Naionya China, isijaribu

Naionya China, isijaribu

Kwa upande wa Russia

1. Alivyomega Crimea sio mabeberu walifurahia, waliruhusu aimege kisha wakalaani kinafki, media zikafunguliwa kumsifia Putin ni mbabe. Asichokijua ni kwamba, walikuwa wanamjaza ili baadae aingie na Ukraine. Hatimae kajaa kweli Ukraine, anatamani kutoka ila akitazama anaona ni aibu nzito kwake.

2. Leo watu wanasifia Russia kuchukua majimbo, wanasahau kuwa mwezi wa 3 au wa 4 nchi za Magharibi zimepanga kutoa bajeti ya vita hii kwa muda wa miaka 5.

3. US akasema kuwa nia yake kule Ukraine ni kutaka Russia atumie muda mwingi ktk hii Vita. Tumesahau hii kauli ya Biden?

HITIMISHO

Russia atachukua miji na vijiji lakini baada ya muda Ukraine itavikomboa tena. Rejea Ukraine alivyoikomboa Kharkiv, Snake Island na sasa Kherson inakaribia kukombolewa.

Hii yote ni kumchosha Russia. Hata hizi kelele Ulaya wanazopiga mfumuko wa bei, kwao wanajua ni kipindi cha muda tu, tayari walishajipanga kukabiliana na Russia.

CHINA V TAIWAN.

Moja ya vitu nisivyovifikiria ni China kuingia Vitani, China ana majirani ambao akiingia Taiwan na akadhoofika kwa namna yoyote ile, basi muda huohuo India na Japan wanaweza nao wakawasha moto hapo China.

India na Japan hawa wana uwezo kabisa wa kuikalisha serikali ya China totally. Hizi nchi mbili teknolojia zao ktk silaha zao za kivita ni nzuri kuliko mchina.

Mziki wa India na Japan sio wa kitoto.
Japan nakubali. Ila India big no
 
Una hoja nzuri.

Wengi wanaona US akiingia vitani na washirika wanahisi US ni weak. Wanashindwa kutambua jamaa anatazama unafuu wa kupambana ktk vita.

Ni mjinga pekee anayedhani Uchumi wa Russia bado uko imara kutokana na vikwazo alivyowekewa. Kila siku nasemaga humu ndani, laiti vyombo vya habari huko Russia vingefunguliwa na kuwa huru kama Ulaya, basi tungesikia mengi zaidi huko Urusi.
Kweli mkuu, vita vya Ukraine vimei cost na kuipa hasara kubwa Russia. Hapo bado hatujazungumzia vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa wa watemi hawa wa dunia ya kwanza. Miaka 3 ijayo Russia itakuwa nyuma hata ya Saudia Arabia kijeshi na kiuchumi.
 
Huu mzozo urusi kauvagaa kwa pupa na kudhania mambo mepesi tu. Tena bora urusi ana resource za muhim ambazo wengine hawana hivo inakuwa ngumu kumpiga sanction akaisha. Chinq akilogwa auvagae huu muziki atapigwa sanction mpaka achakae na soko lake kubwa lipo US na Uerope bidhaa anauza za viwandani ambazo zinakuwa na mbadala muda wowote.
Nahisi anapiga mkwara tu, hawezi kuingia mazima kama mwenzake mrusi. Vita ya urusi imewazindua wengi ambao walifikiri vita ni kitu cha urahisi rahisi tu kama vile kutafuna big jii na kutema.
 
Tujikumbushe kwanza Uchina kama sikosei karibia zaidi ya mara tatu ilijaribu kuivamia Taiwan. Hata pia kwa Taiwan kutaka kufanya mpango wa kurudisha utawala wake Uchina kupitia mpango wa Project National Glory.
Mfano upo mgogoro wa mwaka 1954 ambao ulikuwa mkubwa kiasi kwamba Marekani ilitoa onyo la kutumia mabomu ya Nuclear kama utawala wa Mao Zedong utajaribu kuivamia Taiwan hali iliyomfanya Uchina atulie kwa muda kujitathmini upya. Pitia Taiwan strait crisis 1, 2 na 3.

Hivyo kijana mpango wa Uchina kuivamia Taiwan upo pale pale either through diplomatic process or through armed means, kinachomkwamisha Uchina ni uwepo wa Super Power wa Dunia pale Taiwan ambapo kuwepo kwa Taiwan kunamfanya Marekani aweze kum contain Uchina katika eneo la Pacific ya mbali akisaidiwa na Korea Kusini na Japan.
Uzuri ulijitokeza pale Uchina alipoweza kujitahidi kumtengeneza Communist Ally North Korea la sivyo angekuwa amezingirwa pakubwa sana (Wataalamu wanaelewa hapa madhara ya kuzingwa na adui, ndivyo alivyofanya Urusi baada kuona Ukraine inataka kujiunga NATO).
Katika kila namna Uchina itajaribu kila njia kuichukua Taiwan ila uwepo wa US pale ni nightmare kwa Taifa hilo kwa sababu mbalimbali kama vile uchumi na hali ya usalama maeneo ya Far East itakayo mwarhiri yeye vilevile. Wasalam.
 
U
Hamjambo wakuu.

Ndugu wana Jamii Forum baada ya kufuatilia kile kinachoendelea kutokea kule katika mpaka wa kisiwa cha Taiwan, kuhusu mzozo wa China na Taiwan.

Kama ningekuwa na uwezo wa kuwasiliana na uongozi wa China, basi ushauri wangu mkubwa kwao ingekuwa ni kuwaambia wasithubutu kukivamia kisiwa kile.

Ule ni mtego uliotegwa na hawa wababe wa dunia wakiongozwa na baba lao USA.

Ikumbukwe kwamba hata vita ya Ukraine na Russia ilianza hivi hivi, huku Russia ikiwa na uhakika wa kuisambaratisha Ukraine kwa muda wa siku 3 tu au ikichelewa sana ni week. Sasa kinachoendelea leo kila mtu anakiona.

Russia imekuwa ikitumia kila aina ya njia za kijeshi, rasilimali, na jeshi lake la akiba kuimaliza vita hiyo lkn inashindikana.

Leo hii Russia ishatumia kiasi kikubwa cha silaha zake, ishapoteza kiasi kikubwa cha wanajeshi wake, ishayumbisha uchumi wake na kushuka thamani kwa hela yake (na hili ndio USA na nchi zingine za NATO walilitaka) bila kufanikiwa kuiangusha Serikali ya Ukraine wala kuuteka mji mkuu.

Kile kinachoendelea sasa hivi kimetokana na uzembe wa Putin na serikali yake, sasa wanaona yamekuwa magumu kwao, zile siku 3 ikawa week, ile week ikawa mwezi, mwezi sasa imekuwa miezi.

Na kila wanavyoendelea na vita na ndio jinsi wanavyoendelea kupata hasara kwa kupoteza askari, silaha mbalimbali za kijeshi na kudhoofisha uchumi wao.

Na wamarekani wakishirikiana na ndugu zao wa West wataendelea kuijambisha Russia kwa kujifanya wanaitumia Ukraine silaha (japo nyingi ni za kichovu) ili kuichochea Russia izidi kuendeleza mashambulizi na kudhoofisha nguvu zake kwa miaka kadhaa ijayo.

Ni nani kati ya wana NATO asiejua madhara ya kuingia vitani mzimamzima. Leo hii marekani haiwezi kuthubutu kuingia vitani hata na Mexico, japo kijeshi inaweza kutumia hata jeshi lake lililo katika jimbo la California tu kuisambaratisha Mexico, lakn wanaangalia hasara ambayo inaweza kuipata katika vita hiyo.

Marekani inaweza kutuma silaha au vijana wake kadhaa wa jeshi kwenda kusaidia sehem fulan kwa ajili ya masilahi ya marekani ila haiwezi kuingia vitani moja kwa moja kama ilivyofanya Russia.

Ni mara ngapi Iran imekuwa ikiangamiza ndege zisizo na rubani za Marekani, kuzilipua meli za Marekani na pengine kuteka hata meli za washirika hao wa Marekani, lakn kamwe Marekani haikufikiria na haifikirii kuingia vitani, maana inaelewa kuwa vita kuianza ni vyepesi sana lakin kuimaliza ni vigumu.

Sasa inashangaza kuona China pamoja na kuwa na wasomi wengi pamoja na intelejensi kubwa duniani, lakin inataka kuingia mtegoni kama alivyoingia ndugu yake Russia. USA na swaiba zake wana uwezo wa kutoa msaada kwa Taiwan au Ukraine kwa miaka kumi ili mradi lengo lao litimie.
Marekani na swaiba zake sio wajinga, wanajua vizuri kile wanachokifanya.

Na majibu kuhusu uchumi wa Russia na nguvu zake za kijeshi tutayapata baadae baada ya vita kuisha. Kwa sasa bado inachochewa chochewa ili iweze kutumia hata zile silaha ambazo ingetakiwa kutumia pale inapopambana na nchi kubwa kama USA, China, India nk.
Mwisho wa siku ghala la silaha litabaki tupu.

So naionya China kama inataka kuendelea kuwa nchi ya pili kwa uchumi na ya tatu kwa nguvu za kijeshi, basi iachane na wazo la kuivamia Taiwan maana itapoteza nafasi zake zote mbili, kuanzia kwenye uchumi hadi jeshi. Vikwazo itakavyowekewa na wakubwa hao wa dunia vitakuwa sio vya dunia hii, na hapo ndipo atakapoanza kuona madhara ya kuingia vitani kichwa kichwa bila kutumia akili.
Unafikir hawajui mkuu. Wanajua vizur,ila nchi ikishaongozwa na MTU mmoja inakuaga vigumu kusikiliza washaur,ndio maana marekani hawakurupuk mambo yao yanaamuliwa na vikao
 
Kabisa mkuu, nchi za kidikteta mara nyingi maamuzi yao huwa ni ya mtu mmoja alie mbele ya mstari. Hata kama kuna athari mbele yao wao wataenda tu ili mradi watekeleze matakwa ya dikteta wao.
U

Unafikir hawajui mkuu. Wanajua vizur,ila nchi ikishaongozwa na MTU mmoja inakuaga vigumu kusikiliza washaur,ndio maana marekani hawakurupuk mambo yao yanaamuliwa na vikao
 
Kuna watu wana mahaba Niue humu,wanajifariji kwamba urusi haiathiriki chochote kutokana na hii anayoiita special epereshen,hawajiulizi hata swali la kawaida tu kwamba marekani pamoja na nguvu zake zote alizonanazo, uchumi imara, silaha kibao, mbona hajawai kuingia vitani peke yake mpaka aombe kolabo ya washirika wake?? .., hakuna kitu kinafilisi uchumi kama vita!
Watu hawaelewi bwashee ,kwanza ukiwa vitani ni ngumu wawekezaji kuwekeza kwako kuhofia usalama,pia vita inaharibu diplomatic relationship, vita inatafuna bajet ya nchi,vita vinamaliza wanajeshi muhimu,vita vinaua biashara,yaan nikuambie tuu Russia anasababisha hasara kwa pande zote mbili,,ila navyoona Russia mda si mwing ataomba wayamalize mezan maana kama walimdindia kumwachia yule demu mcheza basketball kwa njia ya SWAP Jana naona Russia wamekubali yaishe.ngoja tuone maana sisikii tena Putin akileta mbwembwe
 
Kwa upande wa Russia

1. Alivyomega Crimea sio mabeberu walifurahia, waliruhusu aimege kisha wakalaani kinafki, media zikafunguliwa kumsifia Putin ni mbabe. Asichokijua ni kwamba, walikuwa wanamjaza ili baadae aingie na Ukraine. Hatimae kajaa kweli Ukraine, anatamani kutoka ila akitazama anaona ni aibu nzito kwake.

2. Leo watu wanasifia Russia kuchukua majimbo, wanasahau kuwa mwezi wa 3 au wa 4 nchi za Magharibi zimepanga kutoa bajeti ya vita hii kwa muda wa miaka 5.

3. US akasema kuwa nia yake kule Ukraine ni kutaka Russia atumie muda mwingi ktk hii Vita. Tumesahau hii kauli ya Biden?

HITIMISHO

Russia atachukua miji na vijiji lakini baada ya muda Ukraine itavikomboa tena. Rejea Ukraine alivyoikomboa Kharkiv, Snake Island na sasa Kherson inakaribia kukombolewa.

Hii yote ni kumchosha Russia. Hata hizi kelele Ulaya wanazopiga mfumuko wa bei, kwao wanajua ni kipindi cha muda tu, tayari walishajipanga kukabiliana na Russia.

CHINA V TAIWAN.

Moja ya vitu nisivyovifikiria ni China kuingia Vitani, China ana majirani ambao akiingia Taiwan na akadhoofika kwa namna yoyote ile, basi muda huohuo India na Japan wanaweza nao wakawasha moto hapo China.

India na Japan hawa wana uwezo kabisa wa kuikalisha serikali ya China totally. Hizi nchi mbili teknolojia zao ktk silaha zao za kivita ni nzuri kuliko mchina.

Mziki wa India na Japan sio wa kitoto.
Na mchina alivyokwaopua Hong Kong ndio hivyo hivyo kama case ya Russia kukwapua Crimea , sasa muache ajichanganye kuingia Taiwan hapo ndio atajua maharage sio mboga
 
Watu hawaelewi bwashee ,kwanza ukiwa vitani ni ngumu wawekezaji kuwekeza kwako kuhofia usalama,pia vita inaharibu diplomatic relationship, vita inatafuna bajet ya nchi,vita vinamaliza wanajeshi muhimu,vita vinaua biashara,yaan nikuambie tuu Russia anasababisha hasara kwa pande zote mbili,,ila navyoona Russia mda si mwing ataomba wayamalize mezan maana kama walimdindia kumwachia yule demu mcheza basketball kwa njia ya SWAP Jana naona Russia wamekubali yaishe.ngoja tuone maana sisikii tena Putin akileta mbwembwe
Hahaha Putin kanywea kama kidonge kinapowekwa ndan ya glas ya maji.
Sasa hivi anamtumia sana waziri wake wa mambo ya nje katika mambo yake.
 
Na mchina alivyokwaopua Hong Kong ndio hivyo hivyo kama case ya Russia kukwapua Crimea , sasa muache ajichanganye kuingia Taiwan hapo ndio atajua maharage sio mboga
China akipima kuivamia Taiwan ataambulia aibu ya karne. Madege yake na vifaru vya jeshi havitamsaidia kushinda vita.
 
Yaani wabongo bana😂😂😂, unakaa nchi ya ulimwengu wa tatu, kwenye dampo la dunia, unajitia kuwashauri viongozi na serikali ya Russia na China yenye agents hatari wanayoijua hii dunia?
Umekula ugali wako na muhogo umeshiba unakuja kudhani una ijua kesho ya Russia kuliko FSB? Raisi tu wa Russia ni former KGB, serikali ya Ukraine ina agents wengi tu wana leak data...

Unaijua China kuliko MSS? Chinese wana puppets wengi tu serikali ya Taiwan, tunajua machache sana...

Russia wanajua walifanyalo, walishajiandaa, kila kitu kipo calculated...

Kama umeshiba ugali better ukae chini ufuatilie bifu ya Harmonize na Diamond na udaku wa insta, huwezi ijua China au Russia kama agents wao ambao hawalali, wana risk afya zao na maisha yao, wamesomea ukachero na wanaishi ukachero na wanakula kikachero hata mapenzi ni kikachero, wakipumua ni ukachero... Ogopa sana hio...

Kwamba Russia imeingia mtegoni😂😂😂, Huyo ni mbongo, hivi vile vichwa vyote vya wale wazee pale Moscow vyenye mvi, makachero wabobezi toka USSR hawakujua plans za US?😂😂

Inaskitisha sana kwa kweli..
 
Huu mzozo urusi kauvagaa kwa pupa na kudhania mambo mepesi tu. Tena bora urusi ana resource za muhim ambazo wengine hawana hivo inakuwa ngumu kumpiga sanction akaisha. Chinq akilogwa auvagae huu muziki atapigwa sanction mpaka achakae na soko lake kubwa lipo US na Uerope bidhaa anauza za viwandani ambazo zinakuwa na mbadala muda wowote.
Shida iliyopo US wanategemea bidhaa za china, kuanzia chupi hadi mitambo,, sababu viwanda vilihamia china kukwepa gharama za uzalishaji marekani,
 
Back
Top Bottom