Hii ndio akili

Hii ndio akili

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
40,710
Reaction score
63,385
Ukishajenga nyumba ya kwanza, ya pili huna haja ya kujenga nyumba za namna hiyo tena.

Akili inatakiwa ikue; tafuta shamba kuanzia ekari ishirini na kuendelea, ndani ya hilo shamba jenga nyumba yako ndogo tu, na weka uzio kwenye hilo eneo lako lote.

Tafuta wale wanaochimba visima virefu, chimba visima 2 na jenga minara mirefu miwili ya matanki ya lita 20,000 kila mnara.

Vuna maji kwenye visima na pandisha kwenye matanki, fanya kilimo cha umwagilia wa mboga mboga unazozifahamu hapa duniani.

Kusanya hela za mauzo.

Wamatumbi watakuwa wanasema, pale ni kwa mu-Israel kwa sababu hii akili wanayo wao tu na mimi basi.

Usione fahari ya kutembelea mabati ya milioni 200+ wakati huna kitu cha namna hii nilichoeleza.

Hii ndio akili.​
 
Back
Top Bottom