Najaribu kukizoea kifo nashindwa kabisa!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,122
Reaction score
871,386
Usiku wa kuamkia hii siku ya leo inayoisha dakika 90 zijazo..Siku hii ya August 12 JF tumepata msiba mwingine tena! Tumeondokewa na mwenzetu.. Wengi hatumfahamu kwa sura zaidi ya utambulisho wake bandia.... Lakini kupitia ile mada wana JF wameonesha hisia zao kupitia maandishi yao...! Simfahamu marehemu lakini kifo chake kimeniumiza kwakuwa kimenikuta katikati ya tafakuri kuu juu ya hiki kitu kinaitwa kifo

Wiki iliyopita kanisani kwetu tulitoa huduma ya chakula cha Bwana kwa wasiojiweza majumbani(mimi sasa ni mtumishi wa Mungu madhabahuni) Mmojawapo wa wagonjwa wale ni mama ambaye sura yake imeshindwa kunitoka kabisa.. Alifariki siku mbili baadae!

Hatuna utashi wa kuamua hatima ya pumzi yetu, sisi ni mateka wa kifo na kila sekunde ,kifo kinaondoka na batch iliyo tayari! Kila sekunde! Bila kujali utakufa na nini ama kifo cha aina gani huna utashi wa kujipangia ama kujiamulia... Batch number tusiyoijua sisi ikiwadia huondoka na watu wake! Inatisha sana ujue..!

Na kila batch ni timilifu.. Ina kila aina ya watu
Wema na wabaya
Waume kwa wake
Vijana kwa wazee
Watoto na vichanga
Wagonjwa kwa wazima
Walio na dini na wasio na dini
Viongozi na wanasiasa
Mimba za abortion na mimba zisizotimia

Hii misiba ya kila siku ina mipangilio yake juu ya uwezo wa mwanadamu kuweza walau kuchagua nani wa kufa nani wa kubaki!
Maswali ni mengi nje ya ufahamu wa kibinadamu
Wapendwa wetu wafao wanaenda wapi!?
Je wanatuona na kutusikia?
Me huko waliko wana furaha na amani au ni tabu na mateso?
Je tutaonana nao wapi? Lini? Katika mazingira gani?
Je tutaweza kuwashika kuwakumbatia na kuteta nao mengi na mengi?
Siri ya fumbo la kifo ni kubwa na yenye kuumiza sana

Nimefanya kazi mochwari
Nimewahudumia walio katika hatua za mwisho kuondoka hapa duniani
Wengine nimewasaidia kufa kifo cha faida..cha amani ..lakini kote huko nimeshindwa kukizoea kifo
Nimeandika mada za vifo nimeandika kuhusu sanaa ya kifo lakini kila nikiona ama kusikia roho imeondoka mwili unasisimka upya!

Muda huu niandikapo haya kuna roho zinaondoka! Ni batch nyingine hiyo ndani ya haya masaa 24.. Tumefiwa na kufiwa
Na wazazi wetu
Na watoto wetu
Na ndugu zetu
Na jamaa zetu
Na marafiki zetu nk
Nasi tutakufa na kusahaulika.. Na kuoza nyama na kubaki mifupa michache ambayo kwayo wala tunaweza tusikubukwe sisi tulikuwa nani....!

Niandikapo haya natafakari mengi sana
Kwamba siku moja nitalala kimya , mke wangu ataniamsha sitaamka, watoto wangu wataniita sitaitika..ndugu na jamaa zangu watanitikisa sitikisiki
Roho yangu itakuwa imeachana na mwili wangu na damu haitatembea tena kwakuwa moyo utakuwa umesimama
Nitabaki nafsi inayoona kila kitu kinachoendelea lakini isiyoweza kufanya lolote
Hata pale kaburini nitakapofukiwa na wapendwa wangu kunililia sana na baadae kuniacha pekeyangu mpweke na kiza totoro cha usiku. ..Inatisha sana ujue.. Nimeshindwa kabisa kukizoea kifo
 
Profesa Mshana mbona leo umekuja na thread ya kutishatisha hivi na kutukosesha usingizi.

Dah, mi mtu akiongelea kufa huwa roho inastuka kidogo.
Kifo hakina bingwa wala hakizoeleki..nimepoteza marafiki wa utotoni, nimepoteza marafiki wa shuleni, nimepoteza marafiki wa ukubwani, wazazi ndugu na jamaa!
Huwa nawakumbuka na kuwaombea sana sana..natamani nipate wasaa niongee nao..tupige story tukumbushane mengi[emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji29][emoji29][emoji29]
 
tatizo ni kwamba, ukihofu sana, utakufa, ukiogopa, utakufa, usipoogopa, utakufa.
Nafikiri tunaopata shida zaidi ni sie tunaobaki duniani, hao wanaoondoka wanaanza safari nyingine ambayo hatujui wanajisikiaje kuhusu sie waliotuacha.

Uchungu, simanzi na ubaya wa kifo tunaupata sie tulioachwa na wapendwa wetu.

Nikishawaza hayo, naona bora kila mmoja kwa imani yake, ajiandae na safari kwa kuwa hatujui siku wala saa mwili utakapoacha roho.

Nakazia

Kuishi ni Kristo, kufa ni faida.
 
Niki nacho ni kifo tayari japo kinatisha! Kuwa na mwisho mbaya kama huu.. Wengine wanafurahia dakika zako za mwisho[emoji2815][emoji3064]

mrangi
 
tizo ni kwamba, ukihofu sana, utakufa, ukiogopa, utakufa, usipoogopa, utakufa.
Nafikiri tunaopata shida zaidi ni sie tunaobaki duniani, hao wanaoondoka wanaanza safari nyingine ambayo hatujui wanajisikiaje kuhusu sie waliotuacha.

Uchungu, simanzi na ubaya wa kifo tunaupata sie tulioachwa na wapendwa wetu.

Nikishawaza hayo, naona bora kila mmoja kwa imani yake, ajiandae na safari kwa kuwa hatujui siku wala saa mwili utakapoacha roho.

Nakazia

Kuishi ni Kristo, kufa ni faida.
Kuishi ni Kristo, kufa ni faida.[emoji1752][emoji1752][emoji1752][emoji1548][emoji1545][emoji1545]
 
Sikumbuki vizuri, kuna nyuzi yako inaeleza kuna maisha baada ya kifo, hizo meditation kumbe hazina faida.
Zina faida kubwa sana lakini si kila mmoja wetu ni meditator.. Hapa nimeandika kwa mtazamo wa kutokizoea kifo kwa wake walio wapendwa wetu na si mchakato mzima wa kifo.
 
Kifo hakina bingwa wala hakizoeleki..nimepoteza marafiki wa utotoni, nimepoteza marafiki wa shuleni, nimepoteza marafiki wa ukubwani, wazazi ndugu na jamaa!
Huwa nawakumbuka na kuwaombea sana sana..natamani nipate wasaa niongee nao..tupige story tukumbushane mengi[emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji29][emoji29][emoji29]

Na hapo ndio hua natulia kwa dakika kadhaa natafakari, ni kipi nnafanya hao jamaa hawakufanya wakatangulia mbele za haki?

Ni wema upi au ni kwa sababu gani bado nna uhai? Zingatia hapo hauna control wala mamlaka ya kuchagua ufe lini na ufe namna gani.

Sawa na kusubiria kitu ambacho unauhakika kitawadia lakini haujui ni lini.

Hapo ndio unapoona thamani yetu ni karibia na sifuri. Ustahimilivu na unyenyekevu vingetawala.

Ndipo nikamkumbuka Ayubu...

Mimi nilitoka tumboni mwa Mama yangu nikiwa uchi, na ntarudi nikiwa uchi..hatuendi na kitu huko hata kama tulimiliki dunia yote.
 
Usiku wa kuamkia hii siku ya leo inayoisha dakika 90 zijazo..Siku hii ya August 12 JF tumepata msiba mwingine tena! Tumeondokewa na mwenzetu.. Wengi hatumfahamu kwa sura zaidi ya utambulisho wake bandia.... Lakini kupitia ile mada wana JF wameonesha hisia zao kupitia maandishi yao...! Simfahamu marehemu lakini kifo chake kimeniumiza kwakuwa kimenikuta katikati ya tafakuri kuu juu ya hiki kitu kinaitwa kifo

Wiki iliyopita kanisani kwetu tulitoa huduma ya chakula cha Bwana kwa wasiojiweza majumbani(mimi sasa ni mtumishi wa Mungu madhabahuni) Mmojawapo wa wagonjwa wale ni mama ambaye sura yake imeshindwa kunitoka kabisa.. Alifariki siku mbili baadae!

Hatuna utashi wa kuamua hatima ya pumzi yetu, sisi ni mateka wa kifo na kila sekunde ,kifo kinaondoka na batch iliyo tayari! Kila sekunde! Bila kujali utakufa na nini ama kifo cha aina gani huna utashi wa kujipangia ama kujiamulia... Batch number tusiyoijua sisi ikiwadia huondoka na watu wake! Inatisha sana ujue..!

Na kila batch ni timilifu.. Ina kila aina ya watu
Wema na wabaya
Waume kwa wake
Vijana kwa wazee
Watoto na vichanga
Wagonjwa kwa wazima
Walio na dini na wasio na dini
Viongozi na wanasiasa
Mimba za abortion na mimba zisizotimia

Hii misiba ya kila siku ina mipangilio yake juu ya uwezo wa mwanadamu kuweza walau kuchagua nani wa kufa nani wa kubaki!
Maswali ni mengi nje ya ufahamu wa kibinadamu
Wapendwa wetu wafao wanaenda wapi!?
Je wanatuona na kutusikia?
Me huko waliko wana furaha na amani au ni tabu na mateso?
Je tutaonana nao wapi? Lini? Katika mazingira gani?
Je tutaweza kuwashika kuwakumbatia na kuteta nao mengi na mengi?
Siri ya fumbo la kifo ni kubwa na yenye kuumiza sana

Nimefanya kazi mochwari
Nimewahudumia walio katika hatua za mwisho kuondoka hapa duniani
Wengine nimewasaidia kufa kifo cha faida..cha amani ..lakini kote huko nimeshindwa kukizoea kifo
Nimeandika mada za vifo nimeandika kuhusu sanaa ya kifo lakini kila nikiona ama kusikia roho imeondoka mwili unasisimka upya!

Muda huu niandikapo haya kuna roho zinaondoka! Ni batch nyingine hiyo ndani ya haya masaa 24.. Tumefiwa na kufiwa
Na wazazi wetu
Na watoto wetu
Na ndugu zetu
Na jamaa zetu
Na marafiki zetu nk
Nasi tutakufa na kusahaulika.. Na kuoza nyama na kubaki mifupa michache ambayo kwayo wala tunaweza tusikubukwe sisi tulikuwa nani....!

Niandikapo haya natafakari mengi sana
Kwamba siku moja nitalala kimya , mke wangu ataniamsha sitaamka, watoto wangu wataniita sitaitika..ndugu na jamaa zangu watanitikisa sitikisiki
Roho yangu itakuwa imeachana na mwili wangu na damu haitatembea tena kwakuwa moyo utakuwa umesimama
Nitabaki nafsi inayoona kila kitu kinachoendelea lakini isiyoweza kufanya lolote
Hata pale kaburini nitakapofukiwa na wapendwa wangu kunililia sana na baadae kuniacha pekeyangu mpweke na kiza totoro cha usiku. ..Inatisha sana ujue.. Nimeshindwa kabisa kukizoea kifo
giphy.gif
Aliyekufa nan Tena wa JF?
 
Na hapo ndio hua natulia kwa dakika kadhaa natafakari, ni kipi nnafanya hao jamaa hawakufanya wakatangulia mbele za haki?

Ni wema upi au ni kwa sababu gani bado nna uhai? Zingatia hapo hauna control wala mamlaka ya kuchagua ufe lini nabufe namna gani.

Sawa na kusubiria kitu ambacho unauhakika kitawadia lakini haujui ni lini.

Hapo ndio unapoona thamani yetu ni karibia na sifuri. Ustahimilivu na unyenyekevu vingetawala.

Ndipo nikamkumbuka Ayubu...

Mimi nilitoka tumboni mwa Mama yangu nikiwa uchi, na ntarudi nikiwa uchi..hatuendi na kitu huko hata kama tulimiliki dunia yote.
Hatukuja na kitu duniani wala hatutoki na kitu ila roho iliyopondeka utakwenda nayo
Uje ndani ya Yesu.. Tua mizigo (ya dhambi)safari imekwisha wadia(kifo)
 
Back
Top Bottom