Last Philosopher
Member
- Nov 2, 2023
- 60
- 50
Tukisia neno kifo huwa tunaingiwa na taharuki na kuchanganyikiwa kwa kuona mwisho wa mtu umefika. Embu tujiulize, kwanini tunahofu sana na kifo?. Ni kweli kifo ni kitu kibaya hivyo kwetu. Au ni kwasababu matendo yetu mengi mabaya sana haya endani na inavyopaswa tunahofia kitatokea nini kwetu. Pengine hatutaki kumaliza raha zetu tunazopata kwenye maisha tunataka tubaki nazo milele.
Kwa tafsiri zetu za kifo tunavyo sikia ni kama mwanzo wa mateso makubwa yasiyo na mfano, na jinsi tunavyoishi maisha yetu inaonyesha ni vigumu kuendana na matakwa ya kufikia sehemu salama hofu huanzia hapo ya kuogopa kifo. Ila hakuna aliye thibitisha kuwa tiketi ya kutenda mema itakusaidia wakati unaishi ama ukishamaliza kuonana na binadamu.
Na akili zetu hazipendi kuishi bila kujua mategemeo yajayo, kwa kuishi kwa akili tu kuwa na mashaka lazima tuogope. Akili zetu zinapenda uhakika wa usalama. Kinachotokea ni hatuelewi maana ya kifo, akili haijawahi kupata jibu kamili ndio maana ni kitendawili mpaka sasa. Je, inakuwaje kama kuna maisha zaidi ya tunachoweza kufikiri, tunaweza kuishi bila hofu ya kifo tunayo itengeneza?.
Tunakuwa na mahusiano mabaya na kifo kwakuwa tumekuwa waathirika wa akili zetu kimawazo. Akili zetu zinajihusisha sana na kuwa salama kwenye wakati kuliko kujihushisha na kinachoendelea muda uliopo chenye uhalisia. Kama tutashindwa kuwa makini na kuupa thamani wakati uliopo kwa kuushi kwa ufahamu zaidi kujitambua nnjee ya vikomo vya akili kwenye mawazo yetu na kubaki na uhalisia wa maisha tu basi tutaishi kwa furaha na amani yote na hatutohisi kama kifo ni kupoteza kitu kwetu.
Tuna mahusiano mabaya na kifo kwakuwa tumeshindwa kujitambua na tunaweka hofu ya kimawazo mbele. Kama uliweza kuwa na mwanzo basi na mwisho unakusubiri na sio jambo lakushangaza kwakuwa viumbe wote ndio mzunguko wetu. Ila ukiwa unataka kukipangana nalo kwa kutojitambua na wewe ni moja wapo wa mzunguko huu itakupashida.
NB: Kutojielewa kwako kwa kuishi kwenye vikomo vya akili kimawazo ndio vinakupashida ya hofu ya kifo. Chamuhimu ni kuishi vyema sasa kwa upendo, amani na furaha yote. Thamani ya maisha si kuwa marefu bali kwa muda wako umeyaishi vipi.