Naishi naye ndio, Lakini...

Naishi naye ndio, Lakini...

Tafuta wazee wako eleza huu ukweli hakika utapata jibu zuri sana,,,,hili jambo haliitaji elimu ya Digrii kuliamua zaidi ya busara za wazee maana unaweza jikuta unafanya maamuzi ya ajabu ambayo yanaweza kugharimu maisha ya huyo mwanamke itakuletea hata wewe shida,,,,,

Ila zingatia hili neno "Mwanamke ni rahisi kusamehe ila mgumu kusahau" tegemea kuwa mtumwa kwake maana hilo ni kovu lisilofutika,,,hapo utaishi kwa mashaka maisha yako yote
Kuna jambo la kujifunza kwakweli...
 
Mistake umefanya umeirudia rudia Mara kumi kumi hayo yamekuwa maamuzi.

From the beginning kabisa ulipogonga siku ya kwanza na nyege zikaisha,akili zikarudi kichwani, ulipaswa kuvunja mahusiano..

Umekaa na mwanamke miaka mitatu then uje utwambie huna hisia nae haya Ni maneno ya kipuuzi kutoka kinywani mwa Mwanaume asiyejua anataka nini

Mtu asiye na msimamo hapaswi kuchagua lolote endelea tu na huyo mwanamke uliyelala nae Miaka tatu zimwi likujualo alikumalizi
 
Kama hukumpenda why udinye bila ndomu??? Alafu kizembe tu unampa mimbaa..bora bhasi upate dhambi ya kutoa kuliko kumpa mateso mwanao na huyo mwanamkee...
Vipi Kuhusu kumsubirisha dada wa watu miaka mingi akisubiri ndoa, akamsaliti akasamehewa, unaona anastahili kuachwa kisa kampa mimba mwanamke mwingine, fikiri angekuwa ameshamwoa na akampa mimba mwingine ungeshauri nini, think twice mkuu
 
kwa sababu umeshayakoroga..

Fanya hili;huyo mchumba naye mtie mimba,ili huyu baby mama wako ajae sumu aondoke mwenyewe..

utekelezaji mwema
 
Vipi Kuhusu kumsubirisha dada wa watu miaka mingi akisubiri ndoa, akamsaliti akasamehewa, unaona anastahili kuachwa kisa kampa mimba mwanamke mwingine, fikiri angekuwa ameshamwoa na akampa mimba mwingine ungeshauri nini, think twice mkuu
Sasa mkuu angejua kama huyo mwingne ni wa muhimu asingemwagia ndanii...!! Kwanza huyo mwingine anamchoraa tuu...Kuna siku ataujua ukweli kuhusu huyo anaedai ana future naee hakika atarudi hapa kushuhudiaa... Hakuna mwanamke utamsaliti na kumpa mimba mwanamke mwingine alafu akakusamehe kizembe hivyooo Trust me Hayupooo tena mpo mbaliii aisee huko ukute ashaanza maisha yake na jamaa anamlaaa na wana future yaooo Wanawake usicheze nao mkuuu
 
Pole sana kijana mimi najua unapitia ugum kiasi gani coz hata mimi tatizo kama hilo lishanikuta lkn nashukuru liliisha.
Umeshafanya bonge la mistake kwanza kuendelea kuishi naye huyo babe mama mda wote huo wakati huku unaona huna hisia naye kabisa. Kwa sababu hiyo baki na huyohuyo babe mama.
Huyo mchumba mwingine achana naye, huna namna nyingne ukiforce kumuacha babe mama na kumuoa huyo mchumba utakuja kutusimulia hadithi nyingine.
Best wishes
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...

HAUJATOFAUTIANA SANA NAMIMI MKUU,SOMA YANGU KISHA MWISHO CONCLUDE KAMA MIMI

Nilikuaga sina mpenzi kabisa Tangu niamue kuanza maisha,nilijua kujiiingiza ktk mahusiano ntapotea haraka so nikaamua kuwa busy na maisha yangu na mihangaiko..lakini katika pitapita za hapa na pale siku moja nikakutana na rafiki yangu school mate tuliosomaga nae shule zamani kidogo,Alikua ni mdada(jina lake ni RODA) tulipokuaga shule nilikua natoka na Pacha ake maana wako mapacha so tulikua tunaitanaga SHEMEJII...

basi siku hiyo aliponiona namimi kumuona tu akaniita Shemejiiiii namimi kumuangalia sura kama inakuja basi akanambia mimi Flani baada ya kuntambulisha nilimkumbatia kwa furaha sana...siku hiyo tukakaa mahali tukapiga story nikamuuliza huku unafanya nini akanambia nipo Chuo,na mimi nkamwambia nipo tu nahangaika na maisha Basi tulipiga story baadae tukaachiana namba tukaachana kila mtu akaendelea na ratiba zake.

Maisha yangu yaliendelea kama kawaida,sinaga mpenzi mimi wala sikua na time na huo muda maana hata kazi nlizokua nafanya hamna mdada nitaemtongoza akanikubali zaidi ya kunidharau so nikawaga zangu nimepata rafiki hata wa kuchati HATA kwenye simu..RODA akawa rafiki angu tukawa tunawasiliana na kwa mara ya kwanza nikapata rafiki wa kwenda hata mtembelea,alikuaga anakaa Hostel.

Nikawa naenda mara kadhaaa,tukazoeana sana na Roda majina yetu ni yale yale yakuitana Shemeji shemejii,na tulikua tukimaanisha na tuliheshimiana ipasavyo...kama kawaida hamna kazi unayofanya ukakosa majanga,siku moja nikiwa kazini kuna mtu alinitibua,nilikasirika nikainua Chupa piga Kichwani Mtu akalala chaliiiii...watu wakaja nikabebwa Juu Juu hadi polisi niliyempiga kakimbizwa Hospitali.

Kumbuka tangu mwanzo sinaga rafiki nashukuru Mungu nilikutanaga na RODA,basi baada ya lile janga nikapelekwa kituoni nikiwa njiani nikampigia RODA nikampa taarifa,basi nikapelekwa ndani nikatulia..kesi ikaenda nikiwa pale pale lock up mapolisi thamana hawataki kunipa maana wanadai hali ya mgonjwa bado mbaya so nisubiri...mahakamani hawataki nipeleka basi kituoni pakageuka GETO nikawa naletewa chakula na Roda asubuhi mchana jioni.

Baadae lile sooo RODA alilimaliza kwa gharama zaidi ya 500,000 nikatoka,maisha yakaendelea nikamshukuru roda maisha yakaendelea...kazi kama kawaida Roda akawa msaada mkubwa sana maisha ni mwangu,ki ufupi alifanya MENGI ambayo siwezi maliza yasimulia hapa.

Siku moja nikiwa zangu nyumbani nikawa nawaza na kujiuliza hivi kwanini RODA ananisaidia hivi namimi sio mpenzi wake?? yani urafiki tu ananisaidia hivi? anakuja home ananisaidia kufanya usafi,kufua,nk nikipata majanga ana clear yani ni mwanamke asiekubali kuona baya linatokea kwangu ingali yeye yupo na anashuhudia.

Nikasema Huyu anafaa kabisa kuwa mpenzi wangu,acha nifanye mpango nimwambie ukweli kuwa namuhitaji awe mpenzi wangu kabisa,RODA ni mwanamke aliyeokoka namfahamu tangu Secondary mwana UKWATA mwenzangu,walikuaga ni hatari kwa maombi sasa nilivyokumbuka hilo nikaona yes Huyu huyu ananifaaaa.

Siku ikafika nikamwita roda nikamweleza haja na nia yangu ya kuwa nae..ki ukweli Alinitolea nnje,sikutaka muudhi wala mkera nikakubaliana nae ila nikatulia siku nyingine tena tena..sikuchoka msumbua na kumuomba kwa Machozi tena,basi siku moja akaniita akanambia SAM njooo,siku hiyo nilitoroka kazini nikaenda kufika Akanambia NIMEKUKUBALIA lile swala lako lakini soma hiki cheti kwanza.

Akanipa cheti ambacho nakumbuka tulipewaga zamani tukiwa FORM TWO kinachohusu SEX engagements..NI kiapo walikula wakaekewa maombi kabisa kwamba THEY WILL NOT ENGAGE THEMSELVES INTO ANY SEXUAL INTERCOURSE UNTILL MARRIAGE...basi niliona nikamuuliza unamaanisha nini?? akanambia SAM nakua na wewe ila SEX NO mpk tutakapo oana,namimi ki ukweli kutoka moyoni sikumuhitaji roda kwa ajili ya SEX nilimpenda kwa anavyojitoa ktk maisha yangu so SEX haikua ishu kbsa kwangu so NIKAMKUBALIA na nikamuahidi.

Tukawa rasmi wapenzi ambao hatu sex..akawa kila weekend akiwa hana vipind anatoka hostel anakuja kwangu analala hadi j3 ila NO SEX mzeee ni kulala kama dada na kaka ila ni wapenzi though romance zilikuepo...basi maisha yakaendelea na nikawa mwaminifu kweli,tutaenda kuoga wote tutafanya kila kitu ila siwezi hata mtamani,ikafika kipindi hata sikua na hamu hata na hyo romance.

Maisha yakasonga ila namimi nikawa na mchepuko wangu nnje(ambae ndio mama watoto wangu wa sasa),ukawa unanipoza kila ukitaka kuja kwangu naupiga calender maana sikua nataka apafahamu asije akaja siku mimi niko na roda..so maisha yakaendelea na kwakua nae alinipenda alikua haoni shida lipia Hotel tulale then kesho yake nirudi home bhasi maisha yakaenda hivyo.

Baadae Roda alimaliza chuo akawa anatafuta kazi so akaja kuishi HOME kbsaaa..huku namimi nikiendelea kukipiga na mama watoto..siku moja mimi nikajitoa ufahamu Nikasema hapa lazima niseme ukweli Nikamwambia mama watoto watoto wangu bwana eeeh mimi naishi na mtu..kuna moja mbili tatu na nne HATUSEX so namimi nimeshindwa kukaa muda wote huo ndio kuja kukupata wewe.

Ki ukweli wife hakuniamini hata kidogo eti nalala na mwanamke halafu si do nae,basi akanambia nimthibitishie nikafanya kila alichotaka na hatimae akaja akaamini,ishu ikaja WIFE anataka niachane na RODA nimwambie asepe kwao ili tuishi na yeye,hapo kwangu pakawa pagumu vibaya mno sasa namuachaje RODA kwa yote alonifanyia namuachaje yani namfukuzaje?

Bwna wakati nikiwa nawaza hayo kumbe roda Alishanishtukia siku mingiiiiii Kua nina mchepuko akawa anauchunaga tuu anasubiria kuona mwisho wake....kabla hata mimi kumuanza siku moja roda akanambia wakat natoka kwenda kazini SAM msalimie MAGE (ndio wife sasa) daaah moyo ulipasuka PAAAH

Nikasepa kazini ila hiyo siku nzima nilihisi kama roda ananitokea yani nilikua natamani kufa,kila kitu sikioni vizuri,masaa yanaenda nikifkiria kurudi HOME ndio nahisi kama naenda kuchomwa kisu na roda leo nikiwa usingizini,bwana niliwehuka.

Ndugu yangu nilichofanya nilimrudia mchepuko (wife) nikamwambia bwana Mimi kumwambia RODA tuachane nimeshindwa,wewe si unataka kukaa na mimi na unanipenda,basi yale yote alionitendea roda tumlipe kwa kumuachia vitu vyote ndani ya ile nyumba..sisis twende tukapange..THANK GOD nikaeleweka...nikarudi home kwa mara yya mwisho nikawa namuangalia RODA uchungu unanijia sema ndo ntafanyaje sasa.

Nikaandika barua then siku naondoka nikaificha kabatini,nikasepa zangu sikuchukua hata kitu kimoja..nikamtext roda aende kabatini sehemu flani kuna ujumbe wake Akaenda akauona...ila HAKUKUBALI,alinambia SAM wewe ni wangu NITAKUPATA TU.

Maisha na mchepuko (wife) yakaendelea... Story ya Roda ni refu kidogo.

Ila point yangu MKUU fanya kama nilivyofanya mimi ila kwakua una mtoto sikushauri uandike barua we fanya kama Unasafiri then kaanze maisha upya mahali na huyo mchumba ako,najua unaweza tishwa kua huyo mchumba ako anakuandalia revenge ila HAPANA kuna wanawake wakisema I LOVE YOU they mean it brother....nenda kwa mchumba ako ila huku ulikozaaa usichukue hata nguo zako mwachie ili ajue bado upo nae yani hata boxa usichukue...GO START YOUR NEW LIFE if you realy care about your baby mama and kid.

Usithubutu kumwambia acha kichwa yake imwambie kua umechwa ila usimwambie,atakapokuja GUndua Utamwambia ukweli..ila jitahidi uende ishi mahali ambapo hatajua hata uko wapi but HUDUMIA MWANAO,wapigie simu..AHADI kibao Wajali kama mwanamke hana kazi msaidie hadi uhakikishe anasimama wima kiasi cha kumuhudumia mwanao bila tatizo...Muda wote huo yuko mbali na wewe Atatongozwa TU na atapata mtu moyo utaomuelewa we muache Hiyo ndio pona yako.

Akija gundua badae una mke haitouma kivileeeeee maana tyr alishazoea maisha ya bila wewe,usimpigie simu ovyo...Hudumia vizuri ila jitoe kwenye akili yake kwa akili as a REAL man UNAE mjali yeye na mwanao.

Umepata kitu MKUU najua.
 
Kosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.

huyu na uhakika anapendwa na wote wawili...Kakutana na wote wamekufa wameoza Chamuhimu ni yeye kuchagua kundi moja ila hili la kwanza asiliache kama kaliokota tuuuu..yahitaji extra akili kupambanua hili...Lazima akubali COST.
 
Sasa mkuu angejua kama huyo mwingne ni wa muhimu asingemwagia ndanii...!! Kwanza huyo mwingine anamchoraa tuu...Kuna siku ataujua ukweli kuhusu huyo anaedai ana future naee hakika atarudi hapa kushuhudiaa... Hakuna mwanamke utamsaliti na kumpa mimba mwanamke mwingine alafu akakusamehe kizembe hivyooo Trust me Hayupooo tena mpo mbaliii aisee huko ukute ashaanza maisha yake na jamaa anamlaaa na wana future yaooo Wanawake usicheze nao mkuuu
mwanamke akikupenda akakolea HATA Umfanyeje hawezi kukuacha...yupo huyo mwanamke mkuu usiseme hayupo...Huyo mchumba ake hajielewi kwa jamaaa hata angamfumania red handed asingemuacha...WHEN A WOMAN LOVE......ndo hiyo sasa wala usiseme hayupo.
 
Pole sana kijana mimi najua unapitia ugum kiasi gani coz hata mimi tatizo kama hilo lishanikuta lkn nashukuru liliisha.
Umeshafanya bonge la mistake kwanza kuendelea kuishi naye huyo babe mama mda wote huo wakati huku unaona huna hisia naye kabisa. Kwa sababu hiyo baki na huyohuyo babe mama.
Huyo mchumba mwingine achana naye, huna namna nyingne ukiforce kumuacha babe mama na kumuoa huyo mchumba utakuja kutusimulia hadithi nyingine.
Best wishes

Afanye anachoona ni sawa...mambo ya ndoa sio ya kushauriwa kabisaaaaaaa Maana unae enda kuishi na mke/mume ni wewe sio tunaotoa ushauri..ukiona Chatu anafaa kuwa mke/mume nenda kaishi nae as long as moyo wako umeridhia kuishi na CHATU...

ndoa is something else...
 
Usitudanganye eti mpenz wako karidhia na kakubali paka leo uko nae nyumbani na mna malengo, acha cinema kaka , usitulishe matango pori, kama karidhia si wote uwaweke ndani gademitiii , unacheza draft tu unakuwa , siku ya leo huyu ,kesho huyu , life is good u know
 
Huyo mchumba wako aliyekusamehe atakuja kukupiga pigo moja takatifu hadi utatamani umrudie huyo mwanamke uliyezaa naye na unayetaka kumuacha akahangaike na damu yako
Hapana mkuuu,hatujui moyo wa huyo mwanamke ila kwa experince zangu Huyo mchumba ake kampenda sana tu mana ingekua ni kumuacha angeweza kumuacha hata saivi,yawezekana hata mchumba wake ana makosa alishayafanya so anaona yeye ni nanai hadi Ahukumu wakati yeye alisamehewa?
 
ha ha ha ha ha ha mkuu endelea na wote mmoja mpangie chumba mbali ukimuacha huyu uliyezaa nae na hana tatizo mtoto atapata shida. Alafu mstahi bwana mbona yeye alikusaidia shida zako wakati unataka kuosha rungu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hii hoja ya polygamy tunaichkulia poa sana lakini kitaeleweka tu
 
Kama unampenda mtoto wako , oa mama yake.
Huyo mchumba wako unadhani amekusamehe ..ila anakuandalia kisasi. She will avenge ..haiwezekani akusamehe na bado unaendelea kuishi na huyo bibie.
Hujawahi kupenda kiasi kwamba hata huyo mwanaume ugundue kafanya kosa Gani huwezi kumuacha??
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Fanya kile kinachoupendeza MOYO wako..usifate ushauri kumbuka haushauriwi aina ya kuku wakufuga unashauriwa mtu utakae ishi nae MPAKA KIFO KIWATENGANISHE BROTHER sio kuku hao useme wakigoma utabadilisha TYPE sikiliza MOYO wako maana tutakao kushauri wengine NDOA zishatushinda,wengine Hatuna hata mpango wa kuoa,wengine yalishatukuta,nk nk so kila mtu atakuaja na VIEWS zake so mwisho wa Yote ni wewe,moyo wako na Akili yako.
 
mwanamke akikupenda akakolea HATA Umfanyeje hawezi kukuacha...yupo huyo mwanamke mkuu usiseme hayupo...Huyo mchumba ake hajielewi kwa jamaaa hata angamfumania red handed asingemuacha...WHEN A WOMAN LOVE......ndo hiyo sasa wala usiseme hayupo.
Haya sawa mkuu... Acha tuone muda ni hakimu mzurii
 
Back
Top Bottom