Utata mkubwa kifo cha Dkt. Mkamilo wa TARI

Bunge la Wananchi

New Member
Jan 30, 2023
3
4
TARI_3.jpg
Dk. Mkamilo akizungumza wakati wa kukabidhi Ofisi baada ya kumaliza muda wake kama Mkurugenzi wa TARI hii ilikuwa Februari 20, 2024 baada ya kutoka kwenye tukio hilo akafariki tarehe 2.3.2024

Kifo cha Dk. Mkamilo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TARI kimeacha simanzi na huzuni kubwa kwa wanataaluma wa masuala ya utafiti wa Kilimo ndani na nje ya Tanzania.

Kifo cha Dk. Mkamilo kimeacha maswali mengi sana kutokana na utata uliopo kwani Dk. Mkalimo hadi anastaafu alikuwa na afya njema na siku ya tarehe 20 Februari 2024 alikwenda kukabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi mpya Dk. Thomas Bwana na baada ya tukio hilo akafariki dunia huku chanzo cha kifo chake hadi sasa kikiwa hakijulikani.

Sio Serikali, wala Wafanyakazi wa TARI wanaojua sababu ya Kifo cha Dk. Mkamilo, suala hili limeacha simanzi kubwa sana huku kukiwepo minong'ono mingi kuhusu kifo cha Dk. Mkamilo.

Wanaojua ukweli wa suala hili watuambie ili kuondoa sintofahamu kubwa iliyopo sasa.

 
Wengi wanasema Mzee kapata mshtuko baada ya kuona mkeka umemuacha mapema..
Ilitakiwa astaafu mwezi May 2024
 
Back
Top Bottom