa wamekuacha umri gani? Vipi status zao ni wafanyakazi au bado wanakaa majumbani?
 
Njoo kwangu mamaa kisiwa cha maliwazo pepo z kusi zinapovuma.....
Kila kitu kitakuwa sawa na utaleta ushuhuda.... Mi ni faraja kwa wenye mfadhaiko wa maisha.
 
mimi ni mwanamke wa miaka 27,sijaolewa,Sina mtoto,Sina mpenzi,nimepanga naishi na mdogo want mmoja yuko kidato Cha nne Sasa.

Tatizo langu ni moja tangu nianze kujihusisha na mapenzi napata wanaume ama wapenzi wanaoniomba hela na kutaka mie ndiyo niwahudumie.nina kazi ndio ya kawaida tu ila sijui kumwomba mwanaume hela.

Ni mtoto wa pekee,nilolelewa na wajomba baada ya wazazi kuondoka duniani.nilipitia kipindi kigumu sana wakati nakua na kwenye elimu yangu,hiyo ikanojengea kujiamini na kujitafutia vyangu.sijui kujigamba,sichezei pesa kwa mambo yasiyo ya msingi ila nina roho ya huruma sana.naweza kuwa na milioni hata 5 kwenye akaunti na bado nikapanda daladala ama kula kwa mama ntilie mtaani au kazini.

Mpenzi wa Kwanza alikuwa ananipiga mizinga Sana baada ya kuja kwangu na kuona navyoishi,hatukudumu tukaachana sababu hiyo,kwani hakuwahi nipa hata senti yake ila yeye amenilia hela zangu nyingi.

Wa pili ilikuwa hivyohivyo Kila leo alikuwa anapanga mbinu za kunitoa hela,nikaona isiwe shida nikaachana naye.wa tatu alikuwa ananisema niache kuwapa watu hela ila akishika simu yangu anajifowafia hela toka line yangu ya mpesa,halafu ananikashifu kuwa najidai kuwa na hela wakati sijawahi mweleza hayo,ila alikuwa anachunguza akaunti zangu za mp pesa na benki akanifosi nikampa Hadi pasiwed akawa akihitaj hela anatoa bila kunitaarifu.nikaona isiwe tabu nikaachana naye.

Sahivi yapata mwaka niko singo na nimeamua kutokudate tena manake napata magarasa tu.naombeni ushauri nakosea wapi?kiukweli siwezi kuomba hela na nikiomba kama nina uhotaj nisipopewa basi najikalia kimya tu.
Kwanini wanaume waniombe hela?kasoro yangu ni Nini?na katika wote hao hakuna niliyemtongoza walinotongoza wenyewe.mie sipendi kuomba wala kuombwa hela.naumia sana Kama mwanamke.naona wananitongoza kwa lengo la kunichuna,lakin mbona mie navaa kawaida,nala kawaida,siyo mtu wa starehe,tatizo ni nini?
Njooni kwangu mnaosumburiwa na kuelemewa na mizigo nitawapumuzisha
 
Usiseme hivo mkuu juzi watu wametapeliwa humu sijui na mkuu nani wameishia kumlaumu mkuu mshana jr. Huyu kajitangaza ana hela atawadaka wengi sana huko pm subiri
Sijasema nina hela,nimesema naombwa sana hela,hata nikiwaambia sina hawaamini
Ndio sababu nimesitisha kudate najiona nina mkosi kwenye mapenzi,haiwezekan kila anitongozaye baada ya muda ageuke tegemezi kwangu.
 
Sijasema nina hela,nimesema naombwa sana hela,hata nikiwaambia sina hawaamini
Ndio sababu nimesitisha kudate najiona nina mkosi kwenye mapenzi,haiwezekan kila anitongozaye baada ya muda ageuke tegemezi kwangu.
Sasa dada wewe kama Una hela ila Sura huna..Tako huna..!! unategemea nini????
 
Sasa dada wewe kama Una hela ila Sura huna..Tako huna..!! unategemea nini????
Sina sura mbaya,figure ninayo nzuri tu,tako pia lipo
Isitoshe kwanini wanitongoze tena kwa kufosi,hata mtu ukimkataa analazimisha kunidate huoni ni roho ya kuja olewa na hohehahe tuishie sumbuana tu
 
We nae unampaje password zako za miamala mwanaume????


Shida ya kwanza unayo mwenyewe, wewe ni dhaifu..... Mwanaume akitaka Sanaa password mpe ya simu sio namba ya siri ya m pesa au bank


Eti mwanaume akatoe pesa kutoka kwenye akaunti yangu bila kunijuza heheheheheh nitamuweka alama
 
Na sisi wakulima wa mikoani utatatupenda? Ambao hatujawahi kufika dar ila hatuombi pesa tunalima zetu,if yes,embu njoobom chapuuu
 
I think hili ni tangazo la kutafuta mtu ambaye yuko tayari kulelewa.
Sitaki tegemezi ndiomaana nimeleta Uzi
Mimi kulea mwanaume ni dalili ya mkosi kwani mwanaume ameumbwa kulea familia,mtu kama huyo mkijaanza familia hawezi tambua majukumu yake,ataona ni haki yake mama ahudumie kwa kila kitu,halafu baadae wanaanza kulia wanawake hatuwaheshimu ,kwel?
 
Sitaki tegemezi ndiomaana nimeleta Uzi
Mimi kulea mwanaume ni dalili ya mkosi kwani mwanaume ameumbwa kulea familia,mtu kama huyo mkijaanza familia hawezi tambua majukumu yake,ataona ni haki yake mama ahudumie kwa kila kitu,halafu baadae wanaanza kulia wanawake hatuwaheshimu ,kwel?

Mpenzi wa mwisho umeachana naye lini?
 
Sijasema nina hela,nimesema naombwa sana hela,hata nikiwaambia sina hawaamini
Ndio sababu nimesitisha kudate najiona nina mkosi kwenye mapenzi,haiwezekan kila anitongozaye baada ya muda ageuke tegemezi kwangu.
Basi kuna udhaifu pa hala wanaoutumia kuwa tegemezi kwako financially, hawezekani wote hao wawe wanakupiga tu mizinga mpaka mwingine kuchukulia hela pasipo ridhaa yako isitoshe umesema na wao wanafanya kazi, una tatizo pahala sio bure dadaangu, kama hii story ni kweli basi jitafakari upya kabla ya relationship inayofuta
 
bac hao c rizki mkuu,huo ujasiri wa kuomba mwanamke hela huku unafanya kaz unatoka wap?
Tena wasomi wazuri tu,sijawah date ambaye hana kazi
Kuna huyo alikuwa anafosi nimtumie hela kwenye mpesa akisingizia ana matatizo kumbe anaenda kustarehe,halafu tukikutana akawa ananitusi kuwa ninajidai nina hela,najipa majukumu yasiyo yangu wakati alikuwa ananifosi nimtumie hizo hela,sikuwah mpa hela yangu kwa hiari
 
Back
Top Bottom