Naionya China, isijaribu

Naionya China, isijaribu

Hakuna kiongozi kama Mao atakayeiongoza China tena, Mao alipotea na ujamaa wake kabisa na haitajirudia hiyo historia mbovu ya China ya zamani baada ya kuonja utamu wa kibepari.
Kwani hapa tunazungumzia ujamaa wa China chini ya Chairman Mao au tunazungumzia kiongozi mwenye kaliba ya Chairman Mao ili kukamilisha Taiwan Unification ?🤔
 
Kweli kabisa mkuu, ukitaka kumpinga dikteta ujiandae na safari ya kifo. Ukiona kuna wale wanaompinga huku wakiendelea kuwa hai, basi ujue hao ni watu wa kitengo maalum wanaojifanya kupingana nae ili wengine wafate mkumbo waangamizwe.
 
Hamjambo wakuu.

Ndugu wana Jamii Forum baada ya kufuatilia kile kinachoendelea kutokea kule katika mpaka wa kisiwa cha Taiwan, kuhusu mzozo wa China na Taiwan.

Kama ningekuwa na uwezo wa kuwasiliana na uongozi wa China, basi ushauri wangu mkubwa kwao ingekuwa ni kuwaambia wasithubutu kukivamia kisiwa kile.

Ule ni mtego uliotegwa na hawa wababe wa dunia wakiongozwa na baba lao USA.

Ikumbukwe kwamba hata vita ya Ukraine na Russia ilianza hivi hivi, huku Russia ikiwa na uhakika wa kuisambaratisha Ukraine kwa muda wa siku 3 tu au ikichelewa sana ni week. Sasa kinachoendelea leo kila mtu anakiona.

Russia imekuwa ikitumia kila aina ya njia za kijeshi, rasilimali, na jeshi lake la akiba kuimaliza vita hiyo lkn inashindikana.

Leo hii Russia ishatumia kiasi kikubwa cha silaha zake, ishapoteza kiasi kikubwa cha wanajeshi wake, ishayumbisha uchumi wake na kushuka thamani kwa hela yake (na hili ndio USA na nchi zingine za NATO walilitaka) bila kufanikiwa kuiangusha Serikali ya Ukraine wala kuuteka mji mkuu.

Kile kinachoendelea sasa hivi kimetokana na uzembe wa Putin na serikali yake, sasa wanaona yamekuwa magumu kwao, zile siku 3 ikawa week, ile week ikawa mwezi, mwezi sasa imekuwa miezi.

Na kila wanavyoendelea na vita na ndio jinsi wanavyoendelea kupata hasara kwa kupoteza askari, silaha mbalimbali za kijeshi na kudhoofisha uchumi wao.

Na wamarekani wakishirikiana na ndugu zao wa West wataendelea kuijambisha Russia kwa kujifanya wanaitumia Ukraine silaha (japo nyingi ni za kichovu) ili kuichochea Russia izidi kuendeleza mashambulizi na kudhoofisha nguvu zake kwa miaka kadhaa ijayo.

Ni nani kati ya wana NATO asiejua madhara ya kuingia vitani mzimamzima. Leo hii marekani haiwezi kuthubutu kuingia vitani hata na Mexico, japo kijeshi inaweza kutumia hata jeshi lake lililo katika jimbo la California tu kuisambaratisha Mexico, lakn wanaangalia hasara ambayo inaweza kuipata katika vita hiyo.

Marekani inaweza kutuma silaha au vijana wake kadhaa wa jeshi kwenda kusaidia sehem fulan kwa ajili ya masilahi ya marekani ila haiwezi kuingia vitani moja kwa moja kama ilivyofanya Russia.

Ni mara ngapi Iran imekuwa ikiangamiza ndege zisizo na rubani za Marekani, kuzilipua meli za Marekani na pengine kuteka hata meli za washirika hao wa Marekani, lakn kamwe Marekani haikufikiria na haifikirii kuingia vitani, maana inaelewa kuwa vita kuianza ni vyepesi sana lakin kuimaliza ni vigumu.

Sasa inashangaza kuona China pamoja na kuwa na wasomi wengi pamoja na intelejensi kubwa duniani, lakin inataka kuingia mtegoni kama alivyoingia ndugu yake Russia. USA na swaiba zake wana uwezo wa kutoa msaada kwa Taiwan au Ukraine kwa miaka kumi ili mradi lengo lao litimie.
Marekani na swaiba zake sio wajinga, wanajua vizuri kile wanachokifanya.

Na majibu kuhusu uchumi wa Russia na nguvu zake za kijeshi tutayapata baadae baada ya vita kuisha. Kwa sasa bado inachochewa chochewa ili iweze kutumia hata zile silaha ambazo ingetakiwa kutumia pale inapopambana na nchi kubwa kama USA, China, India nk.
Mwisho wa siku ghala la silaha litabaki tupu.

So naionya China kama inataka kuendelea kuwa nchi ya pili kwa uchumi na ya tatu kwa nguvu za kijeshi, basi iachane na wazo la kuivamia Taiwan maana itapoteza nafasi zake zote mbili, kuanzia kwenye uchumi hadi jeshi. Vikwazo itakavyowekewa na wakubwa hao wa dunia vitakuwa sio vya dunia hii, na hapo ndipo atakapoanza kuona madhara ya kuingia vitani kichwa kichwa bila kutumia akili.
Mbona imeshavuka
 
Siku boss wako akija kumtongoza mkeo mbele
yako na kuazimia kumla sebuleni kwako basi naomba uendelee kulinda uchumi wako kupitia hicho kibarua na kubariki ufedhuli huo kwa roho safi.
Yani kabisa umekaa ukafikiria kutoa mfano wa Ukraine na mke?

Je Putin ana uhalali gani wa kumpangia ukraine cha kufanya kama anavokuwa na uhalali mume kumpangia mke wake cha kufanya? Mfano wa kipuuzi kabisa huu.
 
Mbona imeshavuka
Kuvuka sio tatizo mkuu, hata Malawi waliwahi kuvuka mpaka wetu ila ukiiangalia nchi yenyew haina uwezo wa kupambana hata na FFU wetu. Kinachosubiri ni ule uvamizi wa moja kwa moja kama uliofanywa na Urusi dhidi ya Ukraine. Afu utaona baada ya uvamizi huo China itakuwa ktk hali gani?
 
Yani kabisa umekaa ukafikiria kutoa mfano wa Ukraine na mke?

Je Putin ana uhalali gani wa kumpangia ukraine cha kufanya kama anavokuwa na uhalali mume kumpangia mke wake cha kufanya? Mfano wa kipuuzi kabisa huu.
🤣🤣🤣
 
Mkuu nakubaliana na ww kwa namna fulani, lkn pia ujue kwamb Marekani nayo imekuwa na uzoefu wa miaka mingi wa ku deal na watu wa aina hiyo. Tuliona kilichotokea kwa akina Fidel Castor, Sadam Hussein nk.

Kifupi USA na washirika wake walijiandaa muda mrefu kukabiliana na nchi au viongozi wenye mitazamo tofauti na yao. Na mwisho huwa mbaya kwa hizo nchi afu viongozi wao. Korea Kaskazin leo hii milo mitatu kwa siku inaliwa na maofisa wa Ikulu tu peke yake, huku wananchi wa kawaida wakishindia mlo mmoja kwa siku, Iraq tuliona walivyo deal na Sadam baada ya kumlia taiming muda fulan, Cuba hadi ilifika kipindi wenyew wakaomba poo ili angalau waweze kuwaondolea robo ya vikwazo ili wapate pesa za kuwalipa watumishi wa serikali baada ya serikali yao kufilisika.

So hawa watu wakiamua lao, kweli unaweza ku savaivu miezi au miaka kadhaa kama vile Iran, but one day utajikuta umeingia kwenye 18 zao tu. CIA huwa hawalali kwa sababu ya mission za namna hii.
Hii sentensi ya mwisho ungeibold. Jamaa huwa hawalali, na hawaamini ktk kushindwa, wanaamini ktk kukosea, so wanajikusanya ili kesho warudi tena.
 
Russia haifanyi maamuzi kutokana na think tanks au strategists bali kutokana na anavyojisikia dikteta Putin.
Yani maamuzi ya nchi nzima yanategemea na uamkaji wa Putin, akiamka vibaya na maamuzi yanakuwa mabaya, akiamka vizuri na maamuzi yanakuwa mazuri 🤣🤣🤣
 
Hii sentensi ya mwisho ungeibold. Jamaa huwa hawalali, na hawaamini ktk kushindwa, wanaamini ktk kukosea, so wanajikusanya ili kesho warudi tena.
Ya ni kweli mkuu, thank you kwa ufafanuzi uliojitosheleza.
 
Mkuu

Unaijua sana situation ya China

India na Japan wana long time beef na China na wanasubiri tu aingie mkenge,China atakalishwa vibaya na viutajiri vyake vyote vitabebwa!

Huku upande wa West China an ugomvi na India wa siku nyingi kwa ubabe wake wa kujimegea eneo la India...huku upande wa east kuna Japan ana beef na China la kihistoria na wanagombea visiwa..pia na Taiwan

China ana beef na majrani zake wote 32 na bahari nzima ya South China Sea....Rafiki yake ni mmoja tu pande hizo,North Korea.

Russia mwenyewe kwa upande wa Kaskazini wana beef na China la kitambo sana la eneo la Russia China alijimegea,japo ni marafiki kwa sasa,kikiwaka I doubt kama Russia atakua rafiki wa kweli maana sasa ilitegemewa China asaidie ila kauchuna kama hayupo vile.

China anatafutwa na watu kibao yaani.....na kama akibugi akadhani ni Taiwan tu,basi anafeli..maana hataweza kabiliana na vurugu pande zote za nchi kwa wakati mmoja....watamkamua akauke,we subiri tu
In terms of military technology, Russia na China ni za kawaida tu. Na hii imekuja baada ya sote kushuhudia mbungi ya hapo Ukraine.

Tumeshaona namna mambo halivyobana kwa Russia, ametumia Hypersonic Missiles, Laser Weapons, Jets za kisasa n.k na bado vyote hivi havijaweza kufua dafu kama alivyotarajia.

Sasa je, China yeye tec yake itafua dafu huko Taiwan? Russia alitegemea huu mwiba angekaa nao kwa mwezi wa sita sasa? If hakutegemea, Je China ina uhakika gani wa kutumia muda mfupi wa vita hiyo akitaka kuanzisha?

Wakati vita vinaanza, China alitoa msaada kwa waathirika wa Ukraine. Huu ni usaliti mzito mno kwa best yake Russia. China leo akiingia Taiwan, Russia atamuunga mkono kinafki mno China kutokana na sababu mbili, moja ni ile ya yeye kuwa bado ana mwiba wake ambao ni Ukraine. Na mbili ni usaliti wa China kwa Russia.

Japan, India n.k nahisi wao watakuwa na hamu kubwa mno ya kutaka China aingie hapo Taiwan. Tukumbuke pia, endapo Taiwan ikamtikisa vyema China, kuna uwezekano maeneo mengine ya china yakataka kujitenga na China kama Hong Kong n.k

Wakati naandika hii comment kuna kitu hapa nakifkiria mkuu, hivi sio kwamba pengine CIA walipanga Russia apate vita yoyote ya kumsumbua ili ikitokea Vita ya China na Taiwan basi Russia asipate nguvu ya kumtetea China?
 
Mkuu unaelewa sana hawa hii geopolitics ya USA na China na Russia

Paragraph yako ya mwisho you are 100% right.....

Ile ni kumuweka Russia busy ili China akijichanganya upande ule wamnyooshe....Ndio maana nina uhakika vita pale Ukraine itaenda miaka ya kutosha mpaka Russia aishiwe pumzi kabisa!

West wanajua fujo dunia hii na wanajua jinsi ya kuzipanga na wanaelewa....sasa hii chess China akibugi ameisha

China anatafutwa sana maana amekua too powerful economically and this scares the shit outta the West going forward.
 
Mkuu, China hawezi kuingiza pua yake Town kivita, maana anajua kitakachomkuta kabla ya kujipanga vizuri.
 
Kumbuka America ilivyochapwa na Vietcong wakakimbia Saigon miaka ya 70's, na mwaka jana 2021 wakafukuzwa Afghanistan na Taliban kwa aibu kubwa! Waamerika wanataka kuogopwa na watu kama were mleta uzi huu, ili waitawale DUNIA, na kusambaza sera za unyonyaji, ushoga, kuruhusu mihadarati n.k.
Hata Mrusi Alisha nyooshwa na japan ,Finland ,Chechnya , Afghanistan alipojaribu kuvamia territory za hizo nchi , mvamizi yeyote lazima abondwe Tu awe USA au kenge yeyote Maana hata watu wanakuwa wanapigana jihad (do or die )
 
Hamjambo wakuu.

Ndugu wana Jamii Forum baada ya kufuatilia kile kinachoendelea kutokea kule katika mpaka wa kisiwa cha Taiwan, kuhusu mzozo wa China na Taiwan.

Kama ningekuwa na uwezo wa kuwasiliana na uongozi wa China, basi ushauri wangu mkubwa kwao ingekuwa ni kuwaambia wasithubutu kukivamia kisiwa kile.

Ule ni mtego uliotegwa na hawa wababe wa dunia wakiongozwa na baba lao USA.

Ikumbukwe kwamba hata vita ya Ukraine na Russia ilianza hivi hivi, huku Russia ikiwa na uhakika wa kuisambaratisha Ukraine kwa muda wa siku 3 tu au ikichelewa sana ni week. Sasa kinachoendelea leo kila mtu anakiona.

Russia imekuwa ikitumia kila aina ya njia za kijeshi, rasilimali, na jeshi lake la akiba kuimaliza vita hiyo lkn inashindikana.

Leo hii Russia ishatumia kiasi kikubwa cha silaha zake, ishapoteza kiasi kikubwa cha wanajeshi wake, ishayumbisha uchumi wake na kushuka thamani kwa hela yake (na hili ndio USA na nchi zingine za NATO walilitaka) bila kufanikiwa kuiangusha Serikali ya Ukraine wala kuuteka mji mkuu.

Kile kinachoendelea sasa hivi kimetokana na uzembe wa Putin na serikali yake, sasa wanaona yamekuwa magumu kwao, zile siku 3 ikawa week, ile week ikawa mwezi, mwezi sasa imekuwa miezi.

Na kila wanavyoendelea na vita na ndio jinsi wanavyoendelea kupata hasara kwa kupoteza askari, silaha mbalimbali za kijeshi na kudhoofisha uchumi wao.

Na wamarekani wakishirikiana na ndugu zao wa West wataendelea kuijambisha Russia kwa kujifanya wanaitumia Ukraine silaha (japo nyingi ni za kichovu) ili kuichochea Russia izidi kuendeleza mashambulizi na kudhoofisha nguvu zake kwa miaka kadhaa ijayo.

Ni nani kati ya wana NATO asiejua madhara ya kuingia vitani mzimamzima. Leo hii marekani haiwezi kuthubutu kuingia vitani hata na Mexico, japo kijeshi inaweza kutumia hata jeshi lake lililo katika jimbo la California tu kuisambaratisha Mexico, lakn wanaangalia hasara ambayo inaweza kuipata katika vita hiyo.

Marekani inaweza kutuma silaha au vijana wake kadhaa wa jeshi kwenda kusaidia sehem fulan kwa ajili ya masilahi ya marekani ila haiwezi kuingia vitani moja kwa moja kama ilivyofanya Russia.

Ni mara ngapi Iran imekuwa ikiangamiza ndege zisizo na rubani za Marekani, kuzilipua meli za Marekani na pengine kuteka hata meli za washirika hao wa Marekani, lakn kamwe Marekani haikufikiria na haifikirii kuingia vitani, maana inaelewa kuwa vita kuianza ni vyepesi sana lakin kuimaliza ni vigumu.

Sasa inashangaza kuona China pamoja na kuwa na wasomi wengi pamoja na intelejensi kubwa duniani, lakin inataka kuingia mtegoni kama alivyoingia ndugu yake Russia. USA na swaiba zake wana uwezo wa kutoa msaada kwa Taiwan au Ukraine kwa miaka kumi ili mradi lengo lao litimie.
Marekani na swaiba zake sio wajinga, wanajua vizuri kile wanachokifanya.

Na majibu kuhusu uchumi wa Russia na nguvu zake za kijeshi tutayapata baadae baada ya vita kuisha. Kwa sasa bado inachochewa chochewa ili iweze kutumia hata zile silaha ambazo ingetakiwa kutumia pale inapopambana na nchi kubwa kama USA, China, India nk.
Mwisho wa siku ghala la silaha litabaki tupu.

So naionya China kama inataka kuendelea kuwa nchi ya pili kwa uchumi na ya tatu kwa nguvu za kijeshi, basi iachane na wazo la kuivamia Taiwan maana itapoteza nafasi zake zote mbili, kuanzia kwenye uchumi hadi jeshi. Vikwazo itakavyowekewa na wakubwa hao wa dunia vitakuwa sio vya dunia hii, na hapo ndipo atakapoanza kuona madhara ya kuingia vitani kichwa kichwa bila kutumia akili.
China sio wajinga km walivyo Russia.
Wale jamaa ni watu wanaokupiga kijanja.
We rudi tu Hongkong,walichofanyiwa Hongkong walikatiwa vitu muhimu vya kuwaendesha kiuchumi vikahamishiwa Macau na kukitwa Shanghai.
Kilichotokea shirika la ndege laenda kihasara, unemployment rate imeongezeka n.k n.k
Mpaka hiyo imefanya Hongkong wakuu wapingane na wale wanaotaka Hong Kong ijitenge.
Na hapo Taiwan China anafanya psychological war.
Sidhani kama anataka vita ya Moja Kwa Moja maana China anajua Taiwan haitapigana pekeake.
Pia anajua akijiingiza ktk vita uchumi wake utazorota na kufanya gap kat yake na USA kuongezeka.
 
Back
Top Bottom