Naishindaje hofu ya kifo inayoniandama?

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,813
Wakuu salama?

Hivi karibuni, hasa kwa mwaka huu wa 2021 nimoepoteza watu wa karibu wengi sana tangu huu mwaka uanze; Nimepoteza wazee wangu-baba wakubwa wanne, pia nimepoteza marafiki zangu wale wa inner cycle watatu,akiwemo rafiki yangu mmoja wa karibu sana aliefariki kwa kansa ya utumbo, na jamaa zangu wengine kadhaa (ndugu wa mbali na marafiki).

Pia, kuna vifo viwili vya wana JF vya hivi karibuni ambavyo vimenigusa sana, cha ip_mob na warumi hawa watu nilikua nawakubali sana hapa JF japo sijawahi kukutana nao uso kwa uso.

Hivi vifo kwa huu mwaka vimenifanya nimekua mtu wa hofu sana juu ya kifo; Yaani sasa hivi nawaza sana juu ya kifo na nashikwa na uoga wa kutisha hadi natetemeka.

Mara nyingi usiku nakosa kabisa usingizi, nawaza juu ya kifo hadi machozi yananitoka. Saa zingine naogopa hata kulala usiku na kuufukuza usingizi, maana nawaza kuwa naweza nikalala nisiamke tena, nikapotelea usingizini na kuaga dunia.

Hii hali naona imeanza kuathiri shughuli za mihangaiko yangu, kwani mchana nakua nimechoka sana na pia inanikosesha amani kabisa naishi maisha ya wasiwasi sana.

Ndugu zangu, nimekuja humu kuwauliza je nyie wenzangu mnatumia mbinu gani kuondoa hofu juu ya kifo au kuwafanya msiwaze au kuogopa kifo?

Nimejaribu kuwa nasali sana na kwenda kanisani kila siku, nimeongea pia na mchungaji na amenifanyia maombi na kunipa nasaha, lakini bado imekua ngumu sana kwa mawazo na uoga huo kunitoka.

Naomba mnisaidie ndugu zangu nawezaje kupambana na hii hali?

Naomba mnisaidie wadau.
Ahsanteni.
 
Ukiogopa sana utakufa, usipokua na hofu hali kadhalika utakufa, usipoogopa utakufa, na hauwezi kufanya chochote kuzuia kufa.

Kikubwa shukuru kila iitwapo leo kwamba umepata nafasi ya kuifurahia siku. Ni kitu adimu na tunapewa tu sio kwamba unafanya jitihada yeyote kustahiki.

Siku ukifa, wanaopata shida ni hawa unaowaacha, yanini kujisumbua na huzuni wakati wewe utakua kwenye hali tofauti kabisa na hautaweza kufanya chochote kuhusu hawa uliowaacha?

Hapo ndio unaona kumbe hofu kubwa haisaidii kitu wala kubadili hali halisi kwamba maadam tumezaliwa, kifo hatuwezi kukiepuka.

Ndipo nalimkumbuka Mtume Paul aliposema kuishi ni Kristo, kufa ni faida.
 
Ndo maana najitahidi sana kuishi na kuenjoy maisha kwa kadri ninavyoweza sababu najua siku yeyote isiyo na jina nitaondoka hapa duniani na hilo hali epukiki ..
Unatumia mbinu gani kuyapotezea mawazo ya kifo mkuu?
 
Ukiogopa sana utakufa, usipokua na hofu hali kadhalika utakufa, usipoogopa utakufa, na hauwezi kufanya chochote kuzuia kufa.

Kikubwa shukuru kila iitwapo leo kwamba umepata nafasi ya kuifurahia siku. Ni kitu adimu na tunapewa tu sio kwamba unafanya jitihada yeyote kustahiki.

Siku ukifa, wanaopats shida ni hawa unaowaacha, yanini kujisumbua na huzuni wakati wewe utakua kwenye hali tofauti kabisa na hautaweza kufanya chochote kuhusu hawa uliowaacha?

Hapo ndio unaona kumbe hofu kubwa haisaidii kitu wala kubadili hali halisi kwamba maadam tumezaliwa, kifo hatuwezi kukiepuka.

Ndipo nalimkumbuka Mtume Paul aliposema kuishi ni Kristo, kufa ni faida.
Ahsante mkuu.... Ulichokisema ni sawa kabisa.
Sasa mimi inanitokea tu mawazo ya hofu ya kifo yanatawala akili yangu, japo nafahamu yote uliyoandika hapo.... Sasa nitumie mbinu ipi kuyafukuza hayo mawazo au kuzuia yasije?
 
Unatumia mbinu gani kuyapotezea mawazo ya kifo mkuu?
Kuna kipindi nilianza kuwa na hofu kama yako ila inakubidi tu kukubaliana na ukweli kwamba kufa kupo na hata iweje utakufa tu .. hivyo nirudie point yangu " enjoy as much as you can " kama una uwezo safiri kimatembezi mkoa au hata nchi nyingine kutegemea na uwezo wako na usi ruhusu mtu kukupa stress yani ifanye kila siku kuwa holiday ( yes it's possible if you decide ) ..
 
Mkuu unahofu kwamba ukilala pengine utafia usingizini usiamke kesho - kwangu mie kungekuwa na kuchagua aina ya kifo ningechagua hiki.

Process ya kuteseka kwa kuugua, na pengine kwa muda mrefu, na kuwa tegemezi kwa kutojiweza, ndiyo tishio.
 
Ahsante mkuu.... Ulichokisema ni sawa kabisa.
Sasa mimi inanitokea tu mawazo ya hofu ya kifo yanatawala akili yangu, japo nafahamu yote uliyoandika hapo.... Sasa nitumie mbinu ipi kuyafukuza hayo mawazo au kuzuia yasije?

Kufaham haya mambo yote ni jambo moja, lakini kukubaliana na huo ukweli ni jambo lingine.

Hatua unayotakiwa kuifanya nikuiambia nafsi yako kwamba kifo kipo, ipo siku utaondoka, utaanza maisha mengine. Hii huzuni tunakua nayo mpendwa wetu akiondoka itakua non of your business siku yako ikifika, wewe utakua unapambana na miamala mingine tofauti kabisa ( hakuna hata mmoja wetu anaejua nini hua kinaendelea huko). Sasa usijitaabishe kwa mambo usiyoyajua.

Kama una imani kwamba ipo hukumu baada ya haya maisha, ishi njia iwapasayo watakaokula pepo huko mbinguni.
 
Mkuu, huo upweke uliyonao ndio chanzo cha mawazo na hofu uliyonayo. Tafuta mtu uishi nae, iwe mpenzi au hata ndugu yako. Maana muda mwingi baada ya kazi utakuwa ukipiga nae story mpaka wakati unasinzia.

Hilo ni tatizo la muda tu na baadae hutoweka
 
Kuna kipindi nilianza kuwa na hofu kama yako ila inakubidi tu kukubaliana na ukweli kwamba kufa kupo na hata iweje utakufa tu .. hivyo nirudie point yangu " enjoy as much as you can " kama una uwezo safiri kimatembezi mkoa au hata nchi nyingine kutegemea na uwezo wako na usi ruhusu mtu kukupa stress yani ifanye kila siku kuwa holiday ( yes it's possible if you decide ) ..
Ok... Ahsante mkuu.
 
Back
Top Bottom