Kwa upande wa Russia
1. Alivyomega Crimea sio mabeberu walifurahia, waliruhusu aimege kisha wakalaani kinafki, media zikafunguliwa kumsifia Putin ni mbabe. Asichokijua ni kwamba, walikuwa wanamjaza ili baadae aingie na Ukraine. Hatimae kajaa kweli Ukraine, anatamani kutoka ila akitazama anaona ni aibu nzito kwake.
2. Leo watu wanasifia Russia kuchukua majimbo, wanasahau kuwa mwezi wa 3 au wa 4 nchi za Magharibi zimepanga kutoa bajeti ya vita hii kwa muda wa miaka 5.
3. US akasema kuwa nia yake kule Ukraine ni kutaka Russia atumie muda mwingi ktk hii Vita. Tumesahau hii kauli ya Biden?
HITIMISHO
Russia atachukua miji na vijiji lakini baada ya muda Ukraine itavikomboa tena. Rejea Ukraine alivyoikomboa Kharkiv, Snake Island na sasa Kherson inakaribia kukombolewa.
Hii yote ni kumchosha Russia. Hata hizi kelele Ulaya wanazopiga mfumuko wa bei, kwao wanajua ni kipindi cha muda tu, tayari walishajipanga kukabiliana na Russia.
CHINA V TAIWAN.
Moja ya vitu nisivyovifikiria ni China kuingia Vitani, China ana majirani ambao akiingia Taiwan na akadhoofika kwa namna yoyote ile, basi muda huohuo India na Japan wanaweza nao wakawasha moto hapo China.
India na Japan hawa wana uwezo kabisa wa kuikalisha serikali ya China totally. Hizi nchi mbili teknolojia zao ktk silaha zao za kivita ni nzuri kuliko mchina.
Mziki wa India na Japan sio wa kitoto.