Naishindaje hofu ya kifo inayoniandama?

Jua tu kifo ni tukio la asili, halikwepeki, ponda mali kufa kwaja, subiri kama unavyosibiri X-mas na mwaka mpya
 
Ingekuwa baba na mama wamekufa na wewe ungekufa kabisa eti eeh.

Kifo kipo kinaishi Kama unavyoishi muda wowote cha weza kukukuta.

Vile hujafa ishi kama hutakufa milele,
 
Wakuu salama?

Hivi karibuni, hasa kwa mwaka huu wa 2021 nimoepoteza watu wa karibu wengi sana tangu huu mwaka uanze; Nimepoteza wazee wangu-baba wakubwa wanne, pia nimepoteza marafiki zangu wale wa inner cycle watatu,akiwemo rafiki yangu mmoja wa karibu sana aliefariki kwa kansa ya utumbo, na jamaa zangu wengine kadhaa (ndugu wa mbali na marafiki).

Pia, kuna vifo viwili vya wana JF vya hivi karibuni ambavyo vimenigusa sana, cha ip_mob na warumi hawa watu nilikua nawakubali sana hapa JF japo sijawahi kukutana nao uso kwa uso.

Hivi vifo kwa huu mwaka vimenifanya nimekua mtu wa hofu sana juu ya kifo; Yaani sasa hivi nawaza sana juu ya kifo na nashikwa na uoga wa kutisha hadi natetemeka.

Mara nyingi usiku nakosa kabisa usingizi, nawaza juu ya kifo hadi machozi yananitoka. Saa zingine naogopa hata kulala usiku na kuufukuza usingizi, maana nawaza kuwa naweza nikalala nisiamke tena, nikapotelea usingizini na kuaga dunia.

Hii hali naona imeanza kuathiri shughuli za mihangaiko yangu, kwani mchana nakua nimechoka sana na pia inanikosesha amani kabisa naishi maisha ya wasiwasi sana.

Ndugu zangu, nimekuja humu kuwauliza je nyie wenzangu mnatumia mbinu gani kuondoa hofu juu ya kifo au kuwafanya msiwaze au kuogopa kifo?

Nimejaribu kuwa nasali sana na kwenda kanisani kila siku, nimeongea pia na mchungaji na amenifanyia maombi na kunipa nasaha, lakini bado imekua ngumu sana kwa mawazo na uoga huo kunitoka.

Naomba mnisaidie ndugu zangu nawezaje kupambana na hii hali?

Naomba mnisaidie wadau.
Ahsanteni.
Kifo kinapo kuja haupo tena, ukiwa mzima usiwaze kifo...maana kikija hukioni unakuwa haupo.wanao baki ndio hubaki na hofu.Kifo ni sawa na usingizi.Unapo panda kitandani kulala hujui ni muda gani uli ishia usingizini na huna kumbukumbu yoyote ya jinsi usingizi ulivyo kujia ni sawa na kifo pia.
 
Wewe kuwa tu na matendo mazuri, uliambiwa baada ya kifo kuna maisha mazuri Mbinguni kwa Baba. Kifo ni tukio la asili kama matukio mengine. Subiri kifo kama unavyosubiri mwaka mpya au X-mas.
 
Ahsante mkuu.... Ulichokisema ni sawa kabisa.
Sasa mimi inanitokea tu mawazo ya hofu ya kifo yanatawala akili yangu, japo nafahamu yote uliyoandika hapo.... Sasa nitumie mbinu ipi kuyafukuza hayo mawazo au kuzuia yasije?
mkuu nakushauri kama unaweza kufanya meditation fanya itakusaidia sna mkuu ata kwenye mambo mengne mengi yanayokukabili.
 
Kwanza pole kwa hali hiyo na hongera kwa kuwa muwazi.

Kwa hali yako kuna mawili, na nitayagusia yote hapa iwe msaada kwa wengine pia;

• Kwanza unaweza ukawa unasumbuliwa na hiyo hali kutokana na hayo uliyoyapitia ya kupotelewa na watu wako wa karibu kwa kipindi kifupi, kwahiyo imekupa death anxiety ( hofu ya kifo) akilini mwako kitaalamu inaitwa Thanatophobia

•Pili unaweza pia ukawa unasumbuliwa na gastroesophageal reflux disease ( GERD ) au Gastritis, au ulcers. Haya magonjwa pia hupelekea mgonjwa kupata hali kama ya kukata roho, kuona anaishiwa pumzi wakati mwingine as if anaenda kufa. Stress, ulaji mbaya unaeza ukachangia hii hali.

Solution:

• Kama unahisi una dalili nyingine pia za kuumwa tumbo au tumbo kujaa gesi na constipation then likely hii ndo sababu ya tatizo lako na uende hospital mapema

• Kama sio sababu ya kwanza hiyo then ni death anxiety.

Kwa kuanzia nikutoe hofu mkuu, siku zote anayekufa hajui kwamba sasa nakufa, ikitokea mtu akajua haitaambatana na hofu.
Yaani ukiona unahisi kufa jua huwezi kufa hata siku moja, kifo ni siri na huja bila mtu kuwaza au kujua, ndo maana utasikia nilikuwa naye tu hapa akaniambia nakuja ila ndo akaenda moja kwa moja.

Sasa basi popote ukiisikia hiyo hali iambie nafsi yako mwenyewe maneno haya, Kifo ni Siri aijuaye Mungu, ukiona unahisi kufa huwezi kufa kweli maana ni siri anayeijua Mungu, hivyo kufa kwako itakuwa kama uliweza kuona future kitu ambacho sio kweli ( kwa lugha nyepesi huwezi kupiga chabo kitakachotokea baadaye ) kwa namna hii endelea kujiambia kila mara mpaka ile anxiety na hofu zitapungua na kuisha.. Hii njia kitaalam inaitwa Exposure Therapy, lakini vile vile usali kwa imani yako

Vile vile usikae sana peke yako, kaa hata kwenye vijiwe vya michezo au chochote unachoweza kuenjoy na watu wengi au fuatilia vipindi vya kukukeep busy.


Pole sana chief, ukizingatia hayo hiyo hali itaisha mapema hata wewe mwenyewe utasahau
mkuu andres umeongea ukwel mtupu , mimi nilikua na hali kama hiyo mpka kuna mda nukahisi nausikia moyo unadunda nikiwa kwenye majukumu yangu , nimetumia zaid ya ml 3 kupima vipimo vyote vya moyo , washauri wa saikologia , nilijipanga kwenda india nikihisi nitakua na tundu kwenye moyo, mtu mmoja simple tu alinisanua ni vidonda vya tumbo nmesakata miti shamba , pombe stress na ulaji mbovu nmepiga chini now nipo poa mno.
 
Hii mbinu ya kushinda hofu ya mauti au mauti yenyewe Naweza kukupatia ila itafanya kazi tu endapo umeokoka
 
Back
Top Bottom