Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,650
- 21,014
Gongo ni kiswahili cha spirit.
Duniani kuna aina nyingi sana za mianzi. Mianzi inayopatikana Africa kwa wingi inaitwa Oxytenanthera abyssinica. Hii ni mianzi ya kipekee sana kwa sababu mbili.
Kwanza ni mianzi inayovumilia sana ukame na mbili ni kwasababu ni mianzi pekee inayotoa pombe ya ulanzi.
Unafahamu kuwa hakuna mmea duniani unaokuwa kwa kasi kuliko mianzi?
Pombe( ethanol) ina matumizi mengi lakini makuu ni matatu. Kunywa, sanitizer na fuel. Tuzungumzie kunywa.
Nadharia.
Upande mianzi kwenye ekari moja kwa spacing ya mita 5x8. Ndani ya ekari moja utakuwa na mianzi au mashina ya mianzi 100.
Kila shina uvune ulanzi lita 3. Utakuwa na jumla ya lita 300 kwa ekari.
Ukifanya fermentation , natural fermentation huwa inafika hadi 12% Hivyo kwenye lita 300 utapata lita 36 za pure alcohol.
Tuseme unataka kutengeneza gongo yenye kiasi cha 35%ABV(alcohol by volume) basi hizo lita 36 za pure alcohol utapata lita 102 zenye alcohol ya 35 %(100/35x36).
Hizo lita 100 utoe vinywaji vyenye ujazo wa 200mls. Utapata pcs 500 kila siku.
Tuseme unajumlisha kila pisi kwa 2700. Utapata 1.35m kwakwa siku kwa ekari moja.
Ukiwa na ekari kumi basi utazalisha pombe ya milioni 13.5 kwa siku. Ulanzi unagemwa kila siku kwa muda wa kama wa miezi minne, siku 120. Hii itakupa 160m kwa ekari kwa msimu.
Vitu vinavyohitajika, utatakiwa kuwa na distiller ndogo, nimeziona mtandaoni zipo za bei ndogo. Utahitaji kujenga distillery. Utahitaji kujenga fermentation tanks, hizi utahitaji uwe nazo za kutosha. Store na utahitaji packing machine. Kabla ya yote ni vizuri ukafanya huu utafiti lab au hata home kwako ili uone kama upo feasible.
Kuna watu wametengeneza gongo za kipekee kutokana na vitu vinavyopatikana maeneo yao na zimekuwa brand kubwa sana duniani. Brand kama Amarula na Tequila ni kutoka vitu local tu.
Kama imani yako hairuhusu unaweza tumia hiyo ethanol kutengeneza sanitizer. Pia ije siku tuendeshe magari kwa kutumia ethanol ya ulanzi.