Najaribu kukizoea kifo nashindwa kabisa!

Kikija kingine maumivu na taharuki vinarejea upya
Mkuu Mshana naomba msaada wako mkuu .Nyumbani wanga wamekuwa wanakuja usiku mara wawashe taa .Mara wafungue MAJI na hata kuwasha taa za gari naomba msaada please
 
Mkuu Mshana naomba msaada wako mkuu .Nyumbani wanga wamekuwa wanakuja usiku mara wawashe taa .Mara wafungue MAJI na hata kuwasha taa za gari naomba msaada please

Hii inafanana na zile ishu za haunted house... Inawezekana sio wachawi bali ni maroho ...koroga maji yenye chumvi ya mawe nuiya huku ukimwaga kuzunguka nyumba nzima ndani na nje
Mmh mpaka kuwasha taa za gari? uko mkoa gani? Hili tatizo ni la muda gani? Linatokea mara ngapi kwa wiki?
 
Usiku wa kuamkia hii siku ya leo inayoisha dakika 90 zijazo..Siku hii ya August 12 JF tumepata msiba mwingine tena! Tumeondokewa na mwenzetu.. Wengi hatumfahamu kwa sura zaidi ya utambulisho wake bandia.... Lakini kupitia ile mada wana JF wameonesha hisia zao kupitia maandishi yao...! Simfahamu marehemu lakini kifo chake kimeniumiza kwakuwa kimenikuta katikati ya tafakuri kuu juu ya hiki kitu kinaitwa kifo

Wiki iliyopita kanisani kwetu tulitoa huduma ya chakula cha Bwana kwa wasiojiweza majumbani(mimi sasa ni mtumishi wa Mungu madhabahuni) Mmojawapo wa wagonjwa wale ni mama ambaye sura yake imeshindwa kunitoka kabisa.. Alifariki siku mbili baadae!

Hatuna utashi wa kuamua hatima ya pumzi yetu, sisi ni mateka wa kifo na kila sekunde ,kifo kinaondoka na batch iliyo tayari! Kila sekunde! Bila kujali utakufa na nini ama kifo cha aina gani huna utashi wa kujipangia ama kujiamulia... Batch number tusiyoijua sisi ikiwadia huondoka na watu wake! Inatisha sana ujue..!

Na kila batch ni timilifu.. Ina kila aina ya watu
Wema na wabaya
Waume kwa wake
Vijana kwa wazee
Watoto na vichanga
Wagonjwa kwa wazima
Walio na dini na wasio na dini
Viongozi na wanasiasa
Mimba za abortion na mimba zisizotimia

Hii misiba ya kila siku ina mipangilio yake juu ya uwezo wa mwanadamu kuweza walau kuchagua nani wa kufa nani wa kubaki!
Maswali ni mengi nje ya ufahamu wa kibinadamu
Wapendwa wetu wafao wanaenda wapi!?
Je wanatuona na kutusikia?
Me huko waliko wana furaha na amani au ni tabu na mateso?
Je tutaonana nao wapi? Lini? Katika mazingira gani?
Je tutaweza kuwashika kuwakumbatia na kuteta nao mengi na mengi?
Siri ya fumbo la kifo ni kubwa na yenye kuumiza sana

Nimefanya kazi mochwari
Nimewahudumia walio katika hatua za mwisho kuondoka hapa duniani
Wengine nimewasaidia kufa kifo cha faida..cha amani ..lakini kote huko nimeshindwa kukizoea kifo
Nimeandika mada za vifo nimeandika kuhusu sanaa ya kifo lakini kila nikiona ama kusikia roho imeondoka mwili unasisimka upya!


Muda huu niandikapo haya kuna roho zinaondoka! Ni batch nyingine hiyo ndani ya haya masaa 24.. Tumefiwa na kufiwa
Na wazazi wetu
Na watoto wetu
Na ndugu zetu
Na jamaa zetu
Na marafiki zetu nk
Nasi tutakufa na kusahaulika.. Na kuoza nyama na kubaki mifupa michache ambayo kwayo wala tunaweza tusikubukwe sisi tulikuwa nani....!

Niandikapo haya natafakari mengi sana
Kwamba siku moja nitalala kimya , mke wangu ataniamsha sitaamka, watoto wangu wataniita sitaitika..ndugu na jamaa zangu watanitikisa sitikisiki
Roho yangu itakuwa imeachana na mwili wangu na damu haitatembea tena kwakuwa moyo utakuwa umesimama
Nitabaki nafsi inayoona kila kitu kinachoendelea lakini isiyoweza kufanya lolote
Hata pale kaburini nitakapofukiwa na wapendwa wangu kunililia sana na baadae kuniacha pekeyangu mpweke na kiza totoro cha usiku. ..Inatisha sana ujue.. Nimeshindwa kabisa kukizoea kifo
Hata mimi nilikua na hofu juu ya kifo. na hofu watu wengi wanayo na mara nyingi hali hii usababishwa na mambo ya kutishana sisi kwa sisi kwa bahadhi ya watu kupotosha ukweli juu ya neno la MUNGU hasa viongozi wa dini .

MTU akifa wao wanasema amelala mauti na hapo anasubiri siku ya mwisho hili afufuliwe aende kuojiwa

Baadhi ya madhehebu kama wakatoriki.wanadai kwamba roho inapo uacha mwili uenda baradhani kwa MUNGU kungoja siku ya mwisho hili iukumiwe na endapo kama ikikutwa na dhambi udumbukizwa kwenye tanuru la moto usio isha itaungua kwa kipindi kisicho kua na mwisho yaani milele na milele kwakua roho aifi. nawakati akuna sehemu kwnye biblia yao inasema hivo

Hofu yangu kuhusu kifo ilikuja kuondoka na kuacha kuogopa kifo pale tu nilipo gundua kwamba izi ni njia za mzungu kuweka hofu kwa watu hili watende mema kwa kuofia kwamba wakitenda mabaya kuna kuadhibiwa siku ya mwisho.


Naamini MWENYEZI MUNGU ni wa upendo mwingi rehema na huruma visivyo pimika na ni MUNGU ajuaye yote sasa kama ametuleta duniani alijua kabisa tutatenda matendo wanayoita dhambi kwakua atujakamilika tutatubu na kurudia tena kwa nini asinge tengeneza namna ya sisi kuishi bila kutenda dhambi kwakua yeye ni MUNGU mwnye nguvu na upendo kwa sisi viumbe vyake hili tusimkosee

Napata mashaka na hivi wanavyo hita vitabu vitakatifu naona kabisa ni kama waliandika sheria za dini zao watakazo zifuata wafuasi wao kwa lengo la kuwatawala.


All in all sina ofu na kifo baada ya kuyajua hayo ninajitaidi kutenda matendo mema katika maisha yangu.
 
Na mwanamke mwenyewe aliyesifiwa hufa sasa du!.
9e6d73c6e75778a990ac90c279266812--horror.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom