Najaribu kukizoea kifo nashindwa kabisa!

Leo hii km mkiisikia sauti yake msiifanye migumu mioyo yenu
Yesu ametuhaidi nini kuhusu kifo? imeandikwa Hosea 13:14 "Nitawakomboa na nguvu za kaburi nitawaokoa na mauti ewe mauti yawapi mapigo yako? Ewe kaburi ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafishwa na macho yangu."

Ufufuwaji uko katika nguvu za mungu imeandikwa 1Wakorintho 15:21-22 "Maana ya kuwa mauti ili letwa na mtu kadhalika na kiyama ya wafu italetwa na mtu kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa kadhalika na katika kristo wate wanahuishwa."

Mungu alimpa mwanawe kwa sababu gani? imeandikwa Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenada ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ila kila amwaminiye asipotee bali awena uzima wamilele."
 
Ndoto ya kwanza kuna mambo yako pending..ukiyakamilisha hiyo ndoto itakata
Ndoto ya pili ina mahusiano na ya kwanza kuna vitu vikubwa unataka kufanya lakini kuna changamoto zinakutia ganzi na kujikuta una hofu
Sawa mkuu asante
 
tizo ni kwamba, ukihofu sana, utakufa, ukiogopa, utakufa, usipoogopa, utakufa.
Nafikiri tunaopata shida zaidi ni sie tunaobaki duniani, hao wanaoondoka wanaanza safari nyingine ambayo hatujui wanajisikiaje kuhusu sie waliotuacha.

Uchungu, simanzi na ubaya wa kifo tunaupata sie tulioachwa na wapendwa wetu.

Nikishawaza hayo, naona bora kila mmoja kwa imani yake, ajiandae na safari kwa kuwa hatujui siku wala saa mwili utakapoacha roho.

Nakazia

Kuishi ni Kristo, kufa ni faida.
Hili ndo neno mujarab
 
Kifo hakina bingwa wala hakizoeleki..nimepoteza marafiki wa utotoni, nimepoteza marafiki wa shuleni, nimepoteza marafiki wa ukubwani, wazazi ndugu na jamaa!
Huwa nawakumbuka na kuwaombea sana sana..natamani nipate wasaa niongee nao..tupige story tukumbushane mengi
Unakula nyama mkuu?
 
Kinachoniumiza kwenye kifo ni kimoja tu. Nawaachaje walio hai ambao ilitakiwa niwatengezee njia.......


Yaani nikiambiwa nichague kati ya kufa na kuishi,naona bora kufa... nimeshasema kinachonipa hofu ni nini.

Nikimuwaza mwanangu bado mdogo na sijamtengenezea mazingira mazuri ya kuishi, basi naumia mpaka naghairi kufa. Isingekua yeye, ningesha pumzika kitambo sana
 
[
Kifo hakina bingwa wala hakizoeleki..nimepoteza marafiki wa utotoni, nimepoteza marafiki wa shuleni, nimepoteza marafiki wa ukubwani, wazazi ndugu na jamaa!
Huwa nawakumbuka na kuwaombea sana sana..natamani nipate wasaa niongee nao..tupige story tukumbushane mengi
...Pole bro..kifo hakizoeleki na hakitazoeleka as long as bado tunaishi. Soma 1Wakorintho 15:22-26
 
..Nitabaki nafsi inayoona kila kitu kinachoendelea lakini isiyoweza kufanya lolote.....

Leo hii nimeota Mtumishi wa Mungu mmoja ametwaliwa wiki 3 sasa zimepita nilikuwa naye karibu kihuduma.

nimeota huko aliko ni as before yaani kipindi cha huduma hakipo.

Na kaniambia anataka pesa siyo michango. Jpili hii ndo kanisa tunataka tukae na familia yake tuwafariji.

Niambie mtani hapo iko je
 
..Nitabaki nafsi inayoona kila kitu kinachoendelea lakini isiyoweza kufanya lolote.....

Leo hii nimeota Mtumishi wa Mungu mmoja ametwaliwa wiki 3 sasa zimepita nilikuwa naye karibu kihuduma.

nimeota huko aliko ni as before yaani kipindi cha huduma hakipo.

Na kaniambia anataka pesa siyo michango. Jpili hii ndo kanisa tunataka tukae na familia yake tuwafariji.

Niambie mtani hapo iko je
Na kaniambia anataka pesa siyo michango. Jpili hii ndo kanisa tunataka tukae na familia yake tuwafariji.
Ana uhitaji mkubwa huko aliko ..lakini si yeye bali watu wake wa karibu
 
Kuogopa kifo ni sayansi, hii inatokea bila hiari yako, kwenye mwili wa binadamu kuna hormones na neurochemicals mbali mbali ambazo huzalishwa ili kumfanya mtu aondokane na hatari kwa kumtia hofu au kumfanya akimbie hatari au kifo, maadui n.k

Lukizoea au kutokukiogopa kifo ni dalili za afya kuyumba (ugonjwa wa akili au mwili),
Siku ukiona umekizoea kifo wahi hospitali,
 
Usiku wa kuamkia hii siku ya leo inayoisha dakika 90 zijazo..Siku hii ya August 12 JF tumepata msiba mwingine tena! Tumeondokewa na mwenzetu.. Wengi hatumfahamu kwa sura zaidi ya utambulisho wake bandia.... Lakini kupitia ile mada wana JF wameonesha hisia zao kupitia maandishi yao...! Simfahamu marehemu lakini kifo chake kimeniumiza kwakuwa kimenikuta katikati ya tafakuri kuu juu ya hiki kitu kinaitwa kifo

Wiki iliyopita kanisani kwetu tulitoa huduma ya chakula cha Bwana kwa wasiojiweza majumbani(mimi sasa ni mtumishi wa Mungu madhabahuni) Mmojawapo wa wagonjwa wale ni mama ambaye sura yake imeshindwa kunitoka kabisa.. Alifariki siku mbili baadae!

Hatuna utashi wa kuamua hatima ya pumzi yetu, sisi ni mateka wa kifo na kila sekunde ,kifo kinaondoka na batch iliyo tayari! Kila sekunde! Bila kujali utakufa na nini ama kifo cha aina gani huna utashi wa kujipangia ama kujiamulia... Batch number tusiyoijua sisi ikiwadia huondoka na watu wake! Inatisha sana ujue..!

Na kila batch ni timilifu.. Ina kila aina ya watu
Wema na wabaya
Waume kwa wake
Vijana kwa wazee
Watoto na vichanga
Wagonjwa kwa wazima
Walio na dini na wasio na dini
Viongozi na wanasiasa
Mimba za abortion na mimba zisizotimia

Hii misiba ya kila siku ina mipangilio yake juu ya uwezo wa mwanadamu kuweza walau kuchagua nani wa kufa nani wa kubaki!
Maswali ni mengi nje ya ufahamu wa kibinadamu
Wapendwa wetu wafao wanaenda wapi!?
Je wanatuona na kutusikia?
Me huko waliko wana furaha na amani au ni tabu na mateso?
Je tutaonana nao wapi? Lini? Katika mazingira gani?
Je tutaweza kuwashika kuwakumbatia na kuteta nao mengi na mengi?
Siri ya fumbo la kifo ni kubwa na yenye kuumiza sana

Nimefanya kazi mochwari
Nimewahudumia walio katika hatua za mwisho kuondoka hapa duniani
Wengine nimewasaidia kufa kifo cha faida..cha amani ..lakini kote huko nimeshindwa kukizoea kifo
Nimeandika mada za vifo nimeandika kuhusu sanaa ya kifo lakini kila nikiona ama kusikia roho imeondoka mwili unasisimka upya!


Muda huu niandikapo haya kuna roho zinaondoka! Ni batch nyingine hiyo ndani ya haya masaa 24.. Tumefiwa na kufiwa
Na wazazi wetu
Na watoto wetu
Na ndugu zetu
Na jamaa zetu
Na marafiki zetu nk
Nasi tutakufa na kusahaulika.. Na kuoza nyama na kubaki mifupa michache ambayo kwayo wala tunaweza tusikubukwe sisi tulikuwa nani....!

Niandikapo haya natafakari mengi sana
Kwamba siku moja nitalala kimya , mke wangu ataniamsha sitaamka, watoto wangu wataniita sitaitika..ndugu na jamaa zangu watanitikisa sitikisiki
Roho yangu itakuwa imeachana na mwili wangu na damu haitatembea tena kwakuwa moyo utakuwa umesimama
Nitabaki nafsi inayoona kila kitu kinachoendelea lakini isiyoweza kufanya lolote
Hata pale kaburini nitakapofukiwa na wapendwa wangu kunililia sana na baadae kuniacha pekeyangu mpweke na kiza totoro cha usiku. ..Inatisha sana ujue.. Nimeshindwa kabisa kukizoea kifo
Kifo ni fumbo kubwa kwetu wanadamu. Kifo ni adhabu yetu binadamu ambayo haikwepeki na haizoeleki kwetu binadamu.
Kifo kinatupora wapendwa wetu, na mwisho kinatupora maisha yetu sisi wenyewe.
Leo tangu asubuhi nasikiliza wimbo wa marehemu REMMY, "Kifo hakina huruma", machozi yananilenga machoni kwangu. KIFO HAKINA HURUMA.

 
Kifo ni fumbo kubwa kwetu wanadamu. Kifo ni adhabu yetu binadamu ambayo haikwepeki na haizoeleki kwetu binadamu.
Kifo kinatupora wapendwa wetu, na mwisho kinatupora maisha yetu sisi wenyewe.
Leo tangu asubuhi nasikiliza wimbo wa marehemu REMMY, "Kifo hakina huruma", machozi yananilenga machoni kwangu. KIFO HAKINA HURUMA.

Pole sana Dr... Natambua kipindi unachopitia je kuna updates zozote za mazishi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom