Naionya China, isijaribu

Naionya China, isijaribu

Putin popote alipo bila shaka atakuwa anjipigapiga kifuani akitubu kwa kuanzisha vita vya kipuuzi
Putin anajuta kwa alichokianzisha. Inafika kipindi anaogopa hata kusafiri kwa amani. Akitaka kwenda mahali anaenda kimagutu bila kutoa taarifa huku akiwatanguliza wana usalama wake kwanz mbele 🤣🤣🤣
 
Kwani raia wachina walisema wamechoshwa na uongozi wao?šŸ¤”
Kule vyombo vya habari havipo huru, kwahiyo hata kama wamechoka hawana pa kuongelea hilo swala na wakasikilizwa. Ndio maana wengi wa walioletwa huku Afrika wameamua kujichimbia huku ili kukwepa aina ya siasa na mfumo wa maisha uliyopo nchini kwao. Wengi wanajuta kuumbwa wachina.
 
Mtapata wapi radio za Bluetooth za elf 20 ?? Unaeza nunua JBL ya laki tano ikiwa tv enyewe unakuta unatumia aborder
Iache iporomoke kiuchumi ili isiwe na hela za kuwajaza wachina africa. wamekuwa kero kila mahali africa hawa wachina. halafu lazima walipe hasara ya kuleta siasa za kupeleka vijana vijijini, kukamata wazururaji na kujenga vyuo vya propaganda.
 
Mkuu Mimi Kama Mimi napenda ujamaa tena Sana .Ila sihitaji wala sipendi kuona ardhi yetu ya Tanzania inaongozwa na mfumo wa chama kimoja hicho kitu Mimi mwenyewe nipo mstari wa mbele kukipinga kwa kuwa kimekwisha Leta matokeo hasi kwetu kwa zaidi ya miaka 60 CCM imetawala bila maendeleo yoyote kutuletea . Mimi ni muumini wa mfumo wa vyama vitatu vyenye nguvu na mgombea binafsi . Pia sipendi kuona serikali ikilazimisha nchi kuongozwa kwa ujamaa kwa 100% au ubepari kwa 100% Mimi napenda kuona serikali ikichukua Yale yaliyo mazuri kwenye ujamaa na kuyatumia na kuchukua Yale yaliyo mazuri kwenye ubepari na kuyatumia kwa faida ya maendeleo ya nchi. Ndio maana namejipachika mjamaa wa kisasa kwa sababu napenda ujamaa uwe kisasa wenye faida ukubali kukopa na kuungiza mambo yenye faida yaliyo nje ya ujamaa kwa sababu Mimi naamini ujamaa unapaswa kuwa mfumo ulio hai unapaswa kukua na kubadilika kutokana na wakati , mazingira na watu ili ulete faida role model wangu wa ujamaa wa kisasa ni mtaalamu Deng Xiaoping. Ni hayo tu machache mkuu
Katika Taifa la watu milioni 58 ni wazi kuwa haiwezekani kamwe kuwa na watu wenye mtazamo mmoja (wa ndiyo mzee), ni lazima kuwe na maoni na mawazo tofauti tofauti ili kulijenga Taifa letu pendwa la Tanzania katika njia iliyosahihi. Elimu pamoja na maarifa ndio uwe msingi wetu katika ujenzi wa siasa bora na maendeleo nchini.

Kwa umri wangu huu naamini Taifa hili bado lina vijana wenye nidhamu, uchapakazi na bidii pamoja na akili kubwa walizozaliwa nazo. Japo muda mwingine mfumo unawakataa kutokana na sababu mbalimbali.

Inanisikitisha mno kuona baadhi ya vijana badala ya kuwa Tunu kwa kutoa fikra mpya yenye kuendana na muda na kuleta maendeleo, wanajadili mambo ya ajabu na hovyo ijapojuwa uhuru wa kufanya hivyo wanao.

Nakupa hongera kwa kuwa na mtazamo ambao naamini kwa yakini kabisa kuwa unatamani kuona Taifa likiendelea, Kongole kwako. Tunaweza kutofautiana katika imani na falsafa zetu, hilo halisababishi uadui Blaina yetu kiasi cha kufedheheshana au kutukanana.
 
Kutoa maoni sio dhambi usipangie watu cha kuongea kama dampo unaushi wewe kunguni mkubwa. Unafikili Russia wana mili ya chuma, unafikili askari wa Russia wanavyofanya mauji ya watoto roho haziwaumi baada ya vita Kuna wengine watapata uchizi ( postpartum depression ). Awe beberu wala Russia hakuna anaeweza kushinda vita ya uonezi.
Sisi tunaishi kwenye jalala la dunia...
 
Hamjambo wakuu.

Ndugu wana Jamii Forum baada ya kufuatilia kile kinachoendelea kutokea kule katika mpaka wa kisiwa cha Taiwan, kuhusu mzozo wa China na Taiwan.

Kama ningekuwa na uwezo wa kuwasiliana na uongozi wa China, basi ushauri wangu mkubwa kwao ingekuwa ni kuwaambia wasithubutu kukivamia kisiwa kile.

Ule ni mtego uliotegwa na hawa wababe wa dunia wakiongozwa na baba lao USA.

Ikumbukwe kwamba hata vita ya Ukraine na Russia ilianza hivi hivi, huku Russia ikiwa na uhakika wa kuisambaratisha Ukraine kwa muda wa siku 3 tu au ikichelewa sana ni week. Sasa kinachoendelea leo kila mtu anakiona.

Russia imekuwa ikitumia kila aina ya njia za kijeshi, rasilimali, na jeshi lake la akiba kuimaliza vita hiyo lkn inashindikana.

Leo hii Russia ishatumia kiasi kikubwa cha silaha zake, ishapoteza kiasi kikubwa cha wanajeshi wake, ishayumbisha uchumi wake na kushuka thamani kwa hela yake (na hili ndio USA na nchi zingine za NATO walilitaka) bila kufanikiwa kuiangusha Serikali ya Ukraine wala kuuteka mji mkuu.

Kile kinachoendelea sasa hivi kimetokana na uzembe wa Putin na serikali yake, sasa wanaona yamekuwa magumu kwao, zile siku 3 ikawa week, ile week ikawa mwezi, mwezi sasa imekuwa miezi.

Na kila wanavyoendelea na vita na ndio jinsi wanavyoendelea kupata hasara kwa kupoteza askari, silaha mbalimbali za kijeshi na kudhoofisha uchumi wao.

Na wamarekani wakishirikiana na ndugu zao wa West wataendelea kuijambisha Russia kwa kujifanya wanaitumia Ukraine silaha (japo nyingi ni za kichovu) ili kuichochea Russia izidi kuendeleza mashambulizi na kudhoofisha nguvu zake kwa miaka kadhaa ijayo.

Ni nani kati ya wana NATO asiejua madhara ya kuingia vitani mzimamzima. Leo hii marekani haiwezi kuthubutu kuingia vitani hata na Mexico, japo kijeshi inaweza kutumia hata jeshi lake lililo katika jimbo la California tu kuisambaratisha Mexico, lakn wanaangalia hasara ambayo inaweza kuipata katika vita hiyo.

Marekani inaweza kutuma silaha au vijana wake kadhaa wa jeshi kwenda kusaidia sehem fulan kwa ajili ya masilahi ya marekani ila haiwezi kuingia vitani moja kwa moja kama ilivyofanya Russia.

Ni mara ngapi Iran imekuwa ikiangamiza ndege zisizo na rubani za Marekani, kuzilipua meli za Marekani na pengine kuteka hata meli za washirika hao wa Marekani, lakn kamwe Marekani haikufikiria na haifikirii kuingia vitani, maana inaelewa kuwa vita kuianza ni vyepesi sana lakin kuimaliza ni vigumu.

Sasa inashangaza kuona China pamoja na kuwa na wasomi wengi pamoja na intelejensi kubwa duniani, lakin inataka kuingia mtegoni kama alivyoingia ndugu yake Russia. USA na swaiba zake wana uwezo wa kutoa msaada kwa Taiwan au Ukraine kwa miaka kumi ili mradi lengo lao litimie.
Marekani na swaiba zake sio wajinga, wanajua vizuri kile wanachokifanya.

Na majibu kuhusu uchumi wa Russia na nguvu zake za kijeshi tutayapata baadae baada ya vita kuisha. Kwa sasa bado inachochewa chochewa ili iweze kutumia hata zile silaha ambazo ingetakiwa kutumia pale inapopambana na nchi kubwa kama USA, China, India nk.
Mwisho wa siku ghala la silaha litabaki tupu.

So naionya China kama inataka kuendelea kuwa nchi ya pili kwa uchumi na ya tatu kwa nguvu za kijeshi, basi iachane na wazo la kuivamia Taiwan maana itapoteza nafasi zake zote mbili, kuanzia kwenye uchumi hadi jeshi. Vikwazo itakavyowekewa na wakubwa hao wa dunia vitakuwa sio vya dunia hii, na hapo ndipo atakapoanza kuona madhara ya kuingia vitani kichwa kichwa bila kutumia akili.
Well said
 
Putin anajuta kwa alichokianzisha. Inafika kipindi anaogopa hata kusafiri kwa amani. Akitaka kwenda mahali anaenda kimagutu bila kutoa taarifa huku akiwatanguliza wana usalama wake kwanz mbele 🤣🤣🤣
Ungeshuhudia msafara wa ndege pamoja na magari Ta usalama yanayo sidikiza gari la Rais wa Merikani awapo safarini kuzuru mataifa megine wala usinge shangaa idadi ya body gaurds na magari yanayo mlinda Putin.
 
Katika Taifa la watu milioni 58 ni wazi kuwa haiwezekani kamwe kuwa na watu wenye mtazamo mmoja (wa ndiyo mzee), ni lazima kuwe na maoni na mawazo tofauti tofauti ili kulijenga Taifa letu pendwa la Tanzania katika njia iliyosahihi. Elimu pamoja na maarifa ndio uwe msingi wetu katika ujenzi wa siasa bora na maendeleo nchini.

Kwa umri wangu huu naamini Taifa hili bado lina vijana wenye nidhamu, uchapakazi na bidii pamoja na akili kubwa walizozaliwa nazo. Japo muda mwingine mfumo unawakataa kutokana na sababu mbalimbali.

Inanisikitisha mno kuona baadhi ya vijana badala ya kuwa Tunu kwa kutoa fikra mpya yenye kuendana na muda na kuleta maendeleo, wanajadili mambo ya ajabu na hovyo ijapojuwa uhuru wa kufanya hivyo wanao.

Nakupa hongera kwa kuwa na mtazamo ambao naamini kwa yakini kabisa kuwa unatamani kuona Taifa likiendelea, Kongole kwako. Tunaweza kutofautiana katika imani na falsafa zetu, hilo halisababishi uadui Blaina yetu kiasi cha kufedheheshana au kutukanana.
Nakupongeza mkuu. Maana Ni Kama upo ndani ya fikra na akili zangu . Kwa 100% Umeiongelea mawazo yangu pia kuanzia mwanzo mpaka Mwisho ulipo hitimisha.

- Ni kweli kabisa mkuu utofauti wa itikadi usitufanye tusipeane nafasi za kusikilizana kwa ajili ya manufaa ya taifa hili ndio maana hata Mimi Ni mpenzi wa falsafa za kijamaa lakini katu siwezi kutokumsikiliza na kumtilia maanani mtu eti kisa yeye ni mpenzi wa falsafa za kibepari la hasha sipo hivyo ndio maana napenda kuona taifa letu lisijengwe katika misingi ya kwamba ni taifa la kijamaa 100% au taifa la kibepari 100% hapana tunapaswa kufungua mlango kwa yote yenye faida tu yapatikanayo ndani ya ujamaa kuingia nchini kwetu na kujenga nchi yetu vivo hivyo tunapaswa kufungua mlango kwa yote yenye faida yaliyo ya kipebari kuingia nchini kwetu na kujenga nchi yetu . Kwa kuwa kiukweli kabisa sisi Kama TANZANIA tumechelewa tena tumechelewa Sana tupo nyuma kweli kweli kimaendeleo wakati matifa ya Asia ya mbali na mataifa ya magharibi yapo mbali kimaendeleo sisi bado tupo nyuma ni Kama wao tayari Ni watu wazima katika maendeleo Ila sisi ndio kwanza tumezaliwa kimaendeleo hata hatua za kuanza kutambaa kimaendeleo hatujaanza hivyo yatupasa kuwakimbilia wao walipo kadili tuwezavyo . Tunahitaji kuwa na kizazi Cha vijana shupavu na wenye kujitambua na sio mradi tuna vijana , vijana shupavu na wenye kujitambua ni mtaji tosha wa kufufua uchumi wetu na kuukuza na pia ndio kichocheo cha mabadiliko nchini.

- Taifa letu lina vijana wengi Sana hilo halipingiki lakini je tujiulize je hao vijana Ni vijana wenye faida kwa taifa ? Ni vijana wenye kujitambua na kujua jukumu lao kwa TANZANIA Ni lipi? Au ndio tunavijana wengi lakini Ni wajinga, wapumbavu, washenzi, wahitimu badala ya wasomi , wanaowaza umbea kuliko Mambo ya msingi , walioendekeza ngono, wasiojikita na kujishughulisha na Mambo ya msingi Ila ni watu wanaopenda kufuatilia na kuyapa nafasi Mambo ya kijinga na ya kipumbavu yanayo tokea katika Taifa letu Ila mambo ya msingi wao kujishughulisha nayo ni ukoma, vijana waliojikatia tamaa kimaisha.

- Taifa letu linahitaji vijana walio na afya ya akili wenye kujitambua na kujua Tanzania inahitaji nini kufanyiwa na sio kuiacha inaendelea kuzama hivi hivi taratibu kuliko kuinuka na kukimbizana na waasia ya mbali na wamagharibi.
 
Kule vyombo vya habari havipo huru, kwahiyo hata kama wamechoka hawana pa kuongelea hilo swala na wakasikilizwa. Ndio maana wengi wa walioletwa huku Afrika wameamua kujichimbia huku ili kukwepa aina ya siasa na mfumo wa maisha uliyopo nchini kwao. Wengi wanajuta kuumbwa wachina.
Hawa waliokuja Afrika wamekuja kutengeneza pesa na sio kwamba wamekimbia serikali yao huko China.
 
Hawa waliokuja Afrika wamekuja kutengeneza pesa na sio kwamba wamekimbia serikali yao huko China.
Ya wanaweza kuwa wamekuja kutengeneza pesa, lkn pia kuwa huru katika kufanya maamuzi ya maisha yao kwa njia ya uhuru. Kwa mfano hawa pichan wakija Afrika au wakienda ktk nchi yoyote nje ya China watakuwa na hamu ya kurudi tena nchini kwao?
 

Attachments

  • images (36).jpeg
    images (36).jpeg
    36.1 KB · Views: 11
  • images (34).jpeg
    images (34).jpeg
    41.7 KB · Views: 11
  • images (14).jpeg
    images (14).jpeg
    38.2 KB · Views: 12
Kwa upande wa Russia

1. Alivyomega Crimea sio mabeberu walifurahia, waliruhusu aimege kisha wakalaani kinafki, media zikafunguliwa kumsifia Putin ni mbabe. Asichokijua ni kwamba, walikuwa wanamjaza ili baadae aingie na Ukraine. Hatimae kajaa kweli Ukraine, anatamani kutoka ila akitazama anaona ni aibu nzito kwake.

2. Leo watu wanasifia Russia kuchukua majimbo, wanasahau kuwa mwezi wa 3 au wa 4 nchi za Magharibi zimepanga kutoa bajeti ya vita hii kwa muda wa miaka 5.

3. US akasema kuwa nia yake kule Ukraine ni kutaka Russia atumie muda mwingi ktk hii Vita. Tumesahau hii kauli ya Biden?

HITIMISHO

Russia atachukua miji na vijiji lakini baada ya muda Ukraine itavikomboa tena. Rejea Ukraine alivyoikomboa Kharkiv, Snake Island na sasa Kherson inakaribia kukombolewa.

Hii yote ni kumchosha Russia. Hata hizi kelele Ulaya wanazopiga mfumuko wa bei, kwao wanajua ni kipindi cha muda tu, tayari walishajipanga kukabiliana na Russia.

CHINA V TAIWAN.

Moja ya vitu nisivyovifikiria ni China kuingia Vitani, China ana majirani ambao akiingia Taiwan na akadhoofika kwa namna yoyote ile, basi muda huohuo India na Japan wanaweza nao wakawasha moto hapo China.

India na Japan hawa wana uwezo kabisa wa kuikalisha serikali ya China totally. Hizi nchi mbili teknolojia zao ktk silaha zao za kivita ni nzuri kuliko mchina.

Mziki wa India na Japan sio wa kitoto.
Ha ha eti India wako vizuri kijeshi kuliko China? Hii Ni miujiza mkuu.
Wachina ndege Vita zao advanced Sana ukiachana na J 20 stealth fighterjet jet Bado wanabase Sana na wanna idadai kubwa ya Russian class of flankers Su 35 na linceced produced J17 ambayo Ni modernized Russian su 27.
India wamerely kwenye Russian class of flankers Aina ya Su 30 MKI flankers.
Ukiachana na su 30Mki India wanna Russian mig 29 za kutosha.
Kiuwezo Ni karibu wanalingans na pengine China iko juu coz kwa siku za karibuni wamekua wakijitengenezea makombora na ndege zao advanced kushindana na Superior Russian na America military technologies.
Eg
Chinese stealth fighterjet J 20
Chinese dongfeng missiles.
Chinese made helicopters Nk.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom