Naipenda hii ya mbunge wa Chalinze

Naipenda hii ya mbunge wa Chalinze

ONGEZA

Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiweka kando shughuli nzito za kujenga Taifa na kubeba majukumu ya mzazi kwa kuketi chini na kumfumua nywele binti yake Aziza Tamika Kikwete kabla ya kusukwa upya nyumbani kwake Chalinze.

Mhe Ridhiwani ameiambia Globu ya Jamii kwamba kwake yeye hilo ni jambo la kawaida kabisa kwani anasema anatambua umuhimu kwa viongozi kupata muda na kukaa na familia nyumbani kwani kuna maisha baada ya uongozi. Aziza mwenye unri wa miaka 7 na ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mhe. Ridhwani, kachukua jina la bibi yake yaani mama wa baba yake.

issamichuzi.blogspot.com
 
1485322731343.jpg
 
img_20170125_110353_102-jpg.463579


Nimekusaidia kuiweka vizuri, mbona fresh tu man, mie wife na mtoto nawafanyia sana hizo mambo, tunaishi mara moja tu, na watoto wanakua, mambo yanabadilika, kuonyesha upendo pale nafasi inapopatikana ni muhimu sana. Kuna kipindi utatamani kufanya hivyo lakini nafasi haitakuwepo.
 
Yah.siku moja moja unatoa hata ofa ya kufua nguo za watu wote nyumbani.
 
Huyo kafanya kwa ajili ya picha tu.

Body language inakataa.
 
Mmh! Mbona kama huyu mtoto wa kusingiziwa! Namshauri kaka akapime DNA.. Hii siyo sura ya Msoga kabisaa...
 
Back
Top Bottom