Najihisi nina mkosi kwenye mapenzi

Najihisi nina mkosi kwenye mapenzi

Tatizo ni kuwa huangalii status yaani hali ya hao wanaume wanaokufata na ukawakubalia....yaani unakubali tu ila ungekuwa unawachunguza maisha yao kazi, biashara yao walau kujiridhisha kuwa nao wana shughuli zao za kueleweka. Wanaume nao siku hizi wanaangalia mahala anapoweza kupata pumziko na kulelewa hivyo uwe unaangalia sana kabla hujaingia ktk mahusiano. Pia umesema una huruma sana haina shida kuwa na huruma kama ndivyo Mwenyezi kakuumba hivyo usibadilike ukaanza kuigiza roho ngumu hapana ila kile unachotoa kusaidia kiwe cha ziada isiguse mtaji au akiba yako. Pia nimeelimika sana kutoka kwako yaani unakuwa na mil 5 bank ila bado unapanda daladala na kula kwa mama ntilie nimependa maisha yako nami nitaiba hiyo mbinu ili kunisaidia ktk maendeleo yangu ya kifedha..
Kifupi dada fikiria aina ya mwanaume unayemtaka sifa unazozitaka ili hao wanaokutongoza basi uweze kuwapitisha ktk chujio dhidi ya vigezo vya mwanaume unayemtaka kama kuna mwenye sifa basi mkubalie. Naona umekuwa ukiwakubalia vijana au wanaume wasio na mipango wa muelekeo wa.maisha ndo maana wanaishia kula hela zako tu.na huenda wengi wamekutongoza kwa dhumuni la kula hela zako na si vinginevyo.
 
Kwanza hakuna niliposema akuombe. Pia unaonekana una shida binafsi hiyo. Hata siku moja si me wala ke atachukia akiombwa hela na mpenzi wake.


Hawa tunaowasema kwa kuomba ni wale tunawaona dhahiri hawana upendo , wapo tu kuwanyonya wenzao. Hata ulipoeleza nilikuelewa hivi. Sasa nakuona unasisitiza kwanini uombwe hela? Unaombwa kama binadamu na mpenzi.Ni suala la kawaida kusaidiana.Changamoto ni pale mtu anakuibia tu, hana upendo.

Kingine unachoshangaza ni pale mwanzo umejiita una huruma,ndiyo maana unawapa. Cha ajabu wew mwenyewe unakiri suala hilo hupendi na sasa unahoji kwanin uombwe hela. Huruma gani hiyo? Upo sawa kweli wewe?
Mkuu umenena kweli,
 
Kwanza yaonekana kama unamajivuno fulani hivi, eti kwanin waniombe mbona mi siwaombi, hizo password si uliwapa mwenyewe ama, ktk mapenzi ya kweli hilo ni jambo la kawaida kusaidiana, ila kama ni fake love basi hapo kuna shida
Kwahiyo changamoto wanazo wao tu?
Mie sina?
 
Njo tuoane naona tunafanana.Me pia nina kazi yangu ya kawaida tu.Ila huwa sina tabia ya kuuliza kipato cha KE hata siku 1.Na niliwahi kuwa na KE kwao chapaa balaa but Yule dada hakuamini vile me sitaki wala siombi chochote.

Sharti la kuoana ni hakuna kuonjana mpaka ndoa,ili usije sema oooh umenichezea.
Mkuu je ukikuta ni bwawa au kisima usije kufungua uzi humu na kuanza kulialia
 
Penye miti mingi hakuna wajenzi.. mimi nimeshaoa,upo tayari kuwa mke wa pili. Miki sio wale wanaume wa vizinga. Utapata mapenzi mpaka utasahau ulikupitia.
 
Pyee pyeeee.......

Wajinga ndo waliwaooo
 
Kwa maelezo yako dada hakuna mwanaume ata mmoja aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwako walikuwa wako after money, yawezekana pia walikusoma kuanzia kazi yako upole wako wakakuchapa kotekote pesa na papuchi ila hawajawahi kukupenda. Tuliza akili kwanza unapoingia kwenye mahusiano mapya , kuna mdau kakushauri vizuri sana usiwe mwepesi wa kuweka mambo yako yote wazi kwa just boyfriend utakuwa mtu wakulizwa daily.
 
mimi ni mwanamke wa miaka 27,sijaolewa,Sina mtoto,Sina mpenzi,nimepanga naishi na mdogo want mmoja yuko kidato Cha nne Sasa.

Tatizo langu ni moja tangu nianze kujihusisha na mapenzi napata wanaume ama wapenzi wanaoniomba hela na kutaka mie ndiyo niwahudumie.nina kazi ndio ya kawaida tu ila sijui kumwomba mwanaume hela.

Ni mtoto wa pekee,nilolelewa na wajomba baada ya wazazi kuondoka duniani.nilipitia kipindi kigumu sana wakati nakua na kwenye elimu yangu,hiyo ikanojengea kujiamini na kujitafutia vyangu.sijui kujigamba,sichezei pesa kwa mambo yasiyo ya msingi ila nina roho ya huruma sana.naweza kuwa na milioni hata 5 kwenye akaunti na bado nikapanda daladala ama kula kwa mama ntilie mtaani au kazini.

Mpenzi wa Kwanza alikuwa ananipiga mizinga Sana baada ya kuja kwangu na kuona navyoishi,hatukudumu tukaachana sababu hiyo,kwani hakuwahi nipa hata senti yake ila yeye amenilia hela zangu nyingi.

Wa pili ilikuwa hivyohivyo Kila leo alikuwa anapanga mbinu za kunitoa hela,nikaona isiwe shida nikaachana naye.wa tatu alikuwa ananisema niache kuwapa watu hela ila akishika simu yangu anajifowafia hela toka line yangu ya mpesa,halafu ananikashifu kuwa najidai kuwa na hela wakati sijawahi mweleza hayo,ila alikuwa anachunguza akaunti zangu za mp pesa na benki akanifosi nikampa Hadi pasiwed akawa akihitaj hela anatoa bila kunitaarifu.nikaona isiwe tabu nikaachana naye.

Sahivi yapata mwaka niko singo na nimeamua kutokudate tena manake napata magarasa tu.naombeni ushauri nakosea wapi?kiukweli siwezi kuomba hela na nikiomba kama nina uhotaj nisipopewa basi najikalia kimya tu.
Kwanini wanaume waniombe hela?kasoro yangu ni Nini?na katika wote hao hakuna niliyemtongoza walinotongoza wenyewe.mie sipendi kuomba wala kuombwa hela.naumia sana Kama mwanamke.naona wananitongoza kwa lengo la kunichuna,lakin mbona mie navaa kawaida,nala kawaida,siyo mtu wa starehe,tatizo ni nini?
Naamini mpaka mda huu umepokea pm za kutosha!
Kuwa makini hapa ndio pana mafisi waviziaji Wa fursa
 
un date na ma graduate wa 2015-18,pole sana mkuu,wana hali mbaya sana huku mtaan,wavumilie tu c kupenda kwao
 
Nani akamatwe humu, humu ni vibaka kwa vibaka tu, unauza cheni bandia , unapewa cheni bandia.

Mtu akiwekwa kati huyo atakuwa kabahatika, kapata shule ya dunia ukiacha ile ya wazazi.
Usiseme hivo mkuu juzi watu wametapeliwa humu sijui na mkuu nani wameishia kumlaumu mkuu mshana jr. Huyu kajitangaza ana hela atawadaka wengi sana huko pm subiri
 
Back
Top Bottom