mimi ni mwanamke wa miaka 27,sijaolewa,Sina mtoto,Sina mpenzi,nimepanga naishi na mdogo want mmoja yuko kidato Cha nne Sasa.
Tatizo langu ni moja tangu nianze kujihusisha na mapenzi napata wanaume ama wapenzi wanaoniomba hela na kutaka mie ndiyo niwahudumie.nina kazi ndio ya kawaida tu ila sijui kumwomba mwanaume hela.
Ni mtoto wa pekee,nilolelewa na wajomba baada ya wazazi kuondoka duniani.nilipitia kipindi kigumu sana wakati nakua na kwenye elimu yangu,hiyo ikanojengea kujiamini na kujitafutia vyangu.sijui kujigamba,sichezei pesa kwa mambo yasiyo ya msingi ila nina roho ya huruma sana.naweza kuwa na milioni hata 5 kwenye akaunti na bado nikapanda daladala ama kula kwa mama ntilie mtaani au kazini.
Mpenzi wa Kwanza alikuwa ananipiga mizinga Sana baada ya kuja kwangu na kuona navyoishi,hatukudumu tukaachana sababu hiyo,kwani hakuwahi nipa hata senti yake ila yeye amenilia hela zangu nyingi.
Wa pili ilikuwa hivyohivyo Kila leo alikuwa anapanga mbinu za kunitoa hela,nikaona isiwe shida nikaachana naye.wa tatu alikuwa ananisema niache kuwapa watu hela ila akishika simu yangu anajifowafia hela toka line yangu ya mpesa,halafu ananikashifu kuwa najidai kuwa na hela wakati sijawahi mweleza hayo,ila alikuwa anachunguza akaunti zangu za mp pesa na benki akanifosi nikampa Hadi pasiwed akawa akihitaj hela anatoa bila kunitaarifu.nikaona isiwe tabu nikaachana naye.
Sahivi yapata mwaka niko singo na nimeamua kutokudate tena manake napata magarasa tu.naombeni ushauri nakosea wapi?kiukweli siwezi kuomba hela na nikiomba kama nina uhotaj nisipopewa basi najikalia kimya tu.
Kwanini wanaume waniombe hela?kasoro yangu ni Nini?na katika wote hao hakuna niliyemtongoza walinotongoza wenyewe.mie sipendi kuomba wala kuombwa hela.naumia sana Kama mwanamke.naona wananitongoza kwa lengo la kunichuna,lakin mbona mie navaa kawaida,nala kawaida,siyo mtu wa starehe,tatizo ni nini?