Yaani wabongo bana



, unakaa nchi ya ulimwengu wa tatu, kwenye dampo la dunia, unajitia kuwashauri viongozi na serikali ya Russia na China yenye agents hatari wanayoijua hii dunia?
Umekula ugali wako na muhogo umeshiba unakuja kudhani una ijua kesho ya Russia kuliko FSB? Raisi tu wa Russia ni former KGB, serikali ya Ukraine ina agents wengi tu wana leak data...
Unaijua China kuliko MSS? Chinese wana puppets wengi tu serikali ya Taiwan, tunajua machache sana...
Russia wanajua walifanyalo, walishajiandaa, kila kitu kipo calculated...
Kama umeshiba ugali better ukae chini ufuatilie bifu ya Harmonize na Diamond na udaku wa insta, huwezi ijua China au Russia kama agents wao ambao hawalali, wana risk afya zao na maisha yao, wamesomea ukachero na wanaishi ukachero na wanakula kikachero hata mapenzi ni kikachero, wakipumua ni ukachero... Ogopa sana hio...
Kwamba Russia imeingia mtegoni



, Huyo ni mbongo, hivi vile vichwa vyote vya wale wazee pale Moscow vyenye mvi, makachero wabobezi toka USSR hawakujua plans za US?

Inaskitisha sana kwa kweli..